Baadhi ua Wabunge wa Mkoa wa Kagera Wakifuatilia Mada Katika kikao
Baadhi ya Waandishi wa Habari Wakitekeleza Majukumu yao Katika Kikao cha Bodi ya Barabara Mkoani Kagera
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Kijuu Katikati Akiongea na Wajumbe wa Kikao cha Bodi ya Barabara Mkoani Kagera Hawapo Pichani
Wajumbe Wakifuatilia Mada katika Kikao cha Bodi ya barabara Mkoani Kagera
Na
Sylvester Raphael
Mkuu wa Mkoa wa Kagera aagiza Mkandarasi wa Kampuni ya MECCO aliyeshinda
zabuni ya ujenzi wa barabara zenye
thamani ya shilingi bilioni saba na kukataa kusaini mkataba wa kuanza ujenzi katika Halmashauri ya Manispaa
ya Bukoba kukamatwa na kufikishwa Ofisini kwake akiwa na pingu mikononi ili
kutoa sababu za kuitia Serikali hasara.
Mhe. Meja Jenerali Mstaafu Salum
M. Kijuu alitoa agizo hilo kwa Kamanda wa Polisi Mkoa kwenye kikao cha Bodi ya
Barabara kilichofanyika Mkoani Kagera Machi 8, 2018 ambapo katika kuwasilisha
hoja Mstahiki Meya wa Manispaa ya Bukoba Chief Karumuna kumuomba Mkuu Mkoa kumchukulia hatua
Mkandarasi huyo baada ya kugoma kusaini mkataba wakati alishinda zabuni ya
ujenzi wa barabara hizo.
Chief Karumuna alisema kuwa
Manispaa ya Bukoba imepata hasara baada ya Mkandarasi kukataa kusaini mkataba
wa kuanza ujenzi wa barabara zenye thamani ya shilingi bilioni saba na zabuni
kutangazwa tena upya, pia alisistiza kuwa fedha hizo zilitolewa na Benki ya
Dunia na utekelezaji wa miradi yake ni wa kipindi maalumu kwa hiyo Mkandarasi
huyo amechelewesha muda wa utekelezaji.
Katika kikao hicho ambacho Mkuu
wa Mkoa ni Mwenyekiti aliwasistiza Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini TARURA
Mkoa wa Kagera kuhakikisha wanatengeneza barabara za mipakani ili kuimarsha
ulinzi na usalaama wa mkoa na na chi kwa ujmla. Barabara hizo ni
Bubale-Missenyi Runch- Kakunyu Kilomita
32.5, Bubale – Kamwema Kilomita 17.8
Wilayani missenyi na barabara ya Nyabishenge-Nyakanoni-Ibanda Game
Reserve kilomita 15 Wilayani Kyerwa.
Vilevile Meneja wa Wakala wa
Umeme na Ufundi (TEMESA) Mkoa wa Kagera ameagizwa na kikao hicho kusitisha mara
moja tozo ya shilingi 80,000/= ya ukaguzi wa magari ya Serikali pale
yanapotakiwa kukaguliwa ili yakatengenezwe baada ya wajumbe kuwasilisha sheria
kikaoni inayoelekeza kuwa magari ya Serikali yanatakiwa kukaguliwa bure. Hadi
Mkuu wa mkoa atakapopata walaka unaoruhusu kutoza magari ya Serikali.
Mkoa wa Kagera unahudumia barabara
zenye mtandao wenye jumla ya kilomita 7,505.42 kati ya hizo, kilometa 675.46 ni
barabara za lami, kilometa 2,791.56 barabara za changarawe na kilometa 4,038.96
zikiwa in barabara za udongo.
Mkoa wa Kagera kwa mwaka wa fedha
2017/18 uliidhinishiwa shilingi Bilioni 10,710.05 kwajili ya matengenezo ya
kazi za barabara na ujenzi wa madaraja. Pia mkoa umeidhinishiwa shilingi
bilioni 14,180.937 kwa ajili ya matengenezo ya Barabara
Kuu na Barabara za Mkoa kwa mwaka wa fedha 2017/18
Katika
kuadhimisha Siku ya Wanawake Mkoani Kagera Mkuu wa Mkoa wa Kagera amemwagiza
Mkuu wa Wilaya ya Karagwe Godfrey Mheluka kumkamata na kumpeleka ofisini kwake kijana
anayemtesa mama yake mzazi kwa kutaka kumnyanganya shamba lake na mama huyo
ameshinda kijana huyo mara mbili Mahakamani.
“Mtafute kijana
huyo na kumleta kwangu nijue ana matatizo gani ili tumsaidie maana atamuua mama
yake, hana uchungu na mama yake mzazi. Mama huyoaliwasilisha kilio chake katika
mkutano wa Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi Mhe. Lukuvi Wilayani Karagwe
lakini kijana huyo bado anaendelea kumsumbua mama yake mzazi.” Alifafanua Mkuu
wa Mkoa Kijuu.
0 comments:
Post a Comment