Operesheni Kimbunga yatumika kutapeli

WANANCHI wa maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Bukoba vijijini mkoani Kagera wamekumbwa na taharuki kubwa baada ya askari mgambo kujifanya maofisa wa Operesheni Kimbunga awamu ya tatu, huku wakijitambulisha kama maofisa Usalama wa Taifa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
Kwa mujibu wa taarifa zilizolifikia gazeti hili, mgambo hao walifika katika maeneo mbalimbali ya Tarafa ya Rubale wakiwa wamevalia sare za Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
Akizungumza na Tanzania Daima, Shaban Buruan ambaye ni mmiliki wa duka la bidhaa mbalimbali, alisema akiwa dukani kwake lilifika kundi la watu, wengine wakiwa wamevalia sare za JWT na wengine kiraia, wakamueleza kuwa ni maofisa wa Operesheni Kimbunga awamu ya tatu, wakiongozana na mtendaji wa Kijiji cha Kihumulo, Gidius Alfred.
Buruan alisema baada ya kujitambulisha, walimuomba leseni ya biashara huku wale waliokuwa wamevalia kiraia wakijitambulisha kama maofisa wa TRA.
Alisema kuwa hakuwapa leseni hiyo kwa vile hakuwa nayo mahala hapo, na hivyo wakamtaka awape fedha sh laki moja, jambo ambalo hakuliafiki badala yake akaomba muda awaletee, lakini waliondoka.
Naye Clementina Kakooza ambaye ni raia wa Rwanda aliyeolewa Tanzania, alisema mgambo hao walifika kwake wakiwa na sare za JWTZ wakiongozana na mtendaji wa kijiji na kumtaka awaonyeshe vibali vyake vya kuishi nchini la sivyo watamfikisha polisi.
“Waliponitishia hivyo niliwaeleza kuwa nimebaki kutokana na agizo la serikali kuwa watu tulioolewa na Watanzania tubaki wakati tukifanya utaratibu wa kupata vibali, walikataa na kusema kuwa niwapatie kiasi cha sh 500,000 ambacho sikuwa nacho.
“Nikataka niwape ng’ombe wawili na mbuzi mmoja wakagoma na kulazimisha niwapatie fedha, hapo ndipo tuliposhituka na kupiga simu polisi Rubale,” alisema. 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Philip Kalangi alithibitisha kutokea kwa tukio hilo Oktoba 26 mwaka huu, katika Kijiji cha Kihumulo, Tarafa ya Rubale, Halmashauri ya Bukoba.
Alisema kuwa baada ya Operesheni Kimbunga awamu ya pili kitaifa kumalizika, walikabidhi majukumu yote kwa kamati ya ulinzi na usalama za vitongoji, kata, wilaya na mkoa kuendelea na taratibu za kubaini wahalifu wa makosa mbalimbali.
Kalangi alisema wakiwa katika maeneo mbalimbali ya kutekeleza majukumu ya kikazi, walipata taarifa kuwa kuna mgambo walionekana wakifanya kazi ya kukamata watu na kuwahoji, hususani wahamiaji haramu. Walifika eneo la tukio na kufanikiwa kuwakamata mgambo watatu.
Aliwataja waliowakamatwa kuwa ni Amran Sadick, Abeid Amada na Mathias Sospeter ambao ni mgambo wa Manispaa ya Bukoba na Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Kihumulo, Gidius Alfred.
Alisema mtendaji huyo alikamatwa kwa kosa la kushirikiana na mgambo hao kufanya kazi bila kushirikiana na uongozi wa kata na wilaya.
Kwa mujibu wa Kalangi, walipofikishwa polisi na kuhojiwa hawakuwa na la kujitetea zaidi ya kuomba msamaha.
Alisema watuhumiwa wote wamefikishwa mahakamani kwa kosa la kudai fedha kwa njia ya vitisho na uchunguzi unaendelea ili kuendelea kubaini makosa yao mengine kwa ajili ya kuwasilisha ushahidi mahakamani.
Hata hivyo, alifafanua kuwa wakati watuhumiwa hao wanakamatwa, hawakuwa na sare za jeshi lolote na kwamba uchunguzi bado unaendelea.
Chanzo: Tanzania Daima

Muleba waahidiwa watalaamu wa upimaji ardhi

Wananchi Wilaya ya Muleba Mkoa Kagera wamehaidiwa kuletewa wataalamu wa kupima ardhi ili kutenganisha maeneo ya wakulima na wafugaji.

Ahadi hiyo imetolewa jana na Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Profesa Anna Tibaijuka wakati akihutubia wananchi wa Kata ya Kabilizi iliyoko Wilaya ya Muleba.

Profesa Tibaijuka ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo Muleba Kusini amesema ili kuondoa tatizo la wakulima na wafugaji hakuna budi kuwapimia ili kila kundi litambue maeneo yake bila kuingiliana.

Amesema wafugaji wamekuwa na tatizo la kuwacha mifugo yao iharibu mazao ya wakulima na amemwagiza Mkuu wa Wilaya kuwa mifugo ikikamatwa ndani ya shamba la mtu aishughulikie mara moja..

Kata hiyo ya Kabilizi imekuwa na mgogoro baina ya Wakulima na Wafugaji kwa muda mrefu na hivi sasa kumekuwepo na ufumbuzi baada ya Waziri kutatua tatizo hilo..

BALOZI WA JAPAN ARIDHISHWA NA UJENZI WA DARAJA LINALOUNGANISHA TANZANIA NA RWANDA


  Balozi wa Japan Mheshimiwa Masaki Okada (wa kwanza kushoto) akiwa na Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli (nyuma ya Balozi) pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Maendeleo ya Usafirishaji nchini Rwanda Bw. Guy Kalisa (mwenye tai nyekundu) wakikagua eneo la kituo cha pamoja cha ukusanyaji ushuru kwa upande wa Rwanda.
 Balozi wa Japan Mheshimiwa Masaki Okada (wa pili) akiwa na Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli (nyuma) pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Maendeleo ya Usafirishaji nchini Rwanda Bw. Guy Kalisa (wa pili kutoka nyuma) wakikagua eneo la kituo cha pamoja cha ukusanyaji ushuru kwa upande wa Rwanda.
 Injinia Hitoshi Kameda (kushoto) akitoa maelezo kwa Balozi wa Japan Mheshimiwa Masaki Okada (wa pili kushoto) akiwa na Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli (wa pili kulia) pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Maendeleo ya Usafirishaji nchini Rwanda Bw. Guy Kalisa (kulia) wakikagua eneo la ujenzi wa daraka la Rusumo kwa upande wa Rwanda.


Maporomoko ya Rusumo katika Mto Kagera linapojengwa draja la kuziunganisha nchi za Tanzania na Rwanda katika wilaya ya Ngara mkoani Kagera.
Magari yakipita katika daraja la zamani (kulia) ambalo linatumika hadi sasa na kushoto ni ujenzi wa daraja jipya ukiendelea katika Mto Kagera eneo la Rusumo

******


Balozi wa Japan nchini Tanzania Mheshimiwa Masaki Okada ameelezea kuridhishwa na utekelezaji wa mradi ujenzi wa daraja la kimataifa la Rusumo na kituo cha pamoja cha ukusanyaji ushuru katika eneo la Rusumo mpakani wa Tanzania na Rwanda. 
Miradi hiyo miwili mikubwa inayofadhiliwa na Serikali ya Japan ilianza kujengwa mwezi Machi mwaka huu wa 2013 na imepangwa kukamilika mwezi Novemba mwaka 2014. 
 “Nimeridhishwa na viwango na kasi ya utekelezaji wa mradi huu” alisema Balozi Okada wakati alipotembelea eneo hilo la mpakani mwa Tanzania na Rwanda ambapo alisisitiza kuwa, inatia moyo kuona fedha zilizotolewa na nchi yake zikitumika vizuri kwa lengo la kukamilisha miradi hiyo kwa wakati. 
 Naye Meneja wa Tanroads wa Mkoa wa Kagera Injinia John Kalupale akitoa taarifa kwa Balozi huyo wa Japan ambaye alifuatana na Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli, alielezea kuwa uamuzi wa kujenga daraja jingine katika eneo hilo la mpakani, unatokana na mahitaji halisi ya wakati huu kwani daraja linalotumika hivi sasa lilijengwa miaka 40 iliyopita likiwa na uwezo wa kubeba tani 32. 
Aliendelea kueleza kuwa ingawa miaka ishirini baada ya ujenzi wa daraja hilo kulifanyika ukarabati mkubwa kwa lengo la kuimarisha uwezo wake, bado kumeendelea kuwepo kwa ongezeko kubwa la magari hasa yanayosafirisha bidhaa kati ya Bandari ya Dar es Salaam na nchini jirani ya Rwanda. Injinia Hitoshi Kamega ambaye ni Mhandisi Mkazi wa Kampuni mbili zilizoungana kuusimamia mradi huo ambazo ni Chodei Co. Ltd. na Nippon Koei Co, amelezea kuwa ujenzi wa daraja hilo la Rusumo lenye urefu meta 80 pamoja na kituo cha ushuru, unatekelezwa na Mkandarasi Daiho Co. kutoka Japan kwa gharama ya Shilingi bilioni 31.736. 
 Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli hata hivyo alibainisha kujitokeza kwa mapungufu katika baadhi ya maeneo ya mradi huo ambayo wizara yake kwa kushirikiana na Ubalozi wa Japan hapa nchini wanayafanyiakazi ili kuhakikisha kuwa kunakuwepo na uwiano mzuri wakati wa utekelezaji wa mradi huo na pale huduma zenyewe zitakapoanza kutolewa.. Waziri Magufuli aliyataja baadhi ya mapungufu hayo kuwa ni pamoja na kutotengwa kwa eneo la kutosha la maegesho ya magari kwa upande wa Tanzania na kuhitajika kwa upanuzi wa majengo ya huduma za kiutawala hasa wakati wa kutekeleza mipango ya baadaye kwa kuzingatia ongezeko la shughuli za kibiashara linavyoonekana katika eneo hilo.

PICHA NA MICHUZI BLOG
   
PI


Breaking News: ajali mbaya imetokea eneo la Migela Mjini Bukoba, watu wahofiwa kupoteza maisha


Ajali mbaya muda imetokea muda huu eneo la Migela Mjini Bukoba,uwenda watu wakapoteza maisha kufuatia zoezi la uokoaji linaloendelea kwa kusuasua.  Endelea kufuatilia.


Picha kwa hisani ya Mdau Mc Baraka Galiatano

WACHEZAJI WA YANGA WATUA SALAMA MJINI BUKOBA, TAYARI KWA MPAMBAO NA KAGERA SUGAR JUMAMOSI HII.

Mapema Asubuhi hii Ndege ya Precision Air ikiingia kwenye uwanja wa Ndege wa Bukoba, kuwaleta wachezaji wa Yanga ambao wanatarajia kucheza mchezo wao na Wenyeji Kagera Sugar kesho kutwa Jumamosi.
Wachezaji wa Yanga wakishuka, mbele ni Mbuyu Twite wakishuka uwanja wa Ndege Bukoba
Nizar Khalfani nae yupo kwenye kikosi
Wachezaji wakiendelea kushuka kwenye ndege
Tayari wamekanyaga Ardhi ya Bukoba
Kama kawaida: kushoto ni Khalfan Ngassa kulia ni Niyonzima
Picha ya Pamoja Viongozi na wachezaji
chanzo Vijimambo Blog
 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kagera Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa