Home » » Muleba waahidiwa watalaamu wa upimaji ardhi

Muleba waahidiwa watalaamu wa upimaji ardhi

Wananchi Wilaya ya Muleba Mkoa Kagera wamehaidiwa kuletewa wataalamu wa kupima ardhi ili kutenganisha maeneo ya wakulima na wafugaji.

Ahadi hiyo imetolewa jana na Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Profesa Anna Tibaijuka wakati akihutubia wananchi wa Kata ya Kabilizi iliyoko Wilaya ya Muleba.

Profesa Tibaijuka ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo Muleba Kusini amesema ili kuondoa tatizo la wakulima na wafugaji hakuna budi kuwapimia ili kila kundi litambue maeneo yake bila kuingiliana.

Amesema wafugaji wamekuwa na tatizo la kuwacha mifugo yao iharibu mazao ya wakulima na amemwagiza Mkuu wa Wilaya kuwa mifugo ikikamatwa ndani ya shamba la mtu aishughulikie mara moja..

Kata hiyo ya Kabilizi imekuwa na mgogoro baina ya Wakulima na Wafugaji kwa muda mrefu na hivi sasa kumekuwepo na ufumbuzi baada ya Waziri kutatua tatizo hilo..

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kagera Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa