MBEGU BORA ZA MIGOMBA, VIAZI LISHE NA MIHOGO KUWAKOMBOA WAKULIMA MKOANI KAGERA

Kaimu Ofisa Kilimo Wilaya ya Muleba,  Kokushubila Pesha akipanda mbegu ya muhogo katika shamba darasa la kikundi cha Ujamaa  lililopo Kata ya Magata Karutanga wilayani humo. 


Ofisa Mtendaji wa kata ya Magata Karutanga Joyce Rassia akizungumza na wakulima wakati wa uzinduzi wa upandaji wa shamba darasa la kikundi hicho.










Mjumbe wa kikundi cha Ujamaa,  Liberatha Lespicius akisoma risala wakati wa uzinduzi huo mbele ya mgeni rasmi.


Mtafiti wa mazao ya mizizi kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo Maruku,  Jojianas Kibula akitoa maelekezo kwa wakulima jinsi ya kupanda mbegu hizo bora za mihogo kwa wakulima wa kata ya Magata Karutanga wilayani Muleba.


Baadhi ya wana kikundi cha Ujamaa wakishirikiana kwenye kupanda mbegu hizo bora baada ya uzinduzi rasmi wa shamba darasa hilo.


Kaimu afisa ugani wa wilaya ya Muleba  Kokushubila Pesha akizungumza na wakulima wakati akizungua shamba darasa hilo kwa niaba ya Mkurugenzi mtendaji wa wilaya hiyo.


Afisa mtendaji wa kijiji cha Omurunazi Edga Rumanyika akitoa neno kwa wageni na wanakikundi cha Mendeleo wakati wa uzindizi wa shamba darasa la Migomba.


Muwakilishi wa mk urugenzi mtendaji wa wilaya ya Muleba Kokushubila Pesha akitoa neno kwa wageni na wanakikundi cha Mendeleo wakati wa uzindizi wa shamba darasa la Migomba.


Wanakikundi cha Maendeleo kwenye kijiji cha Omurunazi wilayani Muleba  wakisikiliza maelekezo na maneno ya viongozi na wataalamu kabla ya kuzindua upandaji wa shamba darasa lao la Migomba kijijini hapo.


Afisa kilimo Mkoa wa Kagera Luois Baraka akizungumza na wakulima wa kijiji cha Omurunazi na kutoa salama za ofisi ya mkuu wa mkoa kwa wakulima hao.


Picha ikionyesha shamba darasa lililoandaliwa na wanakikundi cha Omurunazi kikundi cha Maendeleo kwaajili ya kupanda mbegu safi za migomba iliyozalishwa kwa njia ya chupa.


Mtafiti kutoka COSTECH,  Bestina Daniel akizungumza na wakulima na kuwapa salamu za mkurugenzi mkuu wa COSTECH.


Msaidizi wa katibu wa kikundi cha Maendeleo Sekunda Peter akisoma Risala ya kikundi chao


Mtafiti kutoka COSTECH Beatrice Lyimo akizungumza na wakulima wa kikundi cha maendeleo na kuwaeleza malengo na faida za mbegu hizo wilayani humo.






Muwakilishi wa Mkurugenzi mtendaji wa wilaya ya Muleba Kokushubila Pesha akizungua shamba la kikundi cha Maendeleo kwa kupanda mche wa kwanza wa Mgomba kwenye shamba darasa hilo.
Na Dotto Mwaibale, Muleba, Kagera

Imeelezwa kuwa Usambazaji wa mbegu za mazao ya mizizi na Migomba kwa vikundi vya wakulima kwenye Mkoa wa Kagera utasaidia kuwahakikishia wananchi wa mkoa huo usalama wa chakula na mazao mbadala baada ya zao lao kuu la chakula la mgomba kuathiriwa na ugonjwa wa  mnyauko.

Kauli hiyo imetolewa na Afisa Kilimo Mkoa wa Kagera,  Louis  Baraka wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukamilika kwa zoezi la ugawaji wa mbegu bora za mazao hayo kwenye wilaya tano za mkoa huo ambazo ni Missenyi, Karagwe, Kyerwa, Biharamulo na Muleba.

Alisema kuwa wakazi wa mkoa huo wamekuwa na njaa kali kwa misimu miwili iliyopita  kutokana na zao lao kuu la chakula la migomba kushambuliwa na ugonjwa hatari wa mnyauko na hivyo kuwafanya wananchi kuhangaika kutafuta chakula na kuomba chakula cha msaada kutoka Serikalini.

Baraka alisema kuwa upatikanaji wa mbegu bora za migomba safi iliyozalishwa kwa njia ya chupa itafufua zao hilo ambalo wakulima wengi walishalitelekeza kabisa baada ya kuona zao hilo likikauka na kushindwa kuwapatia chakula walichokizoea kwa miaka mingi.

Aidha Baraka  ameishukuru  Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) na Jukwaa la Bioteknolojia kwa Maendeleo ya Kilimo OFAB kwa kuwapelekea pia mbegu bora za Mihogo aina ya Mkombozi na Mbegu bora za viazi lishe ili kuwapatia wananchi wa mkoa huo mazao mbadala baada ya kutegemea zao la mgomba pekee.

Alisema kuwa kwenye wilaya zote tano za mkoa wa Kagera COSTECH imeweza kuwapatia mbegu za marando ya viazi lishe  30,000, Mihogo mbegu 27,000 na Migomba 1,000, ingawa wameongea na wafadhili hao na kuwaahidi kuwaongeza mingine zaidi ya 500.

Kwa upande wake Mtafiti kutoka COSTECH, Bestina Daniel alisema kuwa mpango huo ni mkakati wa utekelezaji wa majukumu ya tume ya kufikisha matunda ya tafiti mbalimbali zinazofanywa hapa nchini kwa walengwa ili ziweze kuzaa matunda yaliyokusudiwa.

Alisema kuwa baada ya watafiti kumaliza kufanya tafiti zao huziacha kwenye vituo vyao vya utafiti lakini COSTECH inasaidia kuhakikisha tafiti hizo zinatoka kwenye vituo hivyo na kwenda kwa wakulima kama ambavyo wameamua kufanya kwenye zao la 
Muhogo,Migomba na viazi lishe ambavyo vinasaidia kuongeza lishe,usalama wa chakula na kipato.

Bestina pia alibainisha kuwa ili kufikia uchumi wa viwanda ni lazima maandalizi ya upatikanaji wa malighafi kwaajili ya viwanda hivyo yafanyike ili wawekezaji wanapokuja wakute tayari malighafi zipo na hivyo kumhakikishia upatikanaji wa 
malighafi hizo zitokananzo na mazao ya kilimo.

Mtafiti huyo kutoka COSTECH alisema mara viwanda vinapoanzishwa vitasaidia wakulima wengi wa mazao hayo kupata soko la uhakika na kuongeza chachu ya uzalishaji kwakuwa wakulima wengi nchini kilio chao kikubwa ni soko la mazao yao.

Hata hivyo amewataka kuendelea kuzalisha mazao hayo kwa wingi hususani mihogo na viazi lishe kwakuwa soko la kwanza ni wao wenyewe na hata sasa mahitaji ya mazao 

kama vile viazi lishe ni makubwa kwenye kaya na maeneo mengi nchini hivyo wasiwe na shaka na soko kwa sasa.

Akizungumzaia umeuhimu wa vikundi,mashamba darasa hayo ya mbegu Mtafiti kutoka  COSTECH Dkt. Beatrice Lyimo alisema kuwa COSTECH haiwezi kuwafikia wakulima wote kwenye mkoa mzima na kuwagawia mbegu hizo bora lakini kupitia vikundi wakulima  wanaweza kuzizalisha na kasha kugawana kwenda kwenye mashamba yao na baadae kuwapatia na wakulima wengine nje ya vikundi hivyo.

Aliwataka kuzitunza na kuhakikisha zinalindwa maana ni lulu na zimenunuliwa kwa gharama kubwa na endapo watazitunza vizuri baadae wataweza kuwauzia wakulima wengine kwenye maeneo mbalimbali na hivyo kuzifanya zienee kwenye maeneo yote ya 
mkoa huo.

Mtafiti wa Mazao ya Miziz kutoka Kituo cha Utafiti wa kilimo ARI-Maruku cha mkoani Kagera Jojianas Kabula aliwaambia wakulima kuwa hekta moja ya muhogo tani 25 hadi 
32 wakati viazi tani 7 hadi 9 kwa Hekta moja.

Alisema kuwa endapo watafuata kanuni bora za kilimo cha mazao hayo kwa kuzingatia nafasi kati ya mche na mche na mstari kwa mstari na matumizi ya mbolea wataweza kuongeza uzalishaji zaidi tofauti na sasa ambapo kwenye hekta moja ya muhogo tani
nane hadi kumi wakati kwenye viazi wanapata tani moja hadi 3.

Mtafiti huyo alisisitiza kuwa mbegu hiyo ya Muhogo ya Mkombozi imefanyiwa utafiti  na kuonekana kustahimili magonjwa hatari ya mihogo ya batobato kali na michirizi ya kahawia ambayo imekuwa ikiwapatia hasara kubwa wakulima wengini kwa kupoteza hadi asilimia 90 za mazao.

Akizungumzia zao la Migomba Mtafiti wa zao hilo kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo Maruku,  Jasmeck Kirangi alisema mbegu hizo zilizozalishwa kwa njia ya chupa ni safi na hazina magonjwa kabisa na endapo wakulima watazipanda kwenye maeneo safi wataweza kupata mavuno bora kulimo matumizi ya mbegu hizo zao za kawaida.

Aliwaondoa hofu kuwa mbegu hizo walizowaletea ni zilezile za asili zinazopendwa na wakulima wengi kama vile Nshakala hivyo wasiwe na shaka kuwa mbegu hizo zilizozalishwa kwa njia ya chupa sio zile walizozizoea.

Kilangi amesema kuwa mbegu hiyo aina ya Nshakala kama mkulima ataipanda vizuri na kuweka mbolea na kwa kuzingatia nafasi zinazoelekezwa na wataalamu mkulima anaweza 
kupata tani kumi na mbili hadi  ishirini na nne kwa ekari mavuno ambayo kwa sasa wakulima wengi hawafikii.

(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com simu namba 0712727062)



WAKULIMA WILAYANI BIHARAMULO WAIPONGEZA COSTECH KWA KUWAPELEKEA MBEGU BORA YA MIHOGO NA VIAZI LISHE


Watafiti, Dk.Beatrice Lyimo (wa tano kushoto) na Bestina Daniel (wa pili kulia), kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH),wakiwakabidhi mbegu bora ya mihogo Wanakikundi cha Chapakazi katika  Kijiji cha Kalebezo wilayani Biharamulo mkoani Kagera jana, kwa ajili ya kuanzisha shamba darasa wakati wa uzinduzi wa shamba hilo wilayani humo. 

 Mwakilishi wa Ofisa Kilimo wa wilaya hiyo, Bruno Ngawagala (kulia), akizungumza na wakulima wakati wa uzinduzi wa upandaji wa mbegu ya mhogo kwenye shamba darasa katika Kijiji Kalebezo wilayani humo.
 Mwenyekiti wa Kikundi cha Chapakazi, Thadeo Kibuka akizungumza katika uzinduzi huo.
 Mtafiti kutoka COSTECH, Bestina Daniel, akizungumza.
 Mtafiti, Dk.Beatrice Lyimo kutoka COSTECH, akizungumzia kuhusu mradi huo wa mbegu bora
 Mtafiti wa mazao jamii ya mizizi kutoka Kituo cha Utafiti cha ARI-Maruku mkoani Kagera, Josianas Kabura (mwenye mbegu), akitoa mafunzo kwa wakulima jinsi ya kupanda mbegu hiyo ya mhogo aina ya Mkombozi iliyozalishwa kitaalamu. 
Mtafiti wa mazao jamii ya mizizi kutoka Kituo cha Utafiti cha ARI-Maruku mkoani Kagera, Josianas Kabura, akielekeza namna ya upandaji wa mbegu ya viazi lishe katika kijijini cha Msenyi
 Mwakilishi wa Ofisa Kilimo wa wilaya hiyo, Bruno Ngawagala, akipanda mbegu hiyo katika shamba darasa kijijini Kalebezo.



 Mwenyekiti wa Kikundi cha Chapakazi, Thadeo Kibuka akipanda mbegu ya mhogo.
 Ofisa Ugani, Jonas Kamugisha akipanda mbegu ya mhogo.
 Ofisa Ugani wa Kijiji cha Kalebezo, Juster Nkuna akipanda mbegu ya mhogo.
 Mbegu ya mhogo ikishushwa kutoka kwenye gari tayari kwa uzinduzi wa shamba darasa katika Kijiji cha Kalebezo.
 Mwenyekiti wa Kikundi cha Chapajembe wa Kijiji cha Msenyi, Josia Kagwingi, akizungumza wakati wa uzinduzi wa shamba darasa la viazi lishe katika kijiji hicho. Kutoka kushoto ni Katibu wa Kikundi hicho, Mariana Mariko na kulia ni mwanakikundi, Zabia Emanuel.


Mkulima wa Kijiji cha Msenyi, Martin Tibenda akipanda mbegu ya viazi lishe katika uzinduzi wa shamba darasa.

Na Dotto Mwaibale, Biharamulo Kagera.

WAKULIMA wilayani Biharamulo mkoani Kagera wameipongeza Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) pamoja na Jukwaa la Bioteknolojia kwa Maendeleo ya Kilimo (OFAB) kwa kuwapelekea mbegu bora ya migomba,mihogo na viazi lishe ambayo itapandwa katika mashamba darasa na kusambazwa kwa wakulima wengine katika wilaya hiyo.

Pongezi hizo zimetolewa na Mwakilishi wa Ofisa Kilimo wa wilaya hiyo, Bruno Ngawagala wakati wa uzinduzi wa upandaji wa mbegu ya mhogo kwenye shamba darasa katika Kijiji Kalebezo wilayani humo.

"Kwa niaba ya Ofisa Kilimo wa wilaya napenda kuishukuru COSTECH kwa kutuletea mbegu hizo katika wilaya yetu hasa baada ya kuona changamoto tuliyokuwa tukikabiliana nayo ya magonjwa ya mihogo kama batobato" alisema Ngawagala.

Ngawagala alisema msaada huo hautapotea bure kwani watahakikisha wanayahudumia vizuri mashamba darasa hayo likiwemo la mihogo lililopo katika Kijiji Kalebezo na lile la viazi lishe lililopo Kijiji cha Msenyi ambayo yamezinduliwa na kuhudhuriwa na wakulima kutoka vikundi vya Chapakazi katika Kijiji cha Kalebezo na Chapajembe cha Kijiji cha Msenyi vyote vya wilaya hiyo.

Mwenyekiti wa kikundi hicho cha Chapakazi, Thadeo Kibuka alisema mbegu hiyo waliyoletewa itakuwa mkombozi wao kwani kwa muda mrefu walikuwa na changamoto ya kupata mazao yenye magonjwa kutokana na kukosa mbegu bora na ukame.

"Tutahakikisha shamba ili tunalo lizindua leo hii kwa msaada wa COSTECH na OFAB linakuwa la mfano wa kuzalisha mbegu bora katika wilaya hii" alisema Kibuka.

Akizungumza kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi wa COSTECH, Mtafiti Dk. Beatrice Lyimo alisema COSTECH kwa kushirikiana na OFAB wanaendesha mradi huo ili kuhakikisha kuhakikisha matokeo mazuri ya kazi za tafiti yanawafikia wakulima na kupata chakula cha kutosha.


Alisema COSTECH ndio mshauri mkubwa wa serikali katika masuala ya kilimo cha kitafiti hivyo wanakila sababu ya kuhakikisha tafiti zinazofanyika nchini zikiwafikia walengwa ili waweze kufanya vizuri katika kilimo.


Dk. Lyimo aliwataka wakulima hao kwa kushirikiana na maofisa ugani kuyatunza mashamba darasa hayo ili kupata mbegu nyingi za mazao hayo na kuzisambaza kwa wakulima wengine.

Ofisa Kilimo Mkoa wa Kagera, Louis  Baraka alisema mkoa huo umepata bahati kubwa kwa kupelekewa mbegu hizo katika wilaya tano ambapo katika kila wilaya vijiji viwili vilichaguliwa kuanzisha shamba darasa la mbegu ya mhogo na migomba na viazi lishe kutegemea uhitaji wa zao gani katika kijiji husika.

"Tuna bahati kubwa kuletewa mradi huu katika mkoa wetu hivyo tusiwaangushe hawa wenzetu tuwe wa mfano tuyatunze haya mashamba ili tupate matokeo mazuri" alisema Baraka.


Mtafiti wa mazao jamii ya mizizi kutoka Kituo cha Utafiti cha ARI-Maruku mkoani Kagera, Josianas Kabura amewataka wakulima hao kutambua kuwa mbegu hizo za mihogo walizokabidhiwa zinatunzwa vizuri kwani zinauwezo wa kutoa tani 32 za mhogo kwa ekari moja na kwa viazi lishe zinatoa tani 7 hadi 9 kwa ekari tofauti na mbegu za zamani ambazo hazina tija.

Mashamba darasa ya mbegu bora za Mihogo,Viazi lishe na Migomba iliyozalishwa kwa njia ya chupa yaliyoanzishwa katika mkoa huo yanajumuisha wilaya tano za Mkoa wa Kagera baada ya COSTECH na OFAB kutoa mafunzo kwa wataalamu wa kilimo wa wilaya hizo na  kata zote ikiwa na lengo la kuwasaidia wakulima kuzalisha mazao yao kwa tija na kuachana na kilimo kisicho bora na tija.


RC KAGERA AONGOZA UZINDUZI WA MASHAMBA DARASA WILAYANI MISSENYI

 Mkuu wa Mkoa wa Kagera,Meja Jenerali Mstaafu, Salum Kijuu  (wa tatu kulia), akikata utepe kuashiria uzinduzi  rasmi wa mashamba darasa ya kilimo bora cha mihogo na migomba iliyozalishwa kwa njia ya chupa (tissue culture), kwa ufadhili  wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kwa kushirikiana na Jukwaa la Bioteknolojia (OFAB) katika vijiji vya  Bunazi na Kashaba wilayani Missenyi mkoani humo leo. Shamba hilo litasimamiwa na Kikundi cha Ushirika cha Batekaka. Kutoka kulia ni Mkuu wa Wilaya hiyo, Luteni Kanali, Denis Mwila, Mwenyekiti wa Kikundi hicho, Belington Kyokwete, Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), ambaye ni Mkurugenzi wa Utawala na Fedha, Shaban Hussein na Mwenyekiti wa Halmshauri ya Wilaya ya Missenyi, Projestus Tegamaisho.

 Miche ya migomba ikiwa tayari kupandwa.
 Ofisa Ugani wa Kata ya Kasambya, Hakika Ibrahim, akizungumza kataika uzinduzi huo.
 Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), ambaye ni Mkurugenzi wa Utawala na Fedha, Shaban Hussein, akizungumza katika uzinduzi huo.
 Mtafiti kutoka OFAB, Dk. Beatrice  Lyimo akizungumza katika uzinduzi huo.
 Mtafiti kutoka Kituo cha Utafiti cha ARI-Maruku akielezea mbegu hiyo mpya ya migomba.
  Mkuu wa Mkoa wa Kagera,Meja Jenerali Mstaafu, Salum Kijuu (wa tatu kulia),  Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), ambaye ni Mkurugenzi wa Utawala na Fedha, Shaban Hussein na Mkuu wa  Mkuu wa Wilaya hiyo, Luteni Kanali, Denis Mwila (kulia), pamoja na Mwenyekiti wa Kikundi cha Ushirika cha Batekaka, Belington Kyokwete, wakiwa wameshika mmoja wa mche wa mgomba katika uzinduzi huo. 

 Mkuu wa Mkoa wa Kagera,Meja Jenerali Mstaafu, Salum Kijuu , akipanda mche wa mgomba kwenye shamba darasa katika Kijiji cha Bunazi.
 Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), ambaye ni Mkurugenzi wa Utawala na Fedha, Shaban Hussein, akipanda mgomba kwenye shamba darasa hilo.



   Mkuu wa Mkoa wa Kagera,Meja Jenerali Mstaafu, Salum Kijuu , akiwahutubia wananchi wa Kijiji cha Kashaba kabla ya kuzindua shamba darasa la zao la mhogo.
 Usikivu katika uzinduzi huo. Kutoka kulia ni Mtafiti kutoka OFAB, Dk. Beatrice  Lyimo, Mwakilishi wa Katibu Tawala Mkoa wa Kagera, Adam Swai na Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), ambaye ni Mkurugenzi wa Utawala na Fedha, Shaban Hussein, akipanda mgomba kwenye shamba darasa hilo.
 Wananchi wa Kijiji cha Kashaba wakiwa kwenye uzinduzi huo.
 Mkuu wa Mkoa wa Kagera,Meja Jenerali Mstaafu, Salum Kijuu , akimpongeza kijana, Shafii Idrisa wa Kijiji cha Kashaba ambaye ameamua kujishughulisha na kilimo kijijini hapo badala ya kukimbilia mjini na kuendesha bodaboda kama walivyofanya wenzake.


 Mtafiti wa mazao ya jamii ya mizizi kutoka Kituo cha Utafiti cha ARI-Maruku, Jasmeck Kilangi, akimueleza Mkuu wa Mkoa namna ya upandaji wa zao la mihogo.
  Mkuu wa Mkoa wa Kagera,Meja Jenerali Mstaafu, Salum Kijuu, akipanda mbegu ya mhogo katika shamba darasa katika Kijiji cha Kashaba.
Mwenyekiti wa Halmshauri ya Wilaya ya Missenyi, Projestus Tegamaisho, akitoa shukurani baada ya uzinduzi huo.


Na Dotto Mwaibale, Missenyi Kagera

WAKULIMA  wilayani Missenyi Mkoani Kagera wametakiwa kuyatumia matunda ya tafiti za kisayansi yanayoletwa na wataalamu kuboresha kilimo chao na kuongeza tija kwenye mazao mbalimbali ili kuweza kuchangia  malengo ya nchi kufikia uchumi wa kati.

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa mkoa wa Kagera, Meja Jenerali Mstaafu,  Salumu Mustafa Kijuu wakati akizungumza na wanakikundi cha Batekaka kwenye Kijiji cha Bunazi na kikundi cha Obumo wa Kijiji cha  Kashaba  kwenye uzinduzi wa zoezi la utoaji wa Mbegu bora za zao la migomba  iliyozalishwa kwa njia ya chupa na Mihogo yenye ukinzani na magonjwa ya batobato na michirizi ya kahawia zoezi lililofadhiliwa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kupitia Jukwaa la Bioteknolojia kwa Maendeleo ya Kilimo Tanzania (OFAB).

Alisema Kilimo pekee ndicho kinachoweza kuwakwamua wananchi kutokana na wimbi la umasikini lakini akasisitiza kuwa kilimo hicho lazima kizingatie mbinu zote za kilimo bora ambacho kitamuwezesha mkulima kulima eneo dogo na kupata mavuno makubwa na kuchana na kile cha zamani na mazoea cha kulima bila kutumia mbinu za kisayansi.

“Tafiti nyingi zinafanyika hapa nchini lakini zinaishia kwenye makabati na haziwafikii wakulima ambao ndio walengwa wa tafiti hizo lakini nawashukuru COSTECH kwa kushirikiana na watafiti wetu kwa kutuletea mbegu hizi bora mlizozitafiti na kujihakikishia kuwa zinauwezo wa kutatua changamoto za wakulima wetu na kuongeza tija”Alisema Mkuu huyo wa mkoa wa Kagera.

Mkuu huyo wa mkoa wa Kagera ameshukuru COSTECH kwa kuamua kusaidia kuwafikishia wakulima mbegu bora za MIhogo na Migomba na kuanzisha mashamba darasa kwenye wilaya zote za mkoa huo ambayo yatawezesha wakulima wengi zaidi kujifunza kwa vitendo na hatimae kuweza kuinga mbinu hizo za kisasa zilizotafitiwa na kwenda kuzitumia kwenye mashamba yao baada ya kuona matunda yatokanayo na mshamba hayo.

Meja Jenerali Mstaafu Kijuu pia alibainisha kuwa hivi sasa mkoa umejipanga kuhakikisha kila wilaya inakuwa na kiwanda kimoja kikubwa cha kuchakata zao moja na kila wilaya kuwa na zao moja la biashara hali ambayo itasaidia katika kuwahakikishia masoko ya uhakika wa mazao ya wakulima na hivyo kuongeza ari ya uzalishaji kwenye maeneo mengi.

Aliwataka maofisa ugani kuwasaidia wakulima katika kutumia mbinu bora za kilimo ili kuweza kuzalisha kwa tija na kuwataka kila mmoja kuwa na shamba lake ambalo wakulima wataweza kuona na kujifunza kwao badala ya kuwa wazungumzaji tuu bila wao kuonyesha mfano.

Awali akizungumza malengo ya mpango huo wa ugawaji mbegu na malengo yake, Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH ambaye pia ni Mkurugenzi wa Utawala na Fedha wa COSTECH, Shabani Hussein alisema kuwa mpango huo ni moja ya utekelezaji wa majukumu ya tume hiyo kwa mujibu wa sheria ya uanzishwaji wake ya kuhakikisha matokeo mazuri ya sayansi na teknolojia yanawanufaisha walengwa kwenye maeneo mbalimbali nchini.

Alisema kuwa ili kuweza kufikia adhima ya serikali ya awamu ya tano ya kuwa Tanzania ya viwanda ni lazima suala la kilimo lipewe msisitizo wa kutosha ili kuweza kuzalisha malighafi za kutosha kulisha vwanda vitakavyojengwa  lakini bila kilimo mpango huo unaweza kukwama.

Alisema pamoja na COSTECH kuwa mshauri mkuu wa serikali katika masuala yote yanayohusu sayansi,teknolojia na uvumbuzi lakini pia wanashirikiana na watafiti na vituo vya utafiti katika kusaidia kufikisha matunda hayo ya tafiti kwa wakulima ili kusaidia kuongeza tija na kuwakwamua wakulima katika wimbi la umasikini.

‘’Naamini mbegu hizi tulizozileta leo na mashamba darasa haya yatakuwa chachu kwa wakulima wengine kuona na kujifunza mbinu bora za kilimo kwenye maeneo yao na baadae mbinu hizo kusambaa kwa wakulima wengine kwenye maeneo ya jirani" alisistiza Hussein

Mwakilishi huyo wa Mkurugenzi mkuu wa COSTECH alisema mbegu hizo bora za Migomba safi isiyo na magonjwa pamoja na mbegu bora ya mihogo aina ya Kiroba yenye ukinzani na magonjwa ya batobato kali na michirizi ya kahawia itagaiwa kwenye vikundi kwenye wilaya zote za mkoa huo wa Kagera na kupewa mbinu bora za kilimo kutoka kwa wataalamu.

Mkuu wa WIlaya ya Missenyi, Luteni Kanali Denis Mwila amewapongeza COSTECH na OFAB kwa kutimiza ahadi yao ya kuwaletea wakulima mbegu hizo na kuwaahidi kuwa watasimamia mashamba darasa hayo vizuri hadi kuvuna ili wakulima waweze kuona umuhimu wa sayansi na mbinu bora za kilimo kwenye uzalishaji.

“ Tumepata bahati kubwa sana wana Missenyi uzinduzi huu kimkoa kufanyika kwenye wilaya yetu maana zipo wilaya nyingi lakini bahati imetuangukia sisi hivyo tuyatunze mashamba na mbegu hizi na tusiwaangushe COSTECH waliotuletea mbegu hizi bora” alisema Mwila.

Pia ameiomba serikali kuangalia uwezekano wa kutoa ruzuku za pembejeo mara mbili kwa mwaka kwenye mkoa wa Kagera kutokana na kuwa na misimu miwili ya kilimo badala ya kuwapatia pembejeo msimu mmoja pekee sawa na mikoa mingine yenye msimu mmoja.

Ameahidi kushirikiana na COSTECH na wataalamu katika kila aina ya teknolojia na mbinu bora inayowafaa wakulima wa wilaya yake ili kuwawezesha kuzalisha chakula kingi na mazao ya biashara ambayo wananchi watauza na kujipatia kipato.

Kwa upande wao wakulima kwenye vikundi hivyo wameahidi kuyatunza na kuyalinda mashamba hayo na mbegu hizo ili kuzizalisha kwa wingi na kuweza kuwasambazia wakulima wengine kwenye maeneo yao ili kujihakikishia usalama wa chakula kwa kulima zao bora la muhogo na kulima migombo bora iliyozalishwa kwa njia ya chupa baada a migomba yao kushambuliwa sana na ugonjwa hatari wa mnyauko.

Pia wakapaza sauti zao kwa serikali kuhakikisha wanawapelekea mbegu bora za mahindi na mazao mengine kwa wakati kupitia mpango wa serikali wa kutoa ruzuku ya pembejeo maana kilimo mbili za mbegu bora ya mahindi wananunua kwa wastani wa shilingi 15  bei ambayo ni kubwa kwa wakulima wengi.

IHEMBE MABINGWA KOMBE LA MBUNGE WA KARAGWE

 Mbunge wa Karagwe Mheshimiwa Innocent Bashungwa akimpokea mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Ndani Mh. Mwigulu Nchemba
 Mgeni rasmi akiwasili katika uwanja wa changarawe ilipofanyika fainali ya Bashungwa Karagwe Cup
 Mheshimiwa Mwigulu Nchemba akikagua vikosi vya Ihembe na Nyaishozi
 Mchezaji wa Ihembe akipiga mpira wa kona
 Uwanja wa Changarawe ulihosheheni mamia ya mashabiki wa mpira wa miguu
  Ihembe wakishangilia baada ya kupata bao la kwanza
 Wadau wakishuhudia mtanange toka jukwaa la “mzunguko”
 Wachezaji wa Ihembe wakiwa wamemzunguka golikipa wao baada ya kupata kash kash
 Mashabiki wa Nyaishozi wakifuatilia kwa makini mchezo wa Bashungwa Karagawe Cup
 Kombe likikabidhiwa kwa mgeni rasmi
Mbunge wa Karagwe Mh. Innocent Bashungwa akitoa neno la pongezi kwa timu zote shiriki
 Kocha wa Kagera Sugar Meck Mexime akimkabidhi kombe nahodha wa Ihembe
 Ihembe wakifurahia kombe lao la ubingwa wa Bashungwa Karagwe Cup
Furaha na shangwe baada ya kutangazwa mabingwa

Timu ya kata ya Ihembe imeibuka mabingwa wa Bashungwa Karagwe Cup 2017 baada ya kuifunga Nyaishozi mabao 2-1. Mchezo huo uliopigwa katika uwanja wa Changarawe huku mgeni rasmi akiwa Waziri wa Mambo ya ndani Mheshimiwa Mwigulu Nchemba uliteka hisia za mamia ya wakazi wa jimbo la Karagwe waliojitokeza kwa wingi.

Ihembe walikuwa wa kwanza kupata goli dakika 25 kupitia kwa Athumani Chuji aliepiga shuti kali la mpira wa adhabu uliomshinda golikipa wa Nyaishozi na kuingia wavuni. Bao hilo lilionekana kuwachanganya Nyaishozi ambao walionyesha kutoelewana katika eneo la ulinzi na kujikuta wakiruhusu bao la pili katika dakika ya 35 lililofungwa na Mshauri Kato aliewatoka walinzi wa Nyaishozi na kufunga goli la kiustadi.  Kipindi cha pili Nyaishozi waliuanza mchezo kwa kasi na kufanikiwa kupata bao katika dakika ya  78 lililofungwa na mshambuliaji MC, hata hivyo jitihada za kusawazisha matokeo zilikwamishwa na mlinda mlango wa Ihembe alieokoa michomo mingi.

Kufuatia ushindi huo Ihembe walijipatia kombe na kiasi cha fedha shilingi milioni moja na nusu huku Nyaishozi wakipata shilingi laki saba na nusu kama kifuta jasho kwa kushika nafasi ya pili. Akizungumza baada ya mchezo huo mbunge wa Karagwe Mheshimiwa Innocent Bashungwa alisema mashindano hayo yatakuwa endelevu kila mwaka ili kuibua vipaji vya vijana wa Karagwe waweze kujiajiri kupitia michezo na kuahidi kuboresha mashindano yajayo kwa kusaka wadau wengine watakaohakikisha wilaya ya Karagwe inakuwa na timu bora ya kushiriki ligi kuu.

Nae kocha bora wa ligi kuu msimu uliopita ambaye pia ni kocha wa Kagera Sugar Meck Mexime aliyapongeza mashindano hayo na kuahidi mchezo wa kirafiki baina ya Kagera Sugar na  kikosi cha wachezaji bora waliochaguliwa toka mashindano hayo.

 
 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kagera Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa