Maafisa Habari na Tehama wakiwa katika mafunzo juu ya namna bora ya uandishi wa habari za Tovuti.
Na:
Sylvester Raphael
Serikali
kupitia Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kwa
kushirikiana na Mradi wa kuboresha Mifumo ya Serikali PS3 waendesha mafunzo ya
siku nne juu ya namna bora ya uandishi wa habari za Tovuti za Serikali kwa
Maafisa Habari na Maafisa Tehama wa Mikoa na Halmashauri zote Tanzania Bara.
Kutokana na umuhimu wa Tovuti za
Serikali hasa katika Mamlaka ya Serikali za Mitaa nchini kuwa chanzo kikuu cha
habari kwa wananchi Serikali kwa kushirikiana na Mradi wa Maboresho ya Mifumo
ya Serikali PS3 waliona kuna umuhimu wa kuendesha mafunzo juu ya uandishi bora
wa habari katika Tovuti za Mikoa na Halmashauri ili wananchi wapate habari muhimu na zenye
uhakika juu ya maendeleo yao.
Kwakuwa siyo Mikoa yote na
Halmashauri zote nchini zina Maafisa Habari na kazi za Habari zinafanywa na
baadhi ya watu kama Maafisa Tehama, Ofisi ya Rais TAMISEMI na Mradi wa
kuboresha Mifumo ya Serikali PS3 wameona kuna umuhimu wa Maafisa hao kupitishwa
katika mafunzo ya namna bora ya uandishi wa habari za Tovuti kwa wananchi ili
kuwa na uelewa wa pamoja na aina moja ya uandishi (House Style)
Katika Mafunzo hayo mada mbalimbali
zihusuzo Uandishi wa Habari zinawasilishwa na wataalamu waliobobea katika mambo
ya habari na uandishi wa habari pia ambapo mada hizo ni pamoja na Malengo ya
Mwongoz wa Tovuti, Sheria na Maadili ya
Habari, Upigaji wa Picha za Kidijitali, Mbinu za Mahojiano, Uandishi wa Aya,
Habari katika mfumo wa 5Ws + H (Piramidi iliyogeuka).
Mafunzo ya namna bora ya uandishi
wa habari za Tovuti za Serikali yanaendeshwa katika makundi ya mikoa mbalimbali
ambapo mikoa ya Geita, Tabora Kigoma na Kagera mafunzo hayo yanafanyika katika
Mkoa wa Kagera Bukoba Hotel Manispaa ya Bukoba aidha, mafunzo hayo yalianza
Februari 19 na yanatarajia kukamilika Februari 22, 2018.
Matarajio ya Serikali baada ya
mafunzo hayo ni kuona Tovuti za Serikali zinakuwa kitovu cha habari kwa wananchi
na si ilimradi habari tu bali habari zenye weledi, ukweli, uhakika na kuisemea
Serikali inafanya nini katika kuwaletea wananchi maendeleo. Pia katika Tovuti
hizo kuwa na taarifa muhimu mbalimbali zinazohusu taasisi husika mfano Mkoa au
Halmashauri husika.
0 comments:
Post a Comment