Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera Kamishina wa Polisi Diwani Athumani Akishika Mwenge Kutoka kwa Mkimbiza Mwenge Kitaifa Charles F Kabeho Kuashiria Kuwa Mwenge Upo Mkoani Kagera
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Charles Kabeho Akitoa Ujumbe wa Mbio za Mwenge Nyakabango Wilayani Muleba.
Mkimbiza Mwenge Kitaifa Charles Francis Kabeho Akipima Kuhakikisha kuwa Vipimo Katika Daraja la Kishara Vipo Sawa
Mkimbiza Mwenge Kitaifa Kiongozi Akizindua Mradi wa Maji Izigo
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Akimpokea Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Mkoani Kagera
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum M. Kijuu (Kulia) Akikabidhiwa Mwenge wa Uhuru na Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel.
Mradi wa Soko la Ndizi Uliozinduliwa na Mwenge wa Uhuru Wilayani Muleba
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Kijuu Kushoto Akimkabidhi Mwenge wa Uhuru Mkuu wa Wilaya ya Muleba Mhandisi Richard Luyango Ili Ukimbizwe Wilayani Muleba
Na:
Sylvester Rapahel
Mwenge wa Uhuru umepokelewa leo
April 8, 2018 Mkoani Kagera na Mkuu wa Mkoa Meja Jenerali Mstaafu Salum M.
Kijuu kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel katika Kijiji
cha Nyakabango mpakani mwa Geita
na Kagera ambapo katika Mkoa wa Kagera Mwenge wa Uhuru utapitia miradi ya
maendeleo 65 yenye thamani ya shilingi bilioni 12,385,330,354.
Katika miradi hiyo 65 Mwenge wa Uhuru
utazindua miradi 33, utakagua miradi 19, utaweka mawe ya msingi katika miradi 13
aidha, mchanganuo wa gharama za miradi
hiyo 65 itakayopitiwa na Mwenge wa Uhuru ni kama ifuatavyo, Serikali kuu
imechangia kiasi cha shilingi bilioni 5,817,795,968 sawa
na asilimia 47%.
Halmashauri za Wilaya zimechangia kiasi cha shilingi 671,940,497 sawa na asilimia 6%. Aidha wananchi
wamechangia shilingi bilioni 2,181,496,962 sawa na asilimia 17%. Wahisani wamechangia shilingi bilioni 3,714,096,927
sawa na asilimia 30%.
Mwenge wa Uhuru mwaka huu 2018 umebeba kaulimbiu
isemayo “Elimu ni ufunguo wa Maisha; Wekeza Sasa kwa Maendeleo ya Taifa letu.” Kauli mbiu hii inawahamasisha wananchi
hususani wa Mkoa wa Kagera kuwekeza katika elimu kwa kuwapeleka watoto shule
ili mkoa wetu na Taifa kwa ujumla lipate wataalam wa kutosha katika kada
mbalimbali za kitaaluma na hapo taifa letu litapiga hatua kubwa ya maendeleo
kwa kuwatumia wataalamu wetu wa ndani.
Pamoja na Kauli
Mbiu tajwa hapo juu Mbio za Mwenge wa Uhuru katika Mkoa wetu zitaendelea
kuwahamasisha wananchi kuhusu Mapambano dhidi ya Rushwa, Mapambano dhidi ya
VVU/UKIMWI, Mapambano dhidi ya Matumizi ya Dawa za Kulevya na Mapambano dhidi
ya Malaria.
Mara baada ya kupokea Mwenge wa
Uhuru Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Kijuu alimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Muleba
Mhandisi Richard Luyango na Mwenge wa Uhuru ukaanza mara moja mbio zake
wilayani humo za kukagua miradi ya maendeleo.
Akitoa ujumbe wa mbio za Mwenge wa
Uhuru Kiongozi wa Mbio hizo Charle Francis Kabeho katika eneo la Nyakabango
aliwasisitiza wanafunzi kusoma kwa bidii masomo ya Sayansi kwani Serikali
imefanya kazi yake ya kujenga shule na vyumba vya mahabara na kuweka vifaa vya
kutoasha katika maabara hizo