KOMREDI KINANA AZIDI KUCHANA MBUGA, ATUA KYERWA, KAGERA
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akitembelea shamba la mkulima bora wa migomba, Eurius Kishinju katika Kata ya Mabira, wilayani Kyerwa, mkoani Kagera. Kinana ambaye ameambatana na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Nape Nnauye wanaanza rasmi ziara mkoani Kagera, ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi pamoja na kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi
Kishinju ambaye ana shamba la migomba heka 3 mchanganyiko na kahawa, kwa mwezi huuza mikungu 43 kwa mwezi ambapo kila mkungu huuza kwa sh. 10,000, hivyo kujipatia kitita cha sh. 430,000, pia hvuna magunia 25 ya kahawa, ambapo sehemu ya mapoato hayo amejengea nyumba ya kisasa na kusomesha watoto wake wawili katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Chuo Kikuu cha Dodoma.PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
Komredi Kinana akioneshwa zao la kahawa alipotembelea shamba hilo
Komredi Kinana akikagua shmba bora la migomba na kahawa katika Kata ya Mabira, linalomilikiwa na mkulima Kishinju
Wananchi wa Kata ya Nkwenda wakimpigia makofi Katibu Mkuu wa CCM, Komredi Kinana alipokuwa akihutubia katika Kijiji cha Nkwenda, wilayani Kyerwa, ambapo aliahidi kufikisha kilio cha bei ndogo ya kahawa katika vikao vya ngazi ya juu na hasa Kamati Kuu ya CCM Julai mwaka huu, ili wakulima wa zao hilo waruhusiwe kuuza watakako kwenye bei kubwa.
Katibuwa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akihutubia katika mkutano wa hadhara katika viwanja vya Shule ya Sekondari ya Kikukuru, Katika Kata ya Mabira, wilayani Kyerwa. Mabira Kikukuru
Wananchi wakishangilia wakati wa mkutano huo
Komredi Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara katika Kata ya Mabira, wilayani Kyerwa, mkoani Kagera
Wananchi wakimsalimia Katibu Mkuu wa CCM, Komredi Kinana alipokwenda kukagua Zahanati yaKijiji cha Kigorogoro wilayani Kyerwa, Kagera.
Wananchi wakiwa na furaha wakati wa kumlaki Komredi Kinana katika Kijiji cha Kigorogoro, wilayani Kyerwa
Komredi Kinana akihutubia alipokagua maendeleo ya ujenzi wa Soko la Kimataifa la Murongom wilayani Kyerwa, ambao hivi sasa umesimama.Soko hilo lipo mpakani mwa Tanzania na Uganda.
Wananchi bwa Kata ya Kaisho, Kijiji cha Kibingo wakishangilia walipokuwa wakimlaki Katibu Mkuu wa CCM, Komredi Kinana ambaye alifanya ziara katika eneo hilo kuzindua mradi wa maji na kuhutubuia wananchi.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, ,AKIWA AMESIMAMA KWENYE GARI AKIANGALIA MWENENDO WA MKUTANO WA HADHARA KATIKA KIJIJI CHA KIBINGO, WILAYANI KYERWA.
Komredi Kinana akihutubia mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Kibingo, Kata ya Murongo.
Wananchi wakiwa na hamu ya kumsalimia alipowasili katika Mji wa Isingiro,Makao Makuu ya Wilaya ya Kyerwa, mkoani Kagera.
Komredi Kinana akisalimiana na wananchi katika Mji wa Isingiro, wilayani Kyerwa, Kagera.
Ni furaha iliyoje kwa wakazi wa Mji wa Isingiro walipokuwa wakimlaki, Komredi Kinana
Mbunge wa Jimbo la Kyerwa, Kategile akielezea miradi mbalimbali aliyoitekeleza jimbo humo ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi wakati wa mkutano huo wa hadhara
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Napoe Nnauye akihutubia katika mkutano huo.
KINANA AMALIZA ZIARA JIMBO LA BUKOBA VIJIJINI LEO, KESHO KUENDELEA MISENYI
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kushoto , Mbunge wa jimbo la Bukoba Vijijini Mh. Jason Rweikiza katikati na Novatus Nkwama Mwenyekiti wa CCM Bukoba Vijijini wakishiriki kufukia mabomba katika mradi wa maji unaotekelezwa na serikali katika kata ya Ibyera Bukoba vijijini wakati Katibu Mkuu huyo akiendelea na ziara yake katika jimbo hilo leo, Katibu Mkuu huyo yuko katika ziara ya kikazi katika mikoa ya Kagera , Geita na Mwanza akikagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kukagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 huku akihimiza uhai wa Chama akiongozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-BUKOBA VIJIJINI)
Wananchi mbalimbali wakimsubiri Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana huku mabango makubwa yanayoonyesha picha za viongozi wa hao yakiwa yamewekwa katika kijiji hicho wakati alipowasili katika Kata ya Rukoma kwa ajili ya kuzungumza na wananchi.
Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mh John Mongela kushoto wakiwasili katika eneo la mkutano wa hadhara uliofanyika latika kata ya Rukoma.
Mbunge wa jimbo la Bukoba Vijijini Mkoani Kagera Mh. Jason Rweikiza akizungumza na wananchi katika kata ya Rukoma Bukoba vijijini wakati wa Ziara ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana katika jimbo hilo.
Baadhi ya watoto wakiushangaa msafara wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakati ulipowasili katika kata ya Rukoma.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa ameshikana mikono na Mbunge wa jimbo la Bukoba Vijijini Mh. Jason Rweikiza , Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kagera Costansia Buhiye na viongozi wa kata wakati wenyeviti hao wa CCM kata za Bukoba Vijijini walipokabidhiwa baiskeli zilizotolewa na Mbunge huyo kwa watendaji wa Chama cha Mapinduzi Bukoba vijijini.
Bw. Pius Rugonzibwa Mmoja wa waandishi wa habari waliokatika msafara wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa amesimama juu ya kilima huku akiwa amenyanyua juu kompyuta mpakato yake wakati akijaribu kutuma habari katika kijiji cha Rukoma ambachi pia kina tatizo kubwa la mnara wa mawasiliano jambo ambalo Kinana amelichukua na kuahidi kulifanyia kazi ili kata hiyo ipate mawasiliano ya simu na mtandao.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia Katorowananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kata ya Katoro Bukoba Vijijini.
Umati wa wananchi waliohudhuria katika mkutano huo uliofanyika kwenye kata ya Katoro.
Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kata ya Katoro Bukoba Vijijini.
Mbunge wa jimbo la Bukoba Vijijini Mh Jason Rweikiza akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kata ya Katoro Bukoba Vijijini.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Ndugu John Mongela akizungumza na wananchi na kuwaambia asiwatishe mtu nendeni mkatumie haki yenu ya kikatiba mkajiandikishe katika daftari la wapiga kura katika kata ya Katoro Bukoba Vijijini.
Baadhi ya wananchi wakinyanyua mikono yao juu kuashiria kukubaliana na mambo mbalimbali yaliyozungumzwa na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana hayupo pichani katika kata ya Rukoma.
