MAELEZO YA JUMLA KUHUSU MKOA
Mkoa wa Kagera unapatikana kaskazini magharibi mwa
nchi ya Tanzania. Makao makuu ya mkoa yapo katika mji wa Bukoba umbali
wa kilometa 1500 kutoka Dar es Salaam, mkoa huu unapakana na nchi ya
Uganda kwa kaskazini, Rwanda na Burundi kwa upande wa magharibi mkoa wa
Kigoma, Mwanza kwa upande wa kusini na ziwa Victoria kwa upande wa
mashariki. Vile vile mkoa wa Kagera uko kusini mwa ikweta kati ya 1 “00”
na 2”45” latitudi. Kwa Iongitudo uko katika nyuzi 30”25” na 32”40”
Mashariki mwa ‘greenwich'.
Mkoa wa Kagera ulijulikana kama “Ziwa Magharibi” jina
hili lilidumu katika kipindi cha ukoloni na baada ya uhuru mpaka mwaka
1979 baada ya vita kati ya Tanzania na Uganda.
Mkoa ulipata jina hili kutokana na mto Kagera ambao
hutiririsha maji yake kutoka Rwanda kupitia kaskazini na kumwaga maji
yake katika ziwa Victoria.
Mkoa wa Kagera una jumla ya eneo la kilomita za mraba
39,168 kati ya hizo kilometa za mraba 28,513 ni eneo la nchi kavu za
kilomita 10,655 ni eneo la maji. Ukiacha mbali wilaya za Biharamulo na
Chato ambazo ni tambarare sehemu kubwa ya mkoa ni yenye milima na vilima
vilivyogawanywa na mabonde yenye matingatinga. Upande wa magharibi wa
mkoa mito mingi inamwaga maji yale katika mto Kagera ambao nao humwaga
maji yake katika ziwa Victoria.
HALI YA HEWA
Hali ya hewa ya mkoa wa Kagera kwa ujumla ni ya joto
la wastani wa 26.02 sentigredi. Mvua zinanyesha kwa wastani wa milimita
800-1,100 kwa mwaka kati ya mwezi Septemba na Januari na kati ya mwezi
Machi na Mei. Mvua hizi ndizo zinazowezesha kuwepo kwauoto wa asili wa
kuvutia katika maeneo mengi ya mkoa. Kwa miaka ya kawaida mkoa hupata
mvua za uhakika za vuli na masika ambazo ni muhium kwa shughuli za
kilimo na ufugaji.
0 comments:
Post a Comment