Na Anitha Jonas – MAELEZO.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi nchini imefuta
rufaa 38 za wagombea nafasi za ubunge kati ya 54 zilizowasilishwa kupinga baadhi
ya wagombea hao kwa kuwatuhumu kutotimiza vigezo mbalimbali na kusema wagombea
hao wanaweza kuendelea na Kampeni majimboni mwao.
Kauli hiyo ilitolewa jana jijini
Dar es Salaam Mkurugenzi wa Uchaguzi Bw.Kailima
Ramadhan kwenye mkutano na waandishi wa habari.
Alisema kuwa baada ya Wakurugenzi
wanaoshughulikia uchaguzi kuzipitia ,waligundua kuwa rufaa hizo waliziona hazina
mantiki na kukosa ushahidi wa kutosha.
“Wagombea waliokuwa wamewekewa
pingamizi na kuenguliwa katika uchaguzi ni 16 na Tume imewarudisha wagombea 13
kati ya hao na waliobaki watatu ,Tume imeridhia maamuzi ya wasimamizi wa
Uchaguzi”,alisema Bw.Ramadhani.
Aliongeza kuwa Tume hiyo
inaendelea kupitia rufaa za wabunge zilizobaki
kwa kushirikiana na wasimamizi wa uchaguzi ili kupata vielelezo vinavyohusika na pindi itakapokamilisha zoezi
hilo itatoa taarifa yake ikiwa ni pamoja
na rufaa 198 za madiwani kutoka halimashauri mbalimbali nchini.
Aidha alisema kuwa Tume hiyo itaendelea kusimamia haki na kufanya maamuzi
ya kuzingatia sheria kwa wagombea wa vyama vyote vilivyoshiriki katika uchaguzi
wa mwaka huu na kuwataka kuwa na imani na kazi inayofanywa na Tume katika rufaa
hizo.
Mbali na hayo Mkurugenzi wa uchaguzi alisema kuwa Tume inatarajia kuanza zoezi la uhakiki wa
daftari la mpiga kura visiwani Zanzibar kuanzia tarehe keshokuwa (03/09/2015)
ambapo zoezi hilo litadumu kwa muda wa siku saba.
Akiongelea juu ya uhakiki wa
taarifa za mpiga kura aliyejiandikisha
alisema unaweza kuhakiki taarifa zako kwa kupitia mtandao wa tume www.nec.go.tz au kwa kupiga *152*00// katika simu na kupata
taarifa zote.
0 comments:
Post a Comment