MKUU wa Mkoa wa Kagera, Kanali Mstaafu, Fabian
Massawe, amewaonya madereva wa vyombo vya moto mkoani hapa kujiepusha na uvunjaji
wa sheria za barabarani.
Amesema madereva lazima watii sheria za barabarani
bila shuruti, na kwamba serikali haitasita kuwakamata wanaovunja sheria.
Kanali Massawe alitoa onyo hilo juzi wakati wa
sherehe za maadhimisho ya wiki ya usalama barabarani, ambayo kimkoa ilifanyika
Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.
Massawe ambaye alikuwa mgeni rasmi katika
maadhimisho hayo, ambayo kitaifa yalifanyika jijijni Mwanza, alisema lengo la
kuwepo maadhimisho hayo ni kuielimisha jamii juu ya matumizi ya barabara na sheria
za nchi.
“Ajali za barabarani zinaathiri sana maisha ya
wananchi wetu. Kwa hiyo natoa onyo kwa madereva wote kuzingatia sheria,”
alisema.
Alisema jamii kutojua vizuri sheria zikiwemo za
barabarani, kimekuwa chanzo kikubwa cha ukiukwaji wa sheria na kutokea ajali
ambazo nyingi husababisha vifo.
Aliwaomba watembea kwa miguu na waendesha vyombo
vya moto kuwa makini na kuzingatia sheria za barabarani, kani itasaidia
kupunguza ajali.
Chanzo: Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment