Mkoa wa Kagera
umebarikiwa kuwa na uwakilishi mzuri katika tasnia mbalimbali ndani na nje ya
nchi, akina Rweyemamu wanazidi kupasua anga! mfano mzuri ni Mwanamuziki wa kike
Abela ambaye ni mzaliwa wa Bukoba Mkoani Kagera anayepeperusha vyema bendera ya
Tanzania kimziki huko Amerika anakoishi na kufanya kazi zake za muziki.
Abela Kibira alizaliwa
Septemba 22 mwaka 1989 akiwa mtoto wa kwanza katika familia ya Mtanzania Josiah
Kibira mzaliwa wa Bukoba Kagera, Tanzania na Mmarekani, Mrs Josiah Kibira.
Mchanganyiko huo wa
tamaduni mbili kwa binti huyo ambaye ana kipaji cha utunzi na uimbaji, umemfanya
kujimarisha na kujijengea jina katika muziki kutokana na aina ya muziki na
manjonjo anayoyafanya katika mzuiki wake kupendwa.
Abela ni mzaliwa wa
Bukoba, Tanzania lakini kwa sasa anaishi Minneapolis, Marekani. Binti huyu
anasauti nzuri, ya kipekee na ya kuvutia jambo ambalo nyimbo zake nyingi
zimekuwa zikipendwa sana
Onyesho lake la kwanza
Binti huyu alilifanya kanisani na ndipo kipaji chache kilipojifunua machoni mwa
watu wengi na hivyo kuendelea kuimba katika matamasha mbalimbali shuleni na
matamasha maalumu.
Abela amekulia katika
mji wa Wayzata, Minnesota na alipendwa kutokana na kuwa na uwezo wa ajabu
katika kuimba kwaya na matamasha ya pamoja wakati akiwa katika masomo yake ya sekondari
na chuo.
Mwaka 2003 baba yake
mzazi Mr. Josiah Kibira alimshirikisha katika filamu yake aliyoiita Bongoland,
ambapo Abela alitunga wimbo wa kusindikiza filamu hiyo (soundtrack) jambo
lililomuongezea uwezo na umaarufu kwa mashabiki Amerika, Afrika na maeneo mengi
ulimwenguni.
Abela ambaye bado
binti kigoli anayejitambua amekuwa akiiimba na kujifua utumiaji wa sauti takriban
maisha yake yote lakini kwa sasa amejikita zaidi katika utunzi na utengenezaji
wa nyimbo za Hip Hop, Reggae na ni mzuri katika aina tofauti tofauti za muziki.
Abela hana shida juu
ya kufanya collabo na wasanii wa Kitanzania na Africa kwa ujumla kwa hiyo kama
unapenda kumshirikisha kazi ni kwako! Kwa sasa anatamba na video ya wimbo wake
alioutoa mwishoni mwa mwaka jana unaoitwa Ball & Chain.
Kabla ya hapo ametamba
na nyimbo nyingi zikiwemo Rolling Stone,
Someone like you na Hey Ya.
Imeandaliwa na Dotto Kahindi
Imeandaliwa na Dotto Kahindi
0 comments:
Post a Comment