PIGA KURA ILI TUPATE UZI MPYA WA TIMU YA TAIFA



Watanzania wanatakiwa kupigia kura jezi ya timu ya Taifa ya nyumbani na ugenini kupitia mtandao wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) wa www.tff.or.tz ambapo jezi hizo zimewekwa.

TFF ilipokea mapendekezo ya mwonekano mpya wa jezi ya timu ya Taifa kutoka kwa Watanzania 86. Jezi 11 za nyumbani, bukta nane za nyumbani, jezi nane za ugenini na bukta tano za ugenini ndizo zimepitishwa kwa ajili ya kupigiwa kura.

Mwisho wa kupiga kura ni Desemba 31 mwaka huu. Mpigaji kura anatakiwa kubonyeza kwenye jezi na bukta ambayo ameichagua. Anatakiwa kufanya hivyo kwa jezi ya nyumbani na jezi ya ugenini.

Tunawashukuru wote waliojitokeza kupendekeza mwonekano mpya wa jezi ya timu ya Taifa.


IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)


MUHIMU SANA: FAHAMU JUU YA KUCHANGIA DAMU KWA MAMA MJAMZITO (MASWALI NA MAJIBU) SOMA HAPA



Aina za damu
Aina ya damu (pia huitwa kikundi cha damu) ni uainishaji wa damu kwa kuzingatia kuwepo au kutokuwepo kwa dutu za antijeni za kurithiwa kwenye uso wa chembechembe nyekundu za damu (RBCs). Aina ya damu (Kikundi cha damu) inaamuliwa kwa sehemu, na antijeni za aina ya damu ya ABO zilizo kwenye chembechembe nyekundu za damu.
Aina za damu huathiriwa na huwakilisha michango kutoka kwa wazazi wote wawili. Jumla ya mifumo 30 ya aina ya damu ya binadamu (ikiwa ni pamoja na mifumo ya ABO & Rh) sasa inatambuliwa na Shirika la Kimataifa la Upaji wa Damu (ISBT).
Aina ya damu kamili ni seti kamili ya dutu 30 kwenye uso wa chembechembe nyekundu za damu na aina ya damu ya mtu ni mojawapo ya miungano iwezekanayo ya antijeni za aina ya damu. Katika aina hizo 30 za damu, zaidi ya antijeni 600 tofauti za aina ya damu zimepatikana, lakini nyingi ya hizi ni nadra sana au kwa kiasi kikubwa hupatikana katika makabila fulani.
Mfumo wa ABO ni mfumo muhimu zaidi wa aina ya damu katika 


kuongezewa damu kwa binadamu. Kingamwili kinza-A na kingamwili kinza-B zinazohusika kwa kawaida ni kingamwili za Immunoglobulini M, inayofupishwa IgM. Mfumo wa Rh ni mfumo wa pili muhimu zaidi wa aina ya damu katika kuongezewa damu kwa binadamu ukiwa na antijeni 50 kwa sasa.


Wanawake wengi wajawazito hubeba kijusi kilicho na aina ya damu tofauti na yao na mama huweza kutengeneza kingamwili dhidi ya chembechembe nyekundu za damu za kijusi. Wakati mwingine kingamwili hizi za mama zinaweza kuvuka kondo na kusababisha hemolosia ya chembechembe nyekundu za damu, ambayo inaweza kusababisha ugonjwa wa hemolitiki wa mtoto mchanga (HDN), ugonjwa wa hesabu ya chini ya damu ya kijusi.
Karibu kila mara, mtu ana aina moja ya damu maisha yake yote, lakini mara chache sana aina ya damu ya mtu hubadilika kwa sababu ya kuongezeka au ukandamizaji wa antijeni katika maambukizi, donda ndugu au ugonjwa kinga mwili nafsi.
Aina/Makundi ya damu na Upatanifu wa Chembechembe nyekundu za Damu
  1. Watu wenye damu ya aina ya AB wana antijeni zote mbili za A na B kwenye uso wa chembechembe zao nyekundu za damu na majimaji yao ya damu hayana kingamwili zozote dhidi ya antijeni A au B. Kwa hivyo, mtu mwenye damu ya aina ya AB anaweza kupokea damu aina yoyote (aina ya AB inapendekezwa) lakini anaweza kutoa damu kwa mwingine mwenye aina ya AB pekee.
  2. Watu wenye damu ya aina ya A wana antijeni ya A kwenye uso wa chembechembe zao nyekundu za damu na majimaji yao ya damu yana kingamwili za IgM dhidi ya antijeni ya B. Kwa hivyo, mtu mwenye damu ya aina ya ya A anaweza kupokea damu kutoka kwa watu wenye aina ya A au 0 pekee (aina ya A inapendekezwa) na anaweza kutoa damu kwa watu wengine wenye aina ya A au AB.
  3. Watu wenye damu ya aina ya B wana antijeni ya B kwenye uso wa chembechembe zao nyekundu za damu na majimaji yao ya damu yana kingamwili za IgM dhidi ya antijeni ya A. Kwa hivyo, mtu mwenye damu ya aina ya B anaweza kupokea damu kutoka kwa watu wenye aina ya B au O (aina ya B inapendekezwa) na wanaweza kutoa damu kwa watu wenye aina ya B au AB.
  4. Watu wenye damu ya aina ya O (au kikundi cha damu cha sifuri katika nchi kadhaa) hawana antijeni A au B kwenye uso wa chembechembe zao nyekundu za damu lakini majimaji yao ya damu yana kingamwili kinza-A na kingamwili kinza-B za IgM dhidi ya antijeni za aina ya damu za A na B. Kwa hivyo, mtu mwenye damu ya aina ya 0 anaweza tu kupokea damu kutoka kwa mtu mwenye aina ya 0, lakini anaweza kutoa damu kwa watu wa aina yoyote ya ABO (yaani kundi A, B, AB & O).
Masuala ya kuzingatia kabla ya kuchangia damu kwa mama mjamzito
Kabla ya Kuchangia damu
  1. Zingatia ulaji wa vyakula vyenye madini chuma kama nyama nyekundu (mfano nyama ya ng'ombe), samaki, maharage n.k
  2. Pata chakula bora chenye afya yaani mlo kamili. Epuka vyakula vyenye mafuta hasa vilivyokaangwa.
  3. Kunywa maji mengi angalau glasi 6 hadi 8.
  4. Pata usingizi mzuri wa usiku.
  5. Kumbuka kuwa na kitambulisho chako chochote.
Wakati wakuchangia damu
  1. Vaa nguo inayoweza kukunjwa hadi juu ya kiwiko.
  2. Muonyeshe mtoa damu mkono unaotaka utolewe damu, ikiwezekana muonyeshe na mshipa uliofanikisha kutolewa damu wakati uliopita kama umewahi kuchangia damu.
  3. Kuwa mtulivu wakati wa kutolewa damu ikiwezekana ongea na mchangiaji damu aliyekaribu yako au sikiliza muziki wa taratibu.
  4. Punde umalizapo kuchangia damu, tumia muda wako kufurahia vyakula na vinywaji laini vilivyoletwa na wahamasishaji wa kuchangia damu.
Baada ya kuchangia damu
  1. Kunywa maji mengi zaidi na jiepushe na pombe ndani ya masaa 24 yajayo.
  2. Ondoa bandeji/pamba iliyowekwa pale ulipotobolewa kuzuia damu isitoke baada ya saa 1 baada ya kuchangia damu.
  3. Sehemu iliyochomwa sindano kama bado inatoa damu, izibe kwa nguvu na pamba kavu kisha nyoosha mkono juu kwa dakika 5 hadi 10.
  4. Ili kuepuka maambukizi ya ngozi na muwasho osha kwa maji na sabuni sehemu ya mwili iliyotumika kutoa damu.
  5. Usifanye kazi ngumu yoyote kama kubeba vitu vizito ndani ya siku yote ambayo umetoa damu.
  6. Kama unasikia kizunguzungu na kuishiwa nguvu & pumzi baada ya kuchangia damu unapaswa kukaa chini au kulala hadi utakapojisikia vizuri.
  7. Kula vyakula vyenye protini kwa wingi baada ya kuchangia damu mfano nyama ya ng'ombe, kuku, kunde n.k
Mawali na majibu juu ya Uchangiaji damu
Inachukua muda gani kuchangia damu?
Hatua zote mpaka damu kuwa imetolewa inachukua kama saa moja na dakika 15. Muda mahususi kwa kutoa damu chupa moja ya damu ni dakika 8 hadi 10, ingawa muda hutofautiana kwa sababu tofauti kama hali ya afya ya mchangia damu na mahudhurio ya sehemu za kuchangia damu.
Wakati gani mjamzito hupungukiwa damu?
Upungufu wa damu wakati wa ujauzito unaweza kutokea katika mabidiliko ya kawaida ya ujauzito ambapo chembechembe nyekundu huongezeka kwa kiwango kidogo kuliko maji(Physiological hemodilution), hata hivyo mabadiliko haya yanaweza kurekebishwa kwa kutumia madini chuma na folic acid bila kuhitaji kuongezewa damu. Matatizo yanayoweza kusababisha upungufu mkubwa mpaka kuhitaji kuongezewa ni pamoja na lishe duni(isiyo na madini chuma na vitamin stahiki), maambukizi ya minyoo, malaria, kupasuka kwa mimba iliyotungwa nje ya mfuko wa uzazi (Ruptered Ectopic Pregnancy), kutoka/kutoa mimba, kutokwa damu ukeni kabla, wakati wa kujifungua na baada ya kujifungua.
Mama mjamzito huhitaji kuchangiwa damu wakati upi?
Mama mjamzito huhitaji kuchangiwa damu wakati wowote kabla hajapata matatizo yatakayopelekea kupungukiwa damu. Damu inaweza kuhifadhiwa na kusubiri hali ya dharula ikitokea.
Nini madhara ya mjamzito kupungukiwa damu?
Upungufu wa damu wa muda mrefu unaweza athiri maisha ya mama na mtoto aliyetumboni.Mama anaweza kujikuta moyo ukashindwa kufanya kazi vizuri na kupoteza maisha. Mtoto hataweza kukua vizuri na anaweza fia tumboni au akazaliwa akiwa na uzito mdogo sana.Endapo mjamzito atatokwa na damu nyingi sana ukeni kabla ya kujifungua au baada ya kujifungua anaweza kuishiwa nguvu kabisa, kuzimia au hata kupoteza maisha.
Nini hufanyika baada ya kuishiwa damu?
Mgonjwa hukaguliwa haraka na kujua chanzo cha tatizo lake na kuzuia utokaji wa damu zaidi, huku wakizuia asizimie/kupoteza fahamu kwa kumpatia huduma stahiki ikiwa ni pamoja  kurejesha kiwango cha maji yaliyopungua mwilini haraka sana kwa maji ya drip, wakati jitihada za kutafuta kumwongeza damu zinaendelea.
Wapi watakiwa kwenda kuchangia damu?
Nchini Tanzania, sehemu za kuchangia damu zimegawanyika kikanda kama ifuatavyo :-

(a) Kanda ya Mashariki; inayohudumia mikoa ya Dar es salaam, Morogoro, Dodoma & Pwani. Ofisi kuu za kanda zikiwa Mchikichini, Ilala, Dar es salaam. Simu ni 0715339282.
(b) Kanda ya Ziwa; inayohudumia mikoa ya Mwanza, Mara, Kagera & Shinyanga. Ofisi kuu za kanda zikiwa Mwanza karibu na Hospitali ya Bugando. Simu ni 0768479381.
(c) Kanda ya Magharibi; inayohudumia mikoa ya Tabora, Kigoma & Singida. Ofisi kuu za kanda zikiwa Tabora karibu na Hospitali ya Kitete. Simu ni 0785733606.
(d) Kanda ya Kusini; inayohudumia mikoa ya Lindi & Mtwara. Ofisi kuu za kanda zikiwa Mtwara karibu na Hospitali ya Ligula. Simu ni0786852051.
(e) Kanda ya Kaskazini; inayohudumia mikoa ya Kilimanjaro, Tanga, Arusha & Manyara. Ofisi kuu za kanda zikiwa Moshi, Kilimanjaro karibu na Hospitali ya KCMC. Simu ni 0716231406.
(f) Kanda ya nyanda za juu Kusini; inayohudumia mikoa ya Mbeya, Iringa & Songea. Ofisi kuu za kanda zikiwa Mbeya karibu na Hospitali ya Meta. Simu ni 0767502430.

Mawali na majibu zaidi juu ya Uchangiaji damu
Swali : Nitalipwa nikichangia damu?
Jibu : Hapana. Hakuna malipo baada ya kuchangia damu. Wachangiaji hutoa damu kwa kujitolea kwa hiari yao.
Swali : Je, ni salama kwa mjamzito kuchangiwa damu?
Jibu : Ni salama kwa kuwa vigezo vyote vya usalama huchukuliwa kwa uzito.
Swali : Je, ni kweli kuwa kila kundi la mchangia damu lazima liwe sawa na mjamzito anayechangiwa?
Jibu : Kwa kawaida damu ya mchangiaji hukusanywa bila kujali ni kundi gani, endapo mjamzito atahitaji kutiwa damu ndipo kundi la damu ya mchangiaji litatafutwa ili kuendana na kundi la mjamzito.
Swali : Kuna faida gani kuchangia damu?
Jibu : Kuokoa maisha, kufahamu kundi lako la damu, kufahamu hali yako ya maambukizi ya magonjwa kama UKIMWI, Kaswende na Mchochota wa aina B & C, pia ni uzalendo.
Swali : Kuna hasara gani anayopata mchangia damu tokana na kuchangia damu?
Jibu : Hakuna hasara anayopata mchangiaji damu kwa kuwa damu atakayochangia itatumika kuokoa maisha ya wenye uhitaji wa damu.
Swali : Je, damu huuzwa kwa wanaohitaji?
Jibu : Hapana, damu haiuzwi na hutolewa bure kwa anaehitaji
Swali : Ni kina nani watakaopata damu niliyochangia?
Jibu : Watu wenye upungufu wa damu hasa watoto, watu waliofanyiwa upasuaji mkubwa, wagonjwa wenye saratani, majeruhi wa ajari na kina mama wajawazito wenye matatizo ya uzazi kama kutokwa damu nyingi baada ya kujifungua.
Swali : Ni magonjwa gani yanaweza kusambazwa kwa njia ya damu?
Jibu : Magonjwa mengi husambazwa kwa njia ya damu kama UKIMWI, Kaswende & Mchochota wa aina B & C na bacteria.
Swali : Je, unaweza kupata maambukizi ya UKIMWI ukichangia damu?
Jibu : Hapana kabisa. Sindano na vifaa vingine vyenye ncha kali vinavyotumika ni safi & salama. Watumishi wa ukusanyaji damu wanafuata viwango vya usalama na kuzuia maambukizi kama walivyofundishwa.
Swali : Je, ni salama kuchangia damu?
Jibu : Ndiyo, ni salama kuchangia damu kwa kuwa kabla ya kuchangia damu mtu hukaguliwa na kuulizwa maswali kuona kama amekidhi vigezo vya kuchangia damu ikiwa ni pamoja na kuangaliwa wingi wa damu na kupimwa shinikizo la damu.
Swali : Ninaweza kuchangia damu ikiwa sijala?
Jibu : Ukichangia damu hujala unaongeza hatari ya kupata matatizo baada ya kuhangia damu, hivyo inashauriwa kula chakula chepesi ndani ya masaa 4 baada ya kuchangia damu.
Swali : Ni damu kiasi gani huchukuliwa kwa wakati mmoja?
Jibu : Ni kiasi cha Mililita 480 za damu ndio kiwango kinachokubaliwa kisheria.
Swali : Ninaweza kutoa damu kila baada ya muda gani?
Jibu : Unaruhusiwa kuchangia damu kila baada ya siku 52 ili kuhakikisha mwili umepata muda wa kutosha kurudisha chembechembe za damu zilizopotea baada ya kuchangia damu wakati uliopita.
Swali : Ninahitaji kula mlo maalumu baada ya kuchangia damu?
Jibu : Hapana, endelea na mlo wako wa kila siku pia unaweza kuhakikisha ni mlo kamili tu.
Swali : Itachukua muda gani kwa mwili kurudisha kiwango cha damu nilichokitoa?
Jibu : Sehemu ya maji (Plasma) ya damu huweza kuridi ndani ya masaa 24 wakati chembechembe za damu hurudi baada ya wiki mbili.
Swali : Je, damu yangu itapimwa magonjwa kama UKIMWI kabla sijatoa?
Jibu : Hapana, hutolazimika kupima UKIMWI kama hauko tayari kufanya hivyo.
Swali : Damu salama ni nini?
Jibu : Damu salama ni  ile imepimwa na kuonekana haina UKIMWI, Kaswende, Mchochota wa aina B & C wala vimelea vya bacteria.
Swali : Nitapata wapi majibu yangu ya vipimo nilivyofanya wakati wa uchangiaji damu?
Jibu : Utapata majibu katika ofisi za damu salama  zilizo karibu nawe au pale ulipochangia damu.
Swali : Nani anaruhusiwa kumchangia damu mama mjamzito?
Jibu : Mtu yoyote mwanamke au mwanaume anaweza kumchangia damu mama mjamzito ikiwa ana afya njema na anajisikia vizuri, umri kati ya miaka 18 hadi 65, uzito usiopungua kilo 50, wingi wa damu zaidi ya gramu 12 kwa desilita, kutokuwa na shinikizo la juu la damu na kwa mwanamke asiwe mjamzito au anayenyonyesha.

SOMA HAPA-NANI ANACHEZESHA NGOMA YA ESCROW NA IPTL?





Kwa muda sasa kumekuwapo na tuhuma zinazohusu "wizi" wa fedha za akaunti ya escrow iliyofunguliwa katika Benki Kuu ya Tanzania mwaka 2006. Akaunti hiyo ilifunguliwa kwa ajili ya kuhifadhi fedha zilizokuwa zikilipwa na Shirika la Umeme Tanzania {TANESCO} kwa kampuni ya kufua umeme ya IPTL. Chimbuko la akaunti hiyo ni mgogoro wa tozo hiyo kwamba iligubikwa na utata baada ya kudaiwa kwamba Tanesco ilikuwa ikitozwa fedha nyingi kuliko inavyostahili.
           
Tuhuma za huo "wizi" hata hivyo hazikuishia tu kwa wahusika wakuu yaani makampuni ya umeme, bali zimetiririshwa hadi kwa watu binafsi ambao kimsingi hawana uhusiano wowote na mgogoro huo wa malipo na wala kuhusika kwa njia yoyote na hicho kinachodaiwa kwamba ni uporaji wa fedha za akaunti hiyo ya Escrow. 

Akaunti Escrow ni akaunti ya amana ambayo inawekwa chini ya uangalizi wa mtu wa tatu ili huyo mwangalizi aikabidhi kwa mlengwa pale tu masharti kadhaa yatakapokuwa yamekamilishwa. Hivyo basi akaunti hiyo maalum ya amana ilifunguliwa na kuwekwa chini ya Benki Kuu kama wakala anayesubiria kutekelezwa kwa masharti maalumu ili aikabidhi kwa wenye kumiliki fedha hizo watakapomaliza tofauti zao.
          
Ni vizuri kuliangalia suala hili la akaunti maalum ya amana kwa namna ambayo itawafanya wale wenye kiu ya kutaka kujua ukweli kukidhi hamu yao. 

Fedha iliyokuwa ikiwekwa katika akaunti hiyo ni tozo ya uwezo wa mitambo ya kufua umeme ambayo kampuni ya IPTL ilikuwa ikiitoza Tanesco. Baada ya Mahakama ya Kimataifa ya Utatuzi wa Migogoro ya Uwekezaji (ICSID) kupunguza tozo ya IPTL kutoka USD 3.6million kila mwezi mpaka USD 2.6million kila mwezi baadaye TANESCO ilishauriwa vibaya na wanasheria kwamba tozo hiyo bado ni kubwa kuliko mkataba baina ya IPTL na TANESCO Mei 26, 1995 unavyo eleza.
          
Ubishani uliozuka kati ya mtoa huduma ya umeme yaani IPTL na mtumia huduma ya umeme yaani Tanesco ndio uliosababisha kufunguliwa kwa akaunti hiyo maalum ya amana yaani escrow account katika Benki Kuu ya Tanzania {BoT} kama njia salama ya kutunza fedha hizo hadi mgogoro utakapokuwa umetatuliwa. 

Ni muhimu kufanya hivyo ili kuhakikisha kwamba mtoa huduma yaani IPTL hasitishi kufua umeme na mtumiaji wa umeme yaani Tanesco naye hakosi umeme wa kuuza kwa walaji wake. Hiyo ni busara ya kibiashara. Fedha hizo zililipwa katika akaunti hiyo maalum kutokana na hati za madai au ankara kutoka kwa mtoa huduma na si vinginevyo.
          
Kitu kimoja kilichojitokeza wazi ni kwamba suala la akaunti hiyo maalum limekuwa likibeba sura mpya kila kukicha na la kusikitisha zaidi ni kwamba vyombo vya habari vilivyo vingi ama vimekuwa vikipotosha kwa makusudi au kwa kutokuelewa mada yenyewe ipasavyo. Vipo vyombo vya habari kwa mfano ambavyo vimedai kwamba "Benki ya Standard Chartered ndiyo mmiliki wa mitambo ya IPTL baada ya kupewa mamlaka hayo na mahakama - Deed of Assignment- inayoiruhusu kuchukua na kumiliki mali za IPTL kutokana na kushindwa kulipa mkopo.

Aidha kwa mujibu wa gazeti la Mawio la Alhamisi Novemba 20-26, 2014 mkataba huo uliipatia benki ya SCB haki za IPTL ndani ya mkataba wa kuuziana umeme (PPA) na kumiliki mtambo wa kuzalisha umeme wa IPTL.
          
Kwa mujibu wa gazeti hilo la Mawio Benki ya Standard Chartered inaidai Tanesco dola za Marekani 258.7 milioni kama deni linalotokana na gharama za umeme uliozalishwa na IPTL na dola za Marekani 138 milioni zinazotokana na mkopo pamoja na riba. Kwa mujibu wa uchambuzi wa Mawio madai hayo ni halali kwa mujibu wa sheria.
          
 Kwa mujibu wa gazeti hilo "nyaraka za serikali zinaonesha kuwa PAP iliamuriwa kulipa wadai wote wa IPTL lakini haikuilipa Benki ya Standard Charted ambayo inajitangaza kuwa ni moja ya wadai.
         
Ni vyema na busara kuanza uchambuzi huu kwa kufanya nukuu hiyo muhimu sana kutoka katika gazeti la kila wiki la Mawio kwa sababu inatusaidia kuonyesha waziwazi kwamba hiki kinachodaiwa kwamba ni kashfa ya fedha za Escrow kina sura nyingi sana kulingana na maslahi yanayolengwa kutetewa. 

Katika muktadha huu ni wazi kwamba anayetetewa hapa ni Benki ya Standard Chartered ambayo inadaiwa kwamba ndiyo yenye haki ya kulipwa fedha kutoka katika akaunti ya Escrow na kwa mantiki hiyo imeishitaki Serikali ya Tanzania katika Mahakama ya Uingereza.
          
Deni linalodaiwa kwamba Tanesco inadaiwa na Standard Chartered la dola za Marekani linatokana na gharama za umeme uliozalishwa na IPTL na nyingine ni mkopo na riba. Inashangaza kwamba Tanesco inawezaje kudaiwa na Benki ya Standard Chartered wakati aliyezalisha umeme ni IPTL? Abrakadabra hiyo ndiyo inayomfanya ye yote yule mwenye akili timamu kutambua kwamba kuna mchezo wa kiini macho unaochezwa na benki hiyo dhidi ya Tanzania.
         
Ni wazi kabisa kwamba benki hiyo inalazimisha kuwapo na mgogoro wa kuhusu akaunti ya Escrow kwa lengo moja tu nalo ni kuhakikisha kwamba wanapata nafasi ya kukwapua hizo fedha wanazodai kwamba sio halali kuchukuliwa na IPTL. Kwamba zikichukuliwa na Benki ya Standard Chartered ambayo haijazalisha umeme wala kuwa na ushahidi wowote wa kushiriki katika kuzalisha umeme ni halali kabisa na zikichukuliwa na IPTL ambayo imezalisha umeme na inayo mikataba ya kuuziana umeme na Tanesco si sahihi, ni wizi, ni ujambazi ni hila na kashfa. Hii inahitaji maelezo zaidi kushinda haya yanayotolewa hivi sasa.
          
Ukweli wa mambo ni kwamba mazungumzo kuhusu fedha za Escrow na hususan habari za kujaribu kuonyesha kwamba umiliki wake ni batili una lengo moja tu nalo ni kuandaa mazingira kwa ajili ya Benki ya Standard Chartered hatimaye kuzichukua fedha hizo kwa kutumia kigezo cha kwamba imemilikishwa mitambo ya IPTL na kwamba ndiyo iliyokuwa na haki ya kulipwa tozo ya uzalishaji umeme na si kampuni nyingine yoyote. Hivyo ndivyo kampuni hiyo inavyodai katika kesi iliyofungua dhidi ya Serikali ya Tanzania huko Uingereza.
          
Benki ya Standard Chartered inatumia mbinu mbalimbali ili kuhakikisha inafikia lengo lake la kukwapua fedha za kigeni si chini ya dola milioni 200 kutoka kwa serikali ya Tanzania. Moja ya njia inayotumia ni propaganda ambayo hupenyezwa katika vyombo vya habari kwa kutumia majukwaa mbalimbali. 

Moja ya njia zinazotumika ni kujaribu kuufanya umma uamini kwamba fedha zilizotoka katika ufungaji wa akaunti hiyo ya Escrow zimeibwa na kwamba wahusika katika huo wizi ni pamoja na viongozi kadhaa wa Serikali.
          
Kinachosikitisha zaidi ni kwamba kuhusishwa kwa watu hao kunafanyika bila hata ya kuwataka wajieleze kama wanaelewa kile wanachotuhumiwa nacho. Wafadhili wa propaganda hizo hawakubali kujitokeza hadharani moja kwa moja kwa kuhofia kuumbuliwa. Matukio huchukuliwa si kwa ujumla wake bali upande mmoja na kuyatangaza kwa namna ya kukidhi matakwa na matarajio yao tu.
          
Tumezoea kuambiwa kwamba wakati suala linapokuwa mahakamani kwa ajili ya kupatiwa ufumbuzi basi si sahihi kuendelea kulijadili kwenye vyombo vya habari kwani kwa kufanya hivyo ni sawa kabisa na kuingilia uhuru wa mahakama. Ni wazi kwamba hata suala linapokuwa katika uchunguzi au upelelezi uwe kwa kutumia tume maalum au makachero basi ni muhali kulizungumzia hadharani na kuwatuhumu na hata kuwahukumu watu kwa ujasiri usio na kikomo kwamba ni wezi au mafisadi au wakumbatiaji wa madhila hayo yote. Hili linafanyika kila siku kupitia vyombo vya habari na chimbuko lake ni baadhi ya wabunge na wanasiasa ambao hufanya hivyo huku wakitumia kila aina ya takwimu za kweli na za kughushi au kubuni tu kichwani.
         
Nini kinachowafanya au kuwapa jeuri hawa watu wanaowatuhumu na kuwahukumu wengine bila ya kujali kwamba hilo halitakiwi wala kupaswa kufanyika bila ya kupitia katika vyombo vya sheria ili kutoka fursa kwa wengine kujitetea? Swali hilo linastahili kujibiwa kwa umakini mkubwa ili kubaini kama kweli hao wanaodai kwamba wanapigania haki ya kiuchumi ya Watanzania ni kweli wanafanya hivyo kwa dhati ya moyo wao kabisa bila ya kuwa na nia nyingine iliyojificha ambayo hawathubutu kuiweka hadharani kwani kwa kufanya hivyo watageuka viroja. 

Pamoja na kwamba kuna kesi mahakamani dhidi ya Serikali ya Tanzania ni wazi kwamba ukiwauliza Standard Chartered kilichowapeleka mahakamani wanasema kwamba wanaionea nchi yetu huruma, Hata hivyo, kamwe hakuna atayekuambia kwamba amekuja hapa kwa ajili ya kujaribu bahati yake kama wanaweza kufanya mbinu wakatengeneza fedha ya bure. Ili kufanikisha malengo yao tuhuma hurushwa kwa yeyote na popote. Ili kufanikisha malengo hayo mtu yeyote yule aweza kuunganishwa katika lolote lile ili kufikia lengo.
          
Ni kwa utaratibu huo huo ndio tunashuhudia jinsi jitihada za Profesa Anna Tibaijuka za kuendeleza mtoto wa kike kielimu zinavyopakwa matope na kukejeliwa mno kwa sababu tu ameomba msaada mahali na akaupata. 

Tujiulize inakuwaje wanasiasa wetu wanathubutu kumhukumu Profesa Tibaijuka na kumuita kila aina ya majina machafu. Ametuhumiwa kwamba ni mwizi eti kwa sababu aliomba msaada kwa ajili ya shule ya Babro Johansson ambayo ni kwa madhumuni ya kuwasaidia watoto wa kike kupata elimu. 

Profesa Tibaijuka aliomba msaada kwa barua rasmi miaka kadhaa iliyopita na kampuni hiyo haikuweza kumsaidia mapema kutokana na ukata na ni hivi majuzi hali ilipokuwa njema ndipo ikatoa msaada huo.
         
La kustaajabisha ni kwamba msaada huo haukuwa ni siri na ulitolewa kwa uwazi mkubwa bila ya kificho. Sasa huo ujambazi wa Profesa Tibaijuka umetokea wapi? Kosa lake ni kupatiwa fedha alizoomba kwa ajili ya kuisaidia shule ambayo aliianzisha?
          
Tunajiuliza hapa, baada ya VIP kuuza hisa zake kwa PAP na kulipwa na PAP stahili yake, ilifanya kosa gani kutoa msaada kwa shule ya Babro Johansson?
          
Mahitaji na umuhimu wa elimu yanajulikana. Viongozi wanahimiza kila leo umuhimu wa Watanzania kubadilika kuchangia Maendeleo ya Elimu badala ya harusi na sherehe nyinginezo. Leo hii anatokea Mtanzania anaomba msaada wa kuendeleza elimu na anapatikana Mtanzania anakubali kuchangia vizuri maendeleo ya elimu, wawili hawa baadhi ya wanaojiita viongozi wa siasa tena wenye kutaka kuchukua madaraka ya juu kuiongoza nchi, wanalalamika na hata kutamani kutoa roho ya mtu! Watanzania tuzipime dhamira zao. Ni wadanganyifu wasio na uelewa halisi wa matatizo na vipaumbele vya taifa na hivyo kukosa dhamira thabiti ya kuyashughulikia. Wanasukumwa zaidi na tamaa zao binafsi. 
          
Kwa wanaong'ang'ania kudai damu za baadhi ya watu kutokana na hukumu ambayo wao wameipitisha baada ya kufanya kila kitu wao ikiwa ni pamoja na kutuhumu, kupeleleza, kufungua mashitaka, kusikiliza kesi na hatimaye kuhukumu na sasa kutaka kukaza hukumu kwa njia yoyote ile hakuna jambo zuri na jema kama kufanya kile wanachotaka wao yaani kukubali kwamba fedha zote katika akaunti maalum ya escrow ni za serikali na kwamba lazima zirudi serikalini. 

Hata hivyo, wakubwa hao hawataki kurudi nyuma na kujiuliza ni kwa njia gani fedha hizo zimeingia katika akaunti hiyo. Aidha, hawataki kujiuliza kwamba kama Tanesco ndio ilikuwa ikitumbukiza fedha katika akaunti hiyo, ilikuwa ikifanya hivyo kwa kutumia vigezo gani. Swali linguine la kujiuliza, je Serikali hutunza pesa zake kwenye Account zake Benki Kuu au kwenye Escrow Account?
         
Hawaoni mantiki ya kutulia na kujibu swali la msingi kwamba kama Tanesco ingelikuwa inatumbukiza fedha katika akaunti hiyo kwa ajili ya kugharamia tozo la uwezo wa mitambo kuzalisha umeme sasa inakuwaje fedha hizo zirudi tena Tanesco? Ni maswali ambayo wanaojiamini kwamba ukweli wanao wao tu hawataki kuyajibu hata kidogo kwani kwa kufanya hivyo watakuwa wanaumaliza utamu wa mchezo wao wa kuigiza. 

Fedha hizo zinatakiwa zirudi Tanesco ili Benki ya Standard Chartered izichukue kwa madai kwamba ndiye mmiliki halali wa IPTL na kwamba kuna deni kama ilivyoainishwa awali katika makala haya.
          
Kutokana na ufafanuzi huo hapo juu ni wazi basi kwamba Tanesco ilikuwa ikilipia gharama za huduma ambayo ilikuwa inaipata kutoka kwa IPTL. Hilo halina ubishi.
          
Lakini pia suala lingine ambalo sasa halina ubishi japo halisemwi makusudi kwa sababu za upotoshaji ni kwamba katika makampuni yote ambayo yanauzia umeme TANESCO, IPTL ndiyo kampuni pekee inayotoza kiwango kidogo cha malipo ya uwekezaji (capacity charges). Suala la kujiuliza hapa ni inawezekanaje IPTL ambayo inatoza kiwango kidogo cha capacity charges ionekane “kuiibia” Serikali kwa kulipwa halali yake wakati makampuni mengine yanatoza capacity charges kwa kiwango cha juu zaidi ya IPTL na hakuna malalamiko.
       Swali la kujiuliza ni kwamba ni kitu gani kinachowasukuma watuhumu kutafuta kila njia ya kuonyesha kwamba kuna hitilafu kubwa sana kwa namna ambavyo suala la akaunti hiyo lilivyohitimishwa?
         
Ukifuatilia kwa karibu na umakini jinsi ambavyo tuhuma zimekuwa zikitolewa ni kwamba kinacholengwa ni fedha zilizokuwa katika akaunti maalumu ambazo ni tozo ya uwezo wa ufuaji wa umeme. Fedha hizo zinagombewa na Benki ya Standard Chartered ambayo ina matawi yake hapa nchini. 

Benki hiyo inatumia kila njia kujaribu kuonesha kwamba fedha zilizokuwapo katika akaunti ya Escrow ni fedha ya Serikali. Kwa mantiki hiyo inachojaribu kufanya Benki hiyo ni kuonyesha kwamba fedha akaunti ya escrow si kwa ajili ya kulipia gharama za uwezo wa mitambo kufua umeme la hasha. Bali ni fedha za Tanesco na kamwe hakuna anayestahili kuzipunguza kwa njia yoyote ile.
          
Cha kushangaza, hata hivyo, ni kwamba benki hiyo, inayodai kuwa iliikopesha fedha IPTL, katika madai yake yaliyopo mahakamani, inadai kuwa yenyewe ndiyo ilistahili kupata fedha zilizokuwa kwenye escrow account! Swali hapa ni je, hiyo asasi ndiyo Serikali? Je, fedha zilizokuwa kwenye escrow account zinakuwa za Serikali na siyo IPTL kwa sababu benki hiyo  haijalipwa?
       
Jitihada za kutaka kuhalalisha kwamba fedha hizo ni mali ya Tanesco na kwamba haziwezi kumegwa hata kidogo zinafanywa na Benki ya Standard Chartered ambayo inataka kutengeneza mazingira ya kuchota fedha kutoka Tanesco kwa madai kwamba ndiyo inayostahili kuwa mlipwaji wa fedha hizo kutokana na deni ambalo kwa mujibu wa madai yao ndio walioikopesha IPTL fedha kwa ajili ya mradi huo wa umeme.
          
Mchezo ambao benki hiyo inafanya hapa nchini ni kuhakikisha kwamba vyombo vya habari vinaandika habari za kuigonganisha serikali na wananchi kwamba Serikali ni ya mafisadi na inayokumbatia ufisadi, na haina ubavu wowote wa kupambana na rushwa. Aidha, asasi hiyo imevirubuni baadhi ya vyombo vya habari kuandika habari kwamba Mahakama za Tanzania haziaminiki na zinakumbatia ufisadi na kwamba zimekubuhu kwa rushwa.
          
Cha kushangaza, tuhuma hizi za rushwa kwa Mahakama za Tanzania zinakuja muda mfupi tu baada ya benki ya Standard Chartered kuiambia mahakama New York, nchini Marekani iliposhitakiwa na VIP kuwa Mahakama za Tanzania ndizo zenye uwezo wa kusikiliza na kutatua migogoro ya IPTL.
          
Mchezo ambao Standard Chartered Bank inaufanya ni kutumia vyombo vya habari kutoa habari zisizo za kweli na za upotoshi ili kuwachochea watu dhidi ya Serikali yao kutokana na nini kinaendelea ndani ya IPTL.  Mambo mengi yamesemwa na kuandikwa kuhusiana na Mahakama na watendaji wa Serikali kula rushwa.  Madhumuni ya kufanya hivyo ni kutaka kuonyesha kwamba nchini Tanzania haki haiwezi kutendeka.
         
Madai hayo yote, yanatokea wakati Standard Chartered Bank imefungua kesi London, kwa kisingizio kwamba Mahakama za Tanzania haziwezi kutenda haki  
          
Kwa vipi Standard Chartered Bank inatoa madai kulipwa dola za kimarekani 208 milioni kutoka TANESCO (katika kesi ilivyofunguliwa Mahakama ya usuluhishi (ICSID)) kwa mkopo wa dola milioni 84 kwa IPTL, wakati Serikali ya Tanzania na TANESCO tayari walikwishalipa takribani dola 200 milioni kwa IPTL kufikia mwaka 2006.  Kiasi hicho kingelitosha kulipia mkopo uliokuwa umechukuliwa na kulipa gawiwo kwa VIP na MECHMAR.  Mpaka mwaka 2013 VIP ilikuwa haijalipwa hata senti moja kwa jina lolote.
         
Kampuni ya Mechmar ilitumia fedha zilizodaiwa na IPTL kutoka Serikali ya Tanzania na TANESCO kwa kujilipa yenyewe na Kampuni ya Wartsila madeni hewa (kwa makubaliano na benki ya Danaharta na baadaye Standard Chartered Bank (Hong Kong) Ltd.
         

Standard Chartered Bank (Hong Kong) Ltd inajaribu kutekeleza mpango haramu dhidi ya IPTL kwa kutumia dhamana ya Serikali ya Tanzania na hivyo Serikali ina sababu za kutaka Standard Chartered Bank ithibitishe kama inaidai IPTL.

          Mpaka sasa ukweli ni kwamba Standard Chartered Bank imekwepa kutoa ushahidi kuwa ina madai yoyote dhidi ya IPTL na kwa sababu hiyo na zingine VIP na IPTL/PAP wameifungulia kesi za madai ya fidia na hasara ya TZS 787bilioni na USD 3bilioni katika Mahakama Kuu ya Tanzania. (Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com)

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

MAMIA WAMZIKA LEONARD MUTENSA MJINI BUKOBA.‏



MAMIA ya Watu wamejitokeza kwa wingi kumzika mpendwa wao Leonard Mutensa siku ya Jumamosi Nov 22, Nyumbani kwake Kyakailabwa nje kidogo na Mji wa Bukoba. 
Mwili wa Marehemu Leonard Mutensa  ukiwaumebebwa tayari kwa mazishi huko nyumbani kwake Kyakailabwa nje kidogo na Mji wa Bukoba. Picha na Faustine Ruta wa www.bukobasports.comJeneza lililokuwa na mwili wa Marehemu Leonard Mutensa likiwa limebebwa na Vijana Maalum walioteuliwa kwa kazi hiyo wakiwa wabeba Jeneza lenye mwili wa marehemu Mutensa kuutoa ndani ya nyumba yake na kuuleta nje katika Ukumbi, Tayari kwa kuombewa Misa na Mazishi yake. Kikosi kazi Maalum wakiwa wamebeba Jeneza lenye mwili wa Marehemu Mtensa Leonard kutoka ndani ya Nyumba kuelekea Ukumbini. Vijana Smart, watanashati, wakiwa wamevaa suti 'suit' Mbele ni Jamal Kalumuna(jamco) na Rahym Kabyemela wakiongoza wenzao njia.Misa ikiendelea ikiongozwa na Mchungaji KasimbaziWaombolezaji wakiendelea na MisaWaimbaji wa kwayaMc Mutakwa  akiendelea na kazi yake kwa makini.Kwaya wakati wa MisaMwalimu Bube (Leo leo) rafiki wa karibu sana na Marehemu Mutensa  akiteta jambo Jamal Karumuna(kushoto) akiwa na rafiki yake Rahim, Wote ni Moja Vijana wa kikosi maalum cha kubeba Jeneza la Marehemu Mutensa rafiki yao, Ambaye alikuwa mpiganaji mwenzao. Pongezi kubwa kwenu kwa juhudi zenu binafsi kuweza kuweka mambo sawa katika kifo cha Mwenzenu.Mr. Bube wakati anatoa historia fupi ya rafiki yake kipenzi Marehemu MutensaMwalimu Bube akiwa na Mtoto wa kwanza wa Marehemu Leonard Mutensa akimtambulisha mbele ya waombolezaji wakati wa Mazishi ya baba yake Mzazi. Mwalimu Bube akimtambulisha mtoto wa pili wa marehemu rafiki yake MutensaMtoto wa tatu nae (kulia)Mtoto wa mwisho.Mtoto wa pili kuzaliwa akitoa neno fupi kuhusu marehemu Baba yao.Watoto wa marehemu Mutensa wakiwa mbeleDj Max akitoa neno kwa niaba ya wafanyakazi wake marehemu katika Ukumbi wa Lina's Night Club, Ukumbi aliokuwa akiendesha kama Meneja marehemu Leonard Mutensa.Mama Mwainunu nae akitoa neno kwa niamba ya kikundi chao cha "Wanaumoja Kagera" ambao pia Marehemu Mutesa alikuwa akijumuika nao katika shughuli mbalimbali hapa Mjini Bukoba.Mzee ambaye pia alikuwa karibu na marehemu Leonard Mutensa nae alitoa neno.Mtoto wa kwanza wa marehemu Leonard Mutensa akitoa neno Katikati ni Mc Jerry akiteta jambo na baadhi ya Ndugu jamaa wa karibu na Familia ya Marehemu Mutensa aliyefariki hivi karibuni na kuzikwa nyumbani kwake Kyakailabwa nje kidogo na Mji wa Bukoba.Rafiki yake na Marehemu kutoka GeitaMjane wa marehemu Mutensa, Mama Linah WaombolezajiViongozi mbalimbali walijitokeza katika mazishi hayo kumuaga Marehemu Leonard Mutensa. Ni Mzee Rugaibura, Mzee Frank na Mzee Mchuruza.Watu kutoka Nje na Mkoa wa Kagera walijumuika katika Mazishi ya Marehemu L. MutensaWilly O. Ruta kutoka Ofisi ya Kiroyera Tours(kushoto) nae alijumuika na kulia ni Sharobaro wa Kihaya kutoka Jijini Mwanza akiwawakilisha na wenzao Kutoka Kundi la Futuhi.Dada mchekeshaji wa Futuhi nae alikuwepo nyumbaniBaadhi ya wafiwa wakiombeleza kifo cha ndugu yaoKaka yake na Marehemu David akisikitika kuondokewa na mdogo wake..ni Machungu mazitoDj Slay na Steve nao walijumuika katika mazishi hayo.Dada kutoka Mwanza, kulia CettyMc Mutakwa akipewa neno kwa karibu na Sharobaro wa Kihaya kutoka jijini Mwanza.Mkurugenzi wa Kitengo cha Ulinzi na Usalama cha Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Wilfred Rwakatare(kulia) nae alikuwepo katika Mazishi hayo.Mkurugenzi wa shirika lisilo la Kiserikali la COSAD lililopo Marekani,Tanzania Bw Smart Baitan nae alikuwepo.Peter Mugisha ndugu na Marehemu(kulia) nae alitoka Jijini Dar es salaam kuja kumzika Kaka Yake Marehemu Leonard Mutensa.Marafiki wa marehemu Mutensa  wakipita mbele ya jeneza lililokuwa na mwili wa marehemu kutoa heshima za mwisho.Mzee Mchuruza akimpa heshima yake ya mwisho Tutakukumbuka daima...Mr. Ben Kataruga na Mr Justuce Rugaibura (picha ya chini) wakiwa wametoka Jijini Dar es Salaam kushiriki shughuli ya mazishi ya rafiki yao marehemu Mutensa.Wakiendelea kutoa heshima zao.Willy O. Rutta nae alitoa heshia yake kwa mpambanaji mwenzake aliyemtoka Marehemu MutensaSharobaro wa Kihaya kutoka Futuhi Jijini Mwanza nae alikuja kumuaga rafiki yake. Picha na Faustine Ruta wa www.bukobasports.comSuper Self Mkude hapa aliongoza Wanabukoba Veteran kutoa heshima zao za mwisho kwa Mwanabukoba Veteran mwenzao. Picha na Faustine Ruta wa www.bukobasports.comKaka Mkuu Ernest Nyambo akitoa heshima za mwisho kwa rafiki yake kaka yake MutensaBukoba Veteran Queens nao walikuwepo hapo katika Mazishi ya Mwenzao aliyewatangulia mbele ya haki.Chama Umande Chama nae alitoa heshima zakeWanafamilia wakitoa heshima zao za mwisho.Mjane wa marehemu Mutensa, Mama Linah alishindwa kujizuia mbele ya Jeneza lililokuwa limebeba mwili wa Marehemu mumewe na kuamua kuchua muda. Picha na Faustine Ruta wa www.bukobasports.comNguvu ziliwaishia kabisa...mpaka wakasaidiwa kutoka eneo lilipokuwa jeneza la MarehemuNi majonzi matupu!Mama wa Marehemu, Mama Constansia kwa machungu nae akienda kutoa salamu zake za mwisho kwa mwanae akiongozwwa na kiongozi Ernest Nyambo.
Mamia ya Watu walijitokeza kwa wingi Wafanyakazi wake nao walitoa heshima zao za mwisho kwa aliyekuwa bosi waoMwenyekiti wa Kamati ya mazishi Bw.Self Super Mkude akitoa nenoKaka Mkuu Ernest Nyambo kutoka jijini Dar es Salaam nae alikuwepo katika kumuaga rafiki yake mkubwa Marehemu Mutensa leo Kyakailabwa Bukoba. Na hapa alikuwa akitoa neno, Picha na Faustine Ruta wa www.bukobasports.com Wakisikiliza kwa makini neno kutoka kwa Ernest NyamboRafiki zake walikuwepo kumuaga Dada Anitha akisikitika kuondokewa na baba Yake Mdogo.Mr. Benny (kulia) nae alikuwepo katika mazshi hayo. Picha na Faustine Ruta wa www.bukobasports.comWatoto wa Marehemu L. Mutensa wakiusindikiza mwili wa Baba yao kwenye Nyumba yake ya kupuzika.Wakiupeleka Kaburini.Mtoto wa marehemu akiwa ameshika picha ya marehemu baba yake.Wakiwa kwenye majonzi mazitoTayari Mwili wa Marehemu kuwekwa katika nyumba yake ya milele.
wakiteremusha mwili wa Marehemu kaburini nje ya Nyumba yake Kyakailabwa Rafiki yake Bube akishindwa kuamini macho yake kuondokewa na rafiki yake pacha hata siku aliyofariki usiku huo walikuwa wametoka kuonana jioni hiyo!Wakiweka udongo kaburini, Ni Peter Mugisha na Kaka David wote ni Ndugu wa Marehemu MuteMwanae wa pili nae aliweka udongo kumzika Baba yakeMjane wa Marehemu Mutensa akiweka shada la maua katika kaburi la marehemu Mume wakeMama Mzazi wa Marehemu nae akiweka Shada la mauaTutakukumbuka Daima....Picha ya pamoja ilipiigwa..Picha na Faustine Ruta wa www.bukobasports.com

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kagera Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa