WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina ameiagiza Ofi si ya
Mwanasheria Mkuu wa serikali wilayani Misenyi, kukamilisha taratibu za
uhamiaji na mahakama, ili ng’ombe 6,648 waliokamatwa kwa kuingia nchini
kinyemeleza waweze kupigwa mnada.
Ng’ombe hao walikamatwa hivi karibuni katika wilaya hiyo wakitokea
Uganda na kukamatwa. Mpina alisema uvamizi wa kundi kubwa kama hilo la
wanyama linaweza kusabisha madhara katika mazingira kama vile mmomonyoko
wa ardhi, uharibifu wa vyanzo vya maji, kumaliza malisho ya mifugo
iliyoko nchini, kusababisha migogoro ya mara kwa mara kwa wakulima na
wafugaji na hata kuleta maambukizi ya magonjwa ya wanyama.
Mpina alisema suala hilo haliingiliani na ushirika wa Afrika
Mashariki kwani ushirika huo upo kisheria, hivyo wavamizi wanaoingiza
mifugo kinyemela nchini kutoka nchi jirani ni wahalifu kama wahalifu
wengine. “Kwa hiyo naangiza ng’ombe hawa 6,648 waliokamatwa hatua
ziendelee na ambao hawajakamatwa wakamatwe na wataifishwe na serikali.”
alisisitiza. Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Misenyi, Denis Mwila
alisema utaratibu wa kutathmini ng’ombe katika wilaya yake bado
unaendelea na taratibu za kisheria zinafuatwa.
CHANZO HABARI LEO
0 comments:
Post a Comment