Kamishna wa Mamlaka ya mapato nchini(TRA)Charles Kichere(wa pili kutoka kushoto)akiongea na waandishi wa habari kwenye ofisi za mamlaka hiyo Mkoa wa Kagera(hawapo pichani)juu ya ziara yake ya kikazi katika Wilaya zote za Mkoa wa Kagera
Mkurugenzi wa huduma ya elimu kwa mlipa kodi Richard Kayombo(wa kwanza kushoto)akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani)
Na Editha karlo wa blog ya jamii,Kagera
MAMLAKA
ya mapato(TRA)itaendelea kudhibiti na kupambana na wafanyabiashara
wasio waaminifu wanaofanya biashara za magendo katika vituo mbalimbali
na maeneo ya mipakani.
Kamishina
mkuu wa mamlaka ya mapato nchini (TRA) ,Charles Kichere ameyasema hayo
kwenye ofisi za mamlaka hiyo Mkoani Kagera wakati akiongea na waandishi
wa habari juu ya ziara yake ya kikazi aliyoifanya katika Wilaya zote za
Mkoani humo.
Alisema
TRA itazidi kupambana na kuwabana wafanyabiashara wote wanaopitisha
mizigo yao kwa njia ambazo siyo za halali na kufanya serekali ikose
mapato.Aliwataka
wafanyabiashara wanaotumia mpaka wa mtukula kupitisha mizigo yao
kuingia nchini Tanzania na kwenda nchi ya jirani ya Uganda kupitisha
mizigo yao kwani huduma sasa hivi kituoni hapo zinapatika kwa haraka.
"Sasa
hivi tutaziba mianya yote inayosababisha upotevu wa mapato hususani
katika mipaka yetu,nina waomba wafanyabiashara wote watumie njia zilizo
halali kupitisha mizigo yao watakapo kamatwa hatua kali za kisheria
zitachukuliwa dhidi yao ikiwa ni pamoja na kutaifishwa mizigo yao na
kufikishwa katika vyombo vya dola"alisema.Alisema mamlaka haitavumilia vitendo vyovyote vya rushwa bali wataendelea kuwashughulikia mafisadi bila ya uogo wowote.Alisema
tetemeko la ardhi lililotokea Mkoani Kagera miaka ya hivi karibuni
liliathiri ukusanyaji wa kodi za majengo kwani nyumba nyingi
ziliathiriwa na tetemeko.
"Nimeona
wakazi wa Kagera ni walipa kodi wazuri,maeneo niliyotembelea nimeona
wanatumia mashine za kieletroniki za kodi(EFD's)wanapouuza au kutoa
huduma"alisema Kamishna.Alisema mamlaka haitawavumilia
wafanyabiashara wanaoikosesha mapato serekali kwa kuuza au kutoa huduma
bila ya risti za EFD's kwa makusudi.Mkurugenzi
wa huduma ya elimu kwa mlipa kodi Richard Kayombo amewataka wananchi
kuwa mabalozi wa ukusanyaji wa mapato kwa kutimiza wajibu wao wa kudai
risti wanaponunua bidhaa au kupatiwa huduma mbalimbali.
0 comments:
Post a Comment