JPM AMUAGIZA NCHEMBA KUSITISHA KUWAPA URAIA WAKIMBIZI WA BURUNDI

Rais John Magufuli amemtaka Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mwigulu Nchemba kusimamisha kuwapa uraia raia wa Burundi kuanzia sasa.
Akizungumza Alhamisi Julai 20 wakati wa ziara yake mkoani Kagera, akiwa ameambatana na Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza alimtaka asiwape uraia wanaotoka nchi nyingine.
“Rais amezungumza hapa kwa upole, Rais mwenyewe ana hofu ya Mungu, wazazi wake waliuawa, lakini anataka kushirikiana na Warundi wote kwa nini mnataka kuondoka kwenu,” amesema.
Awali, Rais Nkurunziza amezungumza na wananchi hao na kuwataka raia wa Burundi warudi nchini mwao kwani kwa sasa amani imerejea.
Kadhalika, Waziri Nchemba amesema katika kipindi cha 2016/17, Tanzania imewapa uraia wakimbizi wa Burundi 1060.
Pia, Waziri Nchemba amesema kati ya wakimbizi 247,000 waliopo nchini, 5,000 wameomba kurudi kwao.

Chanzo Mwananchi

JPM AAGIZA SH200 MILIONI ZA MRADI WA MAJI JESHINI ZITUMIKE KWA WANANCHI

 Rais John Magufuli ameagiza Sh200 milioni zilizopangwa kutumika katika mradi wa maji katika kambi ya jeshi zianze kuimarisha miradi ya maji kwa wananchi kwanza.

Akizungumza jana, Alhamisi Julai 20 katika ziara yake akiwa ameambatana na Rais wa Burundi, Pierre Nkurunzinza, Magufuli aliema amebaini kuwa pampu za maji wilayani Ngara zimeharibika kwa zaidi ya wiki tatu na kuwa wilaya hiyo ina uhaba mkubwa wa maji.
Alimuita, Mhandisi wa Maji ajieleze ni kwa nini pampu hizo hazifanyi kazi na baada ya kumsikiliza ndipo alipofanya uamuzi huo.
Akifafanua kuhusu hali ya maji, mhandisi huyo alisema awali visima vya maji wilayani hapo vilikuwa vikihudumia watu 400 lakini kwa sasa wilaya hiyo ina watu zaidi ya 240,000 na hivyo visima hivyo havitoshelezi.
“Tulikuwa tuna idadi ndogo ya watu sasa hivi imeongezeka, lakini tangu pampu iharibike, tumetengeneza mbili na kisima kimoja hakina pampu,” alisema.
Baada ya mhandisi huyo kufafanua hayo ndipo Rais alimuita Mkurugenzi wa Halmashauri kueleza mipango yake, ndipo Mkurugenzi huyo aliposema mradi wa maji wa Sh200 milioni utaanza kwanza katika kambi ya jeshi.
Kauli hiyo ndiyo iliyomfanya Rais Magufuli kushauri fedha hizo zitumike katika miradi ya maji katika makazi ya wananchi kwanza.
“Wanajeshi wapo 200 na wananchi wapo zaidi ya 20,000 sasa si bora waanze wananchi kwanza,” alisema.

Chanzo Mwananchi

IGP SIRRO AANZA ZIARA YA KIKAZI MKOANI KAGERA


 Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro (kushoto) akizungumza na Kamanda wa Polisi mkoa wa Kagera Kamishna Msaidizi Muandamizi wa Polisi (SACP) Augusine Ollomi, muda mfupi alipowasili. IGP Sirro yupo mkoani humo kwa ziara ya kikazi yenye lengo la kujitambulisha na kuzungumza na askari pamoja na kujua chamgamoto wanazokutana nazo wakati wakitekeleza majukumu yao
 Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro, akizungumza na baadhi ya askari wa kikosi maalum kinachofanya doria za kupambana na wahalifu aliokutana nao katika eneo la Nyakanazi mkoani Kagera, IGP Sirro yupo mkoani humo kwa ziara ya kikazi yenye lengo la kujitambulisha na kuzungumza na askari pamoja na kujua chamgamoto wanazokutananazo wakitekeleza majukumu yao.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (Mb), akitafakari jambo na Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro walipokutana katika viwanja vya Lemela wilayani Ngara mkoa wa Kagera, wakisubiri kuwasili kwa Rais Dkt. John Magufuli na Rais Pierre Nkurunziza wa Jamhuri ya Burundi. Picha na Demetrius Njimbwi – Jeshi la Polisi.

RAIS NKURUNZIZA AFANYA ZIARA RASMI YA KISERIKALI NCHINI TANZANIA.

Rais wa Burundi Mhe. Pierre Nkurunziza akiwasalimia wananchi wa Mji wa Ngara kwenye Mkutano wa Hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Posta Mjini Ngara 20 Julai 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Rais wa Burundi Mhe. Pierre Nkurunziza mara baada ya Rais wa Burundi kuwahutubia wananchi wa Mji wa Ngara kwenye Mkutano wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Posta Mjini Ngara 20 Julai 2017.
Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia mamia ya wananchi wa Mji wa Ngara kwenye Mkutano wa Hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Posta Mjini Ngara Mkoani Kagera 20 Julai 2017.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpokea Rais wa Burundi Mhe. Pierre Nkurunziza mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Lemela mjini Ngara Mkoani Kagera Julai 2017
Rais wa Jamuhuri ya Burundi Mhe. Pierre Nkurunziza akiwapungia wananchi alipowasili katika viwanja vya Lemela mjini Ngara Mkoani Kagera Julai 20,2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Rais wa Burundi Mhe. Pierre Nkurunziza wakiwa wamesimama wakipokea salamu za heshima kutoka kwa majeshi ya ulinzi na usalama.
Rais wa Burundi Mhe. Pierre Nkurunziza akikagua graride la lililoandaliwa na jeshi la ulinzi la Tanzania JWTZ katika viwanja vya Lemela mjini Ngara Mkoani Kagera Julai 20,2017
Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mgeni wake Rais wa Burundi Mhe. Pierre Nkurunziza mara baada ya Kumpokea katika Uwanja vya Lemela mjini Ngara Mkoani Kagera 20 Julai 2017.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Rais wa Burundi Mhe. Pierre Nkurunziza akiwasalimia wananchi wa Mji wa Ngara kwenye uwanja wa Lemela mjini Ngara Mkoani Kagera 20 Julai 2017.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiteta Jambo na Rais wa Burundi Mhe. Pierre Nkurunziza Mara baada ya kumpokea katika Mji wa Ngara kwenye uwanja vya Lemela mjini Ngara Mkoani Kagera 20 Julai 2017.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha Rais wa Jamuhuri ya Burundi Mhe. Pierre Nkurunziza kwa maongezi mjini Ngara Mkoani Kagera 20 Julai 2017.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na ujumbe wake katika mazungumzo maalum ya kiserikali na Rais wa Burundi Mhe. Pierre Nkurunziza na ujumbe wake Mjini Ngara Mkoani Kagera 20 Julai 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Burundi Mhe. Pierre Nkurunziza pamoja na mama Janeth Magufuli katika Maongezi.
Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na mgeni wake Rais wa Burundi Mhe. Pierre Nkurunziza wakiwapungia mikono wananchimwa mji wa ngara wakati wakiwasili katika uwanja wa posta mjini Ngara kwa ajili ya mkutano wa hadhara.
Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na mgeni wake Rais wa Burundi Mhe. Pierre Nkurunziza wakiwapungia mikono wananchi wa mji wa Ngara waliohudhulia katika uwanja wa posta mjini Ngara kwa ajili ya Mkutano wa hadhara.
Umati wa ananchi wa mji wa Ngara waliohudhulia katika uwanja wa posta mjini Ngara kusikiliza Hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika uwanja wa posta mjini Ngara 20 Julai 2017.
Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na mgeni wake Rais wa Burundi Mhe. Pierre Nkurunziza katika uwanja wa Lemela Mjini Ngara Mkoani Kagera 20 Julai 2017 baada ya kumaliza ziara yake Rasmi ya kiserikali Nchini. PICHA NA IKULU

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUTOKA IKULU






RAIS DKT MAGUFULI AMPOKEA RAIS NKURUNZIZA WILAYANI NGARA MKOANI KAGERA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt John Pombe magufuli akiwa ameambatana na mgeni wake  Rais wa Burundi,Pierre Nkurunziza aliewasili mapema leo katka uwanja wa mpira wa Lemela mjini Ngara,Rais Dkt Magufuli amempokea Rais Nkurunziza akiwa kwenye ziara yake kikazi mkoani Kagera.

Aidha Rais Nkurunziza baada ya kupokelewa na Mwenyeji wake Rais Dkt Magufuli,alipata wasaa wa kuwasalimia wananchi mbalimbali waliofika kumpokea katika uwanja huo wa mpira mjini Ngara.

JPM: SINA UTANI MATUMIZI YA EFDS

Imeandikwa na Mwandishi Wetu, Biharamulo
Rais John Magufuli akiondoa kitambaa kwenye jiwe la msingi, kuashiria ufunguzi wa Barabara ya Biharamulo-Kagoma-Lusaunga ya kiwango cha lami yenye urefu wa Kilometa 154 wilayani Biharamulo, mkoa wa Kagera wakati akiwa kwenye ziara ya siku mbili mkoani humo jana. (Picha na Ikulu).
RAIS John Magufuli ametoa siku 14 kwa wamiliki wa vituo vya mafuta nchini, kuhakikisha kwamba wanafunga mashine za kielektroniki za kutolea risiti (EFDs) na kuonya watakaoshindwa kufanya hivyo watahatarisha biashara zao.
Ametoa agizo hilo jana alipohutubia mkutano wa hadhara mjini Biharamulo mkoani Kagera wakati wa kuzindua barabara ya Kagoma – Biharamulo – Lusahunga yenye urefu wa kilometa 154, ambayo itasaidia kuifungua Tanzania na nchi za jirani katika ukanda huo wa Magharibi.
Katika maagizo yake, pia amewataka wakuu wa mikoa na wilaya kulisimamia jambo hilo kwa karibu. “Kwa muda mrefu baadhi ya wafanyabiashara wanaoendesha vituo vya mafuta, wamekuwa wakikwepa kodi.
Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kuhakikisha kwamba Watanzania wanapata huduma muhimu ikiwemo afya na elimu,” alisema Rais Magufuli. Aliongeza, “Hatuwezi kufanikiwa katika hayo kama baadhi ya wafanyabiashara wanakwepa kulipa kodi na kuacha mzigo mkubwa kwa watumishi wa umma na wakulima kwa miaka yote.”
Dk Magufuli ameiagiza Wizara ya Fedha na Mipango na Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, kuhakikisha vituo vyote vya mafuta nchini vinatumia mashine hizo. Alisisitiza kuwa wamiliki watakaokiuka agizo hilo, vituo vyao vifungwe na kufutiwa leseni.
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) tangu wiki iliyopita, imeendesha kampeni ya kufungia vituo vya mafuta visivyotumia EFDs baada ya kuwapo makubaliano na wafanyabiashara hao tangu Oktoba mwaka jana kufunga mashine hizo.
Juzi, TRA ilieleza kuwa vituo 710 vya mafuta vilifungwa nchi nzima tangu ianze kazi ya kuvikagua vituo hivyo kuona kama vinatumia EFDS. Aidha, vituo 469 kati ya hivyo vimefunguliwa baada ya kukidhi vigezo vilivyowekwa na TRA na vituo vingine 241 havijafunguliwa kutokana na kushindwa kukidhi masharti ya TRA.
Kwa mujibu wa Rais Magufuli, serikali imeongeza bajeti ya kununulia dawa muhimu kutoka Sh bilioni 31 hadi Sh bilioni 250 na kuongeza kuwa lengo ni kuwafanya Watanzania wengi kupata huduma ya afya kwa gharama nafuu.
Alifafanua kwamba serikali imejenga barabara ya Kagoma-Biharamulo- Lusahunga kwa gharama ya Sh bilioni 190, ambazo zote zimelipwa kutokana na mapato ya ndani na kusema hayo ni mafanikio makubwa.
Alisema Tanzania ni miongoni mwa nchi tano za Afrika, zilizomudu kujenga barabara kwa kutumia mapato yao wenyewe. Akasisitiza kwamba ni muhimu miundombinu hiyo ikatunzwa. Rais aliwakumbusha Watanzania kuendelea kutunza amani na utulivu uliopo.
Aliwataka wananchi kujifunza kutoka kwa baadhi ya nchi jirani, ambako maelfu ya watu waliuawa kwenye migogoro ya wenyewe kwa wenyewe na hivyo wasiruhusu mambo kama hayo kutokea nchini.
Alieleza kuwa serikali imeondoa kodi na ushuru kwenye mazao ili kuwawezesha watu wa kipato cha chini kuwa huru. Alisema kwamba kodi hizo ndizo zilizowashawishi watu kujiingiza kwenye biashara ya magendo na nchi jirani ya mazao ikiwemo kahawa.
“Mkulima mwenye tani 20 za mazao ya chakula asikodi lori la tani 20 badala yake akodi tu lori la tani moja na hatatozwa kodi,” alisema Rais Magufuli. Aidha, aliwahakikishia wakazi wa Biharamulo kwamba tatizo la maji wanalokabiliana nalo, litatatuliwa hivi karibuni na kumwagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Maji Bukoba Mjini na Mamlaka ya Usafi (BUWASA), Allen Marwa kuhakikisha mkandarasi aliyepewa kazi kufunga kuunganisha mabomba kabla ya Julai 30, mwaka huu.
Aliwaagiza pia Mkuu wa Mkoa, Salum Kijuu na mkuu wa wilaya ya Biharamulo, kuhakikisha mifugo inayozurura kwenye hifadhi za misitu ukiwemo Burigi wanakamatwa. Rais Magufuli aliwataka Watanzania kuwa na idadi ndogo ya mifugo, ambayo itawaingizia fedha na kuongeza kuwa Tanzania bado haijanufaika vya kutosha kutoka sekta ya mifugo.
Pia aliwahakikishia wachimbaji wadogo wa Biharamulo kwamba serikali itawapatia maeneo ya kuchimba dhahabu, inayopatikana katika eneo hilo. Rais Magufuli yuko kwenye ziara ya siku mbili mkoani Kagera na leo atakuwa wilayani Ngara, ambako pia atahutubia mkutano wa hadhara.
CHANZO HABARI LEO

RAIS DKT. JOHN POMBE MAGUFULI ATEMBELEA SHULE YA SEMINARI KATOKE ALIYOSOMA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli Akimuonyesha Mkewe Mama Janeth Magufuli kitanda alichokuwa akitumia kulala wakati akisoma kidato cha tatu katika shule ya seminari katoke iliyopo Biharamulo Mkoani Kagera, ambapo amemweleza mkewe kuwa alivunja hilo dirisha na mpaka leo halikutengenezwa ambapo leo hii amekabidhi kiasi cha shilingi milioni moja ili kukarabati dirisha na madirisha mengine ya shule hiyo, Mh Rais yupo mkoani Kagera kwa ziara ya siku mbili mkoani humo, 19 julai 2017.
Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, akiingia kwenye  Bweni alilokuwa akilala wakati akisoma kidato cha tatu katika shule ya seminari katoke iliyopo Biharamulo Mkoani Kagera wakati akiwa kwenye ziara ya siku mbili mkoani humo, 19 Julai 2017
Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli, akiongea na Wanafunzi Shule ya Seminari Katoke iliyopo Biharamulo Mkoani Kagera wakati akiwa kwenye ziara ya siku mbili mkoani humo, 19 Julai 2017.
Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli, akiwa katika picha ya pamoja na Wanafunzi Shule ya Seminari Katoke iliyopo Biharamulo Mkoani Kagera wakati akiwa kwenye ziara ya siku mbili mkoani humo, 19 julai 2017
Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli, akisalimiana na kuwaaga Wanafunzi Shule ya Seminari Katoke iliyopo Biharamulo Mkoani Kagera wakati akiwa kwenye ziara ya siku mbili mkoani humo, 19 julai 2017

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUTOKA IKULU





RAIS DKT MAGUFULI AFUNGUA BARABARA YA KAGOMA-BIHARAMULO-LUSAHUNGA YENYE UREFU WA KILOMETA 154





 Rais Dkt John pombe Magufuli mapema leo amefungua barabara ya Kagoma-Biharamulo-Lusahunga yenye urefu wa Kilometa 154. Barabara hii ni muhimu kwa uchumi wa mikoa ya kanda ziwa, kanda ya kati na kanda ya magharibi. Inaunganisha mikoa ya Kagera, Geita, Kigoma, Mwanza, Shinyanga na nchi jirani za Burundi, Uganda na Rwanda
 Rais Dkt John pombe Magufuli akiwasalimia baadhi ya akina Mama waliofika kushuhudia hafla fupi ya ufunguzi wa barabara ya Kagoma-Biharamulo-Lusahunga yenye urefu wa Kilometa 154. Barabara hii ni muhimu kwa uchumi wa mikoa ya kanda ziwa, kanda ya kati na kanda ya magharibi. Inaunganisha mikoa ya Kagera, Geita, Kigoma, Mwanza, Shinyanga na nchi jirani za Burundi, Uganda na Rwanda.




KAGERA SUGAR WAWEKA KAMBI DAR KWA MAANDALIZI YA MSIMU MPYA



Kikosi cha timu ya Kagera Sugar kimeweka kambi katika Jiji la Dar es salaam kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa ligi Kuu Vodacom 2017/18 inayotarajiwa kuanza mwishoni mwa mwezi Agosti.

Kocha mkuu wa timu hiyo Mecky Mexime amejumuisha kikosi cha zamani na wale wa watakaoungana na wenzao katika kuimarisha timu hiyo kwa ajili ya msimu mpya.

Katika sura mpya za kikosi cha Kagera Sugar ni Juma Nyoso aliyekuwa anatumikia adhabu ya kufungiwa miaka miwili kutokujihusisha na soka, Omary Daga na Abdala Mguhi kutoka African Lyon iliyoshuka daraja.





 Kikosi cha Timu ya Kagera Sugar wakiwa katika mazoezi ya maandalizi ya msimu ujao wa ligi Kuu Vodacom 2017/18 .
Dakatri wa timu ya Kagera Sugar akiganga mchezaji aliyeumia katika  mazoezi ya maandalizi ya msimu ujao wa ligi Kuu Vodacom 2017/18 .
Kikosi cha Timu ya Kagera Sugar wakiwa katika mazoezi ya maandalizi ya msimu ujao wa ligi Kuu Vodacom 2017/18 .

Kocha wa timu ya Kagera Sugar Mecky Mexime akitoa maelekezo kwa wachezaji wake wanaoendelea na mazoezi katika Uwanja wa Karume Jijini Dar es salaam.Picha na Globu ya Jamii

BARABARA YA UYOVU-BWANGA-BIHARAMULO KUKAMILIKA MWISHONI MWA MWAKA



Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa Mkandarasi wa Kampuni ya Sinohydro Corporation Ltd anayejenga barabara ya Uyovu-Bwanga KM 45 kwa kiwango cha lami, mkoani Geita. 
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa barabara ya Bwanga-Biharamulo yenye urefu wa KM 67, mkoani Geita. 
Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), Mkoa wa Geita Eng. Harun Senkuku akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa, kuhusu maendeleo yaliyofikiwa ya mradi wa ujenzi wa barabara ya Uyovu-Bwanga yenye urefu wa KM 45, mkoani Geita. 

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa amesema mradi wa ujenzi wa barabara ya Uyovu-Bwanga-Biharamulo yenye urefu wa KM 112 inayojengwa na mkandarasi wa Kampuni ya Synohydro Corporation itakamilika mwishoni mwa mwaka huu.
Prof. Mbarawa amezungumza hayo mkoani Kagera, wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa barabara hiyo na kumtaka mkandarasi aongeze kasi ili barabara hiyo iweze kukamilika kwa wakati.

“Hakikisheni mnaongeza kasi ya ujenzi ili muweze kukamilisha ujenzi huu kwa wakati iwezekanavyo”, amesema Waziri Prof. Mbarawa.Amemsisitiza mkandarasi kuzingatia viwango vilivyopo katika mkataba kwani mwisho wa siku lazima watanzania wapate barabara inayokidhi mahitaji yao na ubora wake.

Amewapongeza wasimamizi wa barabara hiyo ambao ni kutoka kwa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) kupitia kitengo chake maalum cha wahandisi washauri wazawa (TECU), kwa kuhakikisha wanamsimamia mkandarasi M/S Sinohydro Corporation kwa ukaribu.

Kwa upande wake, Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), mkoa wa Geita Eng. Harun Senkuku amemueleza Waziri Prof. Mbarawa kuwa changamoto ya fidia iliyokuwa inawakabili sasa imemalizika na kiasi cha shilingi milioni 700 zimetumika kukamilisha ulipaji fidia kwa wakazi wote.
 
Amemhakikishia Waziri kuwa TANROADS itaendelea kumsimamia mkandarasi huyo ili kuhakikisha thamani halisi ya fedha ya Serikali inapatikana.Mradi wa ujenzi wa barabara ya Uyovu-Bwanga-Biharamulo KM 112 umehusisha ujenzi wa barabara ya Uyovu-Bwanga yenye urefu wa KM 45 na barabara ya Bwanga-Biharamulo yenye urefu wa KM 67.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

FAHAMU KWA UNDANI HISTORIA YA MKOA WA KAGERA (SEHEMU YA KWANZA)


Kabla ya Uhuru na hadi kufikia mwaka 1961, eneo la sasa la Mkoa wa Kagera, lilikuwa ni moja ya maeneo yaliounda jimbo lililoitwa “Lake Province”. Jimbo hili lilijumuisha Wilaya za Bukoba, Musoma, Shinyanga na Tabora. Baada ya uhuru mwaka 1962 mkoa ulibadilishwa jina na kuitwa ‘West Lake Region’ (Ziwa Magharibi) na kujumuisha Wilaya 4 za Ngara, Biharamuro, Karagwe na Bukoba.

Uchumi wa wenyeji wa mkoa wa Kagera ulijikita katika mashamba ya migomba na kahawa. Chakula chao kikuu ni ndizi katika aina zake mbalimbali. Katika mashamba yao hulima mazao mengine kufuatana na msimu. Mazao hayo ni pamoja na maharage, mihogo, mahindi na mboga.

Baada ya kuja kwa wazungu waliongeza ulimaji wa kahawa kama zao la biashara lililowasaidia kujiongezea kipato. Wakazi wa asili ya Kagera ni wabantu na wengi wao wanaasili ya Bunyoro. Wanaongea lugha sawa na ile ya Wanyoro, Wanyankole, Watoro na Wakiga. Busubi na Bugufi wana lugha na desturi sawa na Watusi, Wahutu na Waha. Lakini makabila hayo ni ya Wabantu wa Ziwa (Interlacustrine Bantu) na yanafanana mila na desturi. 
Itaendelea endelea kufuatilia hapa...

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kagera Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa