WANANCHI mkoani Kagera, wametakiwa kujiunga na Shirika la Taifa la
Hifadhi ya Jamii (NSSF), ili waweze kupata mafao bora ikiwemo bima ya
afya bure kwa familia.
Wito huo ulitolewa mjini hapa jana na Meneja wa Mafao ya Matibabu wa
NSSF, Dk. Ally Mtulia, alipokuwa akisoma taarifa ya utakelezaji mkoani
hapa katika siku ya zoezi la upimaji wa afya bure kwa Kanda ya Ziwa.
Dk. Mtula alisema shirika hilo litaendelea kuwahimiza wananchi
kujiunga nalo, kwani kuna mafao mengi wanaweza kunufaika nayo na pia
wanaweza kujipatia mikopo hasa wajasiriamali wadogo, ushirika wa
bodaboda, wakulima kupitia vyama vya akiba na mikopo.
Alisema mbali na kujiunga na NSSF, amewaomba wananchi hao
kujijengea tabia ya kupima afya zao, ili kujiwekea mfumo bora wa maisha
ikiwa ni pamoja na kuepuka magonjwa sugu.
Zoezi la kila mwananchi kupima afya lilianzia mkoani Mara, Shinyanga, Geita ambako watu wengi walijitokeza kupima afya zao.
Chanzo:Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment