WANANCHI wa Wilaya ya Muleba, mkoani Kagera, wametakiwa kutumia
elimu wanayopewa na maofisa uvuvi kupambana na kutokomeza uvuvi haramu,
ili kuokoa kuangamia kwa Ziwa Victoria.
Kauli hiyo ilitolewa mjini hapa jana na Ofisa Uvuvi Wilaya ya Muleba, Siymphorian Ngaiza, alipozungumza na Tanzania Daima ofisini kwake, kutokana na kuongezeka kwa vitendo vya uvuvi haramu katika ziwa hilo.
“Jamii ina wajibu mkubwa wa kudhibiti vitendo vya uvuvi haramu kwa
vile wao ndio wanaoishi na wavuvi wenye tabia kama hizo,” alisema.
Alisema kuwa aina ya uvuvi haramu ulioshamiri katika Wilaya hiyo ni
ule wa kutumia nyavu zisizoruhusiwa ambazo ziko chini ya kiwango na
zinazonasa samaki wadogo.
Aliwataka wavuvi kuzingatia sheria zilizopo ikiwa ni pamoja na
kulipia ushuru wa usafirishaji wa samaki ili kuepuka usumbufu
unaojitokeza wa kukamatwa.
Pia aliwashauri wakazi wa visiwani humo kuanzisha ulinzi shirikishi,
ili kuwabaini wageni wanaojihusisha na vitendo vya wizi wa injini na
zana nyingine za uvuvi na kuwafikisha katika kituo cha polisi.
Chanzo:Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment