WAKAZI wa Wilaya ya Muleba mkoani Kagera, wametakiwa kuchukua
tahadhari dhidi ya ugonjwa wa malaria ili kupunguza idadi ya vifo vya
watoto na wajawazito.
Kauli hiyo imetolewa jana na Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya, Leontine
Rwamulaza wakati akihojiwa na Tanzania Daima ofisini kwake
kuhusiana na mlipuko wa magonjwa wilayani kwake.
Rwamulaza alisema wilaya hiyo inaongoza kwa ugonjwa huo katika Mkoa
wa Kagera, na hivyo akawataka wananchi kuzingatia sheria na masharti
ambayo wanakuwa wanapewa na wataalamu wanazunguka katika vijiji.
Alisema wamechukua hatua za kupambana na ugonjwa huo kwa kuanzisha
utaratibu wa kutembelea vijiji kupima kila mtu na ambae anabainika kuwa
na ugonjwa huo hupewa dawa ikiwa ni pamoja na kutakiwa kuweka
mazingira safi ili kuondoa mazalia ya mbu.
“Wilaya yetu ni kati ya wilaya tisa hapa nchini zinazoongoza kwa
ugonjwa huu, na hii inatokana na kuwa na mito inayoaminika kuwa na mbu
wengi na ambayo pia wananchi wanaishi karibu nayo,” alisema.
Chanzo:Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment