KAUSTA WAOMBA KUUNGWA MKONO SHULE ZA KATA

UMOJA wa wanafunzi wa vyuo vikuu Tanzania kutoka mkoani Kagera (Kausta), umewaomba wadau wa sekta mbalimbali kujitokeza kuwaunga mkono ili waweze kwenda kujitolea katika shule za kata.
Ombi hilo lilitolewa hivi karibuni na Mwenyekiti wa Kausta Mkoa wa Kagera, David Willbard, wakati alipokuwa akisoma taarifa katika kikao kilichowahusisha viongozi wa kada mbalimbali kwenye Ukumbi wa Mkuu wa Mkoa mjini Bukoba.
Willbard alisema kuwa wameamua kuwaita viongozi hao ili waweze kujadili kwa pamoja ufundishaji na namna bora ya kuanzisha mfuko shirikishi kusaidia wanafunzi wa umoja huo watakaokwenda kujitolea katika shule hizo pamoja na kutafuta suluhu ya kudumu juu ya suala la taaluma katika Mkoa wa Kagera ambao unaonekana kuwa na changamoto kubwa kwa kizazi hiki.
Alisema vyuo vikuu husaidiana baina ya wanafunzi wenyewe katika kutatua changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo wakiwa vyuoni na kuangalia namna bora ya kuinua maendeleo ya Mkoa wa Kagera katika nyanja mbalimbali za kitamaduni, kijamii, kiuchumi na hata kisiasa.
Hata hivyo, alisema kuwa wameamua kwenda kujitolea katika shule za kata, kutokana na kuziona zimekuwa zikifanya vibaya katika mitihani ya kidato cha nne, hivyo kutokana na utafiti uliofanywa na Kausta mwaka 2012, waliona kiwango cha elimu katika mkoa huo ni tofauti na miaka ya70 na 80.
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Kanali mstaafu Fabiani Massawe, alisema kuwa uongozi wa mkoa umepokea suala hilo na watawaunga mkono ili kuona kama ufaulu katika shule za kata utaongezeka.
Pia, amewataka wanafunzi wanaohitimu vyuo vikuu kuachana na tabia ya kukaa nyumbani wakisubiri matokeo, badala yake wajitolee katika shule kama hizo ili kujijengea uelewa zaidi.
Chanzo;Tanzania Daima

MWALIMU ADAIWA KUMUUA MWALIMU MWENZAKE KAGERA

Mwalimu wa Shule ya Msingi Kaiho, Kijiji cha Rwigembe, mkoani Kagera, Tumaini Samson (42) anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kumuua mwalimu mwenzake, Samson Mwenda (26) kutokana na kumchoma kwa kisu kifuani na mgongoni.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Henry Mwaibambe alisema jana kwamba mtuhumiwa anashikiliwa kwa ajili ya kufikishwa mahakamani.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Rwigembe, Fidel Kamugisha alisema marehemu ambaye ni mwenyeji wa Singida aliuawa baada ya kutokea mzozo na mwenzake walipofika nyumbani wakitokea kwenye moja ya baa kijiji hapo.
“Walimu hawa walikuwa marafiki jinsi walivyoishi na hakuna aliyedhani kama wangezozana,” alisema Kamugisha.
Alisema baada ya kutokea tukio hilo, mwalimu Samson alijisalimisha kwa majirani kutaka kuomba msaada ili kumfikisha mwenzake Hospitali ya Ndolage lakini alifariki wakati juhudi za kuokoa maisha yake zikiendelea.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kaiho, Costantine Augustine alisema wakati wa uhai wake, Mwalimu Mwenda alikuwa akitimiza wajibu wake na kwamba, hakuwa na ugomvi na mtu hivyo tukio hilo limewashangaza.
Kuhusu uhusiano wa walimu hao, Augustine alisema licha ya kuishi nyumba moja na kutembelea mazingira ya kijiji, walikuwa wakizozana baada ya kulewa na hatimaye kusameheana.
Chanzo;Mwananchi

WAGOMA KUCHANGIA MIRADI YA MAENDELEO

 
Zaidi ya kaya 600 zenye watu takribani 4,000 kwenye kijiji cha Mpago, kata ya Kaniha, wilayani Biharamulo, wamegoma kuchangia miradi ya maendeleo kutokana na serikali kushindwa kutatua mgogoro wa ardhi kati ya kijiji hicho na Hifadhi ya Taifa ya Nyantakara.
Uamuzi huo ulifikiwa na wananchi hao baada ya Wakala wa Huduma za Misitu nchini (TFS) kuwataka kuondoka kwenye kijiji hicho kwa madai kwamba kimejengwa ndani ya hifadhi kinyume cha sheria za uhifadhi misitu na wanyama. 

Mbali na kuondolewa, pia wananchi hao wametakiwa kutoendeleza shughuli zozote za kibinadamu katika maeneo hayo.

Akizungumzia mgogoro huo wakati akiwasilisha taarifa ya maendeleo ya kata yake kwenye kikao cha madiwani wa Biharamulo, Diwani wa kata hiyo (CCM), Mashauri Paschal, alisema licha ya mgogoro huo kufika kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda. lakini bado haujatatuliwa na kuwafanya wananchi hao kuishi kama wakimbizi.

Alisema shughuli ya ujenzi wa sekondari kwenye kata yake umekuwa ukisuasua kutokana na wananchi wa kijiji cha Mpago kugoma kuchangia maendeleo.

Alisema mpaka sasa wananchi hao hawajui hatma ya maisha yao kutokana na mgogoro huo uliodumu takribani miaka mitatu wakizuiwa kuendelea na shughuli za kilimo na kwamba kuwaomba michango ni sawa na kuwakejeli.

Diwani wa kata ya Bisibo (Chadema), Josephat Kayamba, alisema hali ni tete kwenye kata yake kufuatia kaya 340 zenye watu takribani 2,040 kutakiwa kuondoka kwenye ardhi yao kwa kipindi kisichozidi siku saba kutokana na kudaiwa kuvamia eneo la Hifadhi ya Wanyama ya Burigi, wilayani humo.

Mbunge wa Jimbo la Biharamulo (Chadema), Antony Mbassa, amewataka wananchi kuepuka kununua ardhi yenye migogoro na kwamba wanapolipia ni vyema wakapewa stakabadhi za serikali ili kuepuka fedha zao kuliwa na baadhi ya viongozi wasio waadilifu.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo, Nassib Mmbagga, alisema serikali inaendelea kutafuta ufumbuzi wa migogoro hiyo, ikiwa ni pamoja na kuwasiliana na viongozi wa Hifadhi za Burigi, Nyantakara na Biharamulo, wakati wakiendelea kusubiri majibu ya Waziri Mkuu kuhusiana na migogoro hiyo.

Aidha aliwataka wananchi wa maeneo hayo kuendelea na shughuli zao za kilimo lakini wajiepushe kuongeza maeneo ambayo awali walikuwa hawayatumii.
 
CHANZO: NIPASHE

MAGAZETI YA LEO




















Ikiwa unatukio Lolote au Habari yoyote usisite kututumia kupitia Barua Pepe blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba yetu +255765056399

Tathmini ya ajali za barabarani kuanzia January mpaka June 2014 hii hapa

.
ajali
Kamanda wa Polisi Kikosi cha usalama Barabarani Dcp Mohameed Mpinga katoa tathmini ya ajali za Barabarani kuanzia Mwezi Januaary mpaka June ikiwa n i kipindi cha nusu mwaka na hivi ndivyo hali ilivyo.
mpinga
  TATHIMINI YA MATUKIO YA AJALI ZA
 BARABARAN JAN-JUNE 2013/2014


Takwimu zinaonyesha kuwa juhudi zetu zimefanikiwa kwa kupunguza ajali na majeruhi, ingawa kuna ongezeko la watu waliofarika katika ajali kwa Jan – June 2014.
S/N0
JAN-JUNE 2013JAN –JUNE 2014ONG/PUNG (%)
1IDADI YA AJALI11,3118,405-          2,906     (26%)
2VIFO1,7391,743                 4   (0.2%)
3MAJERUHI9,8897,523-          2,366     (24%)
 MIKOA ILIYOONGOZA KWA AJALI ZA BARABARANI KIPINDI JAN-JUNE 2014:-BOFYA HAPO KUSOMA

i)        Kinondoni   – idadi ya ajali      2,140 (25.5%)
ii)      Ilala              - idadi ya ajali – 1,561 (18.6%)
iii)    Temeke      - idadi ya ajali – 1,351 (16.1%)
iv)    Morogoro     –  idadi ya ajali – 514 (6.1%)
v)      Kilimanjaro – idadi ya ajali – 332 (4%)
Kwa mkoa wa DSM peke yake ni ajali 5,052 ( 60.2%)
MIKOA ILIYOONGOZA KATIKA KUPUNGUZA IDADI
YA AJALI ZA BARABARANI KIPINDI JAN-JUNE 2013/2014

MKOAJan-June 2013Jan-June 2014Punguzo

Kinondoni30592140     919 (30%)

Pwani738303     435 (59%)

Arusha563164     399 (71%)
4Kilimanjaro697332     365 (52%)
5Morogoro631514     117 (19%)
    TAKWIMU ZA MAKUNDI YALIYOATHIRIKA
NA AJALI ZA BARABARANI KIPINDI JAN-JUNE 2013/2014.

     JAN-JUNE 2013JAN- JUNE 2014     TOFAUTI
KUNDIVIFOMAJERUHIVIFOMAJERUHIVIFOMAJERUHI
MADEREVA124725117527-7-198
ABIRIA4764,1125293,13553-977
W/PIKIPIKI3592,4603581,928-1-532
W/BAISKELI202560177304-25-256
W/MIGUU5501,9265481,603-2-323
W/MIKOKOTENI281061426-14-80
JUMLA1,7399,8891,7437,5234-2,366
AJALI ZA PIKIPIKI- JAN-JUNE 2013/2014.
 Takwimu zinaonyesha kuwa tumeweza kupunguza ajali, vifo na majeruhi katika ajali za Pikipiki kwa kipindi cha Jan-June 2013 ikilinganishwa na Jan- June 2014.
Jan-June       2013Jan-June 2014ONG/PUNG
IDADI YA PIKIPIKIZILIZOHUSIKA3,7203,170-          550 (15%)
IDADI YA AJALI30162402-          614 (20%)
VIFO457423-          34 (7%)
MAJERUHI29632301-          662 (22%)
MAO

MWEKEZAJI ADAIWA KUPORA ARDHI HEKARI 3,700

 
BAADHI ya wananchi wa Kijiji cha Bihata, Kata ya Kyebitembe Wilaya ya Muleba mkoani Kagera, wamedai kuporwa ardhi yao ipatayo hekari 3,700 na mwekezaji, Diolex Joseph.
Pia wananchi hao wanalalamikia vitendo vya mwekezaji huyo kuwapiga na kuwajeruhi wazee wa kijiji hicho.
Wakizungumza na gazeti hili jana, walidai kuwa wamekuwa wakiuza ardhi kwa kulazimishwa na mwekezaji huyo.
Akizungumza kwa niaba ya wenzake, Samweli Kakura, alisema kuwa wamekuwa wakipigwa viboko pamoja na kutishiwa maisha kwa madai kwamba hawana sehemu ya kushitaki kwa sababu mwekezaji huyo anawahonga viongozi.
Alisema kutoka na hali hiyo, mwekezaji huyo amekuwa akipora ardhi ya kijiji pamoja na sehemu za wananchi kibabe pasipo kuguswa na uongozi.
Mwenyekiti wa kijiji hicho, Mussa Abdallah, alisema tatizo hilo la mwekezaji huyo kutumia ubabe kupora ardhi limekuwepo kwa kipindi kirefu ambapo hununua hekari kama saba na baadaye hujiongezea nyingine pasipo kumshirikisha kiongozi yeyote wa kijiji.
“Mwekezaji huyo alijimilikisha ardhi ya kijiji pamoja na baadhi ya ardhi za wananchi na anaposhitakiwa katika uongozi wowote, amekuwa akitoa rushwa na kesi kushindwa kusikilizwa.
“Anapita kila sehemu akijigamba na kusema kuwa hakuna mtu wa kumweza kutokana kwamba ana fedha nyingi,” alisema mwenyekiti huyo na kuongeza:
“Baada ya kumiliki ardhi bila kufuata sheria, aliweka mabango ya kuwazuia wananchi wasipite maeneo hayo. Kila anayepita hufanyiwa vitendo vya kikatili ikiwemo kupigwa viboko.”
Mussa aliongeza kuwa pamoja na kujimilikisha ardhi hiyo, pia amevamia hifadhi ya Burigi na kuharibu mazingira kwa kukata miti na kuchana mbao na kukata mkaa kisha kutengeneza mitumbwi inayotumika katika uvuvi haramu ndani ya Ziwa Burigi.
Alisema kuwa walishapeleka malalamiko hayo katika ofisi za kata, lakini hadi sasa hakuna hatua iliyochukuliwa dhidi yake, badala yake viongozi wanamsikiliza zaidi mtuhumiwa.
“Hata Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Muleba alifikishiwa taarifa hizo, alifika hapa kijijini na kumwagiza mwanasheria wa ardhi kufuatilia suala hili, lakini hakuna kilichofanyika,” alisema.
Alipotafutwa Joseph, alikana kupora ardhi hiyo akidai kuwa alinunua kwa wananchi kwa kutumia uwezo wake wa kifedha, na kwamba anakiri kuharibu mazingira ya Burigi, lakini yuko na watu wengine.
Mbunge wa Muleba Kusini, Prof. Anna Tibaijuka ambaye pia ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, alisema kuwa wananchi ndio wenye ridhaa ya kutoa ardhi katika kijiji bila kuzidisha hekari 50 ili mradi zifuatwe taratibu za kupitishwa na mkutano mkuu wa kijiji
Chanzo:Tanzania Daima

MAGAZETI YA LEO













Ikiwa unatukio Lolote au Habari yoyote usisite kututumia kupitia Barua Pepe blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba yetu +255765056399

WAFANYABIASHARA WATAKA UMOJA EA

Wafanyabiashara wataka umoja EABAADHI ya wafanyabiashara walioshiriki Maonyesho ya Sabasaba katika Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera kutoka nchini Kenya, wameitaka Jumuiya ya Afrika ya Mashariki (EA) kuondoa vikwazo mipakani kwa nia ya kuendeleza fursa za masoko na maendeleo.
Mmoja wa wafanyabiashara hao, Elizabert Ogake, ameliambia Tanzania Daima Jumapili kuwa hupata usumbufu mpakani wanaposafisha bidhaa zao na kutozwa fedha nyingi kinyume na sheria.
Alibainisha kuwa hupata misukosuko ya kutozwa ushuru wa bidhaa kutoka Idara ya Uhamiaji ya Uganda.
Alisema uwepo wa Maonyesho ya Sabasaba yanayofanyika kila mwaka, husaidia kukutanisha wafanyabiashara wa nchi hizo ambao hupeana mbinu za kukuza uchumi wa nchi zao.
Mkurugenzi wa Shirika la Kagera Agricultural Industrial Development & Promotion (KAIDEP), Philemon Kamazima, waliodhamini maonyesho hayo, alisema kulikuwa na mwitikio mzuri mwaka huu tofauti na miaka mingine.
Alisema maonyesho ya mwaka huu yalikuwa na washiriki 255  kutoka ndani na nje ya nchi ambapo wengi wao wametoka katika makampuni na taasisi mbalimbali za uzalishaji mali kutoka nchi za Uganda, Kenya na Rwanda.
Chanzo;Tanzania Daima 

RC ASITISHA LIKIZO ZA WAKUU WA WILAYA

MKUU wa Mkoa wa Kagera, Kanali Mstaafu Fabian MassaweMKUU wa Mkoa wa Kagera, Kanali Mstaafu Fabian Massawe, amesitisha likizo zote kwa Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri hadi ujenzi wa majengo ya maabara utakapokamilika.
Mbali na kusitisha kwa likizo hizo, Massawe ametishia kuwawajibisha viongozi watakaoshindwa kutimiza na kukamilisha ujenzi wa maabara katika shule zote za kata za mkoa huo kwa muda uliopangwa.
Kanali Massawe alitoa agizo hilo jana alipozungumza na waandishi wa habari ofisini kmwake, kuhusiana na mkoa kukabiliwa na upungufu wa majengo 457 ya maabara za sayansi kwa wanafunzi wa shule za sekondari za Kata.
Alisema ujenzi wa majengo hayo lazima ukamilike kabla ya Desemba, mwaka huu kama alivyoagiza Rais Jakaya Kikwete.
Alisema kukamilika kwa majengo hayo kutaleta manufaa kwa watoto walioko shuleni sasa na vizazi vijavyo.
Alisema mkoa huo pia bado unakabiliwa na upungufu wa walimu wa masomo ya sayansi, na kwamba wale waliopo ni wa masomo ya sayansi sanaa wanaozalisha wanasiasa wengi kuliko wanasayansi.
Alisema nchi yoyote haiwezi kupata maendeleo kwa kuwa na wanasiasa bila wanasayansi, hivyo  alisema wananchi wa mkoa wa Kagera wataendelea kukusanya vifaa vya ujenzi kujenga maabara hizo
Chanzo;Tanzani Daima 

WEZI WAMNYONGA MZEE KWA CHANDARUA HADI KUFA

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Goerge Mayunga
Mzee Furgensi Batura (72), Mkazi wa Kijiji cha Nyamiyaga Kata ya Bugomora Wilaya ya Kyerwa mkoani Kagera ameuawa kwa kunyongwa kwa chandarua na wezi nyumbani kwake na kumuibia kahawa.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Goerge Mayunga (pichani) alisema kuwa mauaji hayo yalitokea usiku wa kuamkia jana baada ya wezi hao kuvamia nyumbani kwake na kumkuta nje ya nyumba yake akilinda kahawa na mjukuu wake, Shukuru John (16).

 Mayunga alisema  baada ya  wezi  hao kuvamia nyumbani hapo, walimfunga mzee huyo na mjukuu wake kwa chandarua shingoni.

Alisema mzee huyo alikufa baada ya chandarua hicho kumnyonga shingoni na mjukuu wake kunusurika na wezi hao kuiba  magunia saba ya kahawa yenye thamani ya Sh. 700,000.

Alisema polisi wanawashikilia Wakazi wawili wa  Bugomora na kuendelea kuwasaka wegine kwa tuhuma za mauaji hayo na wizi wa magunia hayo ya kahawa.

Mayunga alisema  Spelius Lukokerwa aliyekutwa na kahawa hiyo inayodaiwa kuibwa nyumbani kwake alikufa baada ya kufikishwa kituo cha afya Murongo kutokana na kipigo alichokipata kutoka kwa wananchi.
 
CHANZO: NIPASHE
 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kagera Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa