BAADHI
ya wafanyabiashara walioshiriki Maonyesho ya Sabasaba katika Manispaa
ya Bukoba mkoani Kagera kutoka nchini Kenya, wameitaka Jumuiya ya Afrika
ya Mashariki (EA) kuondoa vikwazo mipakani kwa nia ya kuendeleza fursa
za masoko na maendeleo.
Mmoja wa wafanyabiashara hao, Elizabert Ogake, ameliambia Tanzania
Daima Jumapili kuwa hupata usumbufu mpakani wanaposafisha bidhaa zao na
kutozwa fedha nyingi kinyume na sheria.
Alibainisha kuwa hupata misukosuko ya kutozwa ushuru wa bidhaa kutoka Idara ya Uhamiaji ya Uganda.
Alisema uwepo wa Maonyesho ya Sabasaba yanayofanyika kila mwaka,
husaidia kukutanisha wafanyabiashara wa nchi hizo ambao hupeana mbinu za
kukuza uchumi wa nchi zao.
Mkurugenzi wa Shirika la Kagera Agricultural Industrial Development
& Promotion (KAIDEP), Philemon Kamazima, waliodhamini maonyesho
hayo, alisema kulikuwa na mwitikio mzuri mwaka huu tofauti na miaka
mingine.
Alisema maonyesho ya mwaka huu yalikuwa na washiriki 255 kutoka
ndani na nje ya nchi ambapo wengi wao wametoka katika makampuni na
taasisi mbalimbali za uzalishaji mali kutoka nchi za Uganda, Kenya na
Rwanda.
Chanzo;Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment