Home » » WEZI WAMNYONGA MZEE KWA CHANDARUA HADI KUFA

WEZI WAMNYONGA MZEE KWA CHANDARUA HADI KUFA

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Goerge Mayunga
Mzee Furgensi Batura (72), Mkazi wa Kijiji cha Nyamiyaga Kata ya Bugomora Wilaya ya Kyerwa mkoani Kagera ameuawa kwa kunyongwa kwa chandarua na wezi nyumbani kwake na kumuibia kahawa.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Goerge Mayunga (pichani) alisema kuwa mauaji hayo yalitokea usiku wa kuamkia jana baada ya wezi hao kuvamia nyumbani kwake na kumkuta nje ya nyumba yake akilinda kahawa na mjukuu wake, Shukuru John (16).

 Mayunga alisema  baada ya  wezi  hao kuvamia nyumbani hapo, walimfunga mzee huyo na mjukuu wake kwa chandarua shingoni.

Alisema mzee huyo alikufa baada ya chandarua hicho kumnyonga shingoni na mjukuu wake kunusurika na wezi hao kuiba  magunia saba ya kahawa yenye thamani ya Sh. 700,000.

Alisema polisi wanawashikilia Wakazi wawili wa  Bugomora na kuendelea kuwasaka wegine kwa tuhuma za mauaji hayo na wizi wa magunia hayo ya kahawa.

Mayunga alisema  Spelius Lukokerwa aliyekutwa na kahawa hiyo inayodaiwa kuibwa nyumbani kwake alikufa baada ya kufikishwa kituo cha afya Murongo kutokana na kipigo alichokipata kutoka kwa wananchi.
 
CHANZO: NIPASHE

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kagera Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa