(PICHA NA IKULU).
ZIARA YA RAIS JAKAYA KIKWETE IKIWA INAENDELEA MKOANI KAGERA.
RAIS KIKWETE AFUNGUA JENGO LA MAHAKAMA KUU KANDA YA BUKOBA
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifungua pazia kuzindua rasmi jengo la Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba leo Julai 25, 2013
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kuzindua rasmi jengo la
Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba leo Julai 25, 2013. Aliyeshika utepe ni
Jaji Mkuu, Othman Chande
Rais Kikwete akiwa katika moja ya vyumba vya mahakama hiyo
Rais Kikwete akifuatana na Jaji Mkuu wakati akikagua jengo la mahakama hiyo
Jaji Mkuu Othman Chande akimpa maelezo Rais Kikwete wakati wakiwa kwenye jengo la mahakama hiyo.
Rais Jakaya Kikwete na Jaji Mkuu wakiwa katika picha ya pamoja na
viongozi wengine wa mahakama waliohudhuria uzinduzi wa jengo hilo la
mahakama.
Picha na Ikulu
RAIS DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE AONGOZA MAADHIMISHO YA KUMBUKUMBU YA MASHUJAA KATIKA KAMBI YA KABOYA BUKOBA MKOANI KAGERA LEO.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete
akiweka ngao/sime katika mnara wakati wa maadhimisho ya kumbukumbu ya
Mashujaa katika kambi ya jeshi ya Kaboya, Bukoba, mkoani Kagera leo
Julai 25, 2013.
Viongozi wa dini wakisoma dua kwenye maadhimisho hayo. Pembeni ni Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Mohamed Ali Shein,
Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilali, Jaji Mkuu Mheshimiwa Chande
Othman na Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe Othman Makungu.
Rais Jakaya Kikwete akitembelea makaburi ya mashujaa waliopoteza maisha wakati wa vita na Nduli Iddi Amini wa Uganda.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete
akisalimiana na Wazee ambao ni sehemu ya mashujaa wetu walio hai waliohudhuria maadhimisho ya kumbukumbu ya
Mashujaa katika kambi ya jeshi ya Kaboya, Bukoba, mkoani Kagera leo
Julai 25, 2013.
MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUTURU NA WAKAZI WA KAGERA WILAYA YA MISENYI JANA.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akizungumza na baadhi ya wananchi wa Mkoa wa Kagera, baada ya kufuturu
nao futari ya pamoja aliyoiandaa katika Kiwanda cha Kagera Sugar, jana
Julai 24, 2013. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Misenyi, Kanali Mstaafu, Issa
Njiku (kushoto) ni Mmiliki wa Kiwanda cha Kagera Sugar, Nassor Seif.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib
Bilal, akiagana na Mkurugenzi wa Kiwanda cha Kagera Sugar, Hashim
Ranner, baada ya kumalizika kwa hafla ya Futari ya pamoja na wananchi wa
Mkoa wa kagera iliyofanyika katika Kiwanda cha Kagera Sugar Wilaya ya
Misenyi jana Julai, 24, 2013. Katikati ni Mmiliki wa Kiwanda hicho,
Nassor Seif.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Dkk. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya wananchi
alioshiriki nao Futari ya pamoja katika Kiwanda cha Kagera Sugar Wilaya
ya Misenyi Mkoa wa Kagera, baada ya kumalizika kwa hafla hiyo jana
Julai 24, 2013
Baadhi
ya wananchi waumini wa dini ya Kiislamu waliohudhuria hafla ya futari
ya pamoja, wakimsikiliza Makamu wa Rais Dkt. Bilal, wakati akizungumza
nao jana Julai, 24, 2013.
Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais
UNIC YAHAMASISHA VIJANA WILAYANI KARAGWE KUJIUNGA KATIKA VILABU VYA UMOJA WA MATAIFA
Afisa
Habari wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Usia Nkhoma
Ledama akizungumza na Mkuu wa Shule ya Sekondari Ndama ya Wilayani
Karagwe Mwl. Emmanuel Muganyizi kuhusiana na umuhimu wa wanfunzi wa
shule yake kuanzisha Vilabu vya Umoja wa Mataifa na faida zake.
Afisa
Habari wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Usia Nkhoma
Ledama akizungumza na walimu wa shule ya Sekondari Ndama na kuwapa
hamasa ya kuwa walezi wazuri wa vilabu hivyo vitavyoanzishwa shuleni
hapo ikiwa ni kama somo la ziada kwa wanafunzi wao ili wasipate muda wa
kushiriki matendo ya ajabu na yasiyo na maadili.
Usia
Nkhoma Ledama akiongozwa na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Ndama ya
wilayani Karagwe kuelekea madarasani kuzungumza na wanafunzi wa shule
hiyo.
Afisa
Habari wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Usia Nkhoma
Ledama akizungumza na vijana wa shule za sekondari Ndama wilayani
Karagwe mkoani Kagera, kuwaelezea umuhimu wa kujiunga na vilabu vya
Umoja wa Mataifa (UN Club) vinavyoanzishwa mashuleni kwa kuwa kwanza
vitawasaidia kujitambua.
Amewaambia
kwa vijana kama wao ambao tayari wameanzisha na kuendesha vilabu hivyo
mashuleni kujiunga kwa wingi zaidi na kutawawezesha kujifunza shughuli
za umoja wa mataifa duniani, kuhusishwa na mashirika mengine ya
kimataifa, kushiriki katika mafunzo mbalimbali, warsha na mikutano ndani
na nje ya nchi kama vile National Model UN, the Eastern Africa Model
UN, the Africa Regional Model UN na mengineyo, ikiwemo kupata nafasi ya
kuisaidia jamii zao kupitia program mbalimbali.
Bi.
Usia pia amewafafanulia vijana kuwa katika klabu hizo wataweza kuwa na
mtandao na vijana wengine kitaifa na kimataifa, kupata nafasi ya kufanya
kazi za kujitolea.
Baadhi
ya wanafunzi wa shule ya Sekondari Ndama wakimsikiliza kwa makini Afisa
Habari wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa nchini (UNIC) Usia
Nkhoma Ledama (hayupo pichani).
Usia
Nkhoma Ledama katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Shule ya Sekondari
Ndama pamoja na Mkurugenzi wa Radio Jamii FADECO ya wilayani Karagwe
Bw, Joseph Sekiku (kushoto).
Afisa
Habari wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Usia Nkhoma
Ledama akijitambulisha kwa baadhi ya walimu wa Shule ya Sekondari
Kayanga ya Wilayani Karagwe Mkoani Kagera. Kushoto mwenye suti ni
Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Johnbosco Paul.
Afisa
Habari wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Usia Nkhoma
Ledama akikagua Maktaba ya Shule ya Sekondari Kayanga. Kulia ni Mwl.
Mkuu wa Shule ya Kayanga Johnbosco Paul.
Afisa
Habari wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Usia Nkhoma
Ledama akizungumza na wazazi wa watoto wanaosoma katika shule ya
sekondari ya Kayanga amewaelezea kuwa pindi watoto wao wanapojiunga na
klabu za Umoja wa mataifa zilizopo mashuleni watapata elimu na uzoefu
utakaotengeza thamani ya CV zao na kuzipa uzito zaidi na pia watapata
ufahamu wa mambo mengi utakao wasaidia wasijiunge na vikundi visivyofaa
wala kushiriki matendo ya ajabu na yasiyo na maadili.
Amewaambia
wazazi hao ndani ya klabu hizo hutokea kupata tarajali, uzoefu wa kazi,
na kwamba kwa kupitia klabu hizo vijana wote shule zilizopo mikoa yote
ya Tanzania watakuwa na nafasi ya kuwa karibu na taratibu na kanuni za
Umoja wa Mataifa.
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari Kayanga ya Wilayani Karagwe mkoani Kagera wakiwa mapumzikoni kuelekea kupata uji.
Picha na maelezo kwa hisani ya fullshangweblog.com
YUNA NA UNESCO YAKUSANYA MAONI YA WANANCHI WA KARAGWE KUHUSU UTEKELEZAJI WA MRADI WA AMANI NA DEMOKRASIA KWA KUSHIRIKIANA NA REDIO ZA KIJAMII (FADECO).
Mshauri wa Radio Jamii kutoka UNESCO Rose Haji
Mwalimu akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Karagwe Dary Lwegasira
alipomtembelea ofisini kwake mjini Kayanga mkoani Kagera kutambulisha
mradi wa Amani na Demokrasia wenye lengo la kuhamasisha ushiriki wa
jamii miongoni mwa vijana, wanawake na walemavu katika maendeleo na
kudumisha amani nchini Tanzania. Mradi huo utakuwa unaratibiwa na
UNESCO kwa kushirikiana na UNDP.
Mweka hazina wa Shirikisho la Vijana la Umoja wa
Mataifa (YUNA) Tanzania Bara na Visiwani Bw. Omary Hassan akifafanua
jambo kuhusiana na mradi wa Amani kwa Mkuu wa Wilaya ya Karagwe Dary
Lwegasira (wa tatu kulia) namna utakavyoendeshwa kwa wakazi wa Wilaya
yake. Kushoto ni Mkurugenzi wa Radio jamii FADECO ya Wilaya ya
Karagwe Joseph Sekiku na wa pili kulia ni Mshauri wa Radio Jamii
kutoka UNESCO Rose Haji Mwalimu.
Picha juu na chini ni Bw. Omary Hassan
akikusanya maoni ya vijana wa Chuo cha Ufundi Stadi (KDVTC) kilichopo
kitongoji cha Kayanza wilayani Karagwe mkoa wa
Kagera.
Mweka hazina wa Shirikisho la Vijana
la Umoja wa Mataifa (YUNA) Tanzania Bara na Visiwani Bw. Omary Hassan
na Mkurugenzi wa Radio jamii FADECO ya Wilaya ya
Karagwe Joseph Sekiku (fulana ya Blue) kwenye picha ya pamoja na
walimu na wanafunzi wa Chuo cha ufundi stadi (KDVTC) mara
baada ya kumaliza zoezi la ukusanyaji maoni kwa wananchi wa
Karagwe.
Mweka hazina wa Shirikisho la Vijana la Umoja
wa Mataifa (YUNA) Tanzania Bara na Visiwani Omary Hassan akizungumza
na uongozi wa Perfect Education of Tourism and Institutions (PETI)
kuhusiana na ukusanyaji maoni ya Utekelezaji wa Mradi wa Amani na
Demokrasia Wilayani Karagwe. Kushoto ni Mkuu wa taasisi ya PETI
Devotha Brassio na Makamu Mkuu wa taasisi hiyo Fravian Gedion.
Bw. Omary Hassan akizungumza na wanafunzi wa
Perfect Education of Tourism and Institutions (PETI) kuhusiana na
utekelezaji wa mradi wa Amani ambapo vijana nao wanahusika katika
kujenga Amani ya nchi kwa sababu wao ndio taifa la
leo.
Bw. Omary Hassan katika picha ya pamoja na
uongozi wa taasisi ya PETI na baadhi ya wanafunzi wa taasisi
hiyo.
Mweka hazina wa Shirikisho la Vijana la Umoja wa
Mataifa (YUNA) Tanzania Bara na Visiwani Bw. Omary Hassan akikusanya
maoni kwa wananchi wa wilaya ya Karagwe kufanya tathmini ya
utekelezaji wa mradi wa Amani na Demokrasia.
Kina mama nao walihusika katika kuchangia maoni
ambapo wengi wao wameomba mradi huo utakapoanza kuwepo na kipindi
maalum katika radio jamii ya wilaya ya Karagwe cha kuwaelimisha waume
zao kuhusu swala la unywaji Pombe kupita kiasi ambao unapelekea
uvunjifu wa amani katika nyumba zao.
--
Mashirika ya UNDP na UNESCO yameanzisha mradi wa
pamoja wenye lengo la kuhamasisha ushiriki wa jamii miongoni mwa
vijana, wanawake na walemavu katika maendeleo na kudumisha amani
nchini Tanzania.
Kama inavyojulikana haiwezekani kuwa na
maendeleo bila kuwa na amani, na haiwezekani kuwa na amani bila kuwa
na maendeleo.
Kwa sababu hiyo Jumuiya ya Kimataifa inatambua
kuwa moja ya mikakati msingi ya kujenga amani ni kuwa na msingi
thabiti wa uchumi jamii.Pia kuwezesha raia wote kuhusisha katika kutoa
maamuzi ni kuweka msimamo katika maendeleo
endelevu.
PICHA ZOTE NA
TANGAZO LA MAUZO YA NYUMBA ZA MFUKO WA PENSHENI KWA WATUMISHI WA UMMA (PSPF)
MFUKO WA PENSHENI KWA WATUMISHI WA UMMA
(PSPF)
MAUZO YA NYUMBA ZA PSPF
Mfuko unapenda kuwataarifu wananchi wote kwamba inauza nyumba zilizojengwa na Mfuko katika mikoa ya Dar es Salaam- Ilala (Buyuni), Morogoro (Lukobe), Tabora (Usule), Mtwara (Mang’amba) na Shinyanga (Ibadakuli).
Bei ya nyumba ni kati ya Tsh 59,000,000.00 hadi Tsh 80,000,000.00 (Bila ya VAT) kulingana na ukubwa wa nyumba na Mkoa nyumba ilipo. Ukubwa wa nyumba ni kuanzia vyumba viwili hadi vinne. Fomu zinapatikana kwa gharama ya shilingi elfu tano (TShs. 5,000/=) kwenye ofisi za Mfuko zilizopo mikoa yote nchini.
Waombaji wanaohitaji kuona na kukagua nyumba wawasiliane na Mfuko kupitia namba 2120912/52 au 2127376.
“PSPF - Tulizo la Wastaafu”
Kwa maelezo zaidi wasiliana na:
Mkurugenzi Mkuu,
Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF),
Golden Jubilee Towers,
Front Tower – Ghorofa ya 6-13,
Mtaa wa Ohio/Kibo,
S. L. P. 4843,
DAR ES SALAAM.
Barua Pepe: pspf@pspf-tz.org
Tovuti: www.pspf-tz.org
WALIOKUWA ASKARI POLISI MKOA WA KAGERA WAPANDISHWA MAHAKAMANI KWA TUHUMA ZA MENO YA TEMBO
WATUHUMIWA wanne wakiwemo waliokuwa askari polisi kutoka Biharamulo na
Kagera waliokamatwa na vipande 18 vya meno ya tembo wilayani
Serengeti wamepandishwa kizimbani kwa makosa mawili ya uhujumu uchumi.
Mwandishi wetu Anthony Mayunga anaripoti kutoka SerengetiWaliofikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi mfawidhi wa wilaya hiyoAmoni Kahimba ni Boniphace John Kurwa(31)
Gerard Tuti (33) David Delina(36) wakulima wakazi wa Biharamulo na
Bukoba na Zainabu Hamisi Msabaha(26)fundi cherahani mkazi wa
Biharamulo.
Mwendesha mashitaka wa polisi sajenti wa polisi Paskael Nkenyenge
mahakama iliyofurika wasikilizaji kuwa katika muda ,siku wala tarehe
isiyojulikana watuhumiwa hao walikamatwa kwa kosa la kula njama za
kufanya biashara haramu ya nyara za taifa kinyume na sheria ya kanuni
ya adhabu namba 384(16) iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.
Alisema watuhumiwa hao na wengine ambao hawajakamatwa Tuguro
Zakayo,Nyarata Mewama,Emanuel Kananjire(Mnyarwanda)ambao wanatafutwa
wanakabiliwa na kosa hilo .
Katika kosa la pili mwendesha mashitaha huyo aliliambia mahakama kuwa
katika kosa la pili kuwa mnamo januari 4,2013 majira ya saa 5 usiku
katika eneo la Morotonga wilayani Serengeti alikamatwa na vipande 18
vya meno ya tembo vyenye uzito wa kg 104 vyenye thamani ya
tsh,66,760,000= kinyume cha sheria.
Alisema kosa hilo ni kinyume na sheria ya kanuni ya adhabu namba 86
kifungu cha 1,2 cha sheria namba 5 ya mwaka 2009 pia kifungu cha
14(d)cha sheria za uhujumu uchumi namba 60(ii) sura ya 200
iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.
Kutokana na kosa hilo la uhujumu uchumi mshitakiwa hakutakiwa kujibu
lolote kwa kuwa kosa hilo mpaka wapate kibali cha mwendesha mashitaka
wa serikali(DPP).
Katika kosa la kwanza washitakiwa wote walikana,na mwendesha mashitaka
akaomba siku nyingine ya kutajwa kwa shitaka hilo kwa kuwa upelelezi
haujakamilika na kuwa dhamana .
Hata hivyo mwendesha mashitaka wa polisi Inspekta msaidizi Abdallah
Idd aliyekuwa akishirikiana na Nkenyenge aliomba dhamana izingatie
sheria namba 148 kifungu cha (5)(e)kuwa wadhamini wawasilishe fedha
taslimu zaidi ya tsh,mil.10 au hati ya mali isiyohamishika.
Hata hivyo Hakimu Kahimba alitaka kujua sharti hilo ni kwa washitakiwa
wote ama mmoja,ambapo mwendesha mashitaka Nkenyenge alidai ni kwa
mshitakiwa mmoja Kurwa,madai aliyoyakataa kwa madai kuwa yanawahusu
wote.
Mbali na hilo aliwataka warekebishe mashitaka yao kwa kuwa hayaeleweki
,kwa kutoweka muda na sehemu walikowakamatia inatia shaka ,na kuhoji
wamejuaje wanastahili kushitakiwa Mugumu na si kwingineko.
Akitoa masharti ya dhamana Hakimu Kahimba alisema kila mshitakiwa
anatakiwa atajidhamini mwenyewe kwa dhamana ya tsh,mil.2 ya maneno,pia
mshitakiwa atadhaminiwa na watu wawili wanaoaminika na kueleweka na
wawe wakazi wa Serengeti kwa dhamana ya tsh,mil.10 za maneno.
Sharti la tatu wadhamini ambao ni wakazi wa wilaya hiyo wanatakiwa
kuweka fedha taslimu mil.34 mahakamani ama mali isiyohamishika yenye
thamani ya zaidi ya tsh,mil.35
Na kuwa mali hiyo iwe na hati inayotambuliwa na imefanyiwa uthamini na
mthamini anayetambulika na serikali na wala si barua za watendaji
ambazo amesema zimechangia watu wengi kukimbia kesi zao na
hawaeleweki.
Washitakiwa ,wadhamini na ndugu waliomba mahakama ilegeze masharti kwa
madai kuwa wao ni wageni na hawawezi kuwapata wadhamini wenye sifa
hizo wilayani hapo.
Kabla ya kutoa masharti ya dhamana alitoa angalizo kwa watu
waliojitokeza kuwadhamini washitakiwa hao wakati hawafahamiani na kuwa
watanunua kesi zisizowahusu.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi januari 28 mwaka huu itakapotajwa tena na
watuhumiwa wote wamerudishwa mahabusu baada ya kukosa wadhamini wenye
sifa zilizotajwa na mahakama,na kibali kimetolewa watuhumiwa wengine
watafutwe ili waunganishwe na wenzao.
Kabla ya kufikishwa mahakamani hapo Tuti na Derina ambao walikuwa
askari upepelezi Biharamulo na Kagera walifukuzwa kazi januari 10,2013
baada ya kupatikana na kosa kijeshi ili washitakiwe kiraia.
Washitakiwa hao walikamatwa januari 6,mwaka huu katika nyumba ya
kulala wageni baada ya Kurwa kuwataja na kubainika kuwa walikuwa
askari kanzu kutoka Biharamulo na Kagera ambao ni D/c Gerard Tuti
mwenye namba za F5553 ambaye ni mpelelezi katika ofisi ya kamanda wa
makosa ya jinai wilayani Bukoba .
Askari mwingine ni D/c koplo David Delina mwenye namba E9172 kutoka
ofisi ya upelelezi Biharamulo ambao walikuwa na gari aina ya Toyota
Ballon lenye namba za usajiri T403 BJK mali ya mtuhumiwa
David.Mtuhumiwa mwingine ni Boniphace John Kurwa(31) ambaye ni raia
mkazi wa Geita ambaye alikuwa na pikipiki
yenye namba za usajili T784 CCC aina ya Sunlog.
Ambaye akiwa na mwenzake aliyetajwa kwa jina moja la Nyarata akiwa na
pikipiki yenye namba za usajili T 834 BPH Toyo ambaye alitelekeza
pikipiki na mizigo na kutokomea walikuwa wakitokea kijiji cha
Rwamchanga wakiwa na meno hayo ambayo ni sawa na tembo watatu.
Januari 10 mwaka huu askari hao walifukuzwa kazi rasmi baada ya
mashitaka ya kijeshi kukamilika na kubainika kuwa walitenda kosa la
jinai na hatimaye januari 14 mwaka huu wakapandishwa katika mahakama
ya wilaya kujibu mashitaka yanayowakabili..