Naibu Katibu Mkuu wa
Wizara ya Nishati na Madini, anayeshughulikia masuala ya Nishati, Dkt. Mhandisi
Juliana Pallangyo (wa tatu kutoka kulia) akimweleza jambo Meneja wa Shirika la
Umeme Tanzania (TANESCO), Mkoa wa Kagera, Mhandisi Francis Maze (wa kwanza kutoka
kulia), wakati walipokuwa wakikagua eneo utakapotekelezwa Mradi wa kuzalisha
umeme wa megawati 14 kwa ushirikiano baina ya Tanzania na Uganda, unaojulikana
kama Murongo-Kikagati. Katikati ni Balozi wa Tanzania nchini Uganda, Grace
Mgavano. Wengine pichani ni Maofisa mbalimbali kutoka TANESCO, Ofisi ya
Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Wizara ya Ardhi.
Meneja wa Sheria
anayeshughulikia Mikataba, kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Mwesiga
Mwesigwa (wa pili kutoka kushoto), akifafanua jambo kwa Naibu Katibu Mkuu wa
Wizara ya Nishati na Madini, anayeshughulikia Nishati, Dkt. Mhandisi Juliana
Pallangyo (wa kwanza kulia) na Balozi wa Tanzania nchini Uganda, Grace Mgavano
(katikati) wakati walipokuwa wakikagua eneo utakapotekelezwa Mradi wa kuzalisha
umeme wa megawati 14 kwa ushirikiano baina ya Tanzania na Uganda, unaojulikana
kama Murongo-Kikagati. Wa kwanza kushoto ni Meneja wa Uwekezaji kutoka TANESCO,
Rwebangi Luteganya na wa pili kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Mikataba kutoka
Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Evelyni Makala.
Meneja wa Shirika la
Umeme Tanzania (TANESCO) wa Mkoa wa Kagera, Mhandisi Francis Maze (kulia),
akifafanua jambo kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini
anayeshughulikia masuala ya Nishati, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (katikati)
na Balozi wa Tanzania nchini Uganda (wa pili kutoka kulia), wakati walipokuwa
wakikagua eneo utakapotekelezwa Mradi wa kuzalisha umeme wa megawati 35 wa
Nsongezi kwa ushirikiano baina ya Tanzania na Uganda. Wengine kutoka kushoto ni
Meneja wa Uwekezaji kutoka TANESCO, Rwebangi Luteganya, Mkurugenzi wa Mikataba
kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Evelyni Makala na Meneja wa
Sheria anayeshughulikia Mikataba, kutoka TANESCO, Mwesiga Mwesigwa.
Kutoka kushoto ni Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, anayeshughulikia Nishati, Dkt.
Mhandisi Juliana Pallangyo, Balozi wa Tanzania nchini Uganda, Grace Mgavano na
Meneja wa Sheria anayeshughulikia Mikataba, kutoka Shirika la Umeme Tanzania
(TANESCO), Mwesiga Mwesigwa, wakitoka kukagua eneo la Nsongezi, utakapotekelezwa
Mradi wa ushirikiano baina ya Tanzania na Uganda, wa kuzalisha umeme wa
megawati 35.
Meneja wa Uwekezaji
kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Rwebangi Luteganya (kushoto),
akiwaeleza jambo Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini,
anayeshughulikia Nishati, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (katikati) na Balozi
wa Tanzania nchini Uganda, Grace Mgavano (kulia), wakati walipokuwa wakikagua
eneo utakapotekelezwa Mradi wa kuzalisha umeme wa megawati 35 wa Nsongezi kwa
ushirikiano baina ya Tanzania na Uganda.
Sehemu ya Mto Kagera,
unavyoonekana katika eneo la Nsongezi, mpakani mwa Tanzania na Uganda. Maji ya
Mto huo yatatumika kuzalisha umeme wa megawati 35 kwa ushirikiano baina ya nchi
hizo mbili kwa manufaa ya wananchi wake.
Sehemu ya viongozi na
wataalam mbalimbali kutoka Tanzania, wakiongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara
ya Nishati na Madini, anayeshughulikia Nishati, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo
(wa pili kutoka kushoto), wakitoka kukagua eneo utakapotekelezwa Mradi wa
kuzalisha umeme wa megawati 14 kwa ushirikiano baina ya Tanzania na Uganda,
unaojulikana kama Murongo-Kikagati.
Naibu Katibu Mkuu wa
Wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (katikati), akisaini
Kitabu cha Wageni katika Kituo cha Forodha Murongo, kilichopo mpakani mwa
Tanzania na Uganda, alipokuwa katika ziara ya kazi kukagua maeneo
itakapotekelezwa Miradi ya umeme kwa ushirikiano baina ya nchi hizo mbili.
Kushoto ni Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Kagera,
Mhandisi Francis Maze na kulia ni Ofisa Mfawidhi wa Kituo hicho cha Forodha,
Ezekia Nonkwe.
Kutoka kushoto ni
Balozi wa Tanzania nchini Uganda, Grace Mgavano, Ofisa Uhamiaji wa Kituo cha
Murongo, Mnubi Mtaka na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini,
anayeshughulikia Nishati, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo, wakijadiliana jambo
wakati Ujumbe wa Naibu Katibu Mkuu ulipopita mpakani hapo wakiwa katika ziara
kukagua maeneo itakapotekelezwa Miradi ya umeme kwa ushirikiano baina ya nchi
za Tanzania na Uganda.
Kutoka kushoto ni
Balozi wa Tanzania nchini Uganda, Grace Mgavano, Meneja wa Shirika la Umeme
Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Kagera, Mhandisi Francis Maze, Naibu Katibu Mkuu wa
Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dkt. Mhandisi Juliana
Pallangyo na Meneja Uwekezaji kutoka TANESCO, Rwabangi Luteganya, wakiangalia
eneo utakapotekelezwa Mradi wa kuzalisha umeme wa megawati 14 wa
Murongo-Kikagati kwa ushirikiano baina ya nchi za Tanzania na Uganda.
Na
Veronica Simba – Kagera
Baadhi ya viongozi na
maofisa mbalimbali wa Serikali ya Tanzania, wamefanya ziara ya siku moja
mpakani mwa Tanzania na Uganda, katika maeneo ya Nsongezi, Murongo na Kikagati,
kwa ajili ya kukagua maeneo inapotarajiwa kutekelezwa miradi ya sekta ya
nishati inayohusu ushirikiano baina ya nchi hizo mbili.
Ziara hiyo
iliyoongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini,
anayeshughulikia Nishati, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo, imefanyika leo Julai
27 ikiwa ni maandalizi ya Mkutano wa Mawaziri wa Tanzania na Uganda kuhusu
ushirikiano kwenye masuala ya mpakani, unaotarajiwa kufanyika Julai 29,
wilayani Bukoba Mkoa wa Kagera.
Kiongozi mwingine wa
Serikali aliyeambatana na Naibu Katibu Mkuu Pallangyo katika ziara hiyo ni
Balozi wa Tanzania nchini Uganda, Grace Mgavano.
Kwa mujibu wa Meneja
wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Kagera, Mhandisi Francis Maze,
miradi ya ushirikiano kwa sekta ya Nishati kwenye mpaka wa Tanzania na Uganda
inahusisha Mradi wa kuzalisha umeme wa Murongo-Kikagati wenye megawati 14,
Mradi wa kuzalisha umeme wa Nsongezi wa megawati 35 pamoja na Mradi wa kupeleka
umeme kwenye vijiji vya mpakani mwa nchi hizo mbili.
Mkutano wa Mawaziri
wa Tanzania na Uganda utatanguliwa na Mkutano wa Makatibu Wakuu wa Wizara
mbalimbali kutoka nchi hizo mbili wanaoshughulika na masuala ya ushirikiano
katika maeneo ya Mpaka, uliopangwa kufanyika kesho, Julai 28.
Maofisa wengine wa
Serikali walioshiriki ziara ya kukagua maeneo itakapotekelezwa miradi ya
nishati ni pamoja na Meneja wa Uwekezaji kutoka TANESCO, Rwebangi Luteganya,
Mkurugenzi wa Mikataba kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Evelyni
Makala, Meneja wa Sheria anayeshughulikia Mikataba, kutoka TANESCO, Mwesiga
Mwesigwa na Mtaalam kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,
Raymond Bagenda.