NIKO FITI KWA AJILI YA KUWATUMIKIA WATANZANIA, NIPENI URAIS NITAFANYA KAZI USIKU NA MCHANA‏

1
Mgombea Urais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dk. John Pombe Magufuli akitoa mpya jukwaani kwa kupiga Push Up kama kumi hivi ili kuwadhihirishia wananchi wa Mjini Karagwe mkoani Kagera kuwa yuko fiti kiafya ili kuwatumikia watanzania mara atakapochaguliwa na watanzania kuiongoza na kuwatumikia watanzania ifikapo Oktoba 25 mwaka huu katika uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani akisema kwamba kazi ya kuwatumikia watanzania siyo rahisi ni muhimu kuwa na afya njema ili kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa na niko tayari kufanya kazi usiku na mchana.
Akizungumza katika mkutano huo ameongeza kuwa atahakikisha anapunguza kwa kiwango kikubwa kodi zinazotozwa kwa wakulima wa zao la kahawa ili bei ya zao hilo iweze kupanda na wakulima hao kufaidika na zao hilo badala ya kuhangaika kupeleka nchini Uganda ambako bei yake iko juu kuliko nchini Tanzania.(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-NGARA)
2
1
Mgombea Urais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wananchi wa jimbo la Kyerwa katika mkutano wa kampeni uliofanyika jimboni humo.
2
Mgombea Urais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dk. John Pombe Magufuli akifurahia jambo katika mkutano huo.
3
Mgombea Urais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dk. John Pombe Magufuli akisisitiza jambo wakati akizungumza na wananchi wa Kyerwa mkoani Kagera.
4
Mgombea Urais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dk. John Pombe Magufuli akimnadi mgombea ubunge wa jimbo la Kyerwa Ndugu Innocent Sebba Bilakwate.
5
Umati wa wananchi ukiwa katika mkutano wa kampeni wa Dk John Pombe Magufuli uliofanyika mjini Ngara
7 9 10
Mgombea Urais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dk. John Pombe Magufuli akimnadi mgombea ubunge wa jimbo la Ngara Ndugu Alex Raphael Gashaza aliyeshika ilani ya Uchaguzi.
11
Mgombea ubunge viti maalum vijana mkoa wa Kagera Bi. Halima Bulembo akizungumza katika mkutano wa kampeni uliofanyika mjini Ngara leo jioni.
12
mgombea ubunge wa jimbo la Ngara Ndugu Alex Raphael Gashaza akiomba kura kwa wana Ngara katika kutano huo.
15
Baadhi ya vijana wakiwa wamekaa katika milingoti ya magoli ya uwanja wa mpira wa shule ya sekondari ya Rumanyika wilayani Kyerwa.
16 17
Katibu Mwenezi wa CCM mkoa wa Kagera Bw. Hamim akizungumza na wananchi katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika jimbo la Kyerwa kwenye uwanja wa shule ya sekondari ya Rumanyika.
18
Mgombea Urais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dk. John Pombe Magufuli akimnadi mgombea ubunge wa jimbo la Karagwe Ndugu Innoncet Bashungwa.
20
Baadhi ya wananchi wakiwa na mabaongo yenye picha ya Dk John Pombe Magufuli katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika mji wa Bunazi wilaya ya Misenyi.
21
Sheikh mkuu wa wilaya ya Mizenyi Abdulkadir Bulembo akifanya sala mara baada ya Mgombea Urais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dk. John Pombe Magufuli kuhutubia mkutano wa kampeni mjini Bunazi wilayani Misenyi.
22
Baadhi ya wananchi wakiwa katika mkutano huo mjini Bunazi.
24
Hii ni kampeni si urembo kichwani.
25
Mgombea Urais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dk. John Pombe Magufuli akimnadi mgombea ubunge wa jimbo la Nkenge Balozi Deodoras Kamala mjini Bunazi.
26
Msafara wa Mgombea Urais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Dk. John Pombe Magufuli ukiwasili katika eneo la mkutano mjini Bunazi wilayani Misenyi.

MAGUFULI AHANI MSIBA WA ALIYEKUWA MGOMBEA UDIWANI KATA YA MULEBA MKOANI KAGERA


 Picha ya aliyekuwa Mgombea wa Udiwani kata ya Muleba kwa tiketi ya chama cha CCM,enzi za uhai wake,aliyefarika jana kwa ajali ya Piki Piki
Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akitoa maneno ya pole kwa ndugu jamaa na marafiki leo asubuhi nyumbani kwa aliyekuwa Mgombea Udiwani wa Kata ya Muleba,Marehemu Osward Peter Rwakabwa katika kijiji cha Kagabilo,Muleba mkoani Kagera. 
Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwasili kutoa pole nyumbani kwa aliyekuwa Mgombea Udiwani wa Kata ya Muleba kwa chama cha CCM,Marehemu Osward Peter Rwakabwa katika kijiji cha Kagabilo,Muleba mkoani Kagera
 Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwapa mkono wa pole ndugu jamaa na marafiki leo asubuhi nyumbani kwa aliyekuwa Mgombea Udiwani wa Kata ya Muleba,Marehemu Osward Peter Rwakabwa katika kijiji cha Kagabilo,Muleba mkoani Kagera,aliyefarika jana kwa ajali ya Piki Piki
 Baadhi ya Ndugu Jamaa na Marafiki wakiwa wamekusanyika nyumbani kwa marehemu Osward Peter aliyefarika jana kwa ajali ya piki piki,Wakiomboleza kufuatia msiba huo.

MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI-AMEN

PICHA NA MICHUZI JR-MULEBA,KAGERA.

LOWASSA ALIVYOPOKELEWA MJINI BUKOBA


Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akisalimiana na mmoja wa wadau wa Mabadiliko, Prof. Azaveli Rwaitama, katika Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa AghaKhan, Mjini Bukoba, Mkoani Kagera leo Septemba 19, 2015. Mjini Bukoba, Mkoani Kagera jana Septemba 19, 2015.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akimpongeza Mke wa Mgombea Ubunge wa Jimbo la Bukoba Mjini kupitia CHADEMA, Willfred Lwakatare, mara baada ya kuzungumza na Wananchi wa Bukoba.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akizungumza na baadhi ya vingozi, mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Mashujaa wa Bunazi, Jimbo la Nkenge, Misenyi Mkoani Kagera.
Wananchi wa Jimbo la Nkenge, Misenyi Mkoani Kagera wakimshangilia Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, alipowasili kwenye eneo la Mkutano.


Wagombea 38 nafasi za Ubunge waliyowekewa pingamizi kuendelea na Kampeni.


Na Anitha Jonas – MAELEZO.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi  nchini  imefuta rufaa 38 za wagombea nafasi za ubunge kati ya 54 zilizowasilishwa kupinga baadhi ya wagombea hao kwa kuwatuhumu kutotimiza vigezo mbalimbali na kusema wagombea hao wanaweza kuendelea na Kampeni majimboni mwao.

Kauli hiyo ilitolewa jana jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Uchaguzi  Bw.Kailima Ramadhan kwenye mkutano na waandishi wa habari.
Alisema kuwa baada ya Wakurugenzi wanaoshughulikia uchaguzi kuzipitia ,waligundua kuwa rufaa hizo waliziona hazina mantiki na kukosa ushahidi wa kutosha.

“Wagombea waliokuwa wamewekewa pingamizi na kuenguliwa katika uchaguzi ni 16 na Tume imewarudisha wagombea 13 kati ya hao na waliobaki watatu ,Tume imeridhia maamuzi ya wasimamizi wa Uchaguzi”,alisema Bw.Ramadhani.

Aliongeza kuwa Tume hiyo inaendelea kupitia rufaa za wabunge zilizobaki  kwa kushirikiana na wasimamizi wa uchaguzi  ili kupata vielelezo  vinavyohusika na pindi itakapokamilisha zoezi hilo itatoa  taarifa yake ikiwa ni pamoja na rufaa 198 za madiwani kutoka halimashauri mbalimbali nchini.

Aidha  alisema kuwa Tume hiyo  itaendelea kusimamia haki na kufanya maamuzi ya kuzingatia sheria kwa wagombea wa vyama vyote vilivyoshiriki katika uchaguzi wa mwaka huu na kuwataka kuwa na imani na kazi inayofanywa na Tume katika rufaa hizo.

Mbali na hayo Mkurugenzi  wa uchaguzi alisema kuwa  Tume inatarajia kuanza zoezi la uhakiki wa daftari la mpiga kura visiwani Zanzibar kuanzia tarehe keshokuwa (03/09/2015) ambapo zoezi hilo litadumu kwa muda wa siku saba.

Akiongelea juu ya uhakiki wa taarifa za mpiga kura  aliyejiandikisha alisema unaweza kuhakiki taarifa zako kwa kupitia mtandao wa tume www.nec.go.tz au kwa  kupiga *152*00// katika simu na kupata taarifa zote.
 

UJUE MKOA WA KAGERA

 
MAELEZO YA JUMLA KUHUSU MKOA
Mkoa wa Kagera unapatikana kaskazini magharibi mwa nchi ya Tanzania. Makao makuu ya mkoa yapo katika mji wa Bukoba umbali wa kilometa 1500 kutoka Dar es Salaam, mkoa huu unapakana na nchi ya Uganda kwa kaskazini, Rwanda na Burundi kwa upande wa magharibi mkoa wa Kigoma, Mwanza kwa upande wa kusini na ziwa Victoria kwa upande wa mashariki. Vile vile mkoa wa Kagera uko kusini mwa ikweta kati ya 1 “00” na 2”45” latitudi. Kwa Iongitudo uko katika nyuzi 30”25” na 32”40” Mashariki mwa ‘greenwich'.

Mkoa wa Kagera ulijulikana kama “Ziwa Magharibi” jina hili lilidumu katika kipindi cha ukoloni na baada ya uhuru mpaka mwaka 1979 baada ya vita kati ya Tanzania na Uganda.
Mkoa ulipata jina hili kutokana na mto Kagera ambao hutiririsha maji yake kutoka Rwanda kupitia kaskazini na kumwaga maji yake katika ziwa Victoria.

Mkoa wa Kagera una jumla ya eneo la kilomita za mraba 39,168 kati ya hizo kilometa za mraba 28,513 ni eneo la nchi kavu za kilomita 10,655 ni eneo la maji. Ukiacha mbali wilaya za Biharamulo na Chato ambazo ni tambarare sehemu kubwa ya mkoa ni yenye milima na vilima vilivyogawanywa na mabonde yenye matingatinga. Upande wa magharibi wa mkoa mito mingi inamwaga maji yale katika mto Kagera ambao nao humwaga maji yake katika ziwa Victoria.


HALI YA HEWA
Hali ya hewa ya mkoa wa Kagera kwa ujumla ni ya joto la wastani wa 26.02 sentigredi. Mvua zinanyesha kwa wastani wa milimita 800-1,100 kwa mwaka kati ya mwezi Septemba na Januari na kati ya mwezi Machi na Mei. Mvua hizi ndizo zinazowezesha kuwepo kwauoto wa asili wa kuvutia katika maeneo mengi ya mkoa. Kwa miaka ya kawaida mkoa hupata mvua za uhakika za vuli na masika ambazo ni muhium kwa shughuli za kilimo na ufugaji.

WATU WANNE WAFARIKI BAADA YA BASI LA SABUNI EXPRESS KUGONGAA USO KWA USO NA TOYOTA LAND CRUISER ENEO LA BUGORORA MKOANI KAGERA

 Watu wanne wanasadikiwa kufariki dunia baada ya Basi la Kampuni ya Sabuni Express linalofanya safari zake kati ya Karagwe na Mwanza kugongana uso kwa uso na Gari ndogo aina ya Toyota Land Cruiser iliyokuwa imebeba Masister eneo la Bugorora,ikitokea Bukoba mjini kuelekea Mutukura.
Baadhi ya miili ya marehemu waliofariki katika ajali hiyo

Askari wa Usalama barabarani akiwa eneo la tukio.

Endelea kutufuatilia kwa taarifa zaidi

UBUNGE VITI MAALUM VIJANA BUKOBA;ANTU MANDOZA AJITOSA KUCHUKUA FOMU

Mgombea Ubunge Viti Maalum Vijana Bukoba Bi. Antu Mandoza(Kulia) akirejesha Fomu ya Kuomba Ridhaa kuteuliwa kugombea Ubunge wa Viti maalum Vijana Bukoba katika ofisi za umoja huo Mjini Bukoba, ahaidi kuinua Vijana Kiuchumi endapo atapata nafasi ya kuwa Mbunge wa Vijana.(Habari Picha na Faustine Ruta/bukobasports).Mcheza kwao hutunzwa, Vijana wazidi kujitokeza kuwania nafasi mbalimbali za Uongozi. Binti Antu Mandoza mwenye kuonekana kuwa na umri miaka 22-25 Amerudisha Fomu za kuwania nafasi ya Ubunge Vijana Viti Maalumu kupitia CCM. Kwa Mahojiano mafupi ameongelea jinsi anavyopanga kuinua Maisha ya Vijana kwa kuwatengenezea Fursa na mbinu mbalimbali za kujiajiri pia kuwaonya kutokukubali kutumika vibaya na MAKUNDI ya Kisiasa tunapoelekea Uchaguzi kwani ni wajibu wetu Vijana kuilinda Amani yetu. Mgombea huyo pia amesema kuwa shauku yake kubwa ni kuwatumikia Vijana kwa kutatua changamoto ya Ajira na pia ametoa ahadi ya kushirikiana na Vijana bega kwa bega kuleta maendeleo katika Mkoa wa Kagera.
Binti Antu Mandoza akiweka sawa Kumbukumbu zake katika kitabu mbele ya karani Bi. Jasinta Benedicto wa Umoja wa Vijana Kagera.
Dada Antu Mandoza akiwa kwenye Ofisi za Umoja wa Vijana BukobaMgombea Ubunge Viti Maalum Vijana Bukoba Dada Antu Mandoza (kulia) akiptia Fomu yake ya Kuomba Ridhaa kuteuliwa kugombea Ubunge wa Viti maalum Vijana. Kushoto ni Bi. Jasinta Benedicto karani wa Umoja wa Vijana Kagera.
Mgombea Ubunge viti maalumu kupitia chama cha Mapinduzi dada Antu Mandoza akitoka katika ofisi za umoja wa vijana wa ccm Mkoa wa Kagera baada ya kuchukua fomu

BUKOBAWADAU MEDIA TUNAWATIA IDD NJEMA‏

 BUKOWADAU MEDIA , tunawatakia waislamu wote na wasomaji wetu popote duniani siku kuu ya njema yenye kheri na baraka.
Tunamuomba Mola wetu mlezi awarehemu wazee wetu wote waliotangulia mbele ya haki na awasamehe makosa yao.
“sifa zote njema ni za Mwenyezi Mungu ambaye ni vyake vyote vilivyomo Mbinguni na Ardhini. Na Akhera, sifa njema ni zake pia; Naye ni Mwenye Hekima na Mwenye Ujuzi wa kila jambo”.
Kwa utukufu wako huo tunakuomba Allah tuondolee madhila, maradhi na kila lililobaya kwetu waja wako wote, tutie imani ya kukutumikia wewe na utupe mwisho mwema hapa duniani na utufunike na rehma zako kesho akhera ili tuwe wenye kufuzu.
IDD MUBARAAK .

ZITTO: HERI NIWE MSALITI WA CHAMA SI TAIFA

KIONGOZI wa Chama cha ACT-Wazalendo, Bw. Zitto Kabwe, amesema ni heri aendelee kuitwa msaliti na watu wasio na dhamira nzuri ya kupigania masilahi ya nchi kuliko kuwasaliti wananchi.


Alisema ataendelea na msimamo wa kuhakikisha masilahi ya Taifa yanawekwa mbele badala ya kukubali kukumbatiwa na watu wenye dhamira ya kunufaisha matumbo na familia zao.

Bw. Kabwe aliyasema hayo Mjini Bukoba, mkoani Kagera juzi kwenye mkutano wa hadhara ikiwa ni mara yake ya kwanza kuwahutubia wakazi wa mji huo tangu aingie kwenye siasa.

Aliongeza kuwa, kabla ya kufumuka mgogoro katika chama chake cha zamani (CHADEMA), wapinzani walikubaliana masuala mbalimbali ya kusimamia likiwemo la kukataa kuchukua posho za vikao, kutotumia mali za umma kwa manufaa ya chama.

Alisema dhamira ya makubaliano hayo ni kuibana Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), hasa inapotaka kusamehe kodi kiholela, kutumia mali za umma kwa masuala yao ya chama na kujipatia posho zisizo na sababu.

"Ndugu zangu wana Bukoba, kilichoniponza ni kusimamia masilahi ya umma si kingine, nilitaka tujitofautishe na CCM lakini wenzangu hawakuwa tayari, kama wote tunachukua posho, kama wote hatutaki kufutiwa msamaha wa kodi na kutumia mali za umma kwa ajili ya vyama vyetu, tofauti yetu itakuwa nini na chama tawala," alihoji Bw. Kabwe.

Aliongeza kuwa, wote wanaomuita msaliti wanapaswa kuwaeleza wananchi wamewafanyia nini ili kutimiza majukumu yao ya kibunge muda wote waliokuwa bungeni.

Alisema kamwe ACT-Wazalendo hakitapita katika makosa ambayo yamefanywa na vyama vingine na kukubaliana kuzindua Azimio la Tabora kutoka katika mazuri ya Azimio la Arusha.

Bw. Kabwe alisema jambo lingine ambalo aliliweka wazi wakati akiwa mbunge na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) ni kutaka vyama vya siasa vikaguliwe hesabu zao kwa kuwa vinapokea ruzuku ya Serikali ambayo ni kodi ya wananchi.

"Katika kulitetea Taifa, mimi nilionekana msaliti kwa sababu nilipigania masilahi ya wananchi ambao bado wana kipato cha chini, nipo tayari kuitumikia nchi si kukitumikia chama kwani chama kinapita," alisema Zitto na kuongeza;

"Fedha hizi lazima zikaguliwe ili ifahamike matumizi halali si vinginevyo, nilipokuwa Mwenyekiti wa PAC, nilisema lazima ukaguzi ufanyike kwa vyama vyote kwani hapa tunatetea masilahi ya umma," alisema.

Aliongeza kuwa, Taifa la Tanzania ni la wananchi ambao wengi wao ni maskini; hivyo wanahitaji kuwa na kiongozi jasiri mwenye uthubutu wa kufanya yale anayohubiri hadharani.

Aliongeza kuwa, Tanzania inahitaji mabadiliko na chama cha ACT-Wazalendo kimeanza kutekeleza kwa kuzindua Azimio
la  Tabora ambalo limehuishwa kutoka Azimio la Arusha.

Bw. Kabwe alifafanua kuwa, kiongozi yeyote wa chama hicho ambaye atachaguliwa kwenye nafasi ya kiserikali, hatapokea posho za  vikao wakiwemo  wabunge kwani vikao vya Bunge ni sehemu ya kazi zao.

Alisema hivi sasa nchi imekithiri kwa rushwa na ufisadi mkubwa kutokana na kundi la watu wachache walio wafanyabiashara na wanasiasa.

"Hata watia nia wa nafasi ya urais waliojitokeza hadi sasa katika vyama mbalimbali, wengi wao hawana dhamira ya kupambana na rushwa kwa kuwa wengi wao ni wala rushwa na mafisadi wakubwa.

"Wakati wa hayati Mwalimu Julius Nyerere, si kwamba hakukuwa na rushwa ilikuwapo ndogo ndiyo maana Mwalimu aliweka miiko
na maadili ya viongozi kwa kufuata Azimio la Arusha, hivi sasa nchi haipo katika rushwa; bali ufisadi hali ambayo ni hatari kwa Taifa letu," alisema Bw. Kabwe.

 Chanzo:Majira

MAPOKEZI YA MH. LOWASSA MJINI BUKOBA HAYANA MFANO, AZIDI KUDHAMINIWA KWA KISHINDO‏

 Sehemu ya Wakazi wa mji wa Bukoba Mkoani Kagera wakiwa nje ya Uwanja wa Ndege wa Bukoba, wakimsubiri kumlaki Mtangaza nia ya Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Mh. Edward Lowassa, tayari kwa kupokea fomu ya wanaCCM wa kumdhamini.
 Wadau wa CCM wakijadiliana jambo.
 Ndege iliyombeba Mh. Edward Lowassa ikiwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Bukoba, Mkoani Kagera leo.
 Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Mh. Edward Lowassa akisalimiana na Mwenyekiti Mstaafu wa CCM Mkoa wa Kagera, Mzee Pius Ngeze wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Bukoba, Mkoani Kagera leo Juni 15, 2015. PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI.
 Mh. Lowassa katika tabasamu.
 Umati wa wanaCCM pamoja na wananchi wa Mji wa Bukoba mkoani Kagera ukiwa umemzunguka Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Mh. Edward Lowassa, wakati alipowasili kwenye ofisi za CCM Mkoa wa Kagera, leo Juni 15, 2015.
 Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Mh. Edward Lowassa akimsikiliza Katibu wa UWT wilaya ya Bukoba Vijijini, Agness Bashemu alipokuwa akitoa taarifa fupi ya namna ya kumkabidhi fomu hizo. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Bukoba Mjini, Yussuf Ngaiza.



 Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Rukwa, Hypolitus Matete akiwasalimia wanaCCM pamoja na wananchi wa Mji wa Bukoba mkoani Kagera leo Juni 15, 2015.

 Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kigoba, Dkt. Aman Kaborou akiwasalimia wanaCCM pamoja na wananchi wa Mji wa Bukoba mkoani Kagera leo Juni 15, 2015. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Hamis Mngeja.
 Mjumbe wa Mkutano Mkuu (NEC) Bukoba, Nazir Karamagi akuzungumza machache mbele ya wanaCCM pamoja na wananchi wa Mji wa Bukoba mkoani Kagera leo Juni 15, 2015. 
 Mwenyekiti Mstaafu wa CCM Mkoa wa Kagera, Mzee Pius Ngeze akizungumza mbele ya umati wa wanaCCM pamoja na wananchi wa Mji wa Bukoba mkoani Kagera leo Juni 15, 2015, na kutangaza kwamba yeye pia ni mmoja ya wana Safari ya Matumaini.
 Shangwe kila kona.
 Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Mh. Edward Lowassa akipongezwa na Bibi huyu (ambaye jina lake halikuweza patikana kwa haraka) mara baada ya kupokea fomu za wanaCCM zaidi ya 6000 waliomdhamini ili apate ridhaa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kuwania Urais wa Tanzania, kwenye Uchachuzi Mkuu, Unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015.  
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Mh. Edward Lowassa akipokea fomu kutoka kwa Katibu wa CCM Wilaya ya Bukoba mjini, Acheni Mwinshehe, zenye majina ya wanaCCM wa Mkoa wa Kagera waliomdhani ili apate ridhaa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kuwania Urais wa Tanzania, kwenye Uchachuzi Mkuu, Unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015. 
 Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Mh. Edward Lowassa akizungumza na umati wa wanaCCM pamoja na wananchi wa Mji wa Bukoba mkoani Kagera leo Juni 15, 2015, Wakati akitoa shukrani zake kwa kumdhamini ili apate ridhaa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kuwania Urais wa Tanzania, kwenye Uchachuzi Mkuu, Unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015. Zaidi ya wanaCCM 6000 wamdhamini mkoani Kagera.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Mh. Edward Lowassa akiwaaga wanaCCM pamoja na wananchi wa Mji wa Bukoba mkoani Kagera leo Juni 15, 2015, mara baada ya kupokea fomu za wanaCCM zaidi ya 6000 waliomdhamini ili apate ridhaa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kuwania Urais wa Tanzania, kwenye Uchachuzi Mkuu, Unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015. 
 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kagera Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa