WAFANYABIASHARA watano wamekufa maji baada ya boti waliyokuwa
wakisafiria ya Mv. Kitoko2 kuzama kwenye Ziwa Victoria kwa madai ya
kuzidisha uzito.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, George Mayunga, alikiri kutokea kwa
ajali hiyo Mei 23, 2014 saa nane usiku baada ya injini ya boti hiyo
kuzima ghafla ikiwa safarini.
Alisema boti hiyo ilikuwa ikitoka Bugombe kupitia Kasenye kuelekea
Mganza na abiria watano, kati yao mwili wa Jane Mlekatete (36) raia wa
Rwanda uliopolewa.
Aliwataja wengine waliokuwepo kwenye boti hiyo kuwa ni Chikola
Filbert (22) na Mapinduzi Daud (38), wengine walitambuliwa kwa jina moja
ambao ni Asha na Suzy.
Chanzo:Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment