Home » » BAWACHA: UWT ACHENI KUWAPUMBAZA WANAWAKE

BAWACHA: UWT ACHENI KUWAPUMBAZA WANAWAKE

BAWACHA: UWT acheni kuwapumbaza wanawake
BARAZA la Wanawake wa CHADEMA, (BAWACHA), limejipanga kuhakikishawanawake nchini wanaamka kudai haki zao huku likiuonya Umoja waWanawake wa CCM, (UWT), kuacha kuwapumbaza kwa kuwaimbisha nyimbo zisizo na tija huku ukishindwa kuwapatia ufumbuzi wa kero zao.
Aidha, limedai kuwa kwa sasa wanawake hawahitaji kufundishwa kupika auKuimba, wanataka kupatiwa fursa zao kiuchumi ili waweze kuzitumiakujiongezea kipato kitakachowawezesha kutunza familia zao.
Hayo yalisemwa juzi na Mwenyekiti wa BAWACHA mkoani Kagera, ConchestaRwamlaza, wakati akiwahutubia wananchi wa Biharamulo kwenye uwanja waSoko Jipya, ambako mkutano huo uliwashirikisha uongozi wa BAWACHATaifa.
Alisema kuwa wanawake nchini, wanahitaji huduma bora za afya wanapokwenda kwenye vituo vya afya na hospitali, wanahitaji watoto wao wapate elimu bora shuleni, wanahitaji kupatiwa fursa zao kwenye ardhi na  kiuchumi, waweze kushiriki shughuli za ujasiriamali na kupata kipato cha kutunza familia zao.
“Tunatangaza vita na UWT, waache kuwaimbisha wanawake ‘hiyena hiyena’
wanawake wa Tanzania kwa sasa hawahitaji mafunzo ya kupika… wameshaamka wanataka waelezwe namna watanufaika na rasilimali zilizo kwenye maeneo yao siyo kuwaimbisha nyimbo zisizo na faida,” alisema mbunge huyo wa viti maalum CHADEMA.
KUIZUIA KASI YA CHADEMA NI SAWA NA KUZUIA UPEPO JANGWANI
Kwa upande wake, Mbunge wa Biharamulo, Dk. Anthony Mbasa, alisema CCMhawataweza kuzuia kasi ya CHADEMA kutoa elimu ya uraia kwa wananchi,kwa kile alichodai kuwa atakayejaribu kufanya hilo hatafanikiwa.
“Kasi ya CHADEMA haizuiliki, tutahakikisha tunapita maeneo yote ya nchitutahamasisha wananchi kuikataa Katiba pendekezwa, imetupa maoni yetuwananchi ikahakikisha inalinda maslahi ya kikundi kidogo cha CCM natutahakikisha tunawang’oa na tunaanza kwenye uchaguzi huu wavitongoji, vijiji na mitaa…
“Kuizuia kasi ya CHADEMA ni kazi ngumu, sisi tunaahidi na tunatekeleza,hakuna wa kutuzuia na atakayejaribu ni sawa na kuzuia upepo jangwanijambo ambalo haliwezekani,” alisema Dk. Mbasa.
MIKATABA IKIWA WAZI CCM WANAHOFU KUSHINDWA KUPIGA ‘DILI’
Mwenyekiti wa Taifa BAWACHA, Halima Mdee, alisema wabunge waCCM wameondoa kipengele kinachotaka uwazi kwenye rasimu ya tume yamabadiliko ya Katiba, kwa hofu kuwa watashindwa kupiga dili.
Alisema kuwa Biharamulo kulikuwa na mgodi wa Tulawaka, ambao hivi sasawawekezaji wamemaliza kuchimba dhahabu wamerudisha mashimo kwaserikali, lakini yeye kama mwakilishi wa wananchi bungeni hajui mkatabaulikuwa unasemaje, kwani mikataba ni siri.
Mdee, alimpongeza mbunge wa jimbo hilo kwa kufanya vema kazi ya kuwawakilisha wananchi wake bungeni, kwani ameweza kufanikisha ujenzi wa barabara ya lami kwenye jimbo hilo, jambo ambalo lilishindikana kwa miaka 50 iliyopita
Chanzo:Tanzania Daima

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kagera Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa