Home » » WASHIKILIWA KWA TUHUMA ZA MAUAJI

WASHIKILIWA KWA TUHUMA ZA MAUAJI

WATU watatu wanashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Kagera kwa tuhuma mbalimbali zikiwemo za mauaji na uhalifu mwingine uliofanyika Oktoba mwaka huu, mkoani humo kwa nyakati tofauti.
Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Henry Mwaibambe alisema kuwa katika tukio la kwanza, waliwakatama watuhumiwa wiwili ambao walikuwa wakijihsusha na mauaji mabalimbali mkoani Kagera likiwemo la mwalimu wa sekondari.
Aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Samitu Haruna (30) fundi pikipiki mwenyeji wa Kyaka wilayani Missenyi ambaye alikiri kuhusika na mauaji ya Ernest Kato (32) fundi ujenzi mkazi wa Kamizilente kata ya Rwamishenye yaliyotokea Oktoba 20, mwaka huu.
Alisema kuwa baada ya polisi kumhoji, alisema kuwa alitumwa na watu ambao polisi wamehifadhi majina yao akafanye uhalifu huo kwa ahadi ya kulipwa ujira wa sh. 450,000 huku akiwa amelipwa sh. 50,000 kama kianzio.
Mtuhumiwa mwingine ni Erick Mwombeki (27), aliyejihusisha na mauaji ya mwalimu Denis Ng’andu (35) wa shule ya Sekondari ya Kagemu mnamo Oktoba 6 mwaka huu, ambapo naye pia alikiri kuhusika na tukio hilo.
Kwa mujibu wa kamanda, polisi wanendelea kuusaka mtandao unaojihusisha na uhalifu huo wa mauji ndani ya Manispaa ya Bukoba ili wachukuliwe hatua kwa mujibu wa sheria.
Wakati huo huo, jeshi hilo linamshikilia Wilfred Thomas (40) fundi wa kuchomelea mkazi wa wilayani Ngara kwa tuhuma za kukutwa na noti bandia zenye thamani ya sh. milioni1.1 kama zingekuwa fedha halali.
Kamnda alisema kuwa, Oktoba 26 mwaka huu, polisi wilayani Karagwe walipata taarifa kutoka kwa raia wema kuwa kuna mtu anafanya biashara ya kuuza noti bandia kwa kubadilishana sh. laki moja kwa sh. 40,000 fedha halali na hivyo kuwekewa mtego.
Alisema kuwa baada kupekuliwa alikutwa na noti 227 za sh. 5,000 za bandia na kwamba alipohojiwa alikiri kujihusisha na biashara hiyo na kutaja kuwa fedha hiyo aliipata nchi jirani ya Uganda.
Chanzo;Tanzania Daima

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kagera Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa