SERIKALI
mkoani Kagera inakusanya kati ya shilingi milioni 35 hadi 38 kila
mwezi, kutokana na uuzwaji nje ya nchi samaki na dagaa waliokaushwa,
wanaovuliwa katika ziwa Victoria
Afisa
mfawidhi kitengo cha udhibiti ubora na usalama wa samaki na mazao
yake katika mkoa wa Kagera, Monica Kishe amesema kuwa kwa mwezi
Oktoba mwaka huu, ziliuzwa nje ya nchi tani 100 za samaki na tani
kumi za dagaa wakavu na kuipatia serikali fedha za kigeni zaidi ya
shilingi milioni 38.
Amezitaka
halmashauri za wilaya ya Bukoba, Muleba na manispaa ya Bukoba,
kushirikiana na wavuvi katika wilaya hizo kutunza mialo saba
inayokarabatiwa na serikali kuu kwa gharama ya shilingi bilioni 28,
ili kuongeza ubora na upatikanaji zaidi wa samaki.
Mialo
iliyokarabatiwa ni Nyamukazi, Igabilo, Rushara, Marehe,
Kerebe, Iramba na Katembe, na kuwa gharama ya kila mwalo ni shilingi
milioni 400.
Hata
hivyo amesema pamoja na mapato hayo samaki katika ziwa Victoria
wanaendelea kupungua kutokana na uvuvi haramu unaoendeshwa na baadhi
ya wavuvi, ikiwamo kuvua kwa sumu, matumizi ya nyavu zisizoruhusiwa
kisheria na vyandarua.
0 comments:
Post a Comment