Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akimkabidhi chaeti, Mkurugeniz wa Kagera Sugar, Bw. Hamadi Yahaya,
ikiwa ni sehemu ya kutambua mchango wake wa kuchangia maendeleo ya Elimu
ya Jimbo la Nkenge mkoa wa Kagera,wakati wa hafla ya harambee ya
kuchangisha fedha kwa ajili ya Mfuko wa Maendeleo ya Elimu Jimbo la
Nkenge kununua madawati ili kusadia shule za msingi za Jimbo hilo.
Harambee hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam, usiku wa kuamkia leo.
Kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Nkenge, Asumpta Mshana na (kushoto kwa
Makamu) ni Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Kanali (mst) Fabian Masawe. Jumla ya
Shilingi milioni 114, pesa taslimu milioni 65.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akizungumza wakati wa hafla ya kuchangisha fedha kwa ajili ya Mfuko wa
Maendeleo ya Elimu Jimbo la Nkenge kununua madawati ili kusadia shule za
msingi za Jimbo hilo. Harambee hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam,
jana usiku. Kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Nkenge, Asumta Mshana na
(kushoto kwa Makamu) ni Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Kanal Fabian Masawe.
- Sehemu ya wageni waalikwa kutoka mkoa wa Kagera waliohudhuria harambee hiyo
Baadhi ya wageni waalikwa kutoka mkoa wa Kagera waliohudhuria harambee hiyo
Meza
Kuu wakijumuika kuimba wimbo maalumu wa mkoa wa Kagera wa kuhamasisha
maendeleo ya mkoa huo, hususan katika suala la elimu na kuchangia
madawati.
Msanii Saida Karoli na kundi lake wakiburudisha wakati
wa hafla ya harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya Mfuko wa
Maendeleo ya Elimu Jimbo la Nkenge kununua madawati ili kusadia shule za
msingi za Jimbo hilo. Harambee hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam,
usiku wa kuamkia leo. Picha na OMR.
0 comments:
Post a Comment