WALIMU wa shule za msingi na sekondari wilayani Karagwe, wameitaka
serikali kurudisha mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kwa mujibu
wa sheria, ili kuwajengea ukakamavu katika maeneo yao ya kazi.
Wakizungumza katika mkutano mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT)
jana, uliowajumuisha walimu wa Wilaya ya Karagwe na Kyerwa, walisema
walimu waliopitia mafunzo ya JKT na ambao hawajapitia wanaonekana wako
tofauti kiukakamavu na katika utendaji kazi wao.
“Serikali itupeleke jeshini tukapate ukakamavu. Tuliwaona walimu
waliopita jeshini walikuja na vitu vingi vya kuiga, nyimbo za hamasa za
mchakamchaka, gwaride, michezo mbalimbali,” alisema.
Chanzo;Tanzania daima
0 comments:
Post a Comment