Mwandishi wetu, Biharamulo-Kagera Yetu
Viongozi wa dini nchini wametakiwa kuacha tabia ya kuhubiri kwa mazoea bali wahubili kwa maono ili kuiletea Jamii maadili yanayo kwenda sambamba na matakwa ya Mungu.
Hayo yamesemwa na Askofu Mkuu wa Kanisa la Angelikana Tanzania Dr Valentino Mokiwa wakati akihubili katika ibada ya ufunguzi wa nyumba ya askofu wa Dayosisi tarajiwa ya Biharamulo (leo jumanne)
Askofu Mokiwa amesema wapo baadhi ya viongozi wa dini ambao wamekuwa wakihubili neno la Mungu kwa mazoea ya kuyarudiarudia kila siku na hivyo kutokea mmomonyoko wa maadili katika jamii na kuwafanya waumini kutopenda kuyasikia.
Aidha amesema katika kuhakikisha jamii inamurudia Mungu viongozi wa dini wakiwemo wachungaji, wainjirist, Mashemasi Mapadri na masikofu kuacha tabi hiyo kwa kuwa wao ni kioo cha jamii inayo wazunguka.
Blogzamikoa
0 comments:
Post a Comment