DKT.BILAL AENDESHA ZOEZI LA HARAMBEE YA KUCHANGIA MADAWATI MFUKO WA MAENDELEO YA ELIMU JIMBO LA NKENGE

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi chaeti, Mkurugeniz wa Kagera Sugar, Bw. Hamadi Yahaya, ikiwa ni sehemu ya kutambua mchango wake wa kuchangia maendeleo ya Elimu ya Jimbo la Nkenge mkoa wa Kagera,wakati wa hafla ya harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya Mfuko wa Maendeleo ya Elimu Jimbo la Nkenge kununua madawati ili kusadia shule za msingi za Jimbo hilo. Harambee hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam, usiku wa kuamkia leo. Kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Nkenge, Asumpta Mshana na (kushoto kwa Makamu) ni Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Kanali (mst) Fabian Masawe. Jumla ya Shilingi milioni 114, pesa taslimu milioni 65.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza wakati wa hafla ya kuchangisha fedha kwa ajili ya Mfuko wa Maendeleo ya Elimu Jimbo la Nkenge kununua madawati ili kusadia shule za msingi za Jimbo hilo. Harambee hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam, jana usiku. Kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Nkenge, Asumta Mshana na (kushoto kwa Makamu) ni Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Kanal Fabian Masawe. 
 - Sehemu ya wageni waalikwa kutoka mkoa wa Kagera waliohudhuria harambee hiyo
 Baadhi ya wageni waalikwa kutoka mkoa wa Kagera waliohudhuria harambee hiyo
 Meza Kuu wakijumuika kuimba wimbo maalumu wa mkoa wa Kagera wa kuhamasisha maendeleo ya mkoa huo, hususan katika suala la elimu na kuchangia madawati.
Msanii Saida Karoli na kundi lake wakiburudisha wakati wa hafla ya harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya Mfuko wa Maendeleo ya Elimu Jimbo la Nkenge kununua madawati ili kusadia shule za msingi za Jimbo hilo. Harambee hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam, usiku wa kuamkia leo. Picha na OMR.



Tibaijuka ataka soko la ndizi Muleba

WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, amewataka madiwani wa Halmashari ya Muleba, mkoani Kagera, kujenga soko la ndizi la kisasa kwa ajili ya mahitaji ya wananchi na kupanua ajira kwa jamii.
Tibaijuka alitoa kauli hiyo juzi mjini Muleba, katika kikao cha Baraza la Madiwani wa halmashauri hiyo kilichofanyika kwenye ukumbi wa halmashauri ya wilaya hiyo.
Kwa mujibu wa Profesa Tibaijuka, ambaye pia ni mbunge wa Muleba Kusini (CCM), madiwani wa wilaya hiyo wanatakiwa kuweka mikakati ya ujenzi wa soko hilo, kwa kuzingatia zao hilo ni muhimu kwa wananchi wa Muleba na mkoa kwa ujumla.
“Naamini sisi madiwani wa Muleba tukijenga soko la ndizi itasaidia kuongeza ajira na kukuza uchumi wa wananchi wetu. Maana itawarahisishia wananchi kupata mahitaji eneo sahihi,” alisema.
Aidha, waziri  aliwataka madiwani kusimamia ardhi ya wananchi kwa umakini, na kuongeza kuwa diwani yeyote  haruhusiwi kugawa ardhi bali anatakiwa kusimamia kwa uangalifu rasilimali hiyo.
Diwani wa Kamachumu, Dunstan Mutagywa (CCM) aliunga mkono wazo la waziri huyo na kusema soko la ndizi linatakiwa kujengwa kwenye eneo ambalo wananchi watapata wateja.
Alisema endapo watajenga soko hilo sehemu nzuri ambayo wananchi atafanya biashara, itasaidia katika upatikanaji wa huduma hiyo muhimu karibu na jamii yenyewe.
Chanzo;Tanzania Daima

WASSIRA: SERIKALI HAINA AJIRA ZA KUTOSHA KWA VIJANA




Vijana kote nchini wametakiwa kubuni mbinu mbadala ya kujiajiri wenyewe ili waweze kujikwamua katika umaskini, badala ya kutegemea ajira za serikali pekee ambazo hazitoshelezi mahitaji yaliyopo.

Rai hiyo imetolewa na waziri ofisi ya Rais, Mahusiano na Uratibu, Stephen Wassira wakati akikagua miradi ya mfuko wa maendeleo ya jamii nchini (TASAF) katika wilaya ya Ngara.

Waziri Wassira alisema kuwa serikali haina uwezo wa kuajiri vijana wote hapa nchini,  inachokifanya ni kubuni namna wananchi watakavyotumia fursa zilizopo kujiajiri kupitia sekta mbalimbali hasa ya kilimo.

Miongozi mwa miradi ya Tasaf aliyoitembelea ni pamoja na mradi wa kikundi cha vijana 25 walioibua mradi wa kufuga mbuzi  katika kijiji cha Ibuga kata Kabanga, ambao wamejiinua kiuchumi kupitia mradi huo.

Akisoma risala katibu wa kikundi hicho Bahati Philmon, amesema kuwa  baada ya kuona kupata ajira za serikali kumeshindikana, wao kama vijana walijiunga katika kikundi na kupatiwa fedha kutoka Tasaf kwa ajili ya kuanzisha mradi huo wa ufugaji wa mbuzi, ulioibuliwa katika mkutano wa hadhara mwaka 2009.

Philmon amesema kuwa  walipata shilingi milioni 11 kutoka Tasaf, na kununua mbuzi 105, ambapo  kila mmoja wao alipata mbuzi wanne, na kuwa sasa wana jumla ya  mbuzi 200, na kila mmoja amekwishafikisha mbuzi kumi.

Amesema kuwa jumla ya gharama ya mradi huo ni zaidi ya shilingi milioni 12.5 na kuwa mbali na fedha zilizotolewa na Tasaf, wananchi walichangia nguvu zao zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 1.5.

Amesema kuwa kutokana na ufugaji huo vijana  kumi miongoni mwao wameweza kuanzisha kilimo cha mazao mbalimbali katika shamba lenye ukubwa wa ekari nane, ikiwamo mashamba ya migomba ya kisasa, kahawa na magimbi.


Muleba yashauriwa kusogeza huduma za afya kwa wananchi


HALMASHAURI ya Wilaya ya Muleba mkoani Kagera imeshauriwa kusogeza huduma za afya  kwa wananchi  kwa kutekeleza mpango wa serikali  wa kujenga  zahanati kila kijiji sambamba na kuwa na mpango mkakati  wa kudhibiti  mlipuko wa malaria pindi unapotokea.
Ushauri huo ulitolewa na mkuu wa wilaya hiyo Lembris Kipuyo baada ya kutokea kwa mlipuko wa malaria wilayani humo  kipindi cha mwezi Mei na Juni mwaka huu na kusababisha vifo vya watoto wengi chini ya miaka mitano.
Kipuyo alisema kwa sasa katika wilaya hiyo maambukizi ya malaria ni asilimia 22 ambapo alidai kuwa kiwango hicho bado ni kikubwa na kuwataka watendaji na viongozi wote wa halmashauri hiyo kuhamasisha wananchi umuhimu wa kutumia vyandarua na kusafisha mazingira ili kuharibu mazalia ya mbu.
Alisema ni wajibu wa  halmashauri kuwasiliana na idara ya afya  ili iwapatie wataalam wa  afya wa kutosha yakiwemo madawa na vifaa tiba vya kutosha ili kukabiliana na tatizo la malaria katika wilaya hiyo.Chanzo:Tanzania Daima



Wasioendeleza vitalu vya madini kunyang`anywa

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo
Serikali  imetangaza kuwanyang'anya watu waliochukua vitalu vya uchimbaji madini bila kuviendeleza.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, alisema hayo jana wakati wa makabidhiano ya mgodi wa Tulawaka kwa Shirika la Madini la Taifa (Stamico), uliokuwa ukiendeshwa na kampuni ya African Barrick Gold (ABG).

Profesa Muhongo alisema kuna kampuni za nje na ndani zilizochukua vitalu vya madini na kuviacha kwa muda mrefu bila kuviendeleza na kuonya kuwa serikali itawanyang'anya na kuwapa wachimbaji wadogo.

Alisema taratibu za kisheria zimeanza kuchukuliwa ili watu wanaohodhi vitalu hivyo wanyang'anywe.

Aidha, alisema ABG na Stamico zimefikia makubaliano na mgodi wa Tulawaka kuanza uchimbaji wa madini na faida itakayopatikana hisa zitaanza kutolewa kwa Watanzania ili waweze kunufaika na rasilimali hiyo.

Alisema kuanzia sasa migodi yote mipya inayoanzishwa ni lazima serikali iwe na hisa ambazo zitakuwa zikisimamiwa na Stamico.

Profesa Muhongo alisema kilio cha wachimbaji wadogo serikali imekisikia na kuwatengea maeneo kwa ajili ya uchimbaji wa madini.

Alisema pia imekuwa ikiwapatia vifaa pamoja na mikopo kutoka benki ya rasilimali (TIB) ili waweze kufanyakazi zao katika mazingira bora pamoja na vijana hao kupata ajira ikiwa ni sehemu ya kukuza uchumi wao.

Alisema katika kuwasaidia wachimbaji madini wadogo, maeneo yatakayonyang’anywa watapewa ili kuyaendeleza.

Alisema kuna idadi kubwa ya wachimbaji madini wadogo na tayari serikali inawatambua kwa kuwaunganisha katika vyama vyao kuanzia ngazi za chini hadi ya taifa ili Stamico iweze kuwapatia mafunzo dhidi ya kazi yao.

Alisema kumekuwa na tatizo la ulipaji wa kodi kwa wachimbaji hao “Kwa mfano Mirerani zipo kampuni kama 595 lakini kampuni 10 ndizo zinalipa kodi, ndio maana huwa nasema muuguzi kwa mwaka analipa kodi kubwa zaidi ya mchimbaji wa madini,” alisema.

Profesa Muhongo alisema mikataba iliyosainiwa ipo wazi haifanywi kwa kificho kama inavyodaiwa.

Aliongezea kuwa kwa wale wabunge ambao wanataka kuiona mikataba wanaweza kuipata kwa Spika wa Bunge, Anne Makinda.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa bodi ya Stamico, Rumisha Kimambo, alisema amefurahishwa na tukio hilo na kuyatekeleza yote waliyotakiwa kuyasimamia.

 
CHANZO: NIPASHE

NI SIKU TATU TUU ZIMEBAKIA KUPATIKANA KWA MAMA SHUJAA WA CHAKULA , MPENDEKEZE SASA


Tshs. Milioni 5 Kushindaniwa

Kama unamfahamu mkulima yeyote mwanamke, mtanzania, mwenye umri wa miaka 18 na zaidi, anayelima mazao ya chakula, huu ni wakati wako sasa wa kumpa zawadi ya kufungia mwaka.

Kampeni ya Grow inayoendeshwa na shirika la kimataifa la Oxfam kupitia balozi wake Shamim Mwasha (Blogger 8020fashions) inatoa zawadi ya vifaa vya kilimo vyenye thamani ya Tshs. Milioni 5 pamoja na nafasi ya ushiriki katika shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2013 litakalofanyika sambamba na Maisha Plus.

Mpendekeze ashinde sasa kwa kubofya hapa na kujaza nafasi zote  surveymonkey.com/s/growtanzania

Zimebaki siku tatu tu kabla ya shindano kufungwa. Usikubali nafasi hii ikupite. 


Uongozi Kasharunga lawamani



WANAVIJIJI wa vijiji viwili wa kata ya Kasharunga, wilayani Muleba, mkoani Kagera, wameulalamikia uongozi wa vijiji hivyo kwa madai ya kuuza ardhi ya kijiji kinyume cha sheria huku wakishindwa kuwashirikisha wanakijiji hao kuhusu fedha za ruzuku za vijiji hivyo. Wakizungumza katika mkutano wa hadhara ulioitishwa na diwani wa kata hiyo, Khalid Hussein, wananchi hao walidai kuwa hawana imani na viongozi wao kwa kuwa wamekuwa wakiuza ardhi kwa watu wa mikoa mingine pasipo kuwashirikisha wanakijiji.
Wanakijiji hao walidai kuwa viongozi  hao wameshindwa kutoa taarifa za mapato na matumizi ambapo ardhi inayodaiwa kuuzwa ilitengwa kwa ajili ya kujenga wodi ya wagonjwa.
Akizungumzia suala hilo mtendaji wa kijiji cha Nkomero, Pastory Sulusi, alidai kuwa amekuwa akiandika muhtasari wa vikao mbalimbali vikiwemo vya uuzaji wa ardhi lakini umekuwa ukibadilishwa.
“Unakuta mkutano wa kijiji umeuza ardhi hekari tano lakini mwenyekiti amekuwa akibadilisha muhtasari na kuandika ya kwake huku akiwauzia hekari zaidi ya 150 bila kuishirikisha serikali ya kijiji na mkutano mkuu hata mtendaji mwenyewe,” alidai.
Akijibu tuhuma hizo kwa niaba ya Mwenyekiti Edward Kimanzi wa kijiji cha Nkomero, Angelo Mselika, ambaye alikaimu nafasi hiyo alisema tuhuma hizo amezisikia wamekuwa wakimshauri kiongozi huyo kuitisha mkutano lakini jambo hilo limeshindwa kutekelezwa.

Chanzo;Tanzania Daima

WE ARE PROMOTING DOMESTIC TOURISIM : GET TO KNOW ABOUT BHARAMULO GAME RESERVE



Biharamulo Game reserve is part of the North Western Tanzania's Big Game Hunting Reserves, which consists of Biharamulo, Burigi, Rumanyika Orugundu, and Ibanda Game Reserves in Kagera Region. The reserve is located adjacent to the southwest shore of Lake Victoria, covering an area of 1300 square kilometers.
The game reserve shares some of the eco-system with the adjacent Bugiri game reserve and off-shore island national park of Rubondo. Vegetation: The northern part of the reserve is dominated by brachystegia-miombo woodland reverine and savannah woodland


CLICK HERE FOR MORE INFORMATION

CAG amaliza kumkagua meya Bukoba



HATIMAYE Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh, amekamilisha kazi ya siku 35 ya ukaguzi wa tuhuma za ufisadi wa miradi zinazomkabili Meya wa Manispaa ya Bukoba, Anatory Amani.
Akizungumza na Tanzania Daima jana mjini Bagamoyo, mkoani Pwani, Utouh alisema katika ukaguzi huo wameweza kuwahoji wahusika wote pasipo kuacha mtu.
Utouh alisema kuwa wanatarajia kuweka hadharani ripoti hiyo baada ya wiki tatu kuanzia sasa.
Alisema kuwa wakaguzi watakwenda Bukoba kwa ajili ya kukamilisha hatua za mwisho za ripoti hiyo na baada ya hatua hiyo wataweka hadharani suala hilo.
“Hadi sasa kazi imeshakamilika na tuliwahoji wahusika wote, hivi sasa tupo katika hatua za mwisho za kukamilisha ripoti, hatutakuwa na siri, kila kitu kitawekwa hadharani,” alisema.
Timu ya wakaguzi hao ilianza kazi Septemba 30, mwaka huu, huku Utouh akiwaonya viongozi wote wanaotuhumiwa kwa namna moja au nyingine pamoja na watendaji wa manispaa hiyo kujiepusha na vitendo vyenye mwelekeo wa rushwa, akisema vinaweza kuvuruga mwenendo mzima wa ukaguzi huo.
Kamati hiyo ilifanya kazi kwa kuegemea hadidu 14 za rejea huku wakijikita katika maeneo husika kwa mwaka wa fedha 2010/11 hadi 2012/13.
Kwa mujibu wa Utouh, hadidu hizo ni kuchunguza usahihi wa utaratibu uliotumika kumpata mwekezaji wa kituo cha kuoshea magari, yaani Kampuni ya ACE Chemicals Ltd, kuchunguza uhalali wa nyaraka na kiasi kilichowekezwa cha sh milioni 297 kwenye mradi huo.
Nyingine ni kuchunguza tatizo na sababu zilizosababisha viwanja 800 kutogawiwa kwa wananchi waliochangia gharama za upimaji, mradi wa upimaji wa viwanja 5,000, mradi wa ujenzi wa soko na mradi wa kujenga kitegauchumi.
Aliongeza kuwa nyingine ni mradi wa ujenzi wa kituo cha mabasi, ujenzi wa chuo cha ualimu, kituo cha maarifa na ujenzi wa bwawa kwa ajili ya utalii.
Yalikuwepo pia masuala mengine ya matumizi ya fedha yanayoashiria ubadhirifu na wizi au ufujaji wa mali za halmashauri na kutoa ushauri kwa serikali kuhusu namna bora ya kuimarisha usimamizi wa mapato katika halmashauri hiyo.
Ukaguzi huo pia umegusa mradi wa maji wa Benki ya Dunia kwa ajili ya Kata ya Nyanga, kiwanja cha Shule ya Msingi Kiteyagwa, barabara ya kupitia Kagondo Kaifu hadi Kagondo Karagulu, ujenzi wa Soko Kuu la Manispaa ya Bukoba na Ilani ya Uchaguzi.
Chimbuko la mgogoro huo ni madiwani kumlalamikia meya wao kuwa ameiingiza manispaa katika ufisadi kwenye miradi kadhaa.
Miradi hiyo ni upimaji wa viwanja 5,000 unaodaiwa mkopo wake wa sh bilioni 2.9 kutoka Mfuko wa Dhamana ya Uwekezaji (UTT) haukufuata taratibu na wananchi hawakushirikishwa ipasavyo.
Tuhuma nyingine ni mradi wa ujenzi wa soko. Meya anadaiwa kusitisha malipo ya ushuru na kutaka kuwaondoa wafanyabiashara bila kufuata utaratibu.
Anatuhumiwa pia kukopa sh milioni 200 kutoka Benki ya Uwekezaji (TIB) bila kibali cha Baraza la Madiwani.
Vilevile alitoa taarifa kwenye kikao cha baraza hilo kuwa TIB iliwapa ruzuku ya sh milioni 90, lakini hakueleza misingi yake.
Upo pia mradi wa kuosha magari ambao unadaiwa kutumia kiasi cha sh milioni 297 zinazotiliwa shaka.
Ameshindwa pia kutoa mchanganuo wa mapato na matumizi ya mradi wa kiasi cha sh milioni 134 za ujenzi wa kituo cha mabasi.

Chanzo;Tanzania Daima

KAGERA YAKUSANYA MIL35 KILA MWEZI SOKO LA SAMAKI


SERIKALI mkoani Kagera inakusanya kati ya shilingi milioni 35 hadi 38 kila mwezi, kutokana na uuzwaji nje ya nchi samaki na dagaa waliokaushwa, wanaovuliwa katika ziwa Victoria

Afisa mfawidhi kitengo cha udhibiti ubora na usalama wa samaki na mazao yake katika mkoa wa Kagera, Monica Kishe amesema kuwa kwa mwezi Oktoba mwaka huu, ziliuzwa nje ya nchi tani 100 za samaki na tani kumi za dagaa wakavu na kuipatia serikali fedha za kigeni zaidi ya shilingi milioni 38.

Amezitaka halmashauri za wilaya ya Bukoba, Muleba na manispaa ya Bukoba, kushirikiana na wavuvi katika wilaya hizo kutunza mialo saba inayokarabatiwa na serikali kuu kwa gharama ya shilingi bilioni 28, ili kuongeza ubora na upatikanaji zaidi wa samaki.

Mialo iliyokarabatiwa ni Nyamukazi,  Igabilo, Rushara, Marehe, Kerebe, Iramba na Katembe, na kuwa gharama ya kila mwalo ni shilingi milioni 400.

Hata hivyo amesema pamoja na mapato hayo samaki katika ziwa Victoria wanaendelea kupungua kutokana na uvuvi haramu unaoendeshwa na baadhi ya wavuvi, ikiwamo kuvua kwa sumu, matumizi ya nyavu zisizoruhusiwa kisheria na vyandarua.

DC Misenyi adaiwa kuhujumu Hifadhi ya Taifa Minziro

Chapa
Mkuu wa Wilaya ya Misenyi mkoani Kagera, Kanali Mstaafu Issa Njiku
Mkuu wa Wilaya ya Misenyi mkoani Kagera, Kanali Mstaafu Issa Njiku na afisa maliasili Jamesi Matekere wanadaiwa kuhujumu Hifadhi ya Taifa ya Msitu wa Asili wa Minziro kwa kuruhusu tani zaidi ya 200,000 kuvunwa kwa kutoa vibali kwa wafanyabiashara isivyo halali.

Vijiji vilivyonufaika na vibali hivyo kwa kisingizio cha kujenga makanisa, vituo vya polisi, mahakama, matanki ya maji ni pamoja na kijiji cha Minziro, Nyakahanga, Kalagala, Kigazi, Kiwelu ambapo kila mfanyabiashara alitakiwa kutoa Sh. 200,000 za kutuma maombi bila kutolewa risiti.

Akiongea na NIPASHE, Mwalimu mkuu wa Shule ya Msingi Minziro, Mkama  Waswa, alisema ana kibali na. KGR/C.4/26/120 cha  22/01/2013 na kuwa walipofika wanajeshi, polisi na jamaa wa usalama wa taifa katika operesheni tokomeza ujangili walidai kibali hicho ni feki na kuwa endapo watampeleka mahakamani ataomba mkuu huyo wa wilaya aunganishwe katika kesi yake na afisa maliasili.

Akiongea na NIPASHE kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, msemaji wa wizara hiyo, Rumisha Chikamdi alisema ni makosa kutoa vibali katika hifadhi ya Minziro na kuwa wanaangalia uwezekano wa kuzuia vibali hivyo.

Kwa mujibu wa kibali cha serikali cha 22/01/2013 kumb. na. KGR/C.4/120 na kibali na. KGR/C.4/26/121 cha  25/01/2013, wakuu hao wameruhusu kupasuliwa mbao ndani ya hifadhi hiyo aina ya afrocarpus dawei (Podo), mimusups bagshawei na beilshrmedia ganaensis.

Wakiongea na NIPASHE kwa nyakati tofauti mkuu huyo wa wilaya, Njiku na Matekere wamekiri kutoa vibali vya uvunaji ndani ya msitu huo kwa maelezo kuwa sheria za misitu zinawalinda kwa kuwa mkuu wa wilaya hiyo ni Mwenyekiti wa kamati ya uvunaji. 

Uchunguzi umebaini kuwa baadhi ya viongozi wa serikali wilayani Misenyi kutoka Idara mbalimbali za serikali wakiwamo polisi na maliasili ndiyo wenye vijana wa kupasua mbao katika hifadhi hiyo ambapo huwalinda kuhakikisha wako salama muda wote.

Mbao za msitu huo huuzwa Bukoba na nchini Uganda ambapo maafisa maliasili huzigonga nyundo kuonyesha kuwa serikali imepokea kodi jambo ambalo siyo sahihi.

Kama alivyoeleza Mtendaji wa serikali ya kijiji cha Misenyi, Eliud Tibaijuka na Mwenyekiti wake, Bonifasi Lugemo, licha ya kuwa na vibali vingi katika kijiji chao hawajawahi kulipa ushuru wa kijiji, halmashauri na serikali kuu kama sheria za misitu zilivyoelekeza ili kibali kiweze kuwa halali.
 
CHANZO: NIPASHE
 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kagera Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa