Kilaini atoa neno la 2014
Alisema mwaka 2014, Watanzania wote wanapaswa kuilinda amani iliyopo hasa kipindi hiki cha mchakato wa kupata Katiba Mpya kwani wapo baadhi ya watu wachache wanaoonesha
Wanasiasa wamchefua January Makamba
Naibu
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Bw.January Makamba,
amekemea tabia ya baadhi ya wanasiasa nchini kutumia mkondo wa dini
kisiasa kwani hilo ni kosa
kubwa kwa mustakabali wa amani ya nchi.
Bw. Makamba aliyasema hayo juzi Mjini Bokoba, mkoani Kagera, wakati akizungumza kwenye Tamasha la Amani ambalo liliandaliwa na Nazareth Singers kwa kushirikiana na wadau mbalimbali.
Alisema wanasiasa wenye tabia hiyo wanaamini kuwa waumini wa dini yake watamuunga mkono katika uchaguzi jambo ambalo ni hatari kwa sababu anapogombea uongozi, wananchi ndio wanaopiga kura bila kujali dini zao.
Aliongeza kuwa, viongozi wa dini wamefanya kazi kubwa ya kulinusuru Taifa kutokana na chokochoko za kidini kupitia mahubiri yao kwani bila wao, hali ingekuwa mbaya zaidi.
Aliwaomba viongozi wa madhehebu ya dini nchini, kuendelea kuhubiri amani, upendo na mshikamano miongoni mwa Watanzania ili kudumisha amani iliyoasisiwa na Hayati Julius Nyerere.
"Baada ya kuibuka kwa
chochoko za kidini nchini, viongozi wa dini wamefanya kazi kubwa ya
kuhubiri amani, upendo na mshikamano miongoni mwa wananchi...mahubiri
yao
yamesaidia kupunguza chokochoko hizo," alisema.
Bw. Makamba alisema madhara ya Taifa kukosa amani ni makubwa na kusisitiza umuhimu wa wananchi kuheshimu imani za watu wengine.
Alikemea tatizo la ukosefu wa haki na usawa katika jamii juu ya upatikanaji wa huduma mbalimbali za msingi ikiwemo elimu na afya miongoni mwa Watanzania.
"Unapoona katika jamii
hakuna haki na usawa hilo ni tatizo,kwa mfano, ukiona kuna watu wanapata
elimu au huduma tofauti na wanayopata wengine, uhakika wa amani
unakuwa hatarini," alisema.
Aliwapongeza waandaaji wa tamasha hilo ambalo liliwakutanisha waumini wa dini mbalimbali mkoani humo na kusisitiza kuwa, ujumbe uliotolewa usambazwe nchi nzima.
Aliahidi kusaidiana na waandaaji hao kuhakikisha ujumbe huo wa amani unafika maeneo mbalimbali nchini.
Awali Mkuu wa Mkoa huo, Kanali mstaafu Fabian Massawe,alisema amani ya Tanzania ipo mashakani kutokana sababu mbalimbali kama malumbano ya kidini, kisiasa, matumizi ya dawa za kulevya kwa unyanyasaji wa kijinsia.
Chanzo;Majira
MISSENYI YATOA MIKOPO MIL 60
Halmashauri ya wilaya ya Missenyi mkoani Kagera
imetoa mikopo ya zaidi ya shilingi milioni 60.1 kwa vikundi mbalimbali vya
wanawake na vijana katika kipindi cha miaka sita iliyopita.
Taarifa iliyotolewa na mkurugenzi wa halmashauri
hiyo Elzaberth Kitundu imesema kuwa mikopo hiyo imetolewa kuanzia mwaka wa
fedha 2007/2008 hadi 2012/2013.
Kitundu amesema kuwa katika kipindi hicho vikundi
vya akina mama vilipatiwa mikopo ya zaidi ya shilingi milioni 40.8 ambapo
vikundi vya vijana vilipatiwa mikopo ya zaidi ya shilingi milioni 19.3.
Amesema kuwa lengo la halmashauri hiyo kuviwezesha
vikundi vya wanawake na vijana kwa kuwapatia mikopo ni kutaka
kuinua mitaji yao, na kuwa hali ya marejesho kwa vijana sio mbaya
isipokuwa kwa upande wa wanawake ndio wanarejesha kwa kusuasua.
Amesema kuwa katika kuhakikisha vikundi hivyo
vinakuwa endelevu, wamekuwa wakiwashauri wanachama wake kuanzisha vyama vya
akiba na mikopo (SACCOS) na kuwa katika wilaya hiyo hadi sasa kuna vyama vya
ushirika 73, vikiwamo vya mazao 28, Saccos 36 ambapo vyama tisa ni vya
mchanganyiko.
Wahamiaji warudi kwa kasi Kagera
Katika
hali isiyo ya kawaida, wahamiaji haramu waliorejeshwa nchini mwao na
serikali katika ‘Operesheni Kimbunga’ wameanza kurejea kwa wingi katika
Wilaya ya Kyerwa, mkoani Kagera wakijiita M23 na kupora mali za wananchi
kwa nguvu.
Mkuu wa Wilaya hiyo, Mhandisi Benedict Kitenga, aliyasema
hayo jana wakati akitoa taarifa kwa Mkuu wa Mkoa huo Kanali mstaafu,
Fabian Massawe ambaye alitembelea wilaya hiyo kukagua shughuli za
maendeleo na ujenzi wa maabara katika shule za sekondari za kata.
Alisema
wahamiaji hao wamejazana katika Kijiji na Kata ya Kibingo wakiwatisha
wananchi ambao hivi sasa wanahofia usalama wa maisha yao na mali zao.
Aliongeza
kuwa, baada ya Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya kupata taarifa
hizo, ilikwenda eneo la tukio na kufanya operesheni kubwa na kufanikiwa
kukamata wahamiaji haramu zaidi ya 20 na baadhi ya Watanzaia waliokuwa
wakiwahifadhi.
Mhandisi Kitenga alisema baada ya kukamatwa,
wahamiaji hao walirudishwa katika nchi zao bila kutaja uraia wao na
Watanzania waliohusika kuwahifadhi wamechukuliwa hatua za kisheria.
“Kutokana na hali ilivyo, wananchi wanapaswa kutoa taarifa wawaonapo wahamiaji haramu katika maeneo yao,” alisema.
Kwa
upande wake, Bw. Massawe alisema, katika “Operesheni Kimbunga”,
wahamiaji haramu walirudishwa katika nchi zao, lakini operesheni hiyo
inaendelea ili kuhakikisha waliobaki wanakamatwa na kurudishwa nchini
mwao.
“Chini ya Kaulimbiu ya Hakuna wa Kubaki na Hakuna wa Kurudi,
tutahakikisha kila mhamiaji haramu anaondoka na Watanzania ambao
watabainika kushirikiana nao pia watachukuliwa hatua za kisheria.
“Naiagiza
Kamati za Ulinzi na Usalama kuendelea na operesheni hadi wahamiaji
haramu wamalizike,” alisisitiza Bw. Massawe na kuwataka wananchi watoe
taarifa kwa viongozi wanapowaona na kutoa namba zake za simu.
Hata
hivyo, baadhi ya wananchi waliohojiwa walisema tatizo la wahamiaji
haramu linachangiwa na baadhi ya watendaji wa Serikali ngazi za chini
ambao wanachukua hongo na kuwarudisha.
Walisema inavyoonekana,
viongozi wa chini kuanzia ngazi ya vitongoji, vijiji hadi kata, wamepewa
mamlaka makubwa pia wamekuwa wakikaa muda mrefu bila kubadilishwa vituo
vya kazi na hivyo kujenga mazoea na wahamiaji hao.
“Serikali
kuanzia ngazi ya Wilaya, iwe na utamaduni wa kuwatembelea viongozi wa
vitongoji na kata kwa kushtukiza ili kukomesha tabia hii ambayo
wamejijengea na kuonekana miungu watu katika maeneo yetu,” alisema mkazi
wa eneo hilo ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini.
Hivi
karibuni Serikali ilifanya “Operesheni Kimbunga” na kushirikisha vyombo
mbalimbali vya ulinzi na usalama baada ya Rais Jakaya Kikwete kutoa wiki
mbili kwa wahamiaji haramu wawe wameondoka nchini kwa hiari yao.
Chanzo;Majira
Waziri Magufuli atajwa kesi ya wizi wa pembejeo
Waziri wa Ujenzi, Dk,John Magufuli
Hatua hiyo imefuatia Mahakama hiyo kuanza kupokea ushahidi wa upande wa mashitaka ukiongozwa na wakili wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Kelvin Murusuri.
Shahidi namba moja ambaye ni mchunguzi wa Takukuru, Said Bakari (39), alidai kuwa kwa kipindi cha mwaka 2010/11 washitakiwa hao walitenda makosa mbalimbali ikiwemo kutumia madaraka yao vibaya kisha kumteua wakala wa usambazaji wa pembejeo asiye na sifa.
Alisema mshitakiwa namba moja Nyembo ambaye alikuwa mkuu wa wilaya ya Chato kabla ya kuhamishiwa Uvinza, akiwa Mwenyekiti wa kamati ya pembejeo ya wilaya hiyo alihusika kuwapitisha wazabuni wa usambazaji wa pembeo wasio na sifa katika kikao kilichofanyika Julai 6, mwaka 2010.
Alidai kuwa mshitakiwa namba mbili Kwikwega anayetetewa na wakali wa kujitegemea Deogratias Rutahindurwa, alidaiwa mahakamani kupitisha baadhi ya nyaraka za kuwatambulisha mawakala waliopitishwa kinyume cha sheria na kamati ya pembejeo ya wilaya kwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera.
Wengine waliofikishwa mahakamani ni aliyekuwa Ofisa Kilimo na Mifugo wa wilaya hiyo, Dk. Pheres Tongora, ambaye pia aanashitakiwa kuteua na kuwapitisha mawakala wasio na sifa.
Wengine ni mshitakiwa namba nne aliyekuwa wakala wa usambazaji wa pembejeo kata ya Buseresere, Mery David pamoja na Kaimu mtendaji wa kijiji cha Mapinduzi, Mageni Mbassa.
Shahidi huyo aliwasilisha vielelezi vinne zikiwemo barua na mihutasari ya vikao vya kamati ya pembeo vilivyoketi na kupitisha maamuzi ya kuwapata mawalala wa usambazaji bila kufuata taratibu za manunuzi ya umma.
Baada ya mashahidi wa kwanza kumaliza kuwasilisha ushahidi wake, wakili wa Rutahindurwa alitaka kujua sababu za Waziri wa ujenzi na mbunge wa jimbo la Chato,Dk Magufuli kushindwa kuhusishwa katika mashitaka hayo licha ya kuwa mmoja wa wajumbe wa kamati ya pembejeo ya wilaya hiyo.
Alisema iwapo kamati ya pembejeo ilifanya maamuzi yasiyo fuata taratibu kanuni na sheria za manunuzi iweje baadhi ya wajumbe wake akiwemo Dk. Magufuli wasihusishwe kwenye mashitaka hayo.
Wakili anayemtetea Mery David,Tuguta Fadhili alihoji kuwa kama kesi hiyo ilifikishwa mahakamani hapo kutokana na shinikizo la Waziri wa Ujenzi Dk. Magufuli.
Alidai kuwa iwapo kikao cha kamati ya pembejeo kiliyoketi Julai 6, 2010 kilikuwa halali iweje maamuzi yake yaonekane hayakuwa sahihi na kumhusisha pia mshitakiwa namba mbili (Kikwega) ambaye siku ya kikao hicho hakuwapo katika maamuzi hayo.
Mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya hiyo, Jovith Katto baada ya upande wa washitakiwa kumaliza kuhoji maswali yao mahakama hiyo iliahilishwa kwa ajili ya kupokea ushahidi wa mashahidi namba mbili ambaye ni Ofisa Ugavi wa wilaya hiyo, Machage Mwema.
CHANZO:
NIPASHE
Ulaji wetu na maradhi ya kisukari-3
Tulijifunza katika makala mbili zilizopita kuwa binadamu hawezi kuishi bila ya kula vyakula vyenye wanga, mafuta na protini.
Njia za kuyakabili maradhi ya kisukari
Tunaweza kuyakabili maradhi ya kisukari kwa njia
kuu nne. Mosi, kuwa na elimu kuhusu maradhi ya kisukari na mtu kuwa na
uwezo wa kujipima kiwango cha sukari mwilini mwake.
Pili, ni kula mlo kamili, tatu kufanya mazoezi na nne ni kupata tiba sahihi ya maradhi ya kisukari.
Njia hizi ni muhimu kuzifahamu kwa wagonjwa wa
kisukari na wale ambao hawajapatwa na maradhi hayo, yanayoongezeka kwa
kasi duniani kutokana na maisha ya kisasa kama vile kula vyakula vyenye
mafuta, sukari na chumvi nyingi.
Kama umepatwa na kisukari
Ingawa maradhi ya kisukari yana kishindo kikubwa,
lakini watu waliopatwa na ugonjwa huo wanashauriwa wasichanganyikiwe
wala kuhuzunika. Kufanya hivyo ni kuongeza maradhi katika miili yao.
Wanachotakiwa ni kuukabili ugonjwa huo kwa
kujiamini. Na hilo litawezekana endapo wagonjwa hao wataelekeza nguvu
zao katika kuujua ugonjwa huo kwa undani.
Kujua huko kutawafanya wabadili mtindo wa maisha
yao kama vile kula mlo kamili, kufanya mazowezi, kuacha kunywa pombe,
kunywa maji ya kutosha, kulala muda wa kutosha, kudhibiti hasira na
msongo wa mawazo.
Wapi utapa elimu?
Elimu kuhusu maradhi ya kisukari inaweza
kupatikana kwa njia mbalimbali kama vile kusoma vitabu na magazeti,
kusoma katika mitandao ya kijamii, kuhudhuria semina, kusikiliza vipindi
vya mada hiyo kutoka katika redio na luninga.
Vilevile, elimu ya ugonjwa wa kisukari inaweza
kupatikana kwa wataalamu wa maradhi hayo waliopo katika kniniki za
kisukari na hospitali mbalimbali.
Baadhi ya wagonjwa wa kisukari pia, wanaelimu kubwa ya maradhi
hayo baada ya kuhangaika kwa muda mrefu kuitafuta elimu hiyo na uzoefu
wao wa maisha kama wagonjwa.
Kuujua ugonjwa wa kisukari
Kama tunavyofahamu, binadamu ameweza kuleta
mapinduzi makubwa katika maisha yake tangu enzi za zana za mawe mpaka
sasa, enzi za dijitali kutokana na elimu.
Ni dhahiri pia, kuwa tutaweza kuyakabili maradhi ya kisukari kikamilifu kama tutakuwa na uwelewa wa kutosha juu ya maradhi hayo.
Tufahamu nini kama wananchi?
Kujua tunakokukusudia hapa sio kama vile wanavyofahamu wataalamu wa afya.
Wananchi wajue maana ya ugonjwa wa kisukari, aina za kisukari, sababu za kupata maradhi ya kisukari na dalili za kisukari.
Halikadhalika, watu wanatakiwa watambue hali gani
mtu akiwa nayo (risk factors) yuko katika hatari ya kupata maradhi ya
kisukari kama vile unene uliopitiliza, kuwa na shinikizo la damu, kuwa
na msongo wa mawazo, ujauzito, kutokufanya mazoezi au kazi za kutoka
jasho, na kuwa na miaka arobaini au zaidi.
Zaidi ya hayo, watu wanatakiwa wazijue athari
mbaya za ugonjwa wa kisukari kama vile kuharibika kwa viungo vingine
mfano macho, viungo vya uzazi, figo, mishipa ya fahamu na moyo.
Chanzo;Mwananchi
Chanzo;Mwananchi
UWK: Wanawake pazeni sauti zenu
UMOJA wa Wanawake Wajane (UWK) Wilayani Karagwe umesema unyanyasaji
wa kijinsia katika jamii unaweza kutokomezwa iwapo wanawake watavunja
ukimya na kupaza sauti zao.
Akizungumza na waandishi wa habari jana mwenyekiti wa umoja huo,
Grace Mahumbuka, alisema kuwa unyanyasaji wa kijinsia utakoma ikiwa
wanawake watavunja ukimya na kupaza sauti zao na kuripoti matukio ya
kikatili.
Alisema kuwa baadhi ya wanawake na watoto wamekuwa wakifanyiwa
vitendo vya kikatili ikiwa ni pamoja na kubakwa, ukatili wa kingono,
kulawitiwa, ndoa za utotoni na kutakaswa kwa wajane lakini matukio hayo
yanashindwa kuripotiwa.
“Matukio ya unyanyasaji wa kijinsia ni sawa na majanga mengine ya
kitaifa, kwa wanawake wengi na baadhi ya watoto wamefanyiwa vitendo vya
kikatili,” alisema.
Alisema ukatili huo wa kijinsia unahusiana zaidi na vipigo kwa
wanawake kutoka waume zao na hata baadhi kujeruhiwa, kukatwa viungo
vyao vya mwili hali inayoweka rehani ubinadamu wao.
Alisema kuwa kuna umuhimu wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake
(TAMWA) kushirikiana na Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA)
kusambaza elimu vijijini ili kusaidia kupunguza matukio hayo.
Naye Diwani viti maalum (CCM) kata ya Kayanga, Joyce Mirembe
aliwataka waandishi wa habari kuhakikisha hawaegemei upande wowote
wanaporipoti matukio hayo.
Alisema mfumo wa kisheria uliopo unaoonekana kutokuwa na usawa
huchangia wanawake kufanyiwa vitendo hivyo kushindwa kuchukua hatua za
kisheria.
Chanzo;Tanzania Daima
UMOJA wa Wanawake Wajane (UWK) Wilayani Karagwe umesema unyanyasaji
wa kijinsia katika jamii unaweza kutokomezwa iwapo wanawake watavunja
ukimya na kupaza sauti zao.
Akizungumza na waandishi wa habari jana mwenyekiti wa umoja huo,
Grace Mahumbuka, alisema kuwa unyanyasaji wa kijinsia utakoma ikiwa
wanawake watavunja ukimya na kupaza sauti zao na kuripoti matukio ya
kikatili.
Alisema kuwa baadhi ya wanawake na watoto wamekuwa wakifanyiwa
vitendo vya kikatili ikiwa ni pamoja na kubakwa, ukatili wa kingono,
kulawitiwa, ndoa za utotoni na kutakaswa kwa wajane lakini matukio hayo
yanashindwa kuripotiwa.
“Matukio ya unyanyasaji wa kijinsia ni sawa na majanga mengine ya
kitaifa, kwa wanawake wengi na baadhi ya watoto wamefanyiwa vitendo vya
kikatili,” alisema.
Alisema ukatili huo wa kijinsia unahusiana zaidi na vipigo kwa
wanawake kutoka waume zao na hata baadhi kujeruhiwa, kukatwa viungo
vyao vya mwili hali inayoweka rehani ubinadamu wao.
Alisema kuwa kuna umuhimu wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake
(TAMWA) kushirikiana na Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA)
kusambaza elimu vijijini ili kusaidia kupunguza matukio hayo.
Naye Diwani viti maalum (CCM) kata ya Kayanga, Joyce Mirembe
aliwataka waandishi wa habari kuhakikisha hawaegemei upande wowote
wanaporipoti matukio hayo.
Alisema mfumo wa kisheria uliopo unaoonekana kutokuwa na usawa
huchangia wanawake kufanyiwa vitendo hivyo kushindwa kuchukua hatua za
kisheria.
Chanzo;Tanzania Daima `Sheria ya kuzuia shughuli za siasa vyuoni itazamwe upya`
Mwenyekiti mstaafu wa CCM mkoani Kagera,Pius Ngeze.
Ushauri huo ulitolewa na mwakilishi wa wanachuo wa Chuo Kikuu cha St. Augustine (Saut) tawi la Sokoine Kampasi ya Bukoba, wakati wa hafla ya kukabidhi kadi za Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa wanachuo 42 wa chuo hicho waliojiunga na chama hicho.
Risala ya wanachuo hicho ilisomwa na mwakilishi wao, Silas Malima, mbele ya mgeni rasmi, Mwenyekiti mstaafu wa CCM mkoani Kagera, Pius Ngeze.
Malima alisema wanakabiliana na changamoto ya Sheria Vyuo Vikuu Namba 7 ya mwaka 2005.
Kwa mujibu wa Malima, sheria hiyo inayozuia kufanya mikutano na shughuli za vyama vya siasa ndani ya maeneo ya chuo.
Kwa msingi huo, Malima aliishauri serikali kuitazama upya sheria hiyo kwa lengo la kuirekebisha.
Kwa upande wake, mgeni rasmi Mwenyekiti mstaafu wa CCM mkoani Kagera, Ngeze, mbali ya kukabidhi kadi hizo kwa wanachama wapya 42 wa chuoni hapo, pia aliwataka wanachama hao wapya pamoja na wa zamani, kuhakikisha kwamba wanawaeleza wananchi mafanikio yaliyopatikana katika kutekeleza Ilani ya Uchaguzi.
Ngeze alisema vile vile, viongozi wa Chama wanapaswa kuwaeleza wananchi ukweli huo kwani vinginevyo viongozi wa upinzani watawaeleza na kupindisha mafanikio hayo au kuyafanya ni yao.
Ngeze aliyataja baadhi ya mafanikio hayo yalifanywa na serikali chini ya CCM kuwa ni pamoja na usambazaji wa umeme vijijini na mijini, usambazaji wa maji safi na salama mijini na vijijini, mawasiliano ya simu, ujenzi wa barabara za lami na changarawe vijijini na mijini.
Mengine ni usafiri na usafirishaji wa barabara, reli na anga, upanuzi na uboreshaji wa elimu ya msingi, sekondari, vyuo na vyuo vikuu.
Aidha, Ngeze alisema jukumu la tawi la CCM katika vyuo vikuu hususani tawi la Saut Bukoba, ni pamoja na kujenga na kukiimarisha Chama ndani ya Jumuiya ya Chuo Kikuu; kuongeza idadi ya wanachama na kufanya vikao kwa mujibu wa katiba.
Pia aliwataka viongozi na wanachama waendelee kujiendeleza ili kuwaongoza watu; wasome magazeti wasikilize redio, waangalie televisheni na washiriki majadiliano mbalimbali.
CHANZO:
NIPASHE
Mhandisi adaiwa kumuua afisa mauzo wa Sigara
Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania,(IGP) Said Mwema
Kaimu Kamanda wa polisi mkoani Kagera, Henry Mwaibambe, alimtaja aliyeuawa kuwa ni Hassan Mhongoli (38) na kuwa mauaji hayo yalitokea Jumamosi iliyopita saa 3:45 usiku katika eneo la hoteli ya Bukoba Coop inayomilikiwa na Chama Kikuu cha Ushirika mkoani Kagera (KCU 1990 Ltd).
Mwaibambe alisema kuwa kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo kumetokana na taarifa kutoka kwa raia wema ambapo walianza kumfuatilia na kufanikiwa kumkamata juzi saa 9:00 mchana akiwa amejificha nyumbani kwake eneo la Uzunguni katika Manispaa ya Bukoba.
Alisema baada ya kumkamata alionyesha bastola aina ya Glock yenye namba PCH589 anayoimiliki kihalali ambayo inadaiwa aliitumia katika mauaji hayo na kudai kuwa alifikia uamuzi huo baada ya kupigwa ngumi na marehemu.
Alisema kuwa kampuni ya Sigara siku hiyo walikuwa na sherehe ya familia ambayo ilimalizika saa moja jioni na kwamba baadhi ya wafanyakazi waliondoka katika eneo hilo na kumwacha Hassan akiwa na mfanyakazi mwenzake, Amon Lyimo (40).
Alisema watu hao walikaa katika hoteli hiyo hadi saa 3:45 ndipo waliingia katika gari la kampuni, lakini walipoanza kuondoka ghafla ilitokea teksi na kuziba njia. Alisema walipiga honi, lakini haikuwapisha.
Alisema kutokana na kitendo hicho wafanyakazi hao wa Sigara walishuka katika gari na kuanza kuzozana na waliokuwa katika gari hilo na kwamba baadaye alishuka mtu mmoja na kuanza kupigana nao na baadaye kutoa bastola na kumpiga risasi Hassan kichwani na kufariki dunia papo hapo.
Alisema katika purukushani hizo mfanyakazi mwingine wa Sigara, Amon Lyimo, alitaka kuwamua, lakini naye alipigwa risasi mkono wa kulia na ametibiwa katika Hospitali ya Mkoa na kuruhusiwa jana.
Mwaibambe alisema Polisi wanaendelea na uchunguzi na kuwa bastola hiyo ilikutwa na risasi tano na waliokota maganda mawili ya risasi eneo la tukio.
Mwili wa marehemu baada ya kufanyiwa uchunguzi umehifadhiwa katika Hospitali ya Mkoa wa Kagera ukisubiri kuchukuliwa na ndugu na jamaa kwa ajili ya mazishi.
CHANZO:
NIPASHE
Maofisa ugani watakiwa kuwa na mavazi ya shamba
MKUU wa Wilaya ya Muleba, Lembris Kipuyo, amewaagiza maofisa ugani
wa halmashauri hiyo kuwa na mavazi ya shambani yaliyowekewa nembo ili
watambulike kwa wakulima.
Kipuyo alitoa agizo hilo katika kongamano la mtandao wa vikundi vya
wakulima wadogowadogo (Mviwata) mkoani Kagera la kuibua changamoto za
kilimo lililofanyika wilayani hapa.
Mkuu huyo wa wilaya (DC), alisema lengo la kutaka kuwepo na vazi
maalum la kuwatambua maofisa ugani linatokana na maafisa ugani walio
vijijini kufanana na wakulima, hivyo kuwapa wakati mgumu baadhi ya
wakulima kuwatambua pindi wanapowahitaji.
Alisema wataalam hao wa kilimo ni wachache katika halmashauri hiyo
yenye vijiji 161 ambao hawatoshelezi mahitaji ya wakulima kwa wakati
kutokana na ukosefu wa miundombinu ya usafiri.
Alisema wilaya hiyo iko kwenye mkakati wa kuwawezesha maofisa ugani
wachache ambapo mmoja ataweza kuhudumia vijiji vitatu na kuwafikia
wakulima kwa ukaribu zaidi kwa kuwapatia pikipiki.
Alisema mpango huo utasaidia ukusanyaji wa takwimu za kilimo kupitia
maafisa ugani kwa kuwezeshwa usafiri na vitendea kazi vya kutosha.
Mbali na hilo, aliwatahadharisha wakulima kuhusu kuhifadhi mazingira
na kuwataka kuacha tabia ya kulima kwenye vyanzo vya maji.
Chanzo;Tanzania Daima Wafugaji wawasusia DC,DAS
Mbunge wa Kahama,James Lembeli,
Kamati hiyo ipo wilayani Biharamulo, mkoani Kagera kusikiliza na kuchunguza athari zilizotokana na operesheni hiyo ikiongozwa na Mwenyekiti wake ambaye pia ni Mbunge wa Kahama, James Lembeli, na jana ililazimika kuzungumza na kusikiliza hoja za wafugaji bila viongozi hao kuwapo.
Mbali na kuwakataa viongozi hao, walisema uongozi mzima wa wilaya hiyo kwa kushirikiana na askari wa hifadhi ya wanyamapoli na Jeshi la Polisi, ndiyo walikuwa mstari wa mbele kuwahujumu wafugaji wakati wa operesheni hiyo.
Mwenyekiti wa chama hicho, Juvenary Mlashani, alisema licha ya Rais Jakaya Kikwete, kusitisha operesheni hiyo kutokana na baadhi ya viongozi kukiuka taratibu na madhumuni yake, jambo la kushangaza zoezi hilo kwa wilaya ya Biharamulo linaendelea.
Alisema viongozi hao wamekuwa wakipuuza kwa makusudi maagizo ya Rais Kikwete kutokana na kutafuta maslahi binafsi. Projestus Rutimwa, alisema kuwa suala la ufugaji wa ng’ombe ndani ya Hifadhi ya Biharamulo hautakwisha iwapo viongozi waliopewa dhamana na serikali wataendelea kuomba na kupokea rushwa kutoka kwa wafugaji.
CHANZO:
NIPASHE
Mwalimu jela miaka saba kwa kumkata kiganja mwanafuzi
Mwalimu
wa Shule ya Sekondari Rwambai Wilaya ya Karagwe mkoani Kagera, Alliamin
Mtabuzi (25), amehukumiwa kifungo cha miaka saba jela baada ya
kupatikana na kosa la kumkata kiganja cha mkono mwanafunzi wake wa
kidato cha nne.
Mtabuzi alipatikana na kosa la kumsababishia ulemavu mwanafunzi huyo, Annocietha Theobart (16), kutokana na wivu wa mapenzi.
Mbali ya kifungo hicho, pia ameamriwa kumlipa mlalamikaji huyo fidia ya Shilingi milioni tano.
Hukumu hiyo ilitolewa na Novemba 27, mwaka huu na Jaji Peragia Hadai wa Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba.
Akitoa hukumu hiyo, Jaji Hadai alisema itakuwa fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hiyo.
Awali, Wakili wa Serikali, Safina Simba, alidai kuwa mshatakiwa alitenda kosa hilo mwaka 2008 katika kijiji cha Rwambai wilayani Karagwe nyumbani kwa mlalamikaji kwa madai kwamba mwanafuzi huyo alikuwa na mchumba mwingine.
Baada ya kufika nyumbani hapo, mshtakiwa alianza kumshabulia mama mzazi wa mlalamkaji kabla ya kumshambulia malalamikaji kwa panga na kumkata kiganja cha mkono wa kulia pamoja na kidole cha mkono wa kushoto.
Hata hivyo, mwanafunzi huyo katika ushahidi wake alidai mahakamani hapo kuwa hakuwa na makubaliano ya uchumba na mshtakiwa.
Naye wakili wa utetezi, Alliamini Chamani, alidai kuwa mahakama inastahili kumpunguzia adhabu mshtakiwa kwa kuzingatia kuwa alikuwa mchumba wa mlalamkaji kwa makubaliano angemuoa baada ya kumaliza shule.
Alidai kuwa mshtakiwa huyo alikuwa akimgharimia mlalamikaji karo ya shule na mahitaji mengine yote muhimu hivyo alikasirishwa baada ya kubaini alikuwa na mchumba mwingine.
Hata hivyo, Mahakama iliotupilia mbali utetezi huo na kumpa mshtakiwa adhabu ya kifungo cha miaka saba pamoja na kumlipa mlalamikaji fidia ya Sh.milioni 5.
Mtabuzi alipatikana na kosa la kumsababishia ulemavu mwanafunzi huyo, Annocietha Theobart (16), kutokana na wivu wa mapenzi.
Mbali ya kifungo hicho, pia ameamriwa kumlipa mlalamikaji huyo fidia ya Shilingi milioni tano.
Hukumu hiyo ilitolewa na Novemba 27, mwaka huu na Jaji Peragia Hadai wa Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba.
Akitoa hukumu hiyo, Jaji Hadai alisema itakuwa fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hiyo.
Awali, Wakili wa Serikali, Safina Simba, alidai kuwa mshatakiwa alitenda kosa hilo mwaka 2008 katika kijiji cha Rwambai wilayani Karagwe nyumbani kwa mlalamikaji kwa madai kwamba mwanafuzi huyo alikuwa na mchumba mwingine.
Baada ya kufika nyumbani hapo, mshtakiwa alianza kumshabulia mama mzazi wa mlalamkaji kabla ya kumshambulia malalamikaji kwa panga na kumkata kiganja cha mkono wa kulia pamoja na kidole cha mkono wa kushoto.
Hata hivyo, mwanafunzi huyo katika ushahidi wake alidai mahakamani hapo kuwa hakuwa na makubaliano ya uchumba na mshtakiwa.
Naye wakili wa utetezi, Alliamini Chamani, alidai kuwa mahakama inastahili kumpunguzia adhabu mshtakiwa kwa kuzingatia kuwa alikuwa mchumba wa mlalamkaji kwa makubaliano angemuoa baada ya kumaliza shule.
Alidai kuwa mshtakiwa huyo alikuwa akimgharimia mlalamikaji karo ya shule na mahitaji mengine yote muhimu hivyo alikasirishwa baada ya kubaini alikuwa na mchumba mwingine.
Hata hivyo, Mahakama iliotupilia mbali utetezi huo na kumpa mshtakiwa adhabu ya kifungo cha miaka saba pamoja na kumlipa mlalamikaji fidia ya Sh.milioni 5.
CHANZO:
NIPASHE