UMOJA wa Wanawake Wajane (UWK) Wilayani Karagwe umesema unyanyasaji
wa kijinsia katika jamii unaweza kutokomezwa iwapo wanawake watavunja
ukimya na kupaza sauti zao.
Akizungumza na waandishi wa habari jana mwenyekiti wa umoja huo,
Grace Mahumbuka, alisema kuwa unyanyasaji wa kijinsia utakoma ikiwa
wanawake watavunja ukimya na kupaza sauti zao na kuripoti matukio ya
kikatili.
Alisema kuwa baadhi ya wanawake na watoto wamekuwa wakifanyiwa
vitendo vya kikatili ikiwa ni pamoja na kubakwa, ukatili wa kingono,
kulawitiwa, ndoa za utotoni na kutakaswa kwa wajane lakini matukio hayo
yanashindwa kuripotiwa.
“Matukio ya unyanyasaji wa kijinsia ni sawa na majanga mengine ya
kitaifa, kwa wanawake wengi na baadhi ya watoto wamefanyiwa vitendo vya
kikatili,” alisema.
Alisema ukatili huo wa kijinsia unahusiana zaidi na vipigo kwa
wanawake kutoka waume zao na hata baadhi kujeruhiwa, kukatwa viungo
vyao vya mwili hali inayoweka rehani ubinadamu wao.
Alisema kuwa kuna umuhimu wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake
(TAMWA) kushirikiana na Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA)
kusambaza elimu vijijini ili kusaidia kupunguza matukio hayo.
Naye Diwani viti maalum (CCM) kata ya Kayanga, Joyce Mirembe
aliwataka waandishi wa habari kuhakikisha hawaegemei upande wowote
wanaporipoti matukio hayo.
Alisema mfumo wa kisheria uliopo unaoonekana kutokuwa na usawa
huchangia wanawake kufanyiwa vitendo hivyo kushindwa kuchukua hatua za
kisheria.
Chanzo;Tanzania Daima

0 comments:
Post a Comment