HALI ya hewa na mandhari ya Mkoa wa Kagera imeelezwa kuwa ni
kivutio kwa wawekezaji katika sekta mbalimbali zikiwemo za kilimo,
ufugaji na viwanda.
Kauli hiyo ilitolewa mjini hapa juzi na Balozi wa China nchini
Tanzania, Dk. Lu Youging katika kikao cha Mkuu wa Mkoa wa Kagera,
Kanali mstaafu Fabian Massawe kilichokuwa kikielezea fursa za
uwekezaji mkoani hapo.
Dk. Youging alisema Mkoa wa Kagera una ardhi nzuri yenye rutuba
inayofaa kwa kilimo licha ya kuwepo kwa vyanzo mbalimbali vya maji
ambavyo husaidia katika kilimo cha umwagiliaji bila kusubiri kipindi
cha masika.
Alisema pia mkoa wa Kagera una sehemu nzuri ya utalii ambayo ni fursa nzuri ya kuendeleza na kuinua uchumi wa mkoa.
Alisema pamoja na kuwepo kwa fursa nyingi za uwekezaji mkoani hapo,
bado soko si zuri na kueleza kuwa soko likiwa zuri wawekezaji zaidi
watajitokeza.
Chanzo:Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment