MKUU
wa Mkoa wa Kagera, Kanali mstaafu Fabian Massawe, amesema zaidi ya sh
milioni 500 zinahitajika kukamilisha sherehe za kuwasha mwenge kitaifa,
Mei 2, mwaka huu.
Kanali Massawe aliwaomba wadau walioahidi kuchangia katika sherehe
hiyo kukabidhi michango yao mapema ili maandalizi yaweze kukamilika.
Akizungumza na waandishi wa habari mkoani hapa hivi karibuni, Kanali
Massawe alisema sherehe hizo zitafanyika katika Uwanja wa Kaitaba na
mgeni rasmi atakuwa Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilali.
Alisema wakati wa mbio za mwenge, miradi mbalimbali ya kiuchumi na
kijamii itazinduliwa ambapo kwa sasa wanaendelea kuorodhesha miradi hiyo
katika kila wilaya.
Kanali Massawe alisema baada ya mwenge kuwashwa, mbio zake zitaanza katika Manispaa ya Bukoba na kumalizia Wilaya ya Biharamulo.
“Naishukuru sana serikali kuona umuhimu wa mwenge wa uhuru kuwashwa
Kagera kwa lengo la kuchochea maendeleo ya wananchi,” alisema Massawe.
Alisema wananchi wanatakiwa kujitokeza kwa wiki kuupokea mwenge huo
na kusema kuwa patakuwepo na michezo mbalimbali katika sherehe hizo.
Chanzo:Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment