MKURUGENZI wa Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo, mkoani Kagera,
Nassibu Mmbaya, ametoa onyo kwa wafugaji wanaovamia misitu wilayani
hapa na kutaka waache mara moja tabia hiyo.
Mmbaya alitoa onyo hilo juzi alipozungumza na waandishi wa habari ofisini kwake.
Alisema wafugaji hao ambao wanavamia misitu wilayani hapa wanatoka
sehemu mbalimbali ikiwemo Geita, Kahama, Bariadi pamoja na maeneo
mengine nchini.
Alisema kadrii siku zinavyozidi kwenda misitu hiyo itazidi kupukutika kutokana na wafugaji hao kuongezeka.
"Wafugaji hawa wanaingia Biharamulo kwa lengo la kuishi, lakini cha
kushangaza wamekuwa ni watu wa kuvamia maeneo ya misitu, ukiwemo ule
wa Kasindaga.
“Hili jambo linasababisha uharibu wa misitu ikiwa ni pamoja na kutokea mmonyoko wa udongo," alisema mkurugenzi huyo.
Alisema ili kudhibiti uvamizi huo, tayari halmashauri yake
imeshaanzisha operesheni maalumu ya kuwaondoa wafugaji hao katika maeneo
yasiyoruhusiwa.
Chanzo;Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment