IMEELEZWA kuwa wajawazito wengi wanapoteza maisha wakati wa kujifungua kutokana na umaskini wa kipato.
Kauli hiyo ilitolewa juzi na Muuguzi Mkuu wa Wilaya ya Biharamulo, mkoani Kagera, Revocatus Dominick, alipozungumza na Tanzania Daima Jumapili lilipomtembelea ofisini kwake.
Alisema, umbali wa vituo vya afya ni sababu inayochangia kwa kuwa
wengi wao wanakosa fedha za usafiri wa kwenda kwenye vituo hivyo au
hospitali.
“Umaskini unasababisha wanawake wengi kufariki dunia wakati wa
kujifungua… watoto hufia tumboni mwa mama zao kwa vile wanachelewa
kufika hospitalini,” alisema Dominick.
Awali aliwataka wanaume kuwasindikiza wake zao kliniki wakati wa
ujauzito ili kwenda kupata ushauri na maelekezo kutoka kwa wataalamu wa
afya wakiwa pamoja.
“Sababu nyingine ni uelewa mdogo wa jamii kuhusu elimu sahihi ya afya
ya uzazi, ukarimu wa wahudumu, jambo linalochangia wajawazito wengi
kutofika kwenye vituo vya afya,” alisema.
Chanzo:Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment