Wahamiaji haramu 32 raia wa Burundi wamekamatwa na idara ya uhamiaji
mkoni Kagera wakidaiwa kuingia nchini kinyume na sheria.
Afisa uhamiaji mkoani Kagera, George Kombe amesema kuwa
wahamiaji hao walikamatwa jana kutokana baada ya kupata taarifa kutoka
kwa raia wema .
Kombe amesema kuwa wahamiaji hao haramu walikuwa wakisafirishwa kwa gari
aina ya Hiace lenye namba T633 CPZ , na kuwa walipohojiwa baadhi yao walisema
walikuwa wakielekea nchini Burundi huku wengine wakidai walikuwa wakielekea
kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu mkoani Kigoma.
Amesema kuwa utaratibu wa kuwasafirisha wote hadi mpakani mwa nchi yao
umekamilika na kuahidi kumchukulia hatua za kisheria dereva wa gari
hilo kutokana na kuwasaidia wahamiaji haramu hao kuingia nchini
kinyume na sheria.
Baadhi ya wahamiaji hao walipohojiwa na vyombo vya habari
wamesema kuwa wametoroka kutoka kambi ya wakimbizi ya Nyakivary
nchini Uganda kutokana na hali ya maisha kuwa ngumu.
0 comments:
Post a Comment