|
|
|
|
CAG amaliza kumkagua meya Bukoba
KAGERA YAKUSANYA MIL35 KILA MWEZI SOKO LA SAMAKI
SERIKALI
mkoani Kagera inakusanya kati ya shilingi milioni 35 hadi 38 kila
mwezi, kutokana na uuzwaji nje ya nchi samaki na dagaa waliokaushwa,
wanaovuliwa katika ziwa Victoria
Hata
hivyo amesema pamoja na mapato hayo samaki katika ziwa Victoria
wanaendelea kupungua kutokana na uvuvi haramu unaoendeshwa na baadhi
ya wavuvi, ikiwamo kuvua kwa sumu, matumizi ya nyavu zisizoruhusiwa
kisheria na vyandarua.
DC Misenyi adaiwa kuhujumu Hifadhi ya Taifa Minziro
B-pepe
Chapa
Mkuu wa Wilaya ya Misenyi mkoani Kagera, Kanali Mstaafu Issa Njiku
Mkuu
wa Wilaya ya Misenyi mkoani Kagera, Kanali Mstaafu Issa Njiku na afisa
maliasili Jamesi Matekere wanadaiwa kuhujumu Hifadhi ya Taifa ya Msitu
wa Asili wa Minziro kwa kuruhusu tani zaidi ya 200,000 kuvunwa kwa kutoa
vibali kwa wafanyabiashara isivyo halali.
Vijiji vilivyonufaika na vibali hivyo kwa kisingizio cha kujenga makanisa, vituo vya polisi, mahakama, matanki ya maji ni pamoja na kijiji cha Minziro, Nyakahanga, Kalagala, Kigazi, Kiwelu ambapo kila mfanyabiashara alitakiwa kutoa Sh. 200,000 za kutuma maombi bila kutolewa risiti.
Akiongea na NIPASHE, Mwalimu mkuu wa Shule ya Msingi Minziro, Mkama Waswa, alisema ana kibali na. KGR/C.4/26/120 cha 22/01/2013 na kuwa walipofika wanajeshi, polisi na jamaa wa usalama wa taifa katika operesheni tokomeza ujangili walidai kibali hicho ni feki na kuwa endapo watampeleka mahakamani ataomba mkuu huyo wa wilaya aunganishwe katika kesi yake na afisa maliasili.
Akiongea na NIPASHE kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, msemaji wa wizara hiyo, Rumisha Chikamdi alisema ni makosa kutoa vibali katika hifadhi ya Minziro na kuwa wanaangalia uwezekano wa kuzuia vibali hivyo.
Kwa mujibu wa kibali cha serikali cha 22/01/2013 kumb. na. KGR/C.4/120 na kibali na. KGR/C.4/26/121 cha 25/01/2013, wakuu hao wameruhusu kupasuliwa mbao ndani ya hifadhi hiyo aina ya afrocarpus dawei (Podo), mimusups bagshawei na beilshrmedia ganaensis.
Wakiongea na NIPASHE kwa nyakati tofauti mkuu huyo wa wilaya, Njiku na Matekere wamekiri kutoa vibali vya uvunaji ndani ya msitu huo kwa maelezo kuwa sheria za misitu zinawalinda kwa kuwa mkuu wa wilaya hiyo ni Mwenyekiti wa kamati ya uvunaji.
Uchunguzi umebaini kuwa baadhi ya viongozi wa serikali wilayani Misenyi kutoka Idara mbalimbali za serikali wakiwamo polisi na maliasili ndiyo wenye vijana wa kupasua mbao katika hifadhi hiyo ambapo huwalinda kuhakikisha wako salama muda wote.
Mbao za msitu huo huuzwa Bukoba na nchini Uganda ambapo maafisa maliasili huzigonga nyundo kuonyesha kuwa serikali imepokea kodi jambo ambalo siyo sahihi.
Kama alivyoeleza Mtendaji wa serikali ya kijiji cha Misenyi, Eliud Tibaijuka na Mwenyekiti wake, Bonifasi Lugemo, licha ya kuwa na vibali vingi katika kijiji chao hawajawahi kulipa ushuru wa kijiji, halmashauri na serikali kuu kama sheria za misitu zilivyoelekeza ili kibali kiweze kuwa halali.
Vijiji vilivyonufaika na vibali hivyo kwa kisingizio cha kujenga makanisa, vituo vya polisi, mahakama, matanki ya maji ni pamoja na kijiji cha Minziro, Nyakahanga, Kalagala, Kigazi, Kiwelu ambapo kila mfanyabiashara alitakiwa kutoa Sh. 200,000 za kutuma maombi bila kutolewa risiti.
Akiongea na NIPASHE, Mwalimu mkuu wa Shule ya Msingi Minziro, Mkama Waswa, alisema ana kibali na. KGR/C.4/26/120 cha 22/01/2013 na kuwa walipofika wanajeshi, polisi na jamaa wa usalama wa taifa katika operesheni tokomeza ujangili walidai kibali hicho ni feki na kuwa endapo watampeleka mahakamani ataomba mkuu huyo wa wilaya aunganishwe katika kesi yake na afisa maliasili.
Akiongea na NIPASHE kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, msemaji wa wizara hiyo, Rumisha Chikamdi alisema ni makosa kutoa vibali katika hifadhi ya Minziro na kuwa wanaangalia uwezekano wa kuzuia vibali hivyo.
Kwa mujibu wa kibali cha serikali cha 22/01/2013 kumb. na. KGR/C.4/120 na kibali na. KGR/C.4/26/121 cha 25/01/2013, wakuu hao wameruhusu kupasuliwa mbao ndani ya hifadhi hiyo aina ya afrocarpus dawei (Podo), mimusups bagshawei na beilshrmedia ganaensis.
Wakiongea na NIPASHE kwa nyakati tofauti mkuu huyo wa wilaya, Njiku na Matekere wamekiri kutoa vibali vya uvunaji ndani ya msitu huo kwa maelezo kuwa sheria za misitu zinawalinda kwa kuwa mkuu wa wilaya hiyo ni Mwenyekiti wa kamati ya uvunaji.
Uchunguzi umebaini kuwa baadhi ya viongozi wa serikali wilayani Misenyi kutoka Idara mbalimbali za serikali wakiwamo polisi na maliasili ndiyo wenye vijana wa kupasua mbao katika hifadhi hiyo ambapo huwalinda kuhakikisha wako salama muda wote.
Mbao za msitu huo huuzwa Bukoba na nchini Uganda ambapo maafisa maliasili huzigonga nyundo kuonyesha kuwa serikali imepokea kodi jambo ambalo siyo sahihi.
Kama alivyoeleza Mtendaji wa serikali ya kijiji cha Misenyi, Eliud Tibaijuka na Mwenyekiti wake, Bonifasi Lugemo, licha ya kuwa na vibali vingi katika kijiji chao hawajawahi kulipa ushuru wa kijiji, halmashauri na serikali kuu kama sheria za misitu zilivyoelekeza ili kibali kiweze kuwa halali.
CHANZO: NIPASHE
Operesheni Kimbunga yatumika kutapeli
WANANCHI wa maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Bukoba
vijijini mkoani Kagera wamekumbwa na taharuki kubwa baada ya askari
mgambo kujifanya maofisa wa Operesheni Kimbunga awamu ya tatu, huku
wakijitambulisha kama maofisa Usalama wa Taifa na Mamlaka ya Mapato Tanzania
(TRA).
Kwa mujibu wa taarifa zilizolifikia gazeti
hili, mgambo hao walifika katika maeneo mbalimbali ya Tarafa ya Rubale wakiwa
wamevalia sare za Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
Akizungumza na Tanzania Daima, Shaban Buruan ambaye
ni mmiliki wa duka la bidhaa mbalimbali, alisema akiwa dukani kwake lilifika
kundi la watu, wengine wakiwa wamevalia sare za JWT na wengine
kiraia, wakamueleza kuwa ni maofisa wa Operesheni Kimbunga awamu ya
tatu, wakiongozana na mtendaji wa Kijiji cha Kihumulo, Gidius Alfred.
Buruan alisema baada ya kujitambulisha, walimuomba
leseni ya biashara huku wale waliokuwa wamevalia kiraia wakijitambulisha kama
maofisa wa TRA.
Alisema kuwa hakuwapa leseni hiyo kwa vile hakuwa
nayo mahala hapo, na hivyo wakamtaka awape fedha sh laki moja, jambo ambalo
hakuliafiki badala yake akaomba muda awaletee, lakini waliondoka.
Naye Clementina Kakooza ambaye ni raia wa Rwanda
aliyeolewa Tanzania, alisema mgambo hao walifika kwake wakiwa na sare za JWTZ
wakiongozana na mtendaji wa kijiji na kumtaka awaonyeshe vibali vyake vya
kuishi nchini la sivyo watamfikisha polisi.
“Waliponitishia hivyo niliwaeleza
kuwa nimebaki kutokana na agizo la serikali kuwa watu tulioolewa na
Watanzania tubaki wakati tukifanya utaratibu wa kupata vibali, walikataa na
kusema kuwa niwapatie kiasi cha sh 500,000 ambacho sikuwa nacho.
“Nikataka niwape ng’ombe wawili na mbuzi mmoja
wakagoma na kulazimisha niwapatie fedha, hapo ndipo tuliposhituka na kupiga
simu polisi Rubale,” alisema.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Philip
Kalangi alithibitisha kutokea kwa tukio hilo Oktoba 26 mwaka huu, katika Kijiji
cha Kihumulo, Tarafa ya Rubale, Halmashauri ya Bukoba.
Alisema kuwa baada ya Operesheni Kimbunga awamu ya
pili kitaifa kumalizika, walikabidhi majukumu yote kwa kamati ya ulinzi na usalama
za vitongoji, kata, wilaya na mkoa kuendelea na taratibu za kubaini wahalifu wa
makosa mbalimbali.
Kalangi alisema wakiwa katika maeneo mbalimbali ya
kutekeleza majukumu ya kikazi, walipata taarifa kuwa kuna mgambo walionekana
wakifanya kazi ya kukamata watu na kuwahoji, hususani wahamiaji haramu.
Walifika eneo la tukio na kufanikiwa kuwakamata mgambo watatu.
Aliwataja waliowakamatwa kuwa ni Amran Sadick,
Abeid Amada na Mathias Sospeter ambao ni mgambo wa Manispaa ya Bukoba na Ofisa
Mtendaji wa Kijiji cha Kihumulo, Gidius Alfred.
Alisema mtendaji huyo alikamatwa kwa kosa la
kushirikiana na mgambo hao kufanya kazi bila kushirikiana na uongozi wa kata na
wilaya.
Kwa mujibu wa Kalangi, walipofikishwa polisi na
kuhojiwa hawakuwa na la kujitetea zaidi ya kuomba msamaha.
Alisema watuhumiwa wote wamefikishwa mahakamani kwa
kosa la kudai fedha kwa njia ya vitisho na uchunguzi unaendelea ili
kuendelea kubaini makosa yao mengine kwa ajili ya kuwasilisha ushahidi
mahakamani.
Hata hivyo, alifafanua kuwa wakati watuhumiwa hao
wanakamatwa, hawakuwa na sare za jeshi lolote na kwamba uchunguzi bado
unaendelea.
Chanzo: Tanzania Daima
Muleba waahidiwa watalaamu wa upimaji ardhi
Wananchi Wilaya ya Muleba
Mkoa Kagera wamehaidiwa kuletewa wataalamu wa kupima ardhi ili kutenganisha
maeneo ya wakulima na wafugaji.
Ahadi hiyo imetolewa jana na
Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Profesa Anna Tibaijuka wakati
akihutubia wananchi wa Kata ya Kabilizi iliyoko Wilaya ya Muleba.
Profesa Tibaijuka ambaye pia
ni Mbunge wa Jimbo Muleba Kusini amesema ili kuondoa tatizo la wakulima na
wafugaji hakuna budi kuwapimia ili kila kundi litambue maeneo yake bila
kuingiliana.
Amesema wafugaji wamekuwa na
tatizo la kuwacha mifugo yao iharibu mazao ya wakulima na amemwagiza Mkuu wa
Wilaya kuwa mifugo ikikamatwa ndani ya shamba la mtu aishughulikie mara moja..
Kata hiyo ya Kabilizi imekuwa
na mgogoro baina ya Wakulima na Wafugaji kwa muda mrefu na hivi sasa kumekuwepo
na ufumbuzi baada ya Waziri kutatua tatizo hilo..
BALOZI WA JAPAN ARIDHISHWA NA UJENZI WA DARAJA LINALOUNGANISHA TANZANIA NA RWANDA
Balozi wa Japan Mheshimiwa Masaki Okada (wa kwanza kushoto) akiwa na Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli (nyuma ya Balozi) pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Maendeleo ya Usafirishaji nchini Rwanda Bw. Guy Kalisa (mwenye tai nyekundu) wakikagua eneo la kituo cha pamoja cha ukusanyaji ushuru kwa upande wa Rwanda.
Balozi wa Japan Mheshimiwa Masaki Okada (wa pili) akiwa na Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli (nyuma) pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Maendeleo ya Usafirishaji nchini Rwanda Bw. Guy Kalisa (wa pili kutoka nyuma) wakikagua eneo la kituo cha pamoja cha ukusanyaji ushuru kwa upande wa Rwanda.
Injinia Hitoshi Kameda (kushoto) akitoa maelezo kwa Balozi wa Japan Mheshimiwa Masaki Okada (wa pili kushoto) akiwa na Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli (wa pili kulia) pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Maendeleo ya Usafirishaji nchini Rwanda Bw. Guy Kalisa (kulia) wakikagua eneo la ujenzi wa daraka la Rusumo kwa upande wa Rwanda.
Maporomoko ya Rusumo katika Mto Kagera linapojengwa draja la kuziunganisha nchi za Tanzania na Rwanda katika wilaya ya Ngara mkoani Kagera.
WACHEZAJI WA YANGA WATUA SALAMA MJINI BUKOBA, TAYARI KWA MPAMBAO NA KAGERA SUGAR JUMAMOSI HII.

chanzo Vijimambo Blog
OPERESHENI KIMBUNGA AWAMU YA PILI SASA KUHAMIA MIKOA YA KAGERA, KIGOMA NA GEITA
JAMHURI YA
MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA
YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
Awamu ya Pili ya Operesheni Kimbunga imeweza
kukamata majambazi ya kutumia silaha 67 na wahamiaji haramu 134 katika kipindi cha wiki moja tangu kuanza kwake Septemba 21hadi Septemba 27
mwaka huu katika mikoa ya Kagera, Kigoma na Geita.
Silaha zilizokamatwa ni pamoja na bunduki aina
ya SMG Moja, Pistol Moja na Magobole 17 pamoja na risasi 115 zikiwemo za bunduki
aina ya SMG 102 na Risasi za Pistol 13. Aidha, Magazine mbili zilikamatwa pamoja
na Sare za Jeshi la Burundi.
Wahamiaji haramu waliokamatwa wengi wao ni
kutoka nchi za Burundi ambapo raia wake 114 walikamatwa wakiishi nchini kinyume
na sheria wakati raia wa Rwanda 20 walikamatwa katika kipindi hicho.
Aidha, watu Watatu walikamatwa kwa tuhuma za
kuhifadhi wahamiaji haramu nchini huku Lita 271 za gongo , ngozi ya Mbwea, Bangi
kilo Tatu na Makokoro 12 vilikamatwa wakati wa operesheni Kimbunga awamu ya
Pili ikiwa katika wiki yake ya kwanza.
Wakati huo huo, Wilaya
ya Karagwe mkoani Kagera imejipanga kukabiliana na tatizo la wahamiaji haramu
ili kuhakikisha kuwa tatizo hilo linafikia mwisho wake na kuwapa nafasi
wananchi kufanya shughuli zao za kijamii na kimaendeleo bila ya hofu ya
kufanyiwa uhalifu na wahamiaji haramu.
Mkuu wa Wilaya ya
Karagwe Bi Dari Rwegasira amewaambia Maafisa
Tarafa na Watendaji wa Kata aliokutana nao katika Ukumbi wa Halmashauri ya
Wilaya ya Karagwe, mwishoni mwa wiki iiliyopita kuwa kuanzia sasa kila
kiongozi, kuanzia ngazi ya Kiijiji/Mtaa, Kata, Tarafa na Wilaya, atawajibika kwa
jinsi anavyoshughulikia kumaliza tatizo la wahamiaji haramu katika eneo lake.
Wilaya ya Karagwe ni
moja ya wilaya zenye tatizo sugu la wahamiaji haramu ambao wanatuhumiwa
kuwanyanyasa wananchi katika baadhi ya maeneo ya Wilaya hiyo, kwa kuendesha
vitendo vya wizi wa mifugo, kuvamia maeneo ya kilimo, na pia kuchochea uhalifu
wa unyang’anyi wa kutumia silaha na kusababisha mauaji.
Wahamiaji hao haramu
wanashutumiwa kufanya baadhi ya maeneo ya Wilaya ya Karagwe yasipitike kwa
urahisi, mojawapo ikiwa ni eneo la msitu wa Kimisi, ambapo eneo hili limekuwa
na matukio mengi ya ujambazi wa kutumia silaha na wananchi kuvamiwa na kuibiwa
mali zao na hata wengine wakipoteza maisha katika matukio hayo.
Maazimio kadhaa
yalitolewa katika kikao hicho kati ya Mkuu wa Wilaya ya Karagwe na Watendaji
Wakuu wa Wilaya hiyo, ikiwa ni pamoja na kuwa:
·
Viongozi kuanzia ngazi ya
Kijiji/Kitongoji, Kata hadi Tarafa kutia saini mkataba wa kushughulikia
wahamiaji haramu, majambazi wa kutumia silaha na wafadhili wao, mifugo haramu
inayoingia nchini kutoka nchi jirani pamoja na vitendo vyote vya uhalifu katika
maeneo wanayoyaongoza.
·
Kiongozi yoyote wa Kijiji,
Kata au Tarafa atakayeshindwa kushughulikia wahamiaji haramu walioko katika
eneo lake atawajibishwa.
·
Wahamiaji wote haramu ambao
bado wapo katika maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo wasakwe na kurejeshwa kwao
mara moja.
·
Msako uanzishwe mara moja
kuwasaka wahamiaji haramu wote ambao wamejificha katika maeneo ya misitu na
ranchi za mifugo zilizoko katika wilaya hiyo kwa kuvishirikisha vyombo vyote
vya Utawala na vya Ulinzi na Usalama vilivyoko katika Wilaya hiyo.
·
Kila kijiji kiwe na takwimu
sahihi za wageni waliopo katika maeneo yao.
·
Wahamiaji haramu wote
wanaorejeshwa kwao wasipewe nafasi ya kurudi tena nchini na mwananchi yoyote
atakayebainika kuwapokea au kuwasaidia kurejea atolewe taarifa haraka ili hatua za kisheria
zichukuliwe dhidi yake.
·
Vibali vyote vya Ukazi
vilivyotolewa kwa wageni mbalimbali sasa vitakaguliwa upya ili kuhakiki uhalali
wake.
Imeandaliwa na:
Timu
ya Habari ya Operesheni Kimbunga
Septemba30,2013
Madereva wakorofi waonywa
MKUU wa Mkoa wa Kagera, Kanali Mstaafu, Fabian
Massawe, amewaonya madereva wa vyombo vya moto mkoani hapa kujiepusha na uvunjaji
wa sheria za barabarani.
Amesema madereva lazima watii sheria za barabarani
bila shuruti, na kwamba serikali haitasita kuwakamata wanaovunja sheria.
Kanali Massawe alitoa onyo hilo juzi wakati wa
sherehe za maadhimisho ya wiki ya usalama barabarani, ambayo kimkoa ilifanyika
Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.
Massawe ambaye alikuwa mgeni rasmi katika
maadhimisho hayo, ambayo kitaifa yalifanyika jijijni Mwanza, alisema lengo la
kuwepo maadhimisho hayo ni kuielimisha jamii juu ya matumizi ya barabara na sheria
za nchi.
“Ajali za barabarani zinaathiri sana maisha ya
wananchi wetu. Kwa hiyo natoa onyo kwa madereva wote kuzingatia sheria,”
alisema.
Alisema jamii kutojua vizuri sheria zikiwemo za
barabarani, kimekuwa chanzo kikubwa cha ukiukwaji wa sheria na kutokea ajali
ambazo nyingi husababisha vifo.
Aliwaomba watembea kwa miguu na waendesha vyombo
vya moto kuwa makini na kuzingatia sheria za barabarani, kani itasaidia
kupunguza ajali.
Chanzo: Tanzania Daima
CAG KUKAGUA OFISI YA MEYA BUKOBA
Mdhibiti
na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Bw. Ludovick Utouh, amesema ofisi
yake ipo mbioni kwenda mjini Bukoba, mkoani Kagera, ili kufanya ukaguzi wa
mahesabu katika Ofisi ya Meya na kutoa ripoti yenye uhakika.
Bw. Utouh aliyasema hayo Dar es Salaam jana
katika mafunzo yaliyoshirikisha Wahariri na waandishi wa vyombo mbalimbali vya
habari ili kuwajengea uwezo wa kuripoti taarifa za ofisi hiyo.
Alisema ukaguzi wanaokwenda kuufanya mjini Bukoba, hautokani na matakwa ya Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bw. Nape Nnauye; bali ni ombi maalumu lililotolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu.
Alisema ukaguzi wanaokwenda kuufanya mjini Bukoba, hautokani na matakwa ya Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bw. Nape Nnauye; bali ni ombi maalumu lililotolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu.
Aliongeza kuwa, kumekuwa na taarifa za upotoshaji ambazo zimekuwa zikifanywa na baadhi ya makundi ambayo hayana nia njema na ofisi hiyo, hivyo ni vyema ikaeleweka kuwa, ukaguzi huo umezingatia agizo la Waziri Mkuu.
"Ofisi yangu inafanya kazi kikatiba si kwa matakwa ya chama chochote cha siasa, ukaguzi maalumu ambao utafanyika mjini Bukoba, utaanza wiki ijayo...ni jukumu la vyombo vya habari kuwa waangalifu wanaporipoti taarifa hizi.
"Wananchi
wa Bukoba wasiwe na wasiwasi, tunakwenda huko lakini hatutaki chai ya mtu labda
usafiri ambao upo kisheria kwa ajili ya ukaguzi wa miradi yenye utata iweze
kufikiwa na kupatikana taarifa sahihi," alisema.
Bw. Utouh alisema uwajibikaji na uwazi ni mambo yasiyoweza kupatikana katika mfumo wa kuficha taarifa za utekelezaji wa mipango mbalimbali ya Serikali.
Alisema mahali ambapo habari inafichwa, lazima patatokea mvutano, kutoaminiana na hatimaye wananchi kuona Serikali yao ndiyo chanzo cha matatizo hivyo ni muhimu haki ya kikatiba kwa wananchi kupashwa habari ikazingatiwa.
Alitumia fursa hiyo kuvitaka vyombo vya habari nchini k u p u n g u z a u p o t o s h a j i n a kuelimisha jamii ipasavyo ili kusaidia makundi mbalimbali kuzielewa vizuri ripoti za CAG ili kuzuia machafuko yasiyo na lazima nchini.
"Madhara ya kuripoti taarifa za upotoshaji na mipaka ambayo inahitajika ni makubwa kwa jamii ...tunahitaji kufikiria masuala mazito yanayokwamisha kufikia malengo yetu, hivyo ni muhimu kuacha kutoa taarifa zisizo sahihi," alisema
Chanzo: Majira
Zana haramu 9,000 zateketezwa
SERIKALI kupitia Idara ya Uvuvi mkoani Kagera,
imekamata na kuteketeza kwa moto zana haramu 9,809 zilizokuwa zikitumika kwenye
uvuvi ndani ya Ziwa Victoria.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini Bukoba,
Ofisa Mfawidhi wa Uvuvi na Doria Mkoani Kagera, Apolinary Kyojo alisema zana
hizo zilikamatwa kutokana na msako maalumu wa kushitukizwa ndani ya Ziwa
Victoria.
Alisema msako huo wenye lengo la kupambana na uvuvi
haramu ndani ya ziwa hilo ulifanyika kati ya Juni na Agosti mwaka huu.
"Serikali inaendelea kupambana na watu
wanaoshiriki uvuvi haramu ndani ya Ziwa Victoria. Kati ya Juni na Agosti mwaka
huu, tulikamata zana haramu 9,809. kwenye msako wa kushtukiza,” alisema.
Alizitaja zana zilizokamatwa kuwa ni nyavu zenye
matundu madogo zipatazo 7,000, nyavu aina ya timba 2,700, makokoro yenye urefu
wa zaidi ya mita 110,000, vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya sh 750,000.
Kwa mujibu wa Kyojo katika kutekeleza misako ya
namna hiyo, idara yake inakabiliwa na changamoto ya kukosa ushirikiano kutoka
kwa baadhi ya viongozi wa vijiji, kata na hata wasimamizi wa rasiliamali za
Ziwa Victoria (BMU).
Chanzo: Tanzania Daima
Wafugaji wauawa kinyama
WAFUGAJI wawili wameuawa kinyama kwa kukatwa
mapanga na kuchomwa mikuki na wananchi, huku ng'ombe wapatao 12 nao wakiuawa
katika Kijiji cha Kasulo wilayani Ngara, Mkoa wa Kagera.
Chanzo cha mauaji hayo kinadaiwa kuwa ni uhasama wa
muda mrefu kati ya wananchi na wafugaji hao wanaodaiwa kuingiza mifugo kijijini
humo bila ridhaa ya serikali ya kijiji.
Tukio hilo lilitokea Septemba 19 mwaka huu, saa
11:00 jioni na kwamba ng'ombe waliouawa kwa kuchomwa mikuki na kukatwa mapanga,
nyama zake zilichukuliwa na wanawake kwa ajili ya kitoweo.
Akithibitisha tukio hilo, Mwenyekiti wa Kitongoji
cha Ngoma 'B' yalipotokea mauaji hayo, Simeon Nzakaya alilaani kitendo cha
wananchi kujichukulia sheria mkononi na kuwataja waliouawa kuwa ni Ngabo
Godfrey (24) na mwingine ambaye bado hajatambulika jina lake.
Alisema kuwa miili ya marehemu hao
ilipatikana Septemba 20, na watu wanane wanashikiliwa na vyombo vya
usalama kwa mahojiano zaidi kuhusiana na mauaji hayo.
Hata hivyo, taarifa zinadai kwamba baadhi ya
mamlaka zinazolalamikiwa ni pamoja ni Idara ya Uhamiaji Wilaya, Mifugo na Halmashauri
ya Wilaya kupitia kitengo cha sheria kwa kushindwa kuchukua hatua mara baada ya
kuombwa kuingilia kati mambo ya uvamizi wa wafugaji.
Naye Mwenyekiti wa Kijiji cha Kasulo, Yusufu Katula
alithibitisha kuwepo kwa mauaji hayo pamoja na kulaani kitendo hicho.
"Mgogoro huo unafukuta kutokana na idara
husika kutochukua hatua mapema. Hii inachangia kutokea mauaji kama haya, na
hatua za haraka zisipochukuliwa yanaweza kutokea mapigano makali kati ya
wanakijiji na wafugaji wanaoingia kinyemela,"alisema.
Mkuu wa Wilaya ya Ngara, Costantine Kanyasu alionya
kuwa matukio kama hayo hayaruhusiwi kutokea katika jamii, na aliahidi ofisi
yake kuyafanyia kazi malalamiko yote yanayotolewa kwa baadhi ya mamlaka.
"Ni kweli baadhi ya mamlaka za serikali
zinalalamikiwa sana na wananchi. Na sasa nitakachokifanya ni kuchukua hatua za
haraka kuhakikisha tukio kama hilo halitokei tena," alisema.
Chanzo: Tanzania Daima
ABELA KIBIRA: BINTI WA KIHAYA ANAYETIKISA AMERICA KIMUZIKI
Mkoa wa Kagera
umebarikiwa kuwa na uwakilishi mzuri katika tasnia mbalimbali ndani na nje ya
nchi, akina Rweyemamu wanazidi kupasua anga! mfano mzuri ni Mwanamuziki wa kike
Abela ambaye ni mzaliwa wa Bukoba Mkoani Kagera anayepeperusha vyema bendera ya
Tanzania kimziki huko Amerika anakoishi na kufanya kazi zake za muziki.
Abela Kibira alizaliwa
Septemba 22 mwaka 1989 akiwa mtoto wa kwanza katika familia ya Mtanzania Josiah
Kibira mzaliwa wa Bukoba Kagera, Tanzania na Mmarekani, Mrs Josiah Kibira.
Mchanganyiko huo wa
tamaduni mbili kwa binti huyo ambaye ana kipaji cha utunzi na uimbaji, umemfanya
kujimarisha na kujijengea jina katika muziki kutokana na aina ya muziki na
manjonjo anayoyafanya katika mzuiki wake kupendwa.
Abela ni mzaliwa wa
Bukoba, Tanzania lakini kwa sasa anaishi Minneapolis, Marekani. Binti huyu
anasauti nzuri, ya kipekee na ya kuvutia jambo ambalo nyimbo zake nyingi
zimekuwa zikipendwa sana
Onyesho lake la kwanza
Binti huyu alilifanya kanisani na ndipo kipaji chache kilipojifunua machoni mwa
watu wengi na hivyo kuendelea kuimba katika matamasha mbalimbali shuleni na
matamasha maalumu.
Abela amekulia katika
mji wa Wayzata, Minnesota na alipendwa kutokana na kuwa na uwezo wa ajabu
katika kuimba kwaya na matamasha ya pamoja wakati akiwa katika masomo yake ya sekondari
na chuo.
Mwaka 2003 baba yake
mzazi Mr. Josiah Kibira alimshirikisha katika filamu yake aliyoiita Bongoland,
ambapo Abela alitunga wimbo wa kusindikiza filamu hiyo (soundtrack) jambo
lililomuongezea uwezo na umaarufu kwa mashabiki Amerika, Afrika na maeneo mengi
ulimwenguni.
Abela ambaye bado
binti kigoli anayejitambua amekuwa akiiimba na kujifua utumiaji wa sauti takriban
maisha yake yote lakini kwa sasa amejikita zaidi katika utunzi na utengenezaji
wa nyimbo za Hip Hop, Reggae na ni mzuri katika aina tofauti tofauti za muziki.
Abela hana shida juu
ya kufanya collabo na wasanii wa Kitanzania na Africa kwa ujumla kwa hiyo kama
unapenda kumshirikisha kazi ni kwako! Kwa sasa anatamba na video ya wimbo wake
alioutoa mwishoni mwa mwaka jana unaoitwa Ball & Chain.
Kabla ya hapo ametamba
na nyimbo nyingi zikiwemo Rolling Stone,
Someone like you na Hey Ya.
Imeandaliwa na Dotto Kahindi
Imeandaliwa na Dotto Kahindi
Operesheni Kimbunga yanasa wahamiaji haramu 1,851
HATIMAYE
operesheni ya kuwasaka wahamiaji haramu nchini, iliyopewa jina la Kimbunga,
imeanza juzi huku watu 1,851 wakikamatwa. Hatua hiyo, imetokana na agizo la
Rais Jakaya Kikwete la kuwataka watu wanaomiliki silaha na kuishi nchini
kinyume cha sheria, kuondoka wenyewe kwa hiari yao kabla vyombo vya dola
havijaanza kazi ya kuwasaka.
Operesheni hiyo inayovishirikisha vyombo vyote vya dola, imeanza katika Mikoa ya Geita, Kagera na Kigoma.
Akizungumza na waandishi wa habari, Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Kanali mstaafu, Fabian Massawe, alisema hadi jana wahamiaji haramu 1,851 wamekamatwa wakati 11,601 wameondoka kwa hiari yao.
Alisema operesheni hiyo haitamuacha mhamiaji haramu ndani ya mikoa hiyo.
Alisema licha ya wahamiaji 11,601 kuondoka wenyewe, Serikali imelenga wahamiaji 52,053 ambao bado wapo katika mikoa hiyo.
Alisema tangu Rais Jakaya Kikwete alipotoa agizo la wahamiaji haramu kuondoka kwa hiari, bunduki 65 zikiwamo Sub Machine Gun (SMG) tatu, ShortGun 10 na magobole 52 zilisalimishwa.
Naye, Mkuu wa Operesheni Msaidizi wa Jeshi la Polisi, Simon Sirro, alisema vyombo vyote vya dola vinaendelea na kazi ya kuwasaka wahamiaji.
Aliwatahadharisha wananchi mkoani Kagera kujihadhari na kuuziwa mali yoyote kutoka kwa mtu yeyote anayehamishwa bila maandishi kwa ajili ya kuepuka kukamatwa na kuhusishwa kushirikiana na wahamiaji hao.
Alisema walikamata ng’ombe 1,765, sare na vifaa mbalimbali vya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
Operesheni hiyo inayovishirikisha vyombo vyote vya dola, imeanza katika Mikoa ya Geita, Kagera na Kigoma.
Akizungumza na waandishi wa habari, Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Kanali mstaafu, Fabian Massawe, alisema hadi jana wahamiaji haramu 1,851 wamekamatwa wakati 11,601 wameondoka kwa hiari yao.
Alisema operesheni hiyo haitamuacha mhamiaji haramu ndani ya mikoa hiyo.
Alisema licha ya wahamiaji 11,601 kuondoka wenyewe, Serikali imelenga wahamiaji 52,053 ambao bado wapo katika mikoa hiyo.
Alisema tangu Rais Jakaya Kikwete alipotoa agizo la wahamiaji haramu kuondoka kwa hiari, bunduki 65 zikiwamo Sub Machine Gun (SMG) tatu, ShortGun 10 na magobole 52 zilisalimishwa.
Naye, Mkuu wa Operesheni Msaidizi wa Jeshi la Polisi, Simon Sirro, alisema vyombo vyote vya dola vinaendelea na kazi ya kuwasaka wahamiaji.
Aliwatahadharisha wananchi mkoani Kagera kujihadhari na kuuziwa mali yoyote kutoka kwa mtu yeyote anayehamishwa bila maandishi kwa ajili ya kuepuka kukamatwa na kuhusishwa kushirikiana na wahamiaji hao.
Alisema walikamata ng’ombe 1,765, sare na vifaa mbalimbali vya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).










