Karagwe. Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha
Kafunjo, Kata ya Kiruruma, wilayani Karagwe, mkoani Kagera, wamesema
wamekuwa wanakula kinyesi bila kujua kutokana na kutokuwa na vyoo bora.
Wakizungumza kwenye mkutano wa hadhara kijijini
hapo mwishoni mwa wiki iliyopita, baada ya kutembelewa na Ofisa wa Afya
kutoka Ofisi ya Mganga Mkuu Wilaya ya Karagwe, kuwaelimisha jinsi ya
ujenzi wa vyoo bora na matumizi yake.
Mmoja wa wakazi hao, Renatus Kanyabuhura alisema
kutokana na kutokuwa na vyoo bora, walikuwa wakila kinyesi kwa sababu
walikuwa wakitoka chooni bila kunawa mikono na kuvuta sigara huku
wengine kula matunda.
“Kutokana na kutokuwa na vyoo bora, unakuta nzi
wanaotoka chooni wanatua kwenye chakula na huku mlaji anaendelea, jambo
linalojionyesha tunakula kinyesi,” alisema Kanyabuhura.
Naye Ofisa wa Afya, Moses Aligawesa alisema
magonjwa mengi yanatokana na matumizi mabaya ya vyoo na kula kinyesi kwa
njia tofauti.
Aligawesa alitaja magonjwa yanayotokana na kula
kinyesi kuwa ni, kipindupindu, kuhara, kichocho, safura (minyoo) na
kwamba, magonjwa hayo yanaathiri kila mmoja kuanzia familia, kijiji,
kata hadi taifa. Alisema choo bora ni shimo lenye urefu wa futi 12 na
kuendelea, kinachosafishika, kuezekwa bila kusahau kunawa mikono kwa
kutumia maji na sabuni.
Chanzo;Mwananchi
Chanzo;Mwananchi
0 comments:
Post a Comment