Ngara. Mkazi wa Kijiji cha Kihinga, Kata ya
Bugarama wilayani Ngara mkoani Kagera(jina tunalo), anashikiliwa katika
kituo kidogo cha polisi cha kata hiyo baada ya kutuhumiwa kuuza kilo
moja ya nyama ya binadamu kwa Sh100,000.
Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Kihinga,
Hassan Mohamed alisema kuwa jana saa mbili usiku, wananchi walipeleka
fedha nyumbani kwake kununua nyama hiyo na alipowaona alikimbia na
wananchi hao kwa hasira walimkimbiza ili kumuua na hapo hapo kuunguza
nyumba yake.
“Mgambo ndio walimnusuru asiuawe na wananchi wenye
hasira kali na alikimbizwa kituo kidogo cha polisi Kata ya Bugarama ili
kuokoa maisha yake “.
Akizungumza na gazeti hili, Kamanda wa mgambo wa
kijiji hicho, Emanuel Kaloli alisema wananchi waliandamana baada ya
kusikia taarifa za kuwapo mtu anayeuza nyama ya binadamu na kutaka
kuhakikisha ukweli huo.
Alisema baada ya wananchi kufika, walianza
kumshambulia na kutaka kumuua, lakini wanamgambo wa kitongoji walifika
kisha kumuokoa mtuhumiwa na hatimaye kumfikisha kituo cha polisi kwa
ajili ya usalama wake.
“Kijana aliyefahamika kwa jina la Man Balyamwabo
mkazi wa Shina la Kalenge katika kitongoji hicho, ndiye aliyeambiwa kuwa
angeuziwa nyama hiyo ya binadamu na kuleta taarifa katika uongozi wa
kijiji ili uweze kuchukua hatua zaidia”.Alisema Kaloli.
Alisema nyumba aliyounguziwa pamoja na mali
iliyokuwamo ndani hasa maharage, mavazi na vitu vinginevyo inakadiriwa
kuwa na thamani ya Sh2.6milioni. Pamoja na kuwepo kwa tukio hilo, baadhi
ya wananchi walisema mtuhumiwa inasemekana ni raia wa nchi jirani ya
Burundi na alianza kuishi katika kitongoji hicho tangu mwaka 1981 kama
kibarua wa kilimo kwenye mashamba.
Taarifa zinasema kuwa katika kuishi kwake na ndugu
yake aliyefahamika kwa jina la Kahungu walikuwa wakituhumiana kwa
uchawi na ilifikia mahala wakatofautiana na kaka yake ambaye alirejea
kwao.
Polisi wilayani Ngara imethibitisha kumpokea
mtuhumiwa huyo na kwamba linafanya mahojiano ya kina kwa kushirikiana na
viongozi wa kijiji ili kubaini ukweli wa tukio hilo.
Chanzo;Mwananchi
Chanzo;Mwananchi
0 comments:
Post a Comment