WANAWAKE na watoto wametakiwa kuzitambua haki zao za kimsingi
katika jamii ili kuepukana na vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia
vinavyokithiri wilayani Karagwe.
Mkurugenzi Mtendaji wa asasi isiyo ya kiserikali ya Women’s and Men’s
Development Association (WOMEDA) iliyopo mjini Kayanga, wilayani hapa,
Juma Masasi, alitoa kauli hiyo jana alipozungumza na waandishi wa
habari ofisini kwake.
Alisema wanawake wilayani humo wamekuwa wakifanyiwa vitendo vya
ukatili ikiwemo ukatili wa kingono, ukatili wa kimwili na ukatili wa
kisaikolojia.
Masasi alisema shirika lake limeweza kupokea kesi mbalimbali za aina
hiyo zikiwemo za ndoa, talaka, mikataba ya ajira, za madai na mirathi.
Alisema shirika lake kwa kuungana na mashirika mengine kama Chama cha
Wanahabari Wanawake (Tamwa), madawati ya kijinsia watahakikisha
wanapambana na vitendo vya kikatili bila woga.
Chanzo;Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment