Home » » WILAYA YA KYERWA YAPITISHA BAJETI YA BILIONI 20

WILAYA YA KYERWA YAPITISHA BAJETI YA BILIONI 20

Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa Mkoa Kagera imekisia kupata kiasi cha shilingi Biloni 20.37 kwa mwaka wa fedha wa 2014/2015.

Hayo yametolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa Bw.George Mkindo wakati wa kikao cha kwanza cha Madiwani tangu kuanza kwa Halmashauri hiyo kilichokaa kwa ajili ya mapato na matumizi ya Halmashauri hiyo.

Bw.Mkindo amesema makisio ya mapato ya ndani Halmashauri hiyo imekisia kukusanya kiasi cha shilingi bilioni 2.5.


Bw.Mkindo amesema mapato hayo ni pamoja na ushuru wa mazao ya kahawa,ndizi,mahindi,mabango,reseni za biashara,minada ya mifugo ,udhuru wa magulio na masoko.

Amesema kwa upande wa matumizi mengineyo Halmashauri hiyo imepanga kutumia kiasi cha shilingi Bilioni 3.1kutoka serikali kuu ambako matumizi ya mishahara ya watumishi itaendelea kutumika ile kutoka Wilaya ya Karagwe ambako ilikomegwa.

Kikao hicho cha Madiwani kilichokuwa chini ya Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Bw.Kashunju Runyogote kimepitisha kutumia miradi ya maendeleo kiasi cha shilingi Bilioni 14.5 kutoka kwa wahisani,ruzuku toka serikali na vyanzo vya ndani.

Aidha katika bajeti hiyo wametaja changamoto zao kuwa Halmashauri inao upungufu wa watumishi hasa kada za Elimu,Afya Ugavi inayokumba Kilimo na Mifugo.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kagera Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa