ZIMWI LA TEGETA ESCROW LAMTISHA PROFESA TIBAIJUKA, AKATAA KUPOKEA DOLA 300,000 BAADA YA KUPEWA TUZO YA KIMATAIF

A
 Mbunge wa Muleba Kusini, Profesa Anna Tibaijuka akionesha tuzo ya kimataifa (UN) ya Maendeleo Endelevu ya Mwana Mfalme Khalifa Bin Salman Al Khalifa aliyotunukiwa hivi karibuni New York Marekani wakati akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo.
 Profesa Anna Tibaijuka akionesha cheti alichokabidhiwa sanjari na tuzo hiyo.
 Profesa Tibaijuka akisisitiza jambo katika mkutano huo na wanahabari. Kulia ni Mratibu wa mkutano huo, Mussa Ally.
 wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Mkutano na wanahabari ukiendelea.

Na Dotto Mwaibale


MBUNGE wa Muleba Kusini Profesa Anna Tibaijuka amekacha kuchukua dola 300,000 alizopewa baada ya kutunukiwa tuzo ya  Maendeleo Endelevu aliyopewa na Umoja wa Mataifa (UN), kutokana na sakata la fedha za Escrow Tegeta.


Tuzo hiyo aliipokea Septemba 23 mwaka huu New York Marekani ambayo mfadhili wa tuzo hiyo ni wa waziri mkuu wa Bahrain mwana mfalume Khalifa bin Al Khalifa.

Akizungumza jana Dar es Salaam Profesa Tibaijuka alisema kwa sasa umoja wa mataifa umeingia katika awamu ya pili ya maendeleo, ambao umekuja kupisha yale malengo 17 ya mileniam ambayo yote yeye alikuwepo, hivyo aliokuwa wanatoa tuzo walinona kwa namna alivyoshiriki kwa kiasi kikubwa.

"Tuzo hizi si za kuomba, ni watu wanakaa na kupendekeza mtu wa kupewa, na hii ni mara ya pili, mara ya kwanza   nilipewa mwaka 2009 nchini Swideni," alisema na kuongeza.

"Tuzo zinatoka kwa niaba ya jamii inayotoka au kuitumikia na kufanya nayo kazi, hivyo wamatambua mchango wangu katika kuwatumikia wananchi wa Muleba," alisema.

Aidha Profesa tibaijuka alitaja sababu zilizpokekea yeye kutochua dola 300,000 za Marekeni za tuzo hiyo.

"Sikuichukua kwa sababu ya yaliyonikuta hapo mapema, kulikuwa na uwezekano wa kuichukua lakini nikasema kwa hali halisi ya nyumbani, hatuna sheria ya kupokea tuzo, michango na zawadi kwa hiyo mimi nikaicha mezani wao wafanye wanayotaka," alisema na kuongeza. 

"Unapoona mtu kama mimi nafanya kazi nakwenda kuchafulia kwenye kitu ambacho siusiki nacho, sasa Unapoipokea hapa utaonekana kama umevunja maadili au umejinufaisha kwa kuwa ndio mambo ya kwetu, hivyo nikawaachia," alisema.

Aliongeza kwa sasa umeshapeleka mswada binafsi bungeni wa kuweka sheria ya michango ili vitu vya hiari kama hivi vinapokuja katika jamii visimamiwe na si kupotoshwa kisiasa.

"Kwa maana jambo hili halina kificho, yaani huwezi kumzungumzia Anna Tibaijuka bila kutaja suala la Escro, hayo hayakwepeki kwa sababu yalitengenezwa yakawa hivyo, mtu asiyehusika anavalishwa joho lisilo muhusu.

"Lakini kwa sababu jamii haina uwezo wa kuchimba chini, unabaki kuwa uongo na kushindwa kujua ukweli umesimama wapi, lakini wao (UN) wanajua hii ni propanda la sivyo nisingesimama hapa na tuzo," alisema.

Aliongeza licha ya yeye kuwa mstaafu wa umoja wa mataifa bado wanamfuatilia katika shughuli za kimaendeleo ambazo anazifanya akiwa ndani na nje ya nchi.

"Kama ukijikwaa, ukianguka na kusimama watu wanaangalia kulikoni, na huu ni utamaduni wao, kwa hiyo pale uongo na fitina havina nafasi," alisema kwa msisitizo wakati akizungumza na wanahabari.

Diwani wa Kata ya Karambi ambaye pia ni Mjumbe wa mkutano Mkuu wa Taifa wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM),  Felix Bwahama ambaye aliongozana na  Profesa Tibaijuka alishukuru UN kwa kumtunuku tuzo hiyo ambapo alisema ni fahari kwa wanakagera na taifa kwa ujumla licha ya baadhi ya watu nchini kubeza kazi anazizifanya ambazo zinaonekana kimataifa.



TIGO YAWAKUMBUKA WAHANGA WA TETEMEKO MKOANI KWA KUTOA SARUJI MIFUKO 2424



Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Salum Kijuu(kushoto) akipokea sehemu ya mifuko ya saruji 2424 yenye thamani ya Sh 40 Milioni kutoka kwa Mkurugenzi wa Mtandao wa Tigo kanda ya ziwa Ali Mswanya,kwa ajili ya waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera.




Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Salum Kijuu(kulia) akipeana mkono na Mkurugenzi wa Mtandao wa Tigo kanda ya ziwa Ali Mswanya alipomkabidhi sehemu ya mifuko ya saruji 2424 yenye thamani ya Sh 40 Milioni ,kwa ajili ya waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera,wa pili kulia ni Meneja wa Tigo Mkoani humo Sadock Phares.

Mkurugenzi wa Mtandao wa Tigo kanda ya ziwa Ali Mswanya akizungumza na  waanidishi wa habari mkoani Kagera alipomkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Salum Kijuu     sehemu ya mifuko ya saruji 2424 yenye thamani ya Sh 40 Milioni ,kwa ajili ya waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera




NEWS ALERT: Rais Magufuli atengua uteuzi RAS Kagera





Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera, Amantius Msole
Rais Dkt. John Magufuli leo Rais Magufuli ametengua uteuzi wa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera, Amantius Msole na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba, Steven Makonda baada ya kubaini kuwa wamefungua akaunti nyingine ya benki kwa kutumia jina linalofanana na akaunti rasmi ya kuchangia maafa iitwayo "Kamati Maafa Kagera" kwa lengo la kujipatia fedha.
Kwa mujibu wa Ikulu jijini Dar es Salaam taarifa iliyotolewa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa muda mfupi baada ya kupokea hundi ya msaada kutoka kwa Waziri Mkuu wa India, Narendra Modi iimeeleza kuwa pamoja na kutengua uteuzi huo Rais Magufuli ameagiza vyombo vya dola vichukue hatua dhidi ya wote waliohusika katika njama za kufungua akaunti hiyo. Msaada huo ni wa shilingi Milioni 545.
Aidha, Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa amemsimamisha kazi Mhasibu Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Simbaufoo Swai kutokana na kuhusika katika njama hizo.
Hata hivyo Waziri Mkuu ametoa wito kwa wananchi na taasisi mbalimbali kuendelea kuchangia misaada kwa ajili ya walioathirika kwa kutumia akaunti rasmi ya "Kamati Maafa Kagera" ambayo imetangazwa na Serikali.
CHANZO HABARI LEO

Burundi yawafuta machozi Wanakagera kwa tani 183 za vyakula.





Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Suzan Kolimba (kushoto) akikabidhiwa msaada na Waziri wa Afrika Mashariki Bi. Leontine kutoka Serikali ya Jamhuri ya Burundi kwa lengo la kuwasaidia waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera.

TAARIFA RASMI KWA VYOMBO VYA HABARI KUTOKA IKULU LEO



NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE APOKEA MSAADA KUTOKA BURUNDI KUSAIDIA WAATHIRIKA WA TETEMEKO KAGERA

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Susan Kolimba akipokea msaada wa chakula kutoka kwa Mhe. Leontine Nzeyimana, Waziri wa Afrika Mashariki wa Burundi ikiwa ni msaada kutoka Serikali ya Burundi kwa ajili ya Waathirika wa tetemeko la ardhi huko Mkoani Kagera.  Msaada huo ni pamoja na mchele tani 100, sukari tani 30, mahindi tani 50 na majani ya chai tani 3.
Mhe. Dkt. Kolimba akitoa shukrani za dhati kwa niaba ya Serikali kwenda Serikali ya Burundi baada ya kupokea msaada huo wa chakula.
Mhe. Nzeyimana naye akitoa salamu za pole za Rais wa Burundi, Mhe. Pierre Nkurunziza kwa Serikali ya Tanzania kufuatia tetemeko hilo.
Mhe. Dkt. Kolimba akiwa katika picha ya pamoja Mhe. Nzeyimana na wadau wengine. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Meja Jenerali Mstaafu Salim Mustafa Kijuu akifuatiwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani wa Burundi.

WAFANYABIASHARA KARIAKOO WACHANGA SH. MILIONI 60.7 KWA WAATHIRIKA WA TETEMEKO KAGERA

 Mwenyekiti wa Jumuia ya Wafanyabiashara wa Kariakoo, akizungumza jijini Dar es Salaam, baada ya kupokea michango ya fedha na vifaa kutoka kwa wanachama wa jumuia hiyo kwa ajili ya walioathirika kwa tetemeko la ardhi mkoani Kagera.  Jumla walichanga fedha na vifaa vyote vikiwa na thamani ya sh. milioni 60.7. (PICHA NA RICHARD MWAIKENDA)
 Mwenyekiti wa wafanyabiashara Mtaa Muhonda, Kariakoo, akimkabidhi Mwenyekiti wa Jumuia ya Wafanyabiashara Kariakoo (JWK), Philimon Chonde, fedha taslimi mchango kutoka kwa wafanyabioashara hao kwa ajili ya walioathirika  kwa tetemeko Kagera. Wa pili kushoto ni Katibu Mkuu wa JWK, Abdalah Mwinyi na Mweka Hazina wa jumuia hiyo, Silvanus Mande.
 Katibu wa JWK, Mtaa wa Raha Square, Frank Nduta akikabidhi vitenge na bidhaa nyingine kwa Mwenyekiti wa JWK, Philimon Chonde
 Wafanyabiashara wa Mtaa wa Mchikichi Kariakoo, wakitoa msaada wa  misumari kwa ajili ya waathirika wa tetemeke, Kagera.PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG


TCRS yatoa vifaa vya zaidi ya milioni 60 kwa waathirika wa tetemeko Kagera.



Na Eleuteri Mangi, MAELEZO, Bukoba.
Shirika la Kiristo la Kuhudumia Wakimbizi Tanganyika (TCRS) limechangia vifaa vyenye jumla ya Sh. milioni 60.92 ikiwa ni mchango wao wa kuwafuta machozi wanakagera baada ya kuathiriwa na tetemeko la ardhi.

Katika kuhakikisha hali za wananchi na ttaasisi za kutolea huduma za kijamii  zinaimarika na kurudi kwenye hali ya kawaida, wadau mbalimbali wa ndani na nje ya nchi bado michango yao inahitajika.

Akikabidhi mchango huo, Mratibu wa Miradi inayoendeshwa na TCRS Oscar Rutenge pamoja na Jasmine Gwamsy wametaja mchanganuo wa msaada huo kuwa ni pamoja na blanketi, 1680, mashuka 840, ndoo za kutumia 840, nguo za kutumia kwawanawake, wanaume na watoto box 50, sabuni katoni 1680 pamoja na vifaa vingine 2250.

Akipokea msaada huo Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu amemelishukuru shirika hilo kwa mchango wao huo kwani ni wa thamani hasa baada ya tetemeko hilo kuwaaathiri wananchi wa mkoa huo.

Aidha, Meja Jenerali Mstaafu Kijuu amewakaribisha na kuwataka wadau wengine waguswe kwa namna ya kipekee na waendelee kutoa michango yao waweze kuwasaidia wananchi na kurudisha hali yao  na kuendelea na shughuli zao za kijamii na kimaendeleo.

RC KAGERA ATOA TAARIFA KUHUSU HATUA ZA SERIKALI ILIZOCHUKUA KUHUSIANA NA TETEMEKO LA ARDHI


Kampuni ya CHICO yaendelea na uvunjaji wa Shule ya Sekondari Ihungo ili kuruhusu ujenzi mpya wa shule hiyo.


LOWASSA AISIFU SERIKALI URATIBU MAAFA KAGERA



Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Edward Lowassa akisalimiana na
Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Meja Generali Salum Kijuu alipomtembela leo ofisini kwake kumpa pole kutokana na athari ya tetemeko la ardhi katika mkoa wake


Na Mwandishi Wetu-KAGERA

Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Edward Lowassa ameipongeza Serikali kwa namna ilivyojipanga kukabiliana na athari za tetemeko la ardhi lililotokea mkoani humo.


Bw. Lowassa amesema hayo kupitia salamu zake alipomtembelea Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Meja Generali Salum Kijuu, ofisini kwake kumpa pole kutokana na athari zilizotokana na tetemeko hilo.


“Napenda nikupongenze mkuu wa mkoa kwa namna ulivyokabili tukio hili, wala hatukuwa na mashaka wewe ni mtaalam wa majeshi wa siku nyingi kwa hiyo jambo hili limempata mwenyewe mpiganaji na tunaona kwa pamoja mmelishikilia vizuri,” alisema Lowassa.


Adha Mhe. Lowassa alisema kuwa suala hili ni kubwa na halipaswi kuiachia Serikali peke yake katika kulikabili nalo kwani madhara yanaonekana ni makubwa hivyo watanzania wote wana budi kuwasaidia waathirika.


Katika kushirikiana na wananchi wa Kagera, Bw. Lowassa ameahidi kutoa mifuko 400 ya saruji kwa ajili ya ujenzi ya miundombinu iliyoharibika.


Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja, Generali Salum Kijuu ameendelea kuwasisitiza watanzania kuchangia kile walichonacho ili kusaidiana na serikali katika kuwafariji waathirika wa tetemeko hilo.


“Tunashukuru watanzania kwa misaada wanayoendelea kutoa kwa ajili ya kuwasaidia waathirika wa tetemeko ila bado tunaendelea kuwasisitiza tuendele kujitoa kwa ajili ya kuwasaidia watu wenye mahitaji,” alisema  Meja Generali Salum Kijuu.

WANANCHI KYERWA WAHIMIZWA KULIMA MAZO YANAYOKOMAA KWA MUDA MFUPI



Na Eleuteri Mangi, MAELEZO, Kyerwa, Kagera
Ukame unaotokana na mabadiliko ya tabia nchi ulioathari mazao ya ndizi na kahawa wilaya Kyerwa mkoani Kagera umemlazimu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu Jenista Muhagama kuwaomba wananchi wa mkoa huo wabadilike waanze kulima mazao mengine ya chakula yanayokomaa kwa muda mfupi.

Athari hiyo ya ukame imemlazimu Waziri Mhagama kuwataka wananchi wa wilaya hiyo na mkoa wa Kagera kwa ujumla w0aanze kulima mazao mengine yanayokomaa kwa muda mfupi yaweze kuwapunguzia adha ya upungufu wa chakula unaotokana na kutegemea zao la ndizi pekee.

Akiwa katika kijiji cha Ntare kata ya Itera wilayani Kyerwa Waziri Mhagama aliongea na wananchi wa kata hiyo ambapo alisema “Mabadiliko ya tabia nchi ni makubwa, msiendelee kutegemea zao moja tu la chakula la ndizi, ni lazima mkubali sasa tuende kwenye mazao mengine ya chakula, limeni mihogo, limeni mahindi. Nendeni kwenye mazao yanayokomaa kwa muda mfupi, vinginevyo tukisema kila kila mwaka tuendelee kutegemea kahawa na ndizi kwa hali ya hewa ilivyo sasa tutaendelea kukosa chakula”.

Waziri Mhagama aliyataja mazao hayo kuwa yanaweza kukomaa kwa muda mfupi kuanzia miezi mitatu ndiyo yanaweza kuwa mkombozi wa katika kukabiliana na upungufu wa chakula na kuwahakikishia wananchi chakula cha kutosha hatua ambayo itawafanya waendelee na shughuli zenye tija kwa maendeleo yao.

Mkulima wa kata hiyo Shakiru Issa anathibitisha kuwa upo uwezekano wa kulima mazao mengine zaidi ya ndizi na kahawa ambayo yanamuongezea kipato ambapo yeye analima pia zao la viazi mviringo kwa ajili ya chakula pamoja na kuuza hatua inayomsaidia kumuongezea kipato na kuendesha maisha yake ya kila siku.

Ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi Waziri Mhagama amewataka wananchi wa mkoa wa Kagera kuacha tabia ya kuchoma mapori moto mara moja kwa kuwa tabia hiyo huhatarisha maisha ya watu, kupoteza mazao shambani,miti na hifadhi ya misitu ambayo ndiyo kivutio kikuu cha mvua.

Aidha, ziara hiyo wa Waziri Mhagama imekuwa faraja kwa wananchi wa Kata ya Itera ambapo amemwagiza Mkurugenzi Idara ya Kuratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Brigedia Jenerali Mbazi Msuya aende kufanya tahmini ya hali ukame ilivyo athiri wilaya hiyo na kutoa taarifa mapema iwezekanavyo.

Katika kuhakikisha upatikanaji wa chakula cha kutosha wilayani Kyerwa, Waziri Mhagama ametoa wito na kumuagiza Mkuu wa Wilaya hiyo Kanali Mstaafu Shaban Lissu pamoja kulima zao la ndizi, aanza haraka kampeni ya kuwahamasisha wananchi hao kulima mazao yanayokomaa kwa muda mfupi ambayo yataweza kuwapatia chakula cha kutosha kwa mahitaji yao ya kila siku.

MHE. JANUARY MAKAMBA AWATOA WASIWASI WAATHIRIKA WA TETEMEKO KAGERA.

 
Na Benedict Liwenga-WHUSM, Bukoba.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Mhe. January Makamba amewatoa wasiwasi waathirika wa tetemeko la ardhi lilitokea Wilayani Bukoba Mkoani wa Kagera.
 
Mhe. Makamba ameyasema hayo leo mkoani Kagera wakati wa ziara yake ya kutembelea maeneo mbalimbali yaliyokumbwa na tetemeko hilo kwa lengo la kuwapa pole waathirika na kuwap ujumbe wa Serikali kuhusu namna inavyojitahidi kuwasaidia waathirika hao.
 
Amesema kwamba, wananchi wasiwe na wasi wasi kuhusu suala la kupatiwa misaada ya dharura kwani Serikali imejipanga na bado inaendelea na zoezi la kufanya tathmini ya uharibifu uliotokea ingawa zoezi la kuwapatia baadhi ya huduma za msingi linaendele.
 
“Tumekuja kutoa msaada kwa mji kwa ujumla wakati tunapanga namna ya kusaidia katika masuala ya mazingira na tambueni kuwa Serikali inawajali ndiyo maana kuna viongozi wakubwa wako hapa na wengine wanazidi kuja”, alisema Mhe. Makamba.
 
Aliongeza kuwa, suala la kuwasaidia waathirika wa tetemeko hilo limepewa uzito mkubwa na Serikali na suala la kuchelewa kwa kutolewa kwa misaada kunatokana na umakini unaoendelea kufanywa sasa hivi na Serikali ili kuwatendea haki waathirika pekee.
 
Naye Mkuu wa Wilaya ya Misenyi Luteni Kanali Denice Filangali Mwila amesema kuwa katika Wilaya yake sehemu iliyoathirika zaidi ni Kata ya Minziro ambapo jumla ya nyumba 512 haziwezi watu kuishi,pia nyumba 1,524 zenye nyufa mbalimbali zinazohitaji ukarabati, Taasisi za serikali 91 na taaisis 71 za watu binafsi ikiwemo makanisa na misikiti imeathirika na tetemeko hilo.
 
Ameongeza kuwa tayari amepata msaada wa Serikali katika tukio hilo kupitia Kamati ya Maafa ambapo jumla ya maturubai 520 amepewa kwa ajili ya maeneo mbalimbali, chakula, blanketi 240 ambazo pia zimegaiwa kwa waathirika hao.
 
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Bugandika Bw. Amudi Migeyo amewataka wananchi wake kutobeza juhudi za Serikali zinazofanywa sasa na amewataka kuridhika na chochote wakipatacho katika kipindi hiki kigumu.
 
Hivi karibuni siku ya tarehe 10 Septemba, 2016 mkoa wa Kagera ulikumbwa na ukubwa wa nguvu za mtetemo wa ardhi wa tetemeko la 5.7 kwa kutumia skeli ya ‘Ritcher’ ambapo jumla ya watu 17 walipoteza maisha na majeruhi kadhaa ambapo wengi wao wameshapatiwa matibabu na wanaendelea vizuri.
 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kagera Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa