Home » » SEKTA YA KILIMO KAGERA YACHECHEMEA

SEKTA YA KILIMO KAGERA YACHECHEMEA

na Ashura Jumapili, Bukoba
UKUAJI wa sekta ya kilimo katika Mkoa wa Kagera ni mdogo ikilinganishwa na lengo la ukuaji wa asilimia sita ulioainishwa katika mpango wa maendeleo wa miaka mitano 2011/12 hadi 2012/16.
Kauli hiyo ilitolewa na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Kanali mstaafu Fabian Massawe wakati akifunga maonesho ya kilimo ya Nanenane, katika viwanja vya Kyakairabwa mkoani humo.
Kanali Massawe alisema ukuwaji mdogo wa sekta ya kilimo katika mkoa wa Kagera unachangiwa na uwekezaji mdogo pamoja na kuendeleza dhana ya kilimo cha mazoea cha jembe la mkono.
Alisema juhudi zilizofanywa na serikali ni kuendeleza masoko ya mazao kupitia program ya miundombinu ya masoko, uongezaji wa thamani mazao na huduma za kifedha vijijini.
Alisema miradi inayoanzishwa na serikali katika kuleta maendeleo na ustawi wa wananchi wake inahitaji uratibu mzuri, usimamizi madhubuti na utekelezaji wenye ufanisi ili kuweza kufikia tija ambayo inalengwa na serikali.
Alisema akiwa katika ziara ya kutembelea na kukagua baadhi ya miradi ya kilimo na mifugo inayotekelezwa katika wilaya za mkoa wa Kagera chini ya mipango ya kuendeleza kilimo ya DADPs na DASIP, alikuta hali isiyoridhisha katika miradi hiyo.
Chanzo: Tanzania Daima

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kagera Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa