Tuhuma za ufisadi: CAG aiokoa CCM Bukoba

  Meya Amani akwepa kura ya kutokuwa na imani, ajiuzulu
  Kama ilivyokuwa kwa Balozi Kagasheki bungeni, Pinda ahusika
Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utoah
Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utoah, amekiokoa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutoka kwenye mgawanyiko uliodumu miongoni mwa madiwani wake kwa zaidi ya mwaka mmoja.
Taarifa ya CAG kuhusu utata uliodaiwa kuwapo kwenye mikataba iliyosainiwa kuhusu miradi mbalimbali ya maendeleo, imebaini ‘madudu’ yaliyosababisha kujiuzulu kwa Meya wa Manispaa ya Bukoba, Dk Anatory Amani.
Hoja ya kuwapo kwa mikataba yenye utata ikihusishwa na ufisadi, ikidaiwa kukiukwa taratibu na sheria ya manunuzi ya umma, iliwagawa madiwani wa CCM katika manispaa hiyo na kuathiri utendaji wa baraza la madiwani, lenye wawakilishi kupitia vyama vya upinzani.
Pamoja na asili ya mgogoro huo kuwa katika mikataba yenye utata, mpasuko kwa madiwani wa CCM, ulihusishwa na ‘mbio za ubunge’ wa Bukoba Mjini kwa Uchaguzi Mkuu wa mwakani.
Pande mbili za madiwani hao zikagawanyika katika kuwaunga  Dk Amani na Mbunge wa Bukoba Mjini, Balozi Kagasheki.
Wawili hao walishawahi kukutanishwa katika vikao mbalimbali vya CCM kuanzia ngazi ya wilaya hadi Kamati Kuu (CC) ya CCM iliyowahoji mjini Dodoma, Agosti mwaka jana.
Kufuatia kuhitimishwa kwa ukaguzi wa CAG na kugundulika kwa kasoro kadhaa, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, alimshauri Dk Amani kutumia busara ya kujiuzulu wadhifa huo kwa manufaa ya wananchi.  
Akitangaza hatua hiyo jana, Dk Amani ambaye pia ni diwani wa kata Kagondo, alikubaliana na ushauri wa Pinda, kuwa ajiuzulu kwa hiari yake, kabla ya madiwani kupiga kura ya kutokuwa na imani naye.
Kujiuzulu kwa Dk Amani, kumekuja siku 27 baada ya hatua kama hiyo kuchukuliwa na Mbunge wa Bukoba Mjini aliyekuwa pia Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki.
Wakati Dk Amani aliepuka kura ya kutokuwa na imani kutoka kwa madiwani jana, Balozi Kagasheki, alijiuzulu Desemba 21, mwaka jana, muda mfupi kabla ya tamko la Rais Jakaya Kikwete, kuwawajibisha yeye na wenzake watatu. 
Mawaziri wengine waliokuwa kwenye ‘kapu moja’ na Balozi Kagasheki, ambao Rais Kikwete alisitisha uteuzi wao kutokana na kashfa zilizoibuka wakati wa Operesheni Tokomeza Majangili ni pamoja na Emmanuel Nchimbi (Mambo ya Ndani ya Nchi).
Wengine walikuwa na wizara walizokuwa kwenye mabano ni David Mathayo (Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi) na Shamsi Vuai Nahodha (Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa). 
Taarifa ya Pinda kumshauri Dk Amani ajiuzulu, ilisomwa na Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Agrey Mwanri.
Mwanri alisoma taarifa hiyo katika mkutano ulioitishwa na ofisi ya Waziri Mkuu, ikiwa ni hitimisho la taarifa ya ukaguzi wa CAG katika manispaa hiyo na ushauri wake kwa serikali.
Pinda, kupitia kwa Mwanri, alisema kufuatia tuhuma zinazomkabili Dk Amani, kusaini mikataba yenye utata ni bora ajiuzulu kwa manufaa ya umma.
Mbali na Dk Amani,  taarifa ya Pinda iliagiza aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa manispaa hiyo, aliyehamishiwa wilaya mpya ya Momba mkoani Mbeya, Khamis Kaputa, avuliwe madaraka hayo.
Pia, Pinda aliagiza kuvuliwa madaraka kwa wakuu wa idara za uhandisi, Mhandisi Steven Nzihirwa, kitengo cha manunuzi, Baraka Marwa na Mweka Hazina Amduni Uromi.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Pinda, aliagiza uongozi wa manispaa hiyo kupitia upya taarifa ya CAG na kutoa maelezo yake kwa Katibu Mkuu (Tamisemi) ndani ya siku saba, baada ya kukabidhiwa taarifa ya CAG.
Kabla ya tamko la Pinda, Utouh aliwasilisha ripoti ya uchunguzi iliyobaini kuwapo mikataba iliyosainiwa na manispaa hiyo, chini ya uongozi wa Dk Amani.
Mikataba hiyo ilibainika kukiuka taratibu za matumizi ya fedha za umma, ikiwamo kutojadiliwa na kikao cha baraza la madiwani.
Utouh, alisema kuwa mikataba hiyo ilisababishia kuzuka kwa mgogoro na hasara kubwa kwa manispaa hiyo, ikiwamo kukosa mapato ya zaidi ya Shilingi milioni 256.2 katika kipindi cha mwaka 2012/2013 na 2013/2014.
Fedha hizo ni ambazo zingetokana na ushuru wa soko kuu la Bukoba, uliosimamishwa kutokana na mgogoro huo.
Baadhi ya mikataba  iliyothibitishwa na CAG kusainiwa kinyume cha utaratibu ni wa ujezi wa soko kuu jipya na la kisasa na ujenzi wa jengo la kitega uchumi lililopo eneo la kituo kikuu cha mabasi.
Miradi mingine ni ujenzi wa kituo kikuu cha mabasi eneo la Kyakailabwa, zabuni ya kukusanya ushuru katika kituo kikuu cha mabasi  na mradi wa upimaji viwanja.
Utouh, alisema Pinda, aliiomba ofisi ya CAG kufanya ukaguzi maalum katika manispaa ya Bukoba, kutokana na kuwapo kutoelewana kulikosababisha makundi na vikao vya kisheria vya madiwani kutofanyika.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Kanali mstaafu Fabian Massawe, aliwataka madiwani wa halmashauri hiyo na watendaji kuipokea taarifa hiyo na maelekezo ya serikali kwa manufaa ya wananchi wa Bukoba.
Kanali Massawe, alisema kuwa mgogoro huo ambao umedumu kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa, umesababisha kukwamisha miradi ya maendeleo ya wananchi.
Kwa mujibu wa Kanali mstaafu Massawe, miongoni mwa miradi hiyo ilipaswa kufadhiliwa na Benki ya Dunia ikiwa na thamani ya Shilingi bilioni 18.5. 
Pia, alisema madiwani wa manispaa hiyo walishindwa kufanya vikao vya kisheria, kikiwamo cha kupitisha mapendekezo ya bajeti ya mwaka 2014/2015.
CHANZO: NIPASHE

TAARIFA KAMILI : MDHIBITI NA MKAGUZI MKUU WA HESABU ZA SERIKALI AFANYA KIKAO KIZITO BUKOBA LEO.CHAMFUKUZISHA KAZI MEYA NA WENGINE KUCHUKULIWA HATUA ZA KISHERIA.




Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kutoka Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bw. Ludovick Utouh akitoa taarifa ya ukaguzi maalum leo Bukoba. Naibu Waziri wa TAMISEMI Mhe. Agrey Mwanri akiendelea kutoa Maelezo ya Serikali. Kuhusu Suruhisho hilo ambapo yamebainika Makosa ya Meya Anatory kufanya makubaliano bila idhini ya Madiwani na Taratibu za serikali, Basi ajipime Mwenyewe na Kujiuzulu mara moja kwa Maslahi ya Manispaa ya Bukoba. Mkuu wa mkoa wa Kagera Mh.Fabian Massawe akimkaribisha mgeni Rasmi leo kwenye kikao hicho cha kukamilisha Ukaguzi Maalum" Exit Meeting"  Cha mdhibiti na mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali leo Januari 17.2014 Mjini Bukoba ambapo kikao hicho kilianza mapema saa 5 Asubuhi.
Wadau mbalimbali wakiwa kwenye kikao hicho kizito kilichofanyika leo mjini Bukoba na kupelekea Meya Anatory Amani kujiuzulu kufuatia ubadhirifu wa fedha uliobainika.
== SOMA TAARIFA YA CAG HAPA CHINI. ===== =====  ======= TAARIFA YA CAG
Waziri mkuu alituomba tufanye ukaguzi maalum,
Mwaka 2013 tulifika bukoba na kufanya kikao cha kwanza na wadau.
Katika kikao hicho nilitoa maombi ambayo mliyafuata nawashukuru,madiwani na wananchi walitusaidia saan

Natoa taadhari kwamba tulikuwa na adidu za rejea ambazo ndizo tulizofuata,tulipokea mombi ya wananchi wengi lakini hayakuwepo katika adidu za rejea,hatukuyafanyia kazi

Kilichobainika
Tunapohitaji maendeleo,tunafanya vitu kwa nia njema bila kufuata taratibu


Kuhusu uwekezaji wenye mashaka kwenye kituo cha kuosha magari,zabuni haikuwa shindanishi  ni kiyume na taratibu cha taribu anataja kifungu kilichokiukwa
Waliosaini ni Khamis kaputa na anatory amani huku wakijua ilikuwa ni makosa kufanya hivyo bila idhjini ya kikao cha madiwani,pia kamupuni husika ya ASEC ilikuwa haijasajiliwa na BRELA. hailipi kodi TRA


2.Issue ya Viwanja

kati ya wananchi 800 waliotakiwa kugawiwa viwanja ni 300 waliogawawia kutokana na migogo ya viwanja kimila.


Manispaa ilingia makubaliano na UTT kupima viwanja elfu 5 kwa kuggawana faida ya asilimia 50 kwa 50 baina ya UTT manispaa ilisainiwa na kaimu meya ngalinda bila kupata idhini ya baraza la madiwani

Pia walikopa fedha kutoka UTT bila kupata ridhaa ya waziri mwenye thamana.

3.Issue ya matengenzo ya barabara mpya


Manispaa ya bukoba iliingia mkataba na mkandarsai aitwaye KAJUNA INVESTMENT mkataba ulikuwa wa sh 138 milioni alilipwa fedha za dharula amabzo hazikuwa na nyaraka hivyo malipo ya mkandarasi huyu yaliongezwea hadi kufikia sh sh 227 kwa kutumia barua iliyosainwa na tofauti na hali ya awali.haikuwapa idhini ya mkandarsi wa serikali na kinyume na kanuni za manunuzi ya umma.anasoma kifungu kilichokiukwa

 
4.issue ya Ujenzi wa soku kuu

Utaratibu wa kutaka kujenga soko kuu la bukoba haikupata idhini ya madiwani ya kumlipa mkandarasi mshauri OGM milioni 789 huku pia akawaita madiwani na kuwaeleza kuwa mkandarasi anahitaji jumla la miliini 590 mlioni. Mmojawapo wa madiwani mhg lunagisa alikataa pale pale kwenye kikao.

5.Issue ya kuhamisha wafanyabisha wa bukoba

Mh Meya anatory aman aliomba mkopo kwa kazi hiyo bila kibali cha madiwani na mawaziri.mkpo huo hata hivyo haukupoatika
6.Mkandaasi wa OGM hakuwa kwenye orodha ya walioomba zabuni ya kufanya kazi ya ukandarasi ushauri wa kufanya kazi katika ujenzi wa soko kuu lakini alionekana kwenye rodha baadye ya waliolipwa .Wakandarasi wote waliolipwa fedha hizo walikuwa hawalipi kodi TRA-hivyo TRA ina haki ya kuwadaiu hizo kodi.


7.Ujenzi wa stendi kuu ya bukoba

Mradi huu hakutengezwa kwenye gazeti la sertikali lakini walipata mkandarasi na kumlipa fedha za kazi hiyo kinyume na taratibu za serikali.gazeti lilotangaza tenda hiyo halikupatikana.pia timu ya ukaguzi ilitembelea eneo al kazi na kubaini kuwa mkandarasi alilipwa fedha nyhingi tofauti na kazi aliyoifanya


9.Mradi wa maji

Kila kata iliyopangwa kuwekwa mradi wa maji ilitakiwa kuchangia asilimia 2 hivyo kata anakotoka meya ilitiumiza kigezo na kupata huduma hiyo.fedha za kata zilitolewa na meya kwa kata yake.hivyo kitendo cha kata ya meya kupata huduma hakuwa na tatizo.Tuhuma hizi kuwa meya alitoa huduma kwa kata yakle ni uongo.
10.Issue ya uuzwaji viwanja vya wazi.
Mkataba wa kununua kiwanja kinacholalamikiwa hakufuata taratibu za ununuzi
Ni katika bweni la sekondari ya PEACE inayomilikiwa na Meya.Tunapendekeza kuundwa kwa trimu maalum kuchunguza tuhuma hizi kwani katika eneo hili hatukufikia mwisho




11.Ujenzi wa barabara kwa lami kwenye kata ya meya toafuti na fedha zilizoombwa

Manispaa iliomba milioni 30 kukaqrabati barabarab hiyo akini TAMISEMI ilitao milioni 300 na walihoji TAMISEMI walisema hilo ni la kawaida hivyo tuhuma hizo ni UONGO


12.Mradi wa Ujenzi wa Bwawa 

Hakuwahi kujadiliwa na baraza la madiwani,ulikuwa ni mradi wa wajanja tu



13.Issue ya wafganyabishara soko kuu kutolipa kodi

Manispaa Imekosa mapato sh milioni 256 zimpotea kutokana na chanzo hizo cha wafanyabishara wa soko kuu kutolipa kodi kutokana na mgogoro unaondelea


14.Issue ya matumizi ya gari Sm 4663

Gari hili limekuwa likiegeshwa kwa ofisi ya redio kasibante ya kagasheki.kumbukumbu za TRA zinaonesha kuwa ni mali ya halmashauri lakini alipohojiwa kagasheki alidai kuwa alinunua kwa fedha zake. Lakini halmshauri haina kumbukubu zozote juu ya gari hilo



Tunapendekeza alilrejeshwe kwenye halmshauri kama ataona ni manufaa kwa wananchi lakini kama haitawezekana basi gari hilo libadilishiwe usajhili ili lionekbnane ni la kiraia


15.Uteuzi wa wakala wenye upendeleo kwenye ushuru wa basi

Zabubi ya aliyepata rufaa ilitenguliwa kwani haikuwa imesajiliwa na mamlaka husika
Alibadilisha jina na kuomba tena kasha kupata,muombaji aliyeomba kwa tozo ya juu alinyimwa.





Manispaa ilifanya upendeleo na kukosa sh million 46 kwa mwaka




16:Issue ya posho kwa madiwani katika safari ya mafunzo nje ya wilaya.

Madiwani wawili walitakiwa kulipwa sh laki 4 kila mmoja kwa safari hawakusafiri lakini fedha hizo hazikurudishwa kwa manispaa na kukatiwa risiti,.hazionekjani zilipo






17.Issue ya vibanda vya maduka

Ukaguzi hakudhibitisha kuwepo tatizo la katika dai hili kwani nyaraka zinaonesha kutokuwepo tatizo.bali inashauri kuwepo kwa mkanganyiko na wapangaji wake





18.Issue ya deni katika uwanja wa mpira kaitaba.

Uwanja ulikarabatiwa na kiwanda cha sukari kagera kwa madai ya kurejeshewa fedha zake.sehemu ya fedha hazijarudishwa.Tume inapendekeza kufanya muafaka na kiwana au itafute fedha za kulipa deni





19.Kutowajibika ipasavyo kwa ukaguzi wa ndani.

Kipo kwa ajili ya kushauri na kuziba mianya ya matumizi mabaya ya fedha.
Aliyekuwepo amehojiwa juu ya miradi hiyo na kwamba halikuwa hajui lolote na hakuweza kumshauri mkurugenzi ipasavyo





20.Mteuzi katika bodi ya maji.upendeleo kwa mmoja wa madiwani

Waziri mwenye thamana aliteuwa



Hitimisho.

Hatukuweka chumvi,tuliyosema ndiyo ukweli tupu
Namshukuru waziri mkuu kwa kunipa kazi hii ya kukaguzi katika manispaa





Utaratibu wa uwasilisahji wa ripoti maalum tutaipeleka kwa aliyeomba ukaguzi huu.

ASANTENI AMEMALIZA





Mwanry anaongea sasa

Kwa niaba ya waziri mkuu naomba nitoa taarifa hii kama ifuatavyo





Maelekezo ya waziri mkuu.

Makosa ya meya anatory kufanya makubaliano bila idhini ya madiwani na taratibu za serikali basi ajipimemwenyewe na kujiuzuru kwa maslahi ya manispaa ya bukoba.





Akikataa basi madiwani wamuondoe





Watumishi wa manispaa wachukuliwe hatua

Bw Khamis kaputa avuliwe madaraka
Mhandisi,mweka hazina nk wapoteze vyeoi vyao





Wakandarasi wote waliopata fedha bila taratibu wazirejeshwe

Diwani asomewa shtaka kitandani

DIWANI wa Kata ya Magata Kalutanga, Geofrey Ezekiel (CCM), aliyekamatwa juzi na kuwekwa ndani kwa amri ya Mkuu wa Wilaya ya Muleba, Limbris Kipuyo, jana alisomewa shtaka akiwa kitandani katika  Kituo cha Afya Kaigara.
Taarifa zilizolifikia gazeti hili kutoka wilayani humo, zilisema kuwa Ezekiel alisomewa shtaka hilo namba 11/ 2014 saa 4:30 asubuhi akidaiwa kutishia kumjeruhi mkuu wa wilaya kwa kummwagia tindikali.
Akizungumza na gazeti hili kwa simu, mtoa taarifa wetu alisema kuwa diwani huyo alisomewa shtaka hilo na Kaimu Hakimu wa Mahakama ya wilaya aliyetambulika kwa jina moja la Ngonyani.
“Anadaiwa kutenda kosa hilo Januari 6, mwaka huu. Lakini mpaka sasa tunashughulikia dhamana maana alishutukizwa, hakuwa ameandaa wadhamini. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Febuari 3, mwaka huu,” alisema.
Ezekiel alikamatwa juzi akidaiwa kutishia kumuua mkuu wa wilaya na baada ya mahojiano na polisi alipekuliwa nyumbani kwake kisha kushikiliwa kituoni hadi saa 12:00 jioni afya yake ilipobadilika ghafla na kukimbizwa hospitali.
Chimbuko la mzozo huo ni baada ya diwani huyo kuandika barua ya kumshtaki mkuu huyo kwa uongozi wa CCM Wilaya ya Muleba kwa kile kilichoelezwa ni kutuhumiwa kula fedha za miradi.
Kipuyo anadaiwa kumtuhumu diwani huyo katika kikao cha Kamati ya Siasa ya Wilaya cha CCM cha Januari 5, mwaka huu, kuwa anatumia wadhifa wake wa uenyekiti wa Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira kufuja fedha za miradi akishirikiana na wahandisi wa halmashauri.
Pia alidai kuwa diwani huo anakwamisha miradi ya maendeleo kwa makusudi, tuhuma ambazo alizirudia mbele ya kikao cha Kamati Kuu ya Wilaya cha Januari 6, mwaka huu.
Baada ya Kipuyo kubaini ameshtakiwa kwa uongozi wa CCM, alitumia mamlaka yake kuagiza polisi wamkamate diwani huyo na kumchukulia hatua za kisheria, akidai ametishia kumuua kwa tindikali.
Chanzo;Tanzania Daima 

UPDATES: REPOTI YA CAG YAMWAJIBISHA MEYA WA MANISPAA YA BUKOBA, ANATORY AMANI

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Ludovick S.L. Utouh. akisoma ripoti ya CAG kwenye halmashauri ya mansipaa ya Bukoba leo.
 
 Naibu waziri wa TAMISEMI, Mh. Aggrey Mwanri akizungumza wakati wa ripoti ya CAG kwenye manispaa ya mji wa bukoba leo 
 Wa kwanza kulia ni Meya wa  Manispaa ya Bukoba,Bwana Anatory Amani aliyewajibishwa kwenye ripoti ya CAG na pia inamtaka ajiuzuru
Kikao kikiendelea

Breaking News! Repoti ya CAG yamwajibisha meya Anatory Amani

Wakiendelea kusoma mambo mbalimbali..

Endelea kufuatilia ...

Picha kwa hisani ya Bukoba wadau

MFUKO WA PENSHENI KWA WATUMISHI WA UMMA(PSPF) UNAWATAKIA WATU WOTE SIKUKUU NJEMA MAULID



JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
MFUKO WA PENSHENI WA PSPF






MAADHIMISHO YA SIKU YA KUZALIWA KWA MTUME MUHAMMAD (Swalla Allaahu alayhi wa aalihi wa sallam)
Bodi ya Wadhamini na Wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) wanaungana na Waisalamu na Watanzania wote katika kusheherekea siku ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (Swalla Allaahu alayhi wa aalihi wa sallam)
“PSPF TULIZO LA WASTAAFU”
Mkurugenzi Mkuu,

PSPF

SALAM ZA MIAKA 50 YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR KUTOKA MFUKO WA PENSHENI KWA WATUMISHI WA UMMA(PSPF)








JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
MFUKO WA PENSHENI WA PSPF





Bodi ya Wadhamini na Wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) wanaungana na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt Ali Mohamed Sheni pamoja na wananchi wote wa Tanzania katika kuadhimisha miaka hamsini ya Mapinduzi ya Zanzibar, 12 Januari 2014. 

 


Kwa Mahitaji yako ya Hifadhi ya Jamii PSPF ni chaguo lako, Jiunge sasa

“PSPF TULIZO LA WASTAAFU”

Mkurugenzi Mkuu,

PSPF

MFUKO WA PENSHENI KWA WATUMISHI WA UMMA(PSPF) WAOMBOLEZA MSIBA WA ALIYEKUWA WAZIRI WA FEDHA MAREHEMU DKT. WILLIAM A. MGIMWA

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

MFUKO WA PENSHENI WA PSPF
Bodi ya Wadhamini na Wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) unatoa salamu za rambirambi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano  wa Tanzania Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Wizara ya Fedha na Familia ya aliyekuwa Waziri wa Fedha Marehemu Dkt. William A. Mgimwa
Mfuko utamkumbuka kwa ushauri wake na ushirikiano aliouonyesha akiwa Waziri wa Fedha katika kufanikisha maendeleo na ustawi wa Mfuko.
Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi.

AMIN

KATIBU CCM JELA KWA UDANGANYIFU

KATIBU wa Itikadi Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kyerwa, Ferdinand Bishanga (38), amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela baada ya kupatikana na hatia ya kujipatia mali kwa udanganyifu.
Hukumu hiyo ilitolewa jana katika Mahakama ya Wilaya ya Karagwe na Hakimu Mkazi Mfawidhi, Peter Matete, baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo.
Hakimu Matete alisema baada ya kumaliza kifungo, mshitakiwa atalazimika kulipa fedha hizo kwa mlalamikaji.
Alisema ametoa hukumu hiyo ili liwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hizo za kujipatia mali kwa njia ya udanganyifu pamoja na kuhitaji utajiri wa haraka.
Awali, Mwendesha Mashitaka wa Polisi, Juma Lipwata, alieleza kuwa mshitakiwa alifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Oktoba mwaka juzi.
Alidai mshitakiwa alipokea sh milioni 9 kwa udanganyifu kutoka kwa Vedasto Marchela, mkazi wa Kata ya Kayanga kwa lengo la kumnunulia kahawa kwa njia ya magendo.
Chanzo:Tanzania Daima

Muleba yajivunia ziada ya madarasa

WAKATI wanafunzi wengi wakikwama kujiunga kidato cha kwanza mwaka huu kutokana na uhaba wa madarasa unaozikabiri baadhi ya halmashauri nchini, Wilaya ya Muleba, mkoani Kagera imetamba kuwa na madarasa ya ziada.
Mafanikio hayo yalibainishwa hivi karibuni na Ofisa Elimu Taaluma wa wilaya hiyo, Mlashani Rwenyagira alipohojiwa na gazeti hili ofisini kwake.
Alisema kuwa kwa sasa Wilaya ya Muleba inazo sekondari 35 za serikali na nane za binafsi ambazo kwa pamoja zina wanafunzi 15,143 kabla ya uteuzi wa kidato cha kwanza.
“Kwa mwaka huu, tulitarajia kupeleka sekondari asilimia 70 ya wanafunzi kati ya 9,872 waliofanya mtihani wa darasa la saba mwaka jana.
“Kwa idadi hiyo ni kwamba tunahitaji vyumba 179 vya madarasa lakini vilivyopo mpaka sasa ni 201, hivyo hatuna uhaba wa madarasa bali tuna ziada,” alisema.
Kwa mujibu wa Rwenyegira kati ya idadi hiyo, shule mbili ni za kidato cha tano na sita ambazo ni Kishoju na Rutabo.
Kuhusu mahitaji ya walimu, alisema wana uhaba kwa mchepuo wa sayansi kwani wengi wa wanaoletwa ni wale wanofundisha masomo ya sanaa.
Aliongeza kuwa licha ya kuwa na uhaba huo wa walimu wa sayansi, mchakato wa ujenzi wa maabara unaendelea na sasa zimejengwa katika shule 16 huku nyingine nne zikiwa kwenye ujenzi.
“Lakini pia ziko sekondari nne za Ibuga, Mayondwe, Kibanga na Kanyeranyere zinatumia maabara inayotembea (mobile Laboratory).
Pia Rwenyagira aligusia fedha za maendeleo ya shule akisema kuwa zinagawiwa kutegemeana na uwezo wa mfuko wa halmashauri na mahitaji ya shule husika.
Alifafanua kuwa kwa mwaka juzi, mgawo ulikuwa sh milioni 7 na kwa mwaka jana, shule 21 tayari zimepatiwa fedha hizo ambapo kila moja alipata sh milioni 8.8.
Kwa mujibu wa ofisa huyo, mwaka juzi bajeti ya elimu ya wilaya hiyo ilikuwa sh bilioni 1.4 lakini walipatiwa sh milioni 700 pekee ambayo iliunganishwa na ile wanayopewa na halmashauri kupitia vyanzo vyake.
Chanzo;Tanzania daima

Kilaini atoa neno la 2014

Askofu Msaidizi wa Kanisa Katoliki nchini, Jimbo Kuu la Bukoba, mkoani Kagera, Method Kilaini ametoa wito kwa Watanzania kupiga vita viashiria vya uvunjifu wa amani.

Alisema mwaka 2014, Watanzania wote wanapaswa kuilinda amani iliyopo hasa kipindi hiki cha mchakato wa kupata Katiba Mpya kwani wapo baadhi ya watu wachache wanaoonesha
viashiri vya uvunjifu wa amani.

Askofu Kilaini aliyasema hayo jana wakati akizungumza na Majira ili kupata maoni kwa Watanzania ambao leo saa sita usiku, watauanza mwaka mpya wa 2014.

"Amani tuliyonayo hatupaswi kuichezea hata kidogo, nchi nyingine wanaitafuta kwa muda mrefu na hawaipati hivyo tusiruhusu mtu yeyote aichezee amani yetu," alisema.

Aliwataka Watanzania kuendeleza umoja na mshikamano dhidi yao bila kujali dini, ukabila wala rangi

Chanzo;Majira

Wanasiasa wamchefua January Makamba

image

Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Bw.January Makamba, amekemea tabia ya baadhi ya wanasiasa nchini kutumia mkondo wa dini kisiasa kwani hilo ni kosa
kubwa kwa mustakabali wa amani ya nchi.

Bw. Makamba aliyasema hayo juzi Mjini Bokoba, mkoani Kagera, wakati akizungumza kwenye Tamasha la Amani ambalo liliandaliwa na Nazareth Singers kwa kushirikiana na wadau mbalimbali.

Alisema wanasiasa wenye tabia hiyo wanaamini kuwa waumini wa dini yake watamuunga mkono katika uchaguzi jambo ambalo ni hatari kwa sababu anapogombea uongozi, wananchi ndio wanaopiga kura bila kujali dini zao.

Aliongeza kuwa, viongozi wa dini wamefanya kazi kubwa ya kulinusuru Taifa kutokana na chokochoko za kidini kupitia mahubiri yao kwani bila wao, hali ingekuwa mbaya zaidi.

Aliwaomba viongozi wa madhehebu ya dini nchini, kuendelea kuhubiri amani, upendo na mshikamano miongoni mwa Watanzania ili kudumisha amani iliyoasisiwa na Hayati Julius Nyerere.

"Baada ya kuibuka kwa chochoko za kidini nchini, viongozi wa dini wamefanya kazi kubwa ya kuhubiri amani, upendo na mshikamano miongoni mwa wananchi...mahubiri yao
yamesaidia kupunguza chokochoko hizo," alisema.

Bw. Makamba alisema madhara ya Taifa kukosa amani ni makubwa na kusisitiza umuhimu wa wananchi kuheshimu imani za watu wengine.

Alikemea tatizo la ukosefu wa haki na usawa katika jamii juu ya upatikanaji wa huduma mbalimbali za msingi ikiwemo elimu na afya miongoni mwa Watanzania.

"Unapoona katika jamii hakuna haki na usawa hilo ni tatizo,kwa mfano, ukiona kuna watu wanapata elimu au huduma tofauti na wanayopata wengine, uhakika wa amani
unakuwa hatarini," alisema.

Aliwapongeza waandaaji wa tamasha hilo ambalo liliwakutanisha waumini wa dini mbalimbali mkoani humo na kusisitiza kuwa, ujumbe uliotolewa usambazwe nchi nzima.

Aliahidi kusaidiana na waandaaji hao kuhakikisha ujumbe huo wa amani unafika maeneo mbalimbali nchini.

Awali Mkuu wa Mkoa huo, Kanali mstaafu Fabian Massawe,alisema amani ya Tanzania ipo mashakani kutokana sababu mbalimbali kama malumbano ya kidini, kisiasa, matumizi ya dawa za kulevya kwa unyanyasaji wa kijinsia.

Chanzo;Majira

MISSENYI YATOA MIKOPO MIL 60

Halmashauri ya wilaya ya Missenyi mkoani Kagera imetoa mikopo ya zaidi ya shilingi milioni 60.1 kwa vikundi mbalimbali vya wanawake na vijana katika kipindi cha miaka sita iliyopita.

Taarifa iliyotolewa na mkurugenzi wa halmashauri hiyo Elzaberth Kitundu imesema kuwa mikopo hiyo imetolewa kuanzia mwaka wa fedha 2007/2008 hadi 2012/2013.

Kitundu amesema kuwa katika kipindi hicho vikundi vya akina mama vilipatiwa mikopo ya zaidi ya shilingi milioni 40.8 ambapo  vikundi vya vijana vilipatiwa mikopo ya zaidi ya shilingi milioni 19.3.

Amesema kuwa lengo la halmashauri hiyo kuviwezesha vikundi vya wanawake na vijana kwa kuwapatia mikopo  ni kutaka  kuinua mitaji yao,  na kuwa hali ya marejesho kwa vijana sio mbaya isipokuwa kwa upande wa wanawake ndio wanarejesha kwa kusuasua.

Amesema kuwa katika kuhakikisha vikundi hivyo vinakuwa endelevu, wamekuwa wakiwashauri wanachama wake kuanzisha vyama vya akiba na mikopo (SACCOS) na kuwa katika wilaya hiyo hadi sasa kuna vyama vya ushirika 73, vikiwamo vya mazao 28, Saccos 36 ambapo vyama tisa ni vya mchanganyiko.

Wahamiaji warudi kwa kasi Kagera

Katika hali isiyo ya kawaida, wahamiaji haramu waliorejeshwa nchini mwao na serikali katika ‘Operesheni Kimbunga’ wameanza kurejea kwa wingi katika Wilaya ya Kyerwa, mkoani Kagera wakijiita M23 na kupora mali za wananchi kwa nguvu.
Mkuu wa Wilaya hiyo, Mhandisi Benedict Kitenga, aliyasema hayo jana wakati akitoa taarifa kwa Mkuu wa Mkoa huo Kanali mstaafu, Fabian Massawe ambaye alitembelea wilaya hiyo kukagua shughuli za maendeleo na ujenzi wa maabara katika shule za sekondari za kata.
Alisema wahamiaji hao wamejazana katika Kijiji na Kata ya Kibingo wakiwatisha wananchi ambao hivi sasa wanahofia usalama wa maisha yao na mali zao.
Aliongeza kuwa, baada ya Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya kupata taarifa hizo, ilikwenda eneo la tukio na kufanya operesheni kubwa na kufanikiwa kukamata wahamiaji haramu zaidi ya 20 na baadhi ya Watanzaia waliokuwa wakiwahifadhi.
Mhandisi Kitenga alisema baada ya kukamatwa, wahamiaji hao walirudishwa katika nchi zao bila kutaja uraia wao na Watanzania waliohusika kuwahifadhi wamechukuliwa hatua za kisheria.
“Kutokana na hali ilivyo, wananchi wanapaswa kutoa taarifa wawaonapo wahamiaji haramu katika maeneo yao,” alisema.
Kwa upande wake, Bw. Massawe alisema, katika “Operesheni Kimbunga”, wahamiaji haramu walirudishwa katika nchi zao, lakini operesheni hiyo inaendelea ili kuhakikisha waliobaki wanakamatwa na kurudishwa nchini mwao.
“Chini ya Kaulimbiu ya Hakuna wa Kubaki na Hakuna wa Kurudi, tutahakikisha kila mhamiaji haramu anaondoka na Watanzania ambao watabainika kushirikiana nao pia watachukuliwa hatua za kisheria.
“Naiagiza Kamati za Ulinzi na Usalama kuendelea na operesheni hadi wahamiaji haramu wamalizike,” alisisitiza Bw. Massawe na kuwataka wananchi watoe taarifa kwa viongozi wanapowaona na kutoa namba zake za simu.
Hata hivyo, baadhi ya wananchi waliohojiwa walisema tatizo la wahamiaji haramu linachangiwa na baadhi ya watendaji wa Serikali ngazi za chini ambao wanachukua hongo na kuwarudisha.
Walisema inavyoonekana, viongozi wa chini kuanzia ngazi ya vitongoji, vijiji hadi kata, wamepewa mamlaka makubwa pia wamekuwa wakikaa muda mrefu bila kubadilishwa vituo vya kazi na hivyo kujenga mazoea na wahamiaji hao.
“Serikali kuanzia ngazi ya Wilaya, iwe na utamaduni wa kuwatembelea viongozi wa vitongoji na kata kwa kushtukiza ili kukomesha tabia hii ambayo wamejijengea na kuonekana miungu watu katika maeneo yetu,” alisema mkazi wa eneo hilo ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini.
Hivi karibuni Serikali ilifanya “Operesheni Kimbunga” na kushirikisha vyombo mbalimbali vya ulinzi na usalama baada ya Rais Jakaya Kikwete kutoa wiki mbili kwa wahamiaji haramu wawe wameondoka nchini kwa hiari yao.

Chanzo;Majira

Waziri Magufuli atajwa kesi ya wizi wa pembejeo

Waziri wa Ujenzi, Dk,John Magufuli
 
Kesi ya ubadhilifu wa fedha za pembejeo za kilimo inayowakabili aliyekuwa mkuu wa Wilaya ya Chato, Hadija Nyembo, aliyekuwa Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Hamida Kwikwega na wenzao watatu, imechukua sura mpya baada ya mawakili wa washitakiwa kumtaja Waziri wa Ujenzi, Dk, John Magufuli, kuhusika.
Hatua hiyo imefuatia Mahakama hiyo kuanza kupokea ushahidi wa upande wa mashitaka ukiongozwa na wakili wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Kelvin Murusuri.

Shahidi namba moja ambaye ni mchunguzi wa Takukuru, Said Bakari (39), alidai kuwa kwa kipindi cha mwaka 2010/11 washitakiwa hao walitenda makosa mbalimbali ikiwemo kutumia madaraka yao vibaya kisha kumteua wakala wa usambazaji wa pembejeo asiye na sifa.

Alisema mshitakiwa namba moja Nyembo ambaye alikuwa mkuu wa wilaya ya Chato kabla ya kuhamishiwa Uvinza, akiwa Mwenyekiti wa kamati ya pembejeo ya wilaya hiyo alihusika kuwapitisha wazabuni wa usambazaji wa pembeo wasio na sifa katika kikao kilichofanyika Julai 6, mwaka 2010.

Alidai kuwa mshitakiwa namba mbili Kwikwega anayetetewa na wakali wa kujitegemea Deogratias Rutahindurwa, alidaiwa mahakamani kupitisha baadhi ya nyaraka za kuwatambulisha mawakala waliopitishwa kinyume cha sheria na kamati ya pembejeo ya wilaya kwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera.

Wengine waliofikishwa mahakamani ni aliyekuwa Ofisa Kilimo na Mifugo wa wilaya hiyo, Dk. Pheres Tongora, ambaye pia aanashitakiwa kuteua na kuwapitisha mawakala wasio na sifa.

Wengine ni mshitakiwa namba nne aliyekuwa wakala wa usambazaji wa pembejeo kata ya Buseresere, Mery David pamoja  na Kaimu mtendaji wa kijiji cha Mapinduzi, Mageni Mbassa.

Shahidi huyo aliwasilisha vielelezi vinne zikiwemo barua na mihutasari ya vikao vya kamati ya pembeo vilivyoketi na kupitisha maamuzi ya kuwapata mawalala wa usambazaji bila kufuata taratibu za manunuzi ya umma.

Baada ya mashahidi wa kwanza kumaliza kuwasilisha ushahidi wake, wakili wa Rutahindurwa alitaka kujua sababu za Waziri wa ujenzi na mbunge wa jimbo la Chato,Dk Magufuli kushindwa kuhusishwa katika mashitaka hayo licha ya kuwa mmoja wa wajumbe wa kamati ya pembejeo ya wilaya hiyo.

Alisema iwapo kamati ya pembejeo ilifanya maamuzi yasiyo fuata taratibu kanuni na sheria za manunuzi iweje baadhi ya wajumbe wake akiwemo Dk. Magufuli wasihusishwe kwenye mashitaka hayo.

Wakili anayemtetea Mery David,Tuguta Fadhili alihoji kuwa kama kesi hiyo ilifikishwa mahakamani hapo kutokana na shinikizo la Waziri wa Ujenzi Dk. Magufuli.

Alidai kuwa iwapo kikao cha kamati ya pembejeo kiliyoketi Julai 6, 2010 kilikuwa halali iweje maamuzi yake yaonekane hayakuwa sahihi na kumhusisha pia mshitakiwa namba mbili (Kikwega) ambaye siku ya kikao hicho hakuwapo katika maamuzi hayo.

Mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya hiyo, Jovith Katto baada ya upande wa washitakiwa kumaliza kuhoji maswali yao mahakama hiyo iliahilishwa kwa ajili ya kupokea ushahidi wa mashahidi namba mbili ambaye ni Ofisa Ugavi wa wilaya hiyo, Machage Mwema.
 
CHANZO: NIPASHE

Ulaji wetu na maradhi ya kisukari-3

Tulijifunza katika makala mbili zilizopita kuwa binadamu hawezi kuishi bila ya kula vyakula vyenye wanga, mafuta na protini.
 Njia za kuyakabili maradhi ya kisukari
Tunaweza kuyakabili maradhi ya kisukari kwa njia kuu nne. Mosi, kuwa na elimu kuhusu maradhi ya kisukari na mtu kuwa na uwezo wa kujipima kiwango cha sukari mwilini mwake.
Pili, ni kula mlo kamili, tatu kufanya mazoezi na nne ni kupata tiba sahihi ya maradhi ya kisukari.
Njia hizi ni muhimu kuzifahamu kwa wagonjwa wa kisukari na wale ambao hawajapatwa na maradhi hayo, yanayoongezeka kwa kasi duniani kutokana na maisha ya kisasa kama vile kula vyakula vyenye mafuta, sukari na chumvi nyingi.
Kama umepatwa na kisukari
Ingawa maradhi ya kisukari yana kishindo kikubwa, lakini watu waliopatwa na ugonjwa huo wanashauriwa wasichanganyikiwe wala kuhuzunika. Kufanya hivyo ni kuongeza maradhi katika miili yao.
Wanachotakiwa ni kuukabili ugonjwa huo kwa kujiamini. Na hilo litawezekana endapo wagonjwa hao wataelekeza nguvu zao katika kuujua ugonjwa huo kwa undani.
Kujua huko kutawafanya wabadili mtindo wa maisha yao kama vile kula mlo kamili, kufanya mazowezi, kuacha kunywa pombe, kunywa maji ya kutosha, kulala muda wa kutosha, kudhibiti hasira na msongo wa mawazo.
Wapi utapa elimu?
Elimu kuhusu maradhi ya kisukari inaweza kupatikana kwa njia mbalimbali kama vile kusoma vitabu na magazeti, kusoma katika mitandao ya kijamii, kuhudhuria semina, kusikiliza vipindi vya mada hiyo kutoka katika redio na luninga.
Vilevile, elimu ya ugonjwa wa kisukari inaweza kupatikana kwa wataalamu wa maradhi hayo waliopo katika kniniki za kisukari na hospitali mbalimbali.
Baadhi ya wagonjwa wa kisukari pia, wanaelimu kubwa ya maradhi hayo baada ya kuhangaika kwa muda mrefu kuitafuta elimu hiyo na uzoefu wao wa maisha kama wagonjwa.
Kuujua ugonjwa wa kisukari
Kama tunavyofahamu, binadamu ameweza kuleta mapinduzi makubwa katika maisha yake tangu enzi za zana za mawe mpaka sasa, enzi za dijitali kutokana na elimu.
Ni dhahiri pia, kuwa tutaweza kuyakabili maradhi ya kisukari kikamilifu kama tutakuwa na uwelewa wa kutosha juu ya maradhi hayo.
Tufahamu nini kama wananchi?
Kujua tunakokukusudia hapa sio kama vile wanavyofahamu wataalamu wa afya.
Wananchi wajue maana ya ugonjwa wa kisukari, aina za kisukari, sababu za kupata maradhi ya kisukari na dalili za kisukari.
Halikadhalika, watu wanatakiwa watambue hali gani mtu akiwa nayo (risk factors) yuko katika hatari ya kupata maradhi ya kisukari kama vile unene uliopitiliza, kuwa na shinikizo la damu, kuwa na msongo wa mawazo, ujauzito, kutokufanya mazoezi au kazi za kutoka jasho, na kuwa na miaka arobaini au zaidi.
Zaidi ya hayo, watu wanatakiwa wazijue athari mbaya za ugonjwa wa kisukari kama vile kuharibika kwa viungo vingine mfano macho, viungo vya uzazi, figo, mishipa ya fahamu na moyo.
Chanzo;Mwananchi
 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kagera Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa