KATIBU wa Itikadi Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya
Kyerwa, Ferdinand Bishanga (38), amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu
jela baada ya kupatikana na hatia ya kujipatia mali kwa udanganyifu.
Hukumu hiyo ilitolewa jana katika Mahakama ya Wilaya ya Karagwe na
Hakimu Mkazi Mfawidhi, Peter Matete, baada ya kuridhika na ushahidi
uliotolewa mahakamani hapo.
Hakimu Matete alisema baada ya kumaliza kifungo, mshitakiwa atalazimika kulipa fedha hizo kwa mlalamikaji.
Alisema ametoa hukumu hiyo ili liwe fundisho kwa watu wengine wenye
tabia kama hizo za kujipatia mali kwa njia ya udanganyifu pamoja na
kuhitaji utajiri wa haraka.
Awali, Mwendesha Mashitaka wa Polisi, Juma Lipwata, alieleza kuwa
mshitakiwa alifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Oktoba mwaka
juzi.
Alidai mshitakiwa alipokea sh milioni 9 kwa udanganyifu kutoka kwa
Vedasto Marchela, mkazi wa Kata ya Kayanga kwa lengo la kumnunulia
kahawa kwa njia ya magendo.
Chanzo:Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment