Home » » KISWAGA; WANANCHI WACHANGAMKIE KILIMO BADALA YA KUSUBIRI GESI

KISWAGA; WANANCHI WACHANGAMKIE KILIMO BADALA YA KUSUBIRI GESI

Festo Kiswaga
 
Madiwani na watendaji wa wilaya ya Nanyumbu mkoani Mtwara wameagizwa kuwahamasisha wananchi wa wilaya hiyo,  kuchangamkia fursa ya kilimo badala ya kutegemea gesi.
Agizo hilo lilitolewa jana na Mkuu wa wilaya hiyo, Festo Kiswaga, wakati akifungua kikao cha baraza la madiwani.

Alisema wilaya hiyo inategemea zaidi kilimo hususan katika mazao ya karanga, mbaazi, ufuta, korosho na kunde, hivyo kuwaagiza madiwani na watendaji wa wilaya hiyo kuhamasisha wananchi kujikita zaidi katika kilimo.

“Sisi huku tunaishi porini, na kama tuko porini ni lazima tufanye mapinduzi ya kilimo ikiwa ni pamoja na kuwahamasisha wananchi kutegemea zaidi kilimo ambacho ni uti wa mgongo,” alisema na kuongeza "Hata siku moja gesi haiwezi kutunufaisha wakazi wa Nanyumbu kwa kuinua kipato, gesi hii tuitegemee zaidi kwa ajili ya kupata umeme ambao utatusaidia kuleta maendeleo mengine,” alisistiza.

Alisisitiza uwekezaji na ushindani wa biashara hasa katika zao la ufuta ambalo alisema kuwa  Wachina wanahitaji tani 200 za zao hilo hivyo kuwataka wananchi kuboresha kilimo chenye tija.

Alitahadharisha kuwa gesi katika isiwe kisingizio kwa baadhi ya wananchi kuacha kilimo badala yake watumie fursa hiyo kuboresha kilimo cha mazao ya chakula ambayo yatauzika kwa wawekezaji wa gesi na kuwaongezea kipato na kuondokana na umasikini.

Katika kikao hicho halmashauri hiyo inakadiria kukusanya Sh. 17,111,839,126.00 kutoka katika vyanzo mbalimbali vya mapato katika mwaka wa fedha 2014/2015.

Akisoma makisio hayo jana katika kikao hicho, Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo, Eliza Bwana, alisema kuwa kumekuwepo na ongezeko la asilimia 32.2 ikilinganishwa na bajeti ya mwaka 2012/2013 ambayo ni Sh. 12,000,000,000.94

Alisema kuwa ongezeko hilo linatokana na nyongeza za idara na vitego ambapo itahitajika mishahara stahiki kwa watumishi wa  idara  na vitengo hivyo pamoja na gharama za uendeshaji wa ofisi.
 
CHANZO: NIPASHE

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Kagera Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa