Mdhibiti
na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kutoka Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Bw. Ludovick Utouh akitoa taarifa ya ukaguzi maalum leo
Bukoba.
Naibu
Waziri wa TAMISEMI Mhe. Agrey Mwanri akiendelea kutoa Maelezo ya
Serikali. Kuhusu Suruhisho hilo ambapo yamebainika Makosa ya Meya
Anatory kufanya makubaliano bila idhini ya Madiwani na Taratibu za
serikali, Basi ajipime Mwenyewe na Kujiuzulu mara moja kwa Maslahi ya
Manispaa ya Bukoba.
Mkuu
wa mkoa wa Kagera Mh.Fabian Massawe akimkaribisha mgeni Rasmi leo
kwenye kikao hicho cha kukamilisha Ukaguzi Maalum" Exit Meeting" Cha
mdhibiti na mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali leo Januari 17.2014 Mjini
Bukoba ambapo kikao hicho kilianza mapema saa 5 Asubuhi.
Wadau mbalimbali wakiwa kwenye kikao hicho kizito kilichofanyika leo mjini Bukoba na kupelekea Meya Anatory Amani kujiuzulu kufuatia ubadhirifu wa fedha uliobainika.
==
SOMA TAARIFA YA CAG HAPA CHINI.
===== ===== =======
TAARIFA YA CAG
Waziri mkuu alituomba tufanye ukaguzi maalum,
Mwaka 2013 tulifika bukoba na kufanya kikao cha kwanza na wadau.
Katika kikao hicho nilitoa maombi ambayo mliyafuata nawashukuru,madiwani na wananchi walitusaidia saan
Natoa
taadhari kwamba tulikuwa na adidu za rejea ambazo ndizo
tulizofuata,tulipokea mombi ya wananchi wengi lakini hayakuwepo katika
adidu za rejea,hatukuyafanyia kazi
Kilichobainika
Tunapohitaji maendeleo,tunafanya vitu kwa nia njema bila kufuata taratibu
Kuhusu uwekezaji wenye mashaka kwenye kituo cha kuosha magari,zabuni haikuwa shindanishi ni kiyume na taratibu cha taribu anataja kifungu kilichokiukwa
Waliosaini
ni Khamis kaputa na anatory amani huku wakijua ilikuwa ni makosa
kufanya hivyo bila idhjini ya kikao cha madiwani,pia kamupuni husika ya
ASEC ilikuwa haijasajiliwa na BRELA. hailipi kodi TRA
2.Issue ya Viwanja
kati ya wananchi 800 waliotakiwa kugawiwa viwanja ni 300 waliogawawia kutokana na migogo ya viwanja kimila.
Manispaa
ilingia makubaliano na UTT kupima viwanja elfu 5 kwa kuggawana faida ya
asilimia 50 kwa 50 baina ya UTT manispaa ilisainiwa na kaimu meya
ngalinda bila kupata idhini ya baraza la madiwani
Pia walikopa fedha kutoka UTT bila kupata ridhaa ya waziri mwenye thamana.
3.Issue ya matengenzo ya barabara mpya
Manispaa
ya bukoba iliingia mkataba na mkandarsai aitwaye KAJUNA INVESTMENT
mkataba ulikuwa wa sh 138 milioni alilipwa fedha za dharula amabzo
hazikuwa na nyaraka hivyo malipo ya mkandarasi huyu yaliongezwea hadi
kufikia sh sh 227 kwa kutumia barua iliyosainwa na tofauti na hali ya
awali.haikuwapa idhini ya mkandarsi wa serikali na kinyume na kanuni za
manunuzi ya umma.anasoma kifungu kilichokiukwa
4.issue ya Ujenzi wa soku kuu
Utaratibu wa kutaka kujenga soko kuu la bukoba haikupata idhini ya
madiwani ya kumlipa mkandarasi mshauri OGM milioni 789 huku pia akawaita
madiwani na kuwaeleza kuwa mkandarasi anahitaji jumla la miliini 590
mlioni. Mmojawapo wa madiwani mhg lunagisa alikataa pale pale kwenye
kikao.
5.Issue ya kuhamisha wafanyabisha wa bukoba
Mh Meya anatory aman aliomba mkopo kwa kazi hiyo bila kibali cha madiwani na mawaziri.mkpo huo hata hivyo haukupoatika
6.Mkandaasi wa OGM hakuwa kwenye orodha ya walioomba zabuni ya kufanya
kazi ya ukandarasi ushauri wa kufanya kazi katika ujenzi wa soko kuu
lakini alionekana kwenye rodha baadye ya waliolipwa .Wakandarasi wote
waliolipwa fedha hizo walikuwa hawalipi kodi TRA-hivyo TRA ina haki ya
kuwadaiu hizo kodi.
7.Ujenzi wa stendi kuu ya bukoba
Mradi huu hakutengezwa kwenye gazeti la sertikali lakini walipata
mkandarasi na kumlipa fedha za kazi hiyo kinyume na taratibu za
serikali.gazeti lilotangaza tenda hiyo halikupatikana.pia timu ya
ukaguzi ilitembelea eneo al kazi na kubaini kuwa mkandarasi alilipwa
fedha nyhingi tofauti na kazi aliyoifanya
9.Mradi wa maji
Kila kata iliyopangwa kuwekwa mradi wa maji ilitakiwa kuchangia asilimia
2 hivyo kata anakotoka meya ilitiumiza kigezo na kupata huduma
hiyo.fedha za kata zilitolewa na meya kwa kata yake.hivyo kitendo cha
kata ya meya kupata huduma hakuwa na tatizo.Tuhuma hizi kuwa meya alitoa
huduma kwa kata yakle ni uongo.
10.Issue ya uuzwaji viwanja vya wazi.
Mkataba wa kununua kiwanja kinacholalamikiwa hakufuata taratibu za ununuzi
Ni katika bweni la sekondari ya PEACE inayomilikiwa na
Meya.Tunapendekeza kuundwa kwa trimu maalum kuchunguza tuhuma hizi kwani
katika eneo hili hatukufikia mwisho
11.Ujenzi wa barabara kwa lami kwenye kata ya meya toafuti na fedha zilizoombwa
Manispaa iliomba milioni 30 kukaqrabati barabarab hiyo akini TAMISEMI
ilitao milioni 300 na walihoji TAMISEMI walisema hilo ni la kawaida
hivyo tuhuma hizo ni UONGO
12.Mradi wa Ujenzi wa Bwawa
Hakuwahi kujadiliwa na baraza la madiwani,ulikuwa ni mradi wa wajanja tu
13.Issue ya wafganyabishara soko kuu kutolipa kodi
Manispaa Imekosa mapato sh milioni 256 zimpotea kutokana na chanzo hizo
cha wafanyabishara wa soko kuu kutolipa kodi kutokana na mgogoro
unaondelea
14.Issue ya matumizi ya gari Sm 4663
Gari hili limekuwa likiegeshwa kwa ofisi ya redio kasibante ya
kagasheki.kumbukumbu za TRA zinaonesha kuwa ni mali ya halmashauri
lakini alipohojiwa kagasheki alidai kuwa alinunua kwa fedha zake. Lakini
halmshauri haina kumbukubu zozote juu ya gari hilo
Tunapendekeza
alilrejeshwe kwenye halmshauri kama ataona ni manufaa kwa wananchi
lakini kama haitawezekana basi gari hilo libadilishiwe usajhili ili
lionekbnane ni la kiraia
15.Uteuzi wa wakala wenye upendeleo kwenye ushuru wa basi
Zabubi ya aliyepata rufaa ilitenguliwa kwani haikuwa imesajiliwa na mamlaka husika
Alibadilisha jina na kuomba tena kasha kupata,muombaji aliyeomba kwa tozo ya juu alinyimwa.
Manispaa ilifanya upendeleo na kukosa sh million 46 kwa mwaka
16:Issue ya posho kwa madiwani katika safari ya mafunzo nje ya wilaya.
Madiwani wawili walitakiwa kulipwa sh laki 4 kila mmoja kwa safari
hawakusafiri lakini fedha hizo hazikurudishwa kwa manispaa na kukatiwa
risiti,.hazionekjani zilipo
17.Issue ya vibanda vya maduka
Ukaguzi hakudhibitisha kuwepo tatizo la katika dai hili kwani nyaraka
zinaonesha kutokuwepo tatizo.bali inashauri kuwepo kwa mkanganyiko na
wapangaji wake
18.Issue ya deni katika uwanja wa mpira kaitaba.
Uwanja ulikarabatiwa na kiwanda cha sukari kagera kwa madai ya
kurejeshewa fedha zake.sehemu ya fedha hazijarudishwa.Tume inapendekeza
kufanya muafaka na kiwana au itafute fedha za kulipa deni
19.Kutowajibika ipasavyo kwa ukaguzi wa ndani.
Kipo kwa ajili ya kushauri na kuziba mianya ya matumizi mabaya ya fedha.
Aliyekuwepo amehojiwa juu ya miradi hiyo na kwamba halikuwa hajui lolote na hakuweza kumshauri mkurugenzi ipasavyo
20.Mteuzi katika bodi ya maji.upendeleo kwa mmoja wa madiwani
Waziri mwenye thamana aliteuwa
Hitimisho.
Hatukuweka chumvi,tuliyosema ndiyo ukweli tupu
Namshukuru waziri mkuu kwa kunipa kazi hii ya kukaguzi katika manispaa
Utaratibu wa uwasilisahji wa ripoti maalum tutaipeleka kwa aliyeomba ukaguzi huu.
ASANTENI AMEMALIZA
Mwanry anaongea sasa
Kwa niaba ya waziri mkuu naomba nitoa taarifa hii kama ifuatavyo
Maelekezo ya waziri mkuu.
Makosa ya meya anatory kufanya makubaliano bila idhini ya madiwani na
taratibu za serikali basi ajipimemwenyewe na kujiuzuru kwa maslahi ya
manispaa ya bukoba.
Akikataa basi madiwani wamuondoe
Watumishi wa manispaa wachukuliwe hatua
Bw Khamis kaputa avuliwe madaraka
Mhandisi,mweka hazina nk wapoteze vyeoi vyao
Wakandarasi wote waliopata fedha bila taratibu wazirejeshwe
0 comments:
Post a Comment